STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 7, 2014

Dk Ndumbaro kuburuzwa Kamati ya Nidhamu kisa...!

http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/06/ndumbalo1.jpg
Dk Damas Ndumbaro, Mwanasheria wa Klabu 14 za Ligi Kuu zinazopinga agizo la TFF kuwakata asilimia 5 za fedha za wadhamini wao
SAKATA la vilabu 14 vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Bara kupitia kwa mwanasheria wao, Dk Damas Ndumbaro, kupingana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya kukatwa asilimia tano ya fedha za wadhamini wa ligi hiyo na kutishia kutoshiriki ligi na zitapiga kura ya maoni ya kutokuwa na imani na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, ikiwa TFF itatekeleza azma yake, limechukua sura.
Mapema wiki iliyopita, Malinzi aliagiza timu hizo kukatwa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Soka (FDF) ambapo klabu husika zikiwemo Simba na Yanga zimepinga hatua hiyo na kutishia kutocheza ligi kuu kama agizo hilo litatekelezwa na Bodi ya Ligi.
Sasa kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika inaelezwa kwamba Shirikisho la soka nchini limefikia hatua ya kumpeleka mwanasheria huyo Damas Ndumbaro kwenye Kamati ya Nidhamu ya shirikisho hilo kutokana na kitendo chake alichokifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Credit:Shafii Daud

CAF yaitosa Tanzania AFCON 2017

http://i2.cdn.turner.com/cnn/dam/assets/140823175408-afcon-trophy-story-top.jpgSHIRIKISHO  la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefahamishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa Tanzania haitaweza kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika- AFCON 2017 kwa kuwa haijawahi kuandaa fainali zozote za vijana Afrika. Fainali hizo ni zile za vijana wenye umri chini ya miaka 17 na 20.
Hivyo, TFF inaelekeza nguvu zote katika kuandaa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka U17 mwaka 2019.
Tunapenda kuchukua fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania, Jakaya Kikwete kwa kututia moyo katika kuomba uenyeji wa AFCON 2017.
Pia tunamshukuru Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara kwa juhudi binafsi alizozionyesha katika jitihada za Tanzania kuomba uenyeji wa AFCON 2017.
TFF inaamini kwa dhati kuwa uenyeji wa Afrika U17 2019 utaifungulia Tanzania milango ya kuandaa mashindano makubwa zaidi.

Newz Alert! Mwanasheria Mkuu ZNZ afutwa kazi

HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Othman Masoud amefutwa kazi na Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Ali Shein.
Taarifa kutoka visiwani humo zinasema kuwa Mwanasheria huyo aliyeamua kutumia demokrasia yake katika Bunge la Katiba kwa kupigia kura za ndiyo na hapana vipengele na ibara za Rasimu ya Katiba Mpya amefutwa kazi usiku huu.
Inaelezwa maamuzi hayo ya Dk Shein yamekuja ikiwa imesalia saa chache kabla ya rasimu huyo kukabidhiwa kwa viongozi wakuu wa nchi kesho mjini Dodoma na nafasi yake imeelezwa inazibwa na aliyekuwa Mwansheria Mkuu Msaidizi, Said Hassan Said.
hata hivyo haikuelezwa sababu ya kufutwa kazi kwa Mwanasheria huyo ambaye kwa baadhi ya wajumbe na wananchi wa visiwani humo wanamuona kama 'Msaliti' kwa alichokifanya kwenye Bunge Katiba lililomalizika hivi karibuni.

Mkude, Mgeveke waongezwa Stars


http://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2014/05/IMG_7000.jpgKATIKA kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi yao ya Jumapili dhidi ya Benin, Kocha Mart Nooij ameongeza wachezaji watatu kwenye kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ili kukiongezea nguvu.
Taifa Stars inajianda kukabiliana na Benin katika mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)  itakayofanyika Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Wachezaji walioongezwa ni kiungo Jonas Mkude na mlinzi Joram Mgeveke kutoka timu ya Simba, pamoja na mlinzi Gadiel Michael wa Azam.

WANYARWANDA KUZIHUKUMU STARS v BENIN

taifa stars 2014

MAREFA kutoka Rwanda ndiyo watakaochezesha mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kati ya Taifa Stars na Benin itakayofanyika Jumapili jijini Dar es Salaam. Hakizimana Louis ndiye atakayeongoza waamuzi hao wa FIFA kwa kupuliza filimbi kwenye mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 11 jioni. 
Atasaidiwa na Simba Honore na Niyitegeka Jean Bosco.
Mechi hiyo itatanguliwa na ile ya viongozi wa dini- Kiislamu vs Kikristo kudumumisha upendo, amani na ushirikiano itakayoanza saa 9 kamili alasiri. 

Tiketi za elektroniki zitakazotumika kwa mechi hiyo tayari zimeanza kuuzwa kwa kiingilio cha sh. 4,000 na sh. 10,000.

Arsene Wenger apuuzia sakata lake na Mourinho


KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kamwe hajutii kumsukuma kocha wa Chelsea, Jose Mourinho katika mechi ya juzi zikiwa ni dakika 20 tu tangu mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Stamford Bridge kuanza kuchezwa.
Wawili hao walitibuana baada Gary Cahill kumchezea rafu mbaya winga mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na Wenger kukasirishwa na uamuzi wa Mourinho wa kuonyesha kumtetea Cahill.
Hata hivyo, kama si juhudi za refa Martin Atkinson na mwamuzi wa akiba Jonathan Moss kujaribu kuwasuluhisha zingepigwa kavu kavu.
"Cha kujutia nini baada ya hilo? Nilitaka kwenda kutoka (pointi) A hadi B na mtu fulani akanitibua bila kuonyesha ishara ya mapokeo," Wenger alisema.
"B ilikuwa ni kuangalia kama Sanchez aliumia. Ilikuwa ni kusukumwa? Kidogo. Unaweza kuona kama ukweli nimejaribu kumsukuma."
Wenger anasema alimsukuma "kidogo" Mourinho.
Hata hivyo walitenganishwa na mwamuzi wa akiba Jon Moss na refa Atkinson, lakini haitarajiwi FA kuwachukulia hatua zaidi.
Mourinho alisema alitaka "kusahau" kuhusu tukio hilo na Mfaransa huyo, na akasisitiza hakufanya lolote baya.
"Inauma kwa sababu hii ni mechi kubwa, klabu kubwa, mpinzani mkubwa,na mechi muhimu kwa timu zote. Hali hii inaufanya mchezo kuwa na hisia,'' alisema.
"Nimefanya makosa mengi sana katika soka, lakini si kipindi hiki kwa sababu nilikuwa katika eneo langu la kiufundi na halikuwa kosa langu. Mchezo umekwisha. Mwisho wa stori."
Uhusiaano wa makocha hao wawili umekuwa wa maneno maneno katika mechi kwa kipindi kilichopita, kwa Mourinho kumpachika Wenger "mtaalam wa kufeli" hiyo ilikuwa Februari mwaka huu.
Mourinho pia alisema hahofii uamuzi wa kitabibu baada ya Thibaut Courtois kuhaha kutokana na kukwaruzana na mshambuliaji wa Kimataifa wa Chile Sanchez na kwamba pengo hilo likiwamo litazibwa na Petr Cech.

Esha Buheti achekelea tuzo mbili kwa mpigo

Esha Buheti akiwa na tuzo yake ya ACVCA-2014
http://2.bp.blogspot.com/-RLZp_l7brig/VBFh6i_4LAI/AAAAAAAANMA/d5c-rUNNvmE/s1600/2.jpg
Esha Buheti katika pozi
MSHINDI wa Tuzo za filamu za Action & Cuts Viewers Choice (ACVCA-2014) Esha Buheti amesema mafanikio aliyopata kwa kipindi kifupi katika tasnia hiyo imetokana na kipaji cha kuzaliwa, kujituma na kujiheshimu mbele ya jamii.
Esha alisema, amejisikia faraja kuona ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu akinyakua tuzo ya pili baada ya ile ya ZIFF-2014 (Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar) na katu hatavimba kichwa badala yake kuongeza bidii afike mbali zaidi.
Mrembo huyo alisema kuwashinda nyota wa filamu kama Chuchu Hans, Salma Jabu 'Nisha', Shamsa Ford na Blandina Chagula 'Johari' siyo kazi ndogo na kusisitiza anashukuru wote waliopigia kura za kutosha na kunyakua tuzo hiyo ya pili.
"Kwa kweli nimejisikia faraja kubwa kwa lililonitokea, sikuamini kama ningeweza kuibukia mshindi mbele ya washindani wangu ambao naamini ni wakali. Hii ni changamoto kwangu kundelea kufanya vyema ili nitambe kimataifa," alisema.
Muigizaji huyo alishinda tuzo hiyo wiki iliyopita katika kipengele cha Muigizaji Bora Msaidizi, ikiwa ni miezi mitatu tangu alipotwaa tuo ya Muigizaji Bora wa Kike wa ZIFF-2014 kupitia filamu ya 'Mimi na Mungu Wangu' anayoitaja kama kazi bomba kwake.

