STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, October 7, 2014

Arsene Wenger apuuzia sakata lake na Mourinho


KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kamwe hajutii kumsukuma kocha wa Chelsea, Jose Mourinho katika mechi ya juzi zikiwa ni dakika 20 tu tangu mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Stamford Bridge kuanza kuchezwa.
Wawili hao walitibuana baada Gary Cahill kumchezea rafu mbaya winga mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez na Wenger kukasirishwa na uamuzi wa Mourinho wa kuonyesha kumtetea Cahill.
Hata hivyo, kama si juhudi za refa Martin Atkinson na mwamuzi wa akiba Jonathan Moss kujaribu kuwasuluhisha zingepigwa kavu kavu.
"Cha kujutia nini baada ya hilo? Nilitaka kwenda kutoka (pointi) A hadi B na mtu fulani akanitibua bila kuonyesha ishara ya mapokeo," Wenger alisema.
"B ilikuwa ni kuangalia kama Sanchez aliumia. Ilikuwa ni kusukumwa? Kidogo. Unaweza kuona kama ukweli nimejaribu kumsukuma."
Wenger anasema alimsukuma "kidogo" Mourinho.
Hata hivyo walitenganishwa na mwamuzi wa akiba Jon Moss na refa Atkinson, lakini haitarajiwi FA kuwachukulia hatua zaidi.
Mourinho alisema alitaka "kusahau" kuhusu tukio hilo na Mfaransa huyo, na akasisitiza hakufanya lolote baya.
"Inauma kwa sababu hii ni mechi kubwa, klabu kubwa, mpinzani mkubwa,na mechi muhimu kwa timu zote. Hali hii inaufanya mchezo kuwa na hisia,'' alisema.
"Nimefanya makosa mengi sana katika soka, lakini si kipindi hiki kwa sababu nilikuwa katika eneo langu la kiufundi na halikuwa kosa langu. Mchezo umekwisha. Mwisho wa stori."
Uhusiaano wa makocha hao wawili umekuwa wa maneno maneno katika mechi kwa kipindi kilichopita, kwa Mourinho kumpachika Wenger "mtaalam wa kufeli" hiyo ilikuwa Februari mwaka huu.
Mourinho pia alisema hahofii uamuzi wa kitabibu baada ya Thibaut Courtois kuhaha kutokana na kukwaruzana na mshambuliaji wa Kimataifa wa Chile Sanchez na kwamba pengo hilo likiwamo litazibwa na Petr Cech.

No comments:

Post a Comment