STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 4, 2014

Aisha Bui atupa Mshale wa Kifo mtaani

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEia3UxHjhFQAOtMelt-HNeHnCq8_8wf46ChclxFiV2yd_QvEl8doJA8VY0-uwmtjMvo2485UzpHaf1mBS6BXhx2VtKIuhIJGQ7MOGFqX5s0a2QX8Qz0bozYXluvp6KZ6mcuSwwpQhDKvLI2/s1600/20+MSHALE+WA+KIFO.jpeg
https://lh4.googleusercontent.com/-DYmmzqm_7HU/U_R5bP2TcCI/AAAAAAAAGoQ/Wy885VogXTc/1.jpeg
FILAMU mpya ya mwanadada Aisha Bui iitwayo 'Mshale wa Kifo' imeachiwa rasmi huku muigizaji huiyo akijipanga kwa ajili ya kutengeneza kazi nyingine mpya.
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha Bui alisema filamu hiyo inatoka leo na kwa sasa yeye na 'crew' yake ya Bad Girl 'Film's wapo katika matayarisho wa kuandaa kazi mpya ili kuendelea kuwapa burudani mashabiki wao.
Filamu hiyo ya Mshale wa Kifo ni ya kwanza kiwa mwanadada huyo anayetamba na filamu mbalimbali na ndani ya kazi hiyo ameigiza yeye mwenyewe, Ahmed Olotu 'Mzee Chillo', Salim Ahmed 'Gabo' na wengine.
"Ile filamu ya 'Mshale wa Kifo' imetoka leo baada ya kukwama Agosti 25, kwa sasa Bad Girl Film's tunaanza maandalizi ya kuandaa kazi nyingine mpya, tunataka kuwapa burudani mashabiki wetu mwanzo mwisho sambamba na kuleta mapinduzi ya kuondokana na filamu za 'sebuleni' na ufukweni," alisema Aisha Bui mama wa mtoto mmoja.
Kabla ya kutoa filamu hiyo mwanadada huyo, alitamba na filamu kama Saturday Morning, Better Days, Not Without My Son, Continous Love, Revenge of Love, Mirathi, Pain of Love, Crazy Love na The Second Wife.








Sikinde waachia mbili za uhamasishaji Gesi mikoa wa Kusini

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgyQvJbNPmPY9Zp7MmXibkXD186MC54L8sZ79WM1IZ_KxdV5R5Wh9ZWSAd3-nx1OZIXAfVweaIncxaslL1wDR3VQuRmdKX2u7M6swKmwLhBJ4W2tcShvII75vxkD5IjN7HNy3v0uowGg6s/s1600/sikinde.JPGBENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park 'Sikinde' imefytua nyimbo mbili mpya maalum kwa ajili ya kuwahamasisha wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kwa neema walizojaliwa.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sikinde, Hamis Mirambo nyimbo hizo ni 'Fursa Zimefunguliwa' na 'Neema Kubwa ya Gesi' ambazo tayari zimeshasambazwa ili kurushwa hewani.
Mirambo aliiambia MICHARAZO nyimbo hizo zimetungwa maalum kwa ajili ya kuwahamasisha na kuwaelimisha wakazi wa mikoa hiyo juu ya neema zilizogundulika katika mikoa yao ikiwamo Gesi.
"Ni nyimbo ambazo za kuhamasisha na kuelimisha juu ya wakazi wa mikoa hiyo ya Kusini mwa Tanzania kuitumia vyema neema na fursa  zilizopo katika mikoa yao kujiletea maendeleo," alisema.
Mirambo aliongeza kuwa bendi yao tayari imekamilisha nyimbo za albamu yao mpya na wanajipanga kwa ajili ya kuzizidua sambamba na kuzitengenezea video zake.
Albamu hiyo itakayofahamika kama 'Jinamizi la Talaka' itakuwa na nyimbo saba badala ya sita ilivyozoeleka kwa albamu za bendi za muziki wa dansi.
Pia, alidokeza kuwa kuanzia sasa siku ya Jumamosi watakuwa wakitoa burudani kwenye ukumbi wa Wipes Bar Bandari, Kurasini huku siku ya Ijumaa kama kawaida wanakamua Break Point, Posta Mpya na Jumapili uwanja wa nyumbani wa DDC Kariakoo.

Hatari! Kim Kardashian akubali kuvua nguo kupamba jarida la GQ

Kim-Kardashian-Naked-GQ

Kim-Kardashian-Naked-GQ-2
Kim-Kardashian-Naked-GQ-3

MWANADADA nyota wa Marekani, ambaye ni mke wa nyota wa muziki duniani, Kanye West, Kim Kardashian anataka uache kujiuliza maswali inakuwaje awapo bila ya nguo baada ta kukubali kupigwa picha ili kupambana Jarida ya GQ.

Kim atatokelea kwenye Jarida hilo toleo la nchini Uingereza. Tayari Kim ameshinda tuzo ya mwanamke wa mwaka kutoka GQ , akiwa ndio kwanza ana miaka 33. Dah! Hii ni Hatareeee

Rooney aibeba England afunga bao pekee dhidi ya Norway











BAO pekee la kipindi cha pili la mkwaju wa penati uliofungwa na Nahodha mpya wa England Wayne Rooney iliisaidia kuipa ushindi timu hiyo dhidi ya Norway katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa usiku wa jana.
Rooney alifunga bao hilo katika dakika ya 68 kwenye pambano lililochezwa uwanja wa Wembley na kuhudhuria na watazamaji zaidi ya 40,000.

Lahm, Klose watunukiwa Ujerumani ikilala 4-2 kwa Argentina

http://content4.promiflash.de/article-images/w500/philipp-lahm-per-mertesacker-und-miroslav-klose-werden-aus-dfb-team-verabschiedet.jpg 







04 Sep 2014 BAADA ya kazi nzuri waliyoifanyia nchi ya Ujerumani, wachezaji wakongwe Miloslav Klose, Philipp Lahm na Per Mertesacker wamepewa tuzo za heshima jana kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na Argentina Uwanja wa Esprit Arena ambao ulishuhudiwa Ujerumani ikinyukwa mabao 4-2.
Watatu hao waliichezea Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina kabla ya kuamua kustaafu soka ya kimataifa.
Klose, ambaye ni mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani kwa mabao yake 71, ametungika daluga baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.
Hata hivyo furaha yao ya kupokea tuzo hizo ziliingia shubiri baada ya kuishuhudia Ujerumani ikifa mbele ya Argentina.
Winga mpya wa Manchester United,  Angel di Maria ametengeneza mabao matatu na kufunga moja katika mchezo huo uliochezwa mjini Dusseldorf, Ujerumani.
Mchezaji huyo ghali zaidi kusajiliwa Manchester United na Uingereza nzima alipika mabao ya Sergio Aguero, Erik Lamela na Federico Fernandez kabla ya kufunga na lake mwenyewe siku 52 tangu bao la Mario Gotze katika muda wa nyongeza liipe Ujerumani ubingwa wa dunia nchini Brazil. 
Ujerumani walipata mabao yao kupitia Andre Schurrle Gotze aliyefunga la pili kwa mabingwa hao wa dunia.

Yanga yawanyoa Wakenya, Maximo we acha tu!

Simon Msuva akionyesha makali yake. Juu kikosi cha Yanga (Picha zote kwa hisani ya Bin Zubeiry
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Mbrazil Genilson Santos 'Jaja' ameendelea kuwapa raha wana Yanga baada ya kuifungia bao pekee lililowapa vijana wa Jangwani ushindi wao wa nne mfululizo ikiwa chini ya kocha Marcio Maximo katika pambano la kirafiki la kimataifa dhidi ya Thika United ya Kenya.
Mechi hiyo iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa, ilishuhudia Jaja akiifunga bao hilo katika kipindi cha pili na kuwafanya mashabiki waliokuwa wakitaka mchezaji huyo atolewe dimbani kunyamaza kimyaa.
Jaja alifunga goli hilo akimalizia kwa kuugusa kidogo tu mpira wa krosi murua ya dakika ya 58 kutoka kwa winga Simon Msuva ambaye jana alichezeshwa kama straika wa kati.
Goli hilo liliibua shangwe kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa kimya katika kipindi cha kwanza kutokana na ubovu uliooneshwa na safu yao ya ushambuliaji ikiongozwa na Mbrazil huyo katika kipindi hicho.
Yanga waliokuwa wameweka kambi ya siku 10 visiwani Zanzibar wakicheza mechi za kirafiki tatu na kushinda zote dhidi ya Chipukizi FC, Shangani FC na KMKM zote za Ligi Kuu ya Zanzibar, walianza mechi hiyo kwa mpira wa polepole uliochagizwa na pasi fupifupi za mfumo wa Kibrazil wa kocha Marcio Maximo.
Kikosi cha kwanza cha Yanga kilichoanza na wachezaji wawili wapya kutoka Brazil, Andrey Coutinho na Genilson Santos 'Jaja' kilimaliza kipindi cha kwanza kikiwa hakijafunga goli hata moja, sawa na wageni wao Thika United waliomaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Kenya wakiwa nafasi ya tano.
Katika kipindi hicho cha kwanza, kiungo wa kimataifa wa Yanga kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima 'Fabregas' alionyesha kiwango cha juu hasa katika dakika 30 za mwanzo akifuatwa na Coutinho ambaye alionekana wazi kuwa kivutio kikubwa cha Wanayanga kutokana na chenga zake za Kibrazil zilizojaa kila aina ya fedheha.
Kabla ya mechi hiyo kuanza, Maximo aliyekuwa anaingia kwa mara ya kwanza kwenye Uwanja wa Taifa akiwa kocha wa Yanga baada ya kuiongoza kwa mafanikio timu ya taifa (Taifa Stars), aliwanyanyua vitini wapenzi na mashabiki wa Yanga baada ya kuonyesha ishara ya ngumi ambayo ilitafsiriwa kama amedhamiria kurudisha magoli 5-0 ambayo Yanga ilipokea kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba misimu mitatu iliyopita.
Maximo, kocha wa zamani wa Stars, aliendelea kuwa kivutio zaidi pale alipojishika kifuani na kutoa ishara kwamba 'anaweza' kuipa mafanikio zaidi timu ya Yanga.
Mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Hashim Abdallah kutoka Dar es Salaam ambaye ana daraja la kwanza la uamuzi, ilishuhudiwa Maximo akibadilisha wachezaji kadhaa kipindi cha pili akiwatoa Jaja, Dilunga, Niyonzima, Coutinho na Msuva na kuwaingiza Hamis Thabit, Omega Seme, Said Bahanunzi na Nizar Khalfan ambao walibadilisha kwa kiasi kikubwa mechi hiyo na kuifanya iwe kivutio kwa Wanayanga.
Kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki hasa wa Yanga waliofurika upande wa Magharibi na Kusini mwa Uwanja wa Taifa huku baadhi ya mashabiki wa Simba wakikaa kwenye jukwaa lao la Kaskazini mwa uwanja huo na kuendelea upinzani wao wa jadi dhidi ya Yanga kwa kuipa sapoti timu ngeni ya Thika United.
ilikuwa ni mechi ya nne ya kirafiki ya Yanga chini ya Maximo na ya kwanza kwa kocha huyo Mbrazil kwenye Uwanja wa Taifa tangu aanze kuifundisha klabu hiyo.
Kocha Maximo alisema baada ya mechi hiyo jana kuwa timu yake inapaswa kubadilika na kutumia nafasi zinazopatikana huku pia akiisifu Thika United akisema ilicheza vizuri kuliko wao licha ya Wanajangwani kuibuka na ushindi.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema jana kuwa baada ya kushinda mechi zao zote nne za kirafiki wanaangalia uwezekano wa kucheza mechi nyingine moja ya kujipima kabla ya kuwavaa Azam FC katika pambano lao la kuwania Ngao ya Jamii la kuashiria ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya Tanzania Bara Septemba 13.
Vikosi:
Yanga: Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima/ Hussein Javu (dk 73), Hassan Dilunga/ Hamis Thabiti (dk. 46), Genilson Santos 'Jaja' (Said Bahanunzi (dk 75), Simon Msuva/ Omega Seme (dk 73) na Andrey Coutinho/ Nizar Khalfan (dk. 70).
Thika United: Hamza Muwonge, Simon Mbuguo, Sammy Meja, Tonny Kizito, Dirkir Glau, Dennis Odhiambo, Moses Odhiambo, Wyclif Opondo, Michael Olunga, David Kingatua na Joseph Kulia.

