Kipa wa Mazembe akilia huku akitulizwa na mchezaji wa ES Setif |
Ilikuwa vita |
Mazembe ilimejikuta waking'oka kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya matokeo ya mwisho kuwa mabao 4-4 baada ya awali kufungwa ugenini na ES Setif ya Algeria kwa mabao 2-1.
Katika mechi iliyomalizika jioni hii, Mazembe ilihitaji ushindi wa aina yoyote usio wa magoli, kitu ambacho hata hivyo hakikutokea baada ya kuruhusu wageni kupata mabao yaliyowabeba kutinga Fainali.
Wageni waliwaduwaza Mazembe kwa kuandika bao dakika ya 9 tu ya mchezo kupitia Ziaya kabla ya Adjei Nii kusawazisha kwenye dakika ya 21 na kufanya matokeo kuwa bao 1-1.
Coulibaly aliiongezea Mazembe bao katika dakika ya 38 na kufanya waende mapumziko wakiwa nguvu sawa ya jumla ya mabao 3-3 ukijumlisha na mechi yao ya awali.
Mbwana Samatta alimtengenezea Bolingui pande safi na kuandika bao la tatu dakika ya 53 na kuonekana kama Mazembe wanaelekea kufuzu fainali hizo za Afrika.
Hata hivyo Younès kuifungia Setif bao muhimu dakika ya 75 na kufanya hadi mwisho matokeo kuwa mabao 3-2 Mazembe wakishinda, lakini waking'oka na kuwakosesha akina Samatta kuweka rekodi ya kuwa Watanzania wa Kwanza kucheza fainali za Afrika.
ES Setif sasa itapambana na AS Vita pia ya DR Congo ambayo jana iliweka rekodi baada ya kuwang'oa Sfaxien ya Tunisia kwa jumla ya mabao 4-2 kufuatia ushindi wa kushangaza wa mabao 2-1 ugenini.
Katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita Vita ilishinda pia mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment