STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 28, 2014

Kavumbagu hashikiki, Ruvu Shooting 'kavukavu'


http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/09/DSC04592.jpg
Kavumbagu (kushoto) akishangilia moja ya mabao yake na wachezaji wenzake wa Azam
WAKATI Didier Kavumbagu akiendelea kuongoza kwenye orodha ya wafungaji wa mabao mpaka sasa ligi ikiwa imemaliza mechi za raundi ya pili, Ruvu Shooting inayonolewa na kocha Tom Oloba ndiyo timu pekee ambayo haijaambulia pointi hata moja mpaka sasa.
Pia Ruvu ni kati ya timu mbili ambazo hazijatikisa wavu wa timu pinzania katika ligi hiyo ikienda sambamba na ndigu zao wa JKT Ruvu ambayo leo imefumuliwa mabao 2-0 na Kagera Sugar jijini Dar es Salaam.
Azam wamekalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo licha ya kulingana kila kitu na Mtibwa Sugar kutokana na kubebwa na herufi A.
Ndanda waliokuwa wakiongoza msimamo huo baada ya mechi za ufunguzi, imeporomoka hadi katika nafasi ya nne ikipitwa na Mbeya City wanaokamata nafasi ya tatu.
Didier ndiye kinara wa mabao mpaka sasa akiwa na mabao manne, hali inayoashiria kwamba Yanga walifanya kosa kubwa kumuacha mchezaji huyo kutoka Burundi aondoke Jangwani ilihali kwa misimu miwili mfululizo akiwa na kikosi hicho alikuwa kinara wa mabao ya Yanga.
Hata hivyo ni mapema kutabiri kama Kavumbagu atatimiza ndoto za kutwaa kiatu cha Dhahabu alichokikiosa kizembe msimu wa 2012-2013 baada ya kuzidiwa na Kipre Tchetche licha ya kumaliza duru la kwanza la msimu huo akiongoza orodha ya wafungaji.
Didier anafuatiwa na Ame Ally na Shomary Ally wa Mtibwa wenye mabao mawili kila moja huku orodha ya wachezaji wenye bao moja moja ikiongozwa na nyota wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi na Coutinho walianza kufunga mabao katika mechi zao za wikiendi hii dhidi ya timu za Polisi Moro na Prisons.


MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                                                P  W  D  L  F  A  Pts
1. Azam                                   2   2   0   0  5   1   6
2. Mtibwa Sugar                     2   2   0   0  5   1   6
3. Mbeya City                        2   1   1    0  1   0   4
4. Ndanda Fc                          2   1    0   1  5   4   3
5. Prisons                                2   1    0   1  3   2   3
6.Kagera Sugar                      2    1   0   1  2   1   3
7.Yanga                                   2    1    0  1  2   2   3
8. Mgambo JKT                     2    1   0   1  1    1  3
9.Stand Utd                             2    1   0   1   2   4  3
10.Simba                                 2    0   2   0   3   3  2
11.Coastal Union                    2    0   1   1   2   3  1
12. Polisi Moro                       2    0   1    1  2   4  1
13.JKT Ruvu                          2    0   1    1  0   2  1
14. Ruvu Shooting                  2    0   0    2  0   4  0

TCAA yatumia Sh. Mil 490 kusomesha marubani wa5

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2013/08/IMG-1.jpg
Bestina Magutu (kushoto)
Na Kipimo Abdallah
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA imetumia dola 310,000 sawa na shilingi milioni 496 kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi watano ambao wanasomea urubani wa ndege nchini Afrika Kusini.
Hayo yamebainishwa na Afisa habari wa TCAA  Bestina Magutu wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dar es Salaam.
Alisema wanafunzi hao wamepatikana baada ya mchujo wa wanafunzi 270 ambao waliomba ambapo walibakia 11 na baadae ndio  wakapatikana hao awatano ambao wanalipiwa na TCAA.
Magutu alisema ufadhili ni kwa kila mwanafunzi kupatiwa dola 62,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 99 za Kitanzania ambapo watasoma kwa miezi 14 na mwishoni mwa mwa huu watakuwa wanahitimu.
Alisema jitihada za TCAA ni kuhakikisha kuwa idadi ya marubani inaongezeka kila mwaka ukizingatia kuwa wapo ambao wanastaafu na wengine wakifariki hivyo bu wajibu wa mamlaka hiyo kuongeza watu wa tasnia hiyo.
“TCAA tunajitahidi kuwapatia ufadhili wanafunzi ambao wanakuwa na sifa za kusoma urubani ambapo kwa sasa wapo watano wako Afrika Kusini ila gaharama ni kubwa hivyo tunaomba wadau kujitokeza kufanikisha zoezi hilo”, alisema Magutu.
Afisa Habari huyo wa TCAA alisema hadi kufikia mwezi Julai mwaka huu idadi yamarubani ilikuwa 562 idadi ambayo ni ndogo kutokana na ukweli kuwa kumekuwepo kwa ongezeko kubwa la uwekezaji katika sekta hiyo.
Magutu alisema iwapo Serikali itaachiwa yenyewe katika kutoa mafunzo ya urubani ni wazi kuwa idadi itakuwa ndogo hali ambayo itachangia kazi nyingi kuchukuliwa na watu kutoka nje.
Alitoa wito kwa jamii kushirikiana ili kuhakikisha kuwa nchi inakuwa na idadi kubwa ya watu wenye fani ya urubani ili kuhakikisha kuwa fursa zinazojitokeza wanaziitumia ipasavyo.
Aidha akizungumzia ni kwa nini wanafunzi hao wanaenda kusoma nje ya nchi na sio hapa nchini Ispecta Mwandamizi wa Idara ya Udhibiti Masuala ya Usalama wa Ndege Redemptus Bugomola alisema vyuo vilivyopo hapa nchini vinatoa elimu ya urushaji ndege za watu binafsi jambo ambalo haliwezi kukidhi hitaji la ndege za kibiashara na zile kubwa.
Bugomole alisema sekta anga ni moja ya sekta ambayo inahitaji uwepo wa watu wenye nia madhubuti ya kusoma kutokana na ukweli kuwa matumizi yake yanhitaji umakini wa hali ya juu.

Pambano la Nasibu na Matumla Jr hakuna mbabe

Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jana katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana pointi.
Bondia Mohamed Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Nasibu Ramadhani wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam mpambano huo ulitoka droo za kufungana pointi
Bondia Lulu Kayage akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Fatuma Yazidu wakati wa mpambano wao Yazidu alishinda kwa pointi mpambano huo.
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo.
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa pointi.
Mabondia wa kike Fatuma Yazidu kushoto na Lulu Kayage wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa Friends Corne Manzese Dar es salaam Yazidu alishinda kwa point mpambano huo.
Bondia Lulu Kayage akilalamikia matokeo ya kupigwa na Fatuma Yazidu kulia ni bondia Ibrahimi Class 'King Class Mawe'
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo pamoja na mashabiki mbalimbali
Mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe'  kushoto na Shomari Milundi wakifuatilia mpambano huo
 
Mabondia Juma Bigilee kushoto,Ibrahimu Class ; King Class Mawe' na Rashidi Mhamila wakiwa katika pozi baada ya mchezo kumalizika

Kingunge awashushua wanaoiota Tanganyika


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1ZYzBGLwXu0x9UUT0731EMnVXnS3ORTl2ardjjCveW-DptFDEfVH4KiZtdRSjy-RZaWJ6k-0A3U6UVSj9aE2xoIG-Si79w_J4GMZifJDM8J2GG4KTLYy16Jly2XJvEc7vHbKbLanG6w59/s1600/DSCF0347.JPG 
Na Kipimo AbdallahWAKATI suala la Utanganyika na Utanzania liendelea kukuna vichwa vya wanasiasa na wananchi wa kada mbalimbali Mwanasiasa Mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amewataka watanzania wasahau hilo na kujitambua kuwa wao ni Watanzania.
Kauli hiyo ya Ngombale Mwiru inakuja ikiwa ni muda mchache baada ya Mjumbe mwenzake ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la  Maalumu la Katiba John Cheyo kusema itakuwa ngumu kwa jamii kuondolewa dhana ya kuwaTanganyika haipo.
Mzee Ngombale Mwiru alisema ni jambo la kusikitisha kuona watu wanaitaja Tanganyika wakati wakijua kuwa hiyo ni historia ya aibu kwa Watanzania ambao walikuwepo katika kipindi hicho cha ukombozi wa Taifa hili.
Ngombale Mwiru alisema jambo la kushangaza wapo watu ambao hata Tanganyika hawajaishuhudia lakini wameonekana kuwa na nguvu ya kuhitaji uwepo wake jambo ambalo linapotosha jamii.
“Kwa kweli sikuwa na dhamira ya kulizungumzia suala hili ila nimeshawishika baada ya kuona mzee mwenzangu kuongea na kuonyesha kuhitaji Tanganyika jambo ambalo mimi nalipinga kwa nguvu zote kwa sababu najua historia yake haina maana kwa Watanzania wa leo” alisema.
Aidha Mzee Ngombale Mwiru alitoa wito kwa jamii kusoma historia ya nchi hii ili kuhakikisha kuwa wanapata takwimu sahihi za nchi yao ili kuacha tabia ya kufuata mkumbo ambao hauna tija kwa maslahi ya Taifa.
Akichangia katika Bunge hilo Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo alisema itakuwa ngumu kuisahau Tanganyika kutokana na ukweli kuwa ndiyo msingi wa uwepo wa Tanzania.
Cheyo alisema haiwezekani Zanzibar ikaendelea kuwepo na kutambulika na Tanganyika ikasahaulika katika mazingira ya kawaida kama baadhi ya viongozi wengine wanavyotaka.
Mjumbe huyo wa Bunge la Katiba alisema ni vema jamii ikapatiwa elimu ya kutosha ili kuhakikisha kuwa ufahamu unakuwepo wa kutosha ili kila Mtanzania aweze kuwa na uelewa juu ya nchi yao.
 Kwa upande mwingine Cheyo amewataka wabunge kutoka Zanzibar wasije kuzuia haki za Watanzania Bara wanaozidi milioni 47 wakati wa upigaji kura ili kuhakikisha kuwa Katiba hiyo inayopendekezwa inapita.
Cheyo alisema idadi ya wazanzibari ni ndogo ila ina nguvu katika mchakato mzima wa kupatikana kwa katiba ambayo itaweza kulinda muungano wa nchi au kuuvunja.
Alisema lipo suala la aina ya muungano ambalo limeweza kuleta malumbano makubwa sana katika Bunge hilo hivyo ni vema suala hilo likatafakariwa vizuri ili kuhakikisha kuwa kila upande unaridhika kwa maslahi ya Taifa.
Cheyo alisema itakuwa vizuri iwapo fursa itapatikana kwa wahusika kutoa nafasi kwa wananchi kupiga kura dhidi ya aina gani ya muungano wanaoutaka ili kuhakikisha kuwa suala hilo limetatuliwa.
Mbunge huyo wa Bunge la Katiba alitoa rai kwa baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao wanaendelea na harakati za kuhamasisha jamii kupinga Bunge hilo waachane na mpango huo kwani wao wapo kihalali.
Alisema Kituo Cha Demokrasia (TCD) kipo hivyo wanapaswa kukitumia ili kuhakikisha kuwa wanafikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na sio kung’amg’ania maandamano ambayo yanahatarisha maisha ya watanzania.