Hammer Q kuweka kibakuli chake videoni

http://4.bp.blogspot.com/-w6MTWT1zfeM/Ufs-69Ti9II/AAAAAAAAAvM/9Lsk-xVF3-Q/s1600/Hammer+Q.jpgMUIMBAJI mahiri wa muziki wa taarab, Hammer Q ameachiwa wimbo wake binafsi uitwao 'Kibakuli', ambao anajipanga kuutengenezea video yake mapema hivi karibuni.
Hammer Q aliyewahi kutamba kwenye muziki wa kizazi kipya na wimbo wa 'Lady' kabla ya kuhamia kwenye taarab, ameachiwa wimbo huo uliopo kwenye mduara.
Wimbo huo umetengenezwa na mtayarishaji aitwae Anta Nation na  umeanza kutamba kwenye redio na mitandao ya kijamii.
Msanii huyo amesema kwa sasa anafanya mchakato ili kutengeneza video ya wimbo huo mapema kuwapa burudani zaidi mashabiki wake.
Hammer Q mbali na kufanya muziki kama 'solo artist' pia analiimbia kundi maarufu na miondoko ya mduara ya Zanzibar la Offside Trick sambamba na kufanya kazi na mkewe Salha Abdallah 'Salha wa Hammer'

Ligi ikienda mapumziko, Yanga yapumua, Mtibwa Sugar inatisha

Yanga wanaenda mapumziko wakipumua nafasi ya tatu
Coastal Union bado wanajikongoja

Watetezi Azam wakiporomoka hadi nafasi ya pili wakiwapisha Mtibwa kuwaongoza
Mtibwa timu pekee iliyoshinda mechi zake 100%

Ruvu Shooting ndiyo ambayo haijafunga bao hata mmoja mpaka sasa. Ni kwamba pengo la Maguli (kushoto) halijapata mrithi wa kuliziba?
http://3.bp.blogspot.com/-Z35Pf9TZhqU/VDAWaV__VvI/AAAAAAABKQ8/hgwGc4Wi6Nc/s1600/HMB_8265.JPG
Simba wataivaa Yanga mechi ijayo ikiandamwa na mdudu wa sare
RAUNDI ya tatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara umemalizika  mwishoni mwa wiki na kushuhudia jumla ya mabao 44 yakitinga wavuni, huku mshambuliaji wa Azam Didier Kavumbangu akiongoza kwa kupachika mabao manne kati ya hayo.
Kavumbagu aliyetua Azam akitokea Azam anafuatiwa kwa karibuni na Ally Shomari wa Mtibwa mwenye mabao matatu kiisha kufuatiwa na wachezaji wanne wenye mabao mawili kila mmoja.
Timu yenye fowadi kali mpaka sasa wakati lihi ikienda mapumziko kwa wiki moja ni Mtibwa Sugar na Ndanda FC zenye mabao sita kila moja, kisha kufuatiwa na Azam yenye mabao matano kisha Yanga na Simba zikafuatia zikiwa zimetumbukiza kimiani mabao manne kila moja.
Pamoja na kuwa kinara wa kufunga mabao Ndanda pia ndiyo timu yenye ukuta mwepesi ikiruhusu mabao sita mpaka sasa ikifuatiwa na timu za Stanmd United na Polisi waliopanda pamoja ligi ya msimu huu zikiwa zimeruhusu mabao matano.
Ruvu Shooting ndiyo timu iliyo na safu butu mpaka sasa ikiwa haijafunga bao lolotewakifuatiwa na Mbeya City, Mgambo na JKT Ruvu wenye bao moja moja.
Ukuta wa chuma wa ligi hiyo mpaka sasa ni ule wa klabu ya Mbeya City ambayo haujaruhusu bao lolote kwake huku Mtibwa Sugar na Azam zikifuata kwa kufungwa bao moja tu kila moja.
Yanga ambayo ilianza kwa kipigo katika ligi ya msimu huu imechupa toka maeneo ya kati hadi nafasi ya tatu wakiwaacha watani zao watakaoumana nao katika mechi yao ijayo wakiwa na pointi tatu wakishika nafasi ya 10.


MSIMAMO KAMILI WA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                               P   W    D    L    F    A   GD   Pts

01. Mtibwa Sugar     03  03   00  00  06   01  +5   09
02. Azam                 03  02   01  00  05   01  +4   07
03.Yanga                  03  02   00  01  04   04  00   06
04. Mbeya City          03  01  02  00  01   00  +1   05
05.Kagera Sugar       03  01  01   01  03   02 +1   04
06. Prisons                03  01  01   01  03  02  +1  04
07.Coastal Union       03  01  01   01  04  04   00  04
08.Stand Utd             03  01  01   01  03   05  -2   04
09. Ndanda Fc           03  01  00   02  06    06  00  03
10.Simba                  03  00  03   00  04    04  00  03
11. Mgambo JKT       03  01  00   02   01    02  -1  03
12. Polisi Moro          03  00   02  01   03    05   -2  02
13.JKT Ruvu             03  00   01  02   01   04   -3  01
14. Ruvu Shooting     03  00  01   02  00   04   -4  01

http://static.goal.com/462500/462526_heroa.jpg
Didier Kavumbangu  (kushoto) akipongezwa na wenzake
Wafungaji Bora:
4- Didier Kavumbagu(Azam)


3-
Ally Shomari (Mtibwa)


2-
Shaaban Kisiga (Simba), Nassor Kapama (Ndanda), Ame Ally (Mtibwa), Rashind Mandawa (Kagera)


1- Emmanuel Okwi, Amissi Tambwe (Simba), Coutinho, Kelvin Yondan, Haruna Niyonzima, Simon Msuva (Yanga), Deo Julius (Mbeya City), Danny Mrwanda, Nicolaus Kabipe, Bakari (Polisi-Moro),  Salum Kanoni,  (Kagera), Aggrey Morris  (Azam), Ernest Joseph, Paul Ngalema, (Ndanda), Jacob Mwaitalako, Ibrahim Kihaka, Laurian Mpalile (Prisons), Lutimba Yayo, Rama Salimu, Joseph Mahundi, Hussein Sued, (Coastal), Ramadhani Pella (Mgambo), Mussa Mgosi (Mtibwa), Jabir Aziz (JKT Ruvu), Salum Kamana, Heri Mohammed, Mussa Said(Stand Utd)

Baby Madaha 'ala shavu' Ujerumani

STAA wa 'Amore' na 'Summer Holliday', Baby Madaha amekula shavu baada ya kuteuliwa kwenda kushiriki filamu ya kimataifa nchini Ujerumani iitwayo 'Saint & Ghost'.
Muigizaji huyo aliliambia MICHARAZO kuwa, anajiandaa kupaa kwenda Ujerumani kushiriki filamu hiyo itakayotengenezwa na mtayarishaji maarufu Dittiman.
Baby Madaha alisema filamu hiyo itawashirikisha pia waigizaji wengine kutoka nchini Ujerumani na kutamba ni nafasi yake ya kujitangaza zaidi kimataifa.
"Nashukuru Mungu nimepata bahati ya kuteuliwa kwenda kushiriki katika filamu inayotengenezwa na Prodyuza Dittiman iitwayo 'Saint and Ghost' kazi hiyo itafanyika nchini Ujerumani," alisema Baby Madaha.
Msanii huyo anayepanda farasi wawili kwa wakati mmoja kwa maana ya kuimba muziki na kucheza filamu, alisema uteuzi wake umekuja baada ya kuwavutia waratibu wa filamu hiyo kupitia kazi mbalimbali alizocheza ambazo zimekuwa zikifanya vyema kimataifa.
Baadhi ya filamu alizocheza mwanadada huyo ni 'Desperado', 'Ray of Hope', 'The Gal Bladder', 'The Lost' na 'House No. 44'.