Falcao adai kutimiza ndoto, baba yake akifichua mbio za usajili wake

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj50uj4azVYQV9K1swq8oLz1YdrwmF3ZCcWreW8jp-zesvohIn_fLQqgBZCSLLyz0w0_zU4bmENmfRK_4D2v5EmRWci16t2fMdxHuG0FTNrAj5fIjiVp26G-db_N5JNK7hB3nQ3mRPdr0vu/s1600/Radamel+FALCAO%27s+father+with+his+son+in+Venezuela.png
Baba na mwana

WAKATI baba yake Radamel Garcia, akibainisha kuwa Arsenal, Liverpool, Manchester City na Juventus, zilikuwa zikipigana mkumbo kumsajili kabla ya kuhamia Manchester United, mshambuliaji nyota wa Colombia aliyekuwa As Monaco ya Ufaransa, Radamel Falcao amebainisha kuwa ametimiza ndoto zake baada ya kukamalisha usajili wa mkopo kwenda kwa Mashetani Wekundu.  Falcao aliiambia runinga ya Manchester Utd, MUTV kuwa alikuwa na ndoto za siku nyingi kukipiga katika Ligi Kuu nchini Uingereza kutokana na ushindani uliopo. 
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ametua katika klabu ambayo ni bora kabisa nchini humo na sasa kila kitu kinakwenda sawa. 
Falcao, 28 alisafiri kwenda jijini Manchester kwa ajili ya vipimo vya afya Jumatatu jioni huku United wakithibitisha dili hilo baada ya kupita saa mbili na nusu toka dirisha la usajili lifungwe. 
United wameilipa Monaco kitita cha paundi milioni sita ili kupata huduma ya Falcao kwa msimu mmoja huku wakiwa na chaguo la kumsajili moja kwa moja wakitoa kitita kingine cha euro milioni 55.
Hata hivyo baba yake mzazi amebainisha kabla ya kutua Old Trafford, Falcao alikuwa akiwindwa na klabu nne tofauti zikiwamo tatu za England ili kunasa saini yake kabla mshambuliaji huyo hajaamua kutuma Manchester United kwa mkopo akitokea Monaco. 
Mzee huyo Ramadel Garcia alinukuliwa na The Mirror kuwa alisema Real Madrid waliamua kutomfuatilia Falcao, tofauti na Juventus, Arsenal, Manchester City na Liverpool.

Odemiwngie kupasuliwa, van Persie akwepa 'kisu'