Kapteni Ligora awapasha wanasiasa wanaolumbana

http://3.bp.blogspot.com/-eqAX732KQAk/U_CoM9ap3ZI/AAAAAAAAWP4/wTE9EfEZszs/s1600/WAZEE%2B01.jpg
Na Kipimo AbdallahKATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Kapteni Mstaafu Mohammed Ligora amewataka wanasiasa kuacha kulumbana juu aina ya katiba kwani wenye maamuzi ya mwisho ni wananchi ambao watapiga kura.
Ligora alisema hayo jana ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana hali ya sintofamu juu ya hatma ya katiba pendekezwa ambayo imesomwa na Mweyekiti wa Kamati ya Uandishi Adrew Chenge.
Alisema anapatwa na mshangao dhidi ya baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari huku wakitambua kuwa wenye maamuzi ya mwisho dhidi ya aina ya serikali na mambo mengine ni wananchi.
Kapteni Mstaafu huyo alisema ni vema viongozi wa kisiasa pamoja na wale wanaoitwa watetezi wa haki za wananchi kujikita katika harakati za kujenga nchi hasa pale ambapo inaonekana kuwa Chama Tawala na Serikali yake kimeshindwa kufanya vizuri.
“Napenda kutoa rai kwa wanasiasa na wanaharakati kujitikita katika masuala mengine yenye tija kwa nchi kwani hili la katiba muafaka wake upo chini ya wananchi wenyewe ambao ndio wataamua kuwa katiba iwepo au la”, alisema Ligora.
Katibu Mstaafu huyo alisema jamii ya Kitanzania ina watu wengi ambao wameelimika hivyo hawahitaji kufanyiwa maamuzi ambayo yanaweza kuwa na maslahi kwa watu wengine ambao wanajiita wanasiasa.
Aliwataka wananchi kufanya maamuzi ambayo yatakuwa yamezungukwa na utashi wao bila kushurutishwa na mtu yoyote kwani nchi ya Tanzania ni ya kila mtanzania bila kuangalia rangi, elimu na ukabila.
Kwa upande mwingine Kapteni Mstaafu huyo alisema ni wakati wa vyama vya siasa kuonyesha ushirikiano mkubwa ili kuweza kudumisha umoja, amani na utulivu wa Taifa la Tanzania ambalo limejaliwa jamii yenye upendo.
Alisema kasoro ambazo zimeonekana katika mchakato mzima wa kutengeneza katiba zisiwe sababu ya kupelekea Taifa katika machafuko kwani madhara yake yatakuwa ya muda mrefu kwa jamii ya Watanzania.
“Unajua suala la kujitambua ni muhimu katika maamuzi ili kuhakikisha kuwa maamuzi yote tunayofanya yanakuwa na weledi jambo ambalo mimi naamini asilimia 80 ya watanzania inajitambua”, alisema.

Yanga yaizima Prisons, Coutinho atupia, Kagera yaiua JKT Ruvu

http://api.ning.com/files/TQDVHBx0tuW3uYd3Hlc1u9fa7CEF04w*k4I94R9HrkYatgIrq-g2atl0ZzYAt9xFoxdmCIGWif22TfQkM6XSLf9MqO1vd*6b/COUTINHO.jpg
Coutinho aliyerejea na bahati jangwani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_4EFuv2AZMTxTK507IEk38peIzLAvmxPWIcSIvLbGm663MNQQM752-EFBTwep6sws02MX1e0tsQRe-9Bs8XPyf_EXN47h0kQW7lAgkPsiZ2GecmjTGDD69kMxpjOPUXh57GikV7gUB081/s1600/Yanga+iliyobeba+Ngao+ya+Jamii.JPG
Yanga
Prisons-Mbeya
KIUNGO mshambuliaji Andrey Coutinho amerejea dimbani na mguu wa Bahati baada ya kuisaidia Yanga kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Prisons-Mbeya katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Coutinho aliyekuwa majeruhi aliifungia Yanga bao dakika ya 34 kwa mkwaju wa adhabu baada ya Mrisho Ngassa aliyesumbua katika mechi ya leo kuangushwa mita 25 toka lango la Prisons.
Bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya Yanga kukosa mabao mengi ya wazi kupitia kwa Genilson Santana 'Jaja' huku Prisons wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na mwamuzi Andrew Shamba dakika chache baada ya bao la Yanga kwa kumchezea vibaya Ngassa.
Kipindi cha Prisons waliingia wakiwa tofauti na kuliandama lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 64 kupitia kwa Ibrahim Kihaka, ingawa Yanga ilijibu mapigo dakika mbili baadaye kupitia kwa Simon Msuva aliyefunga bao la pili lililoisaidia kuipa Yanga pointi tatu za kwanza na kuchupa toka mkiani hadi katika nafasi za kati ikiwa na pointi nne.
Katika mechi nyingine ya pili hiyo iliyochezwa uwanja wa Chamazi, maafande wa JKT Ruvu wameshindwa kuhimili vishindo vya wakata miwa wa Kagera Sugar baada ya kukubali kipigo cha amabo 2-0.
Mabao ya washindi yalifungwa kila kipindi na wachezaji Salum Kanoni na Rashid Mandawa na kuifanya kagera kufikisha pointi tatu baada ya mechi mbili tangu kuanza kwa ligi hiyo wiki iliyopita.

TP Mazembe yashinda, ila yakwamba kucheza Fainali Afrika

tpess22
Voir l'image sur Twitter
Kipa wa Mazembe akilia huku akitulizwa na mchezaji wa ES Setif
Voir l'image sur Twitter
Ilikuwa vita
LICHA ya kupata ushindi wa mabao 3-2 nyumbani mjini Lubumbashi, TP Mazembe imeshindwa kuwapa fursa nyota wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kucheza kwa mara ya kwanza Fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mazembe ilimejikuta waking'oka kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya matokeo ya mwisho kuwa mabao 4-4 baada ya awali kufungwa ugenini na ES Setif ya Algeria kwa mabao 2-1.
Katika mechi iliyomalizika jioni hii, Mazembe ilihitaji ushindi wa aina yoyote usio wa magoli, kitu ambacho hata hivyo hakikutokea baada ya kuruhusu wageni kupata mabao yaliyowabeba kutinga Fainali.
Wageni waliwaduwaza Mazembe kwa kuandika bao dakika ya 9 tu ya mchezo kupitia Ziaya kabla ya Adjei Nii kusawazisha kwenye dakika ya 21 na kufanya matokeo kuwa bao 1-1.
Coulibaly aliiongezea Mazembe bao katika dakika ya 38 na kufanya waende mapumziko wakiwa nguvu sawa ya jumla ya mabao 3-3 ukijumlisha na mechi yao ya awali.
Mbwana Samatta alimtengenezea Bolingui pande safi na kuandika bao la tatu dakika ya 53 na kuonekana kama Mazembe wanaelekea kufuzu fainali hizo za Afrika.
Hata hivyo Younès kuifungia Setif bao muhimu dakika ya 75 na kufanya hadi mwisho matokeo kuwa mabao 3-2 Mazembe wakishinda, lakini waking'oka na kuwakosesha akina Samatta kuweka rekodi ya kuwa Watanzania wa Kwanza kucheza fainali za Afrika.
ES Setif sasa itapambana na AS Vita pia ya DR Congo ambayo jana iliweka rekodi baada ya kuwang'oa Sfaxien ya Tunisia kwa jumla ya mabao 4-2 kufuatia ushindi wa kushangaza wa mabao 2-1 ugenini.
Katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita Vita ilishinda pia mabao 2-1.