Coutinho aliyerejea na bahati jangwani |
Yanga |
Prisons-Mbeya |
Coutinho aliyekuwa majeruhi aliifungia Yanga bao dakika ya 34 kwa mkwaju wa adhabu baada ya Mrisho Ngassa aliyesumbua katika mechi ya leo kuangushwa mita 25 toka lango la Prisons.
Bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko licha ya Yanga kukosa mabao mengi ya wazi kupitia kwa Genilson Santana 'Jaja' huku Prisons wakiwa pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na mwamuzi Andrew Shamba dakika chache baada ya bao la Yanga kwa kumchezea vibaya Ngassa.
Kipindi cha Prisons waliingia wakiwa tofauti na kuliandama lango la Yanga na kufanikiwa kusawazisha bao dakika ya 64 kupitia kwa Ibrahim Kihaka, ingawa Yanga ilijibu mapigo dakika mbili baadaye kupitia kwa Simon Msuva aliyefunga bao la pili lililoisaidia kuipa Yanga pointi tatu za kwanza na kuchupa toka mkiani hadi katika nafasi za kati ikiwa na pointi nne.
Katika mechi nyingine ya pili hiyo iliyochezwa uwanja wa Chamazi, maafande wa JKT Ruvu wameshindwa kuhimili vishindo vya wakata miwa wa Kagera Sugar baada ya kukubali kipigo cha amabo 2-0.
Mabao ya washindi yalifungwa kila kipindi na wachezaji Salum Kanoni na Rashid Mandawa na kuifanya kagera kufikisha pointi tatu baada ya mechi mbili tangu kuanza kwa ligi hiyo wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment