STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, September 28, 2014

Kapteni Ligora awapasha wanasiasa wanaolumbana

http://3.bp.blogspot.com/-eqAX732KQAk/U_CoM9ap3ZI/AAAAAAAAWP4/wTE9EfEZszs/s1600/WAZEE%2B01.jpg
Na Kipimo AbdallahKATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Kapteni Mstaafu Mohammed Ligora amewataka wanasiasa kuacha kulumbana juu aina ya katiba kwani wenye maamuzi ya mwisho ni wananchi ambao watapiga kura.
Ligora alisema hayo jana ikiwa ni siku chache baada ya kuonekana hali ya sintofamu juu ya hatma ya katiba pendekezwa ambayo imesomwa na Mweyekiti wa Kamati ya Uandishi Adrew Chenge.
Alisema anapatwa na mshangao dhidi ya baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakiendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari huku wakitambua kuwa wenye maamuzi ya mwisho dhidi ya aina ya serikali na mambo mengine ni wananchi.
Kapteni Mstaafu huyo alisema ni vema viongozi wa kisiasa pamoja na wale wanaoitwa watetezi wa haki za wananchi kujikita katika harakati za kujenga nchi hasa pale ambapo inaonekana kuwa Chama Tawala na Serikali yake kimeshindwa kufanya vizuri.
“Napenda kutoa rai kwa wanasiasa na wanaharakati kujitikita katika masuala mengine yenye tija kwa nchi kwani hili la katiba muafaka wake upo chini ya wananchi wenyewe ambao ndio wataamua kuwa katiba iwepo au la”, alisema Ligora.
Katibu Mstaafu huyo alisema jamii ya Kitanzania ina watu wengi ambao wameelimika hivyo hawahitaji kufanyiwa maamuzi ambayo yanaweza kuwa na maslahi kwa watu wengine ambao wanajiita wanasiasa.
Aliwataka wananchi kufanya maamuzi ambayo yatakuwa yamezungukwa na utashi wao bila kushurutishwa na mtu yoyote kwani nchi ya Tanzania ni ya kila mtanzania bila kuangalia rangi, elimu na ukabila.
Kwa upande mwingine Kapteni Mstaafu huyo alisema ni wakati wa vyama vya siasa kuonyesha ushirikiano mkubwa ili kuweza kudumisha umoja, amani na utulivu wa Taifa la Tanzania ambalo limejaliwa jamii yenye upendo.
Alisema kasoro ambazo zimeonekana katika mchakato mzima wa kutengeneza katiba zisiwe sababu ya kupelekea Taifa katika machafuko kwani madhara yake yatakuwa ya muda mrefu kwa jamii ya Watanzania.
“Unajua suala la kujitambua ni muhimu katika maamuzi ili kuhakikisha kuwa maamuzi yote tunayofanya yanakuwa na weledi jambo ambalo mimi naamini asilimia 80 ya watanzania inajitambua”, alisema.

No comments:

Post a Comment