SHIWATA kuadhimisha Miaka 10 kwa sherehe la nguvu

Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher' akifafanua jambo kwenye mkutano na wanahabari hivi karibuni
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (Shiwata) wenye maskani yake Ilala jijini Dar es Salaam, unatarajia kufanya sherehe ya kutimiza miaka kumi tangu ulipoanzishwa Desemba mwaka 2004.
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtandao huo, Cassim Talib, sherehe hizo zitafanyika Desemba mwaka huu katika kijiji cha wasanii kilichopo Mwanzega wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.
Talib alisema kuwa katika sherehe hizo ambazo zitapambwa na burudani za mpira wa miguu, ngumi, ngoma za asili na nyingine nyingi kutoka kwa wasanii ambao ni wanachama wa Shiwata.
"Katika sherehe yetu hiyo ya kutimiza miaka kumi tangu tulipoanzisha mtandao huu kutakuwa na zoezi la kugawa nyumba kwa wasanii ambazo zitakuwa zimekamilika wakati huo wa Desemba," alisema Talib.
Alisema kuwa mtandao huo una wanachama 8,000 ambao baadhi yao wamekuwa wakichangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wasanii na sasa Shiwata imegawa 66 ambazo tayari zimekamilika..
Mwenyekiti huyo alisema kuwa kuna nyumba 45 ambazo zinaendelea kujengwa hadi sasa na kwamba ana uhakika kufikia Desemba zitakuwa zimekamilika na kugawiwa kwa wahusika wakati huo wa sherehe za kutimiza miaka kumi.
 "Tunatarajia kusherekea miaka kumi ya kuanishwa kwa mtandao wetu tukiwa tumepitia changamoto nyingi zikiwamo za kuzushiwa kuwa sisi ni matapeli na kila aina ya uzushi, lakini tumeshinda hizo njama za kutuhujumu na sasa tunaendelea kusonga mbele," alisema.

Baby J kutanguliza Katapila lake videoni

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/01/baby-J.jpg
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya kutoka visiwani Zanzibar, Jamila Abdullah 'Baby J' amesema ameamua kubadili mawazo ya kuachia 'audio' ya 'Katapila' na badala yake ataanza na video.
Akizungumza na MICHARAZO, Baby J alisema ameamua kutoa video kabla ya 'audio' kwa nia ya kuwapa ladha tofauti mashabiki wake.
Baby J alisema video hiyo inayoendelea kurekodiwa na kampuni ya Visual Lab (Next Level) chini ya mtaalam Adam Juma na ataiachia hewani mara baada ya kukamilika kurekodiwa.
"Badala ya kuanza kuachia 'audio' ya 'Katapila' nimeamua nitoe kwanza video ambayo inaendelea kutengenezwa na Adam Juma,' alisema Baby J.
Wimbo huo mpya unaokuja baada ya 'Nimempenda Mwenyewe' kufanya vema hewani, umetengenezwa na maprodyuza wawili tofauti, Shirko na Lil Ghetto.

Wasanii wahimiza kuhudhuria semina ya Haki Miliki

Kama wanavyopeana sapoti kwenye tuzo wasanii wanapaswa pia kuhudhuria semina mbalimbali kupata uelewa na wa mambo yanayowakwaza
Na Kipimo Abdallah
UMOJA wa Mashirikisho ya Sanaa Tanzania umewaomba wasanii nchini kujitokeza katika semina ambayo inatarajia kufanyaka Oktoba mwaka huu katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Umoja huo Godfrey Ndimbo wakati akizunumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam.
Alisema umoja wao unatoa pongezi kwa taasisi hiyo ya Haki Neel Production Company ambayo imetambua msanii wa Tanzania.
Ndimbo alisema semina hiyo itajikita katika kuwaelimisha wasanii kuhusu mafao ya uzeeni, matibabu kupitia bima ya afya, Haki Miliki, Haki Shiriki na Kodi.
“Napenda kuwaomba wasanii wa Tanzania kujitokeza kwa wingi katika semina hiyo kwani itawajengea uwezo mzuri katika kutambua haki zao nyingi ambazo zinakiukwa, ” alisema.
Ndimbo alisema katika semina hiyo wanatarajia kuwahusisha watumishi kutoka taasisi mbalimbali kama Poilisi, Uhamiaji na Mahakimu.
Katibu Mkuu huyo alisema lengo la kushirikisha sekta hizo ni kuhakikisha kuwa wanakuwa na ufahamu dhidi ya kazi hizo za wasanii nchini ili wajione kuwa wana haki ya kutetea kazi hizo.
Alisema lengo ni kuhakikisha kuwa sheria inayotumika kutoa hukumu kwa husika inakuwa na tija kwani kwa sasa ni ndogo jambo ambalo linakwamisha maendele ya tasnia hiyo.
Katibu Mkuu huyo alisema pia wanawakaribisha waandishi wa habari katika semina hiyo ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na ufahamu mzuri wa kutosha kuhusiana na tasnia hiyo.
Alitoa wito kwa wadau wengine kujitokeza kwa wingi ili kusaidia na taasisi ya Haak Neel Production Company ambayo imeonyesha jitihada za kutambua nafasi ya msanii.
mwisho