![]() |
| Jamie Vardy |
Kwa mujibu wa Daily Star, The Kop imekuwa ikimwania mkali huyo wa mabao mwenye umri wa miaka 29 kwa misimu miwili sasa.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, tayari ndani ya kikosi chake kina wanaume wa shoka katika safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na Daniel Sturridge, Divock Origi, Christian Benteke na Danny Ings.
Hata hivyo inaelezwa kuwa Vijogoo hao wa Anfield wapo tayari kumuuza mmoja wa mastraika hao, huku Benteke akihusishwa zaidi ili kumpisha Vardy, kwa vile ni kama hayupo kwenye mipango ya Kocha Klopp.
Klabu ya Arsenal imekuwa nayo ikimsaka straika huyo, ila mwenyewe amedaiwa hajaamua lolote kwa sasa mpaka baada ya michuano ya fainali za Euro 2016 inayoanza kesho Ijumaa huko Ufaransa akiiwakilisha nchi yake ya England.

HANA namna. Maumivu ambayo yamekuwa yakimuandama mara kwa mara nyota wa zamani wa Liverpool, Daniel Agger yamemfanya atundike daluga. Agger ametangaza kustaafu soka akiwa ndio kwanza ana umri wa miaka 31 tu. Beki huyo amekuwa akisumbuliwa kwa kipindi kirefu cha soka lake la majeruhi aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kuelezea uamuzi wake huo. Agger aliandika katika twitter akiwashukuru wale wote waliomuunga mkono katika kipindi chote na kuongeza japo ni uamuzi mgumu, lakini anadhani ni sahihi kwa afya yake.
WANANUKA pesa. Labda ubishe tu, lakini imefichuliwa kuwa nyota wanaochuana kwa sasa duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ndio wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani.