WAKATI mshambuliaji nyota wa Manchester United anayetokea Uholanzi, Robin van Persie akinusurika kupigwa 'kisu', mshambuliaji was kimataifa wa Nigeria, Peter Odemwingie amebainisha kuwa sasa anahitaji kufanyiwa upasuaji kutokana na majeraha ya goti aliyonayo. 
Odemwingie sasa anategemewa kukosa sehemu ya msimu wa Ligi Kuu kufuatia kuumia katika mchezo ambao Stoke City waliitandika Manchester City kwa bao 1-0 Jumamosi iliyopita. 
Taarifa zinadai kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi 10 au zaidi. 
Odemwingie mwenye umri wa miaka 33 alithibitisha hayo jana katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter kwa kudai kuwa atakosa mechi nyingi za ligi msimu huu. 
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa atafanya kila awezalo kuhakikisha anarejea tena uwanjani akiwa fiti zaidi na kuendelea kuisaidia timu yake ya Stoke.
Majeruhi ya Odemwingie ambaye anachukuliwa kama mchezaji muhimu katika kikosi cha Stoke yamemlazimisha meneja Mark Hughes kumsajili winga wa kimataifa wa Morocco Oussama Assaidi kwa mkopo kutoka Liverpool katika siku ya mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili majira ya kiangazi.
Hali ikiwa hivyo kwa Odemwingie, Robin van Persie ameiambia Fox Sports NL kuwa hatafanyiwa upasuaji wa goti na kwamba kwa sasa anajipanga kuwania namba dhidi ya mshambuliaji mpya Radamel Falcao ambaye alijiunga na Manchester United Jumatatu.
Wakati United ikimsajili kwa mkopo mshambuliaji huyo raia wa Colombia akitokea klabu ya Monaco, iliripotiwa kuwa Mholanzi huyo atafanyiwa upasuaji hivyo kuwa nje kwa muda mrefu.
Lakini Van Persie, ambaye amekuwa akisumbuliwa na goti mapema katika wasifu wake kisoka, alipuuzia taarifa hizo: "Ninashangaa watu hao kutengeneza hisia kama hizo.
"Sijui yanatokea wapi na ninaweza kusema ukweli kutoka moyoni sitakuwapo hospitali kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji."
Falcao aliigharimu Monaco Euro milioni 60 miezi 12 iliyopita na amefunga mabao 155 katika mechi 200 za mwisho akiwa Porto, Atletico Madrid na klabu hiyo ya Ligue 1. 

Ngumi! Said Yazidu, Mualgeria kuzipiga YMCA-Moshi

MABONDIA wa Tanzania Said Yazidu na Ally Ramadhani 'Alibaba' wanatarajiwa kupanda ulingoni wiki ijayo kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Tanzania katika mapambano mawili tofauti ya kimataifa dhidi ya mabondia kutoka nchi za Malawi na Algeria.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa PST, Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, Anthony Rutta, Yazidu atazipiga na Djamel Dahou wa Algeria katika pambano la kuwania ubingwa wa Dunia wa WBO la raundi 12 na Alibaba atapigana na Alick Mwenda wa Malawi kuwania ubingwa wa UBO Afrika litakalokuwa la raundi 10.
Michezo yote pamoja na ile ya utangulizi ipatayo 10 itachezwa siku ya Septemba 12 kwenye ukumbi wa YMCA, Moshi mkoani Kilimanjaro chini ya kampuni ya Green Hill Promotion na kusimamiwa na PST.
Rutta alisema maandalizi ya michezo hiyo imekamilika na kuwataka wakazi wa Moshi na mikoa ya jirani kujiandaa kupata burudani ikiwa ni kwa mara ya kwanza kushuhudia ngumi za kulipwa katika hadhi ya kimataifa kama hiyo.
Katibu huyo alisema mbali na michezo hiyo ya kimataifa ya kuwania mataji ya UBO, siku hiyo kutakuwa 'vita' vingine kwa mabondia wa mikoa tofauti ikiwamo wenyeji Kilimanjaro  katika michezo ya utangulizii ya kuwasindikiza akina Yazidu na Alibaba.
Rutta aliyataja mapambano hayo ni lile la wanadada Fatuma Yazidu wa Dar atakayepigana na Joyce Adam wa Dodoma, Emmanuel Alex wa Kilimanjaro dhidi ya Ali Bugingo wa Dar, Pascal Bruno wa Kilimanjaro dhidi ya Cosmas Kibuga wa Arusha, George Allen wa Kilimanjaro atayepigana na Ssebo Husseni wa Dar na Raymond Muabwango wa Kilimanjaro watakayenyooshana na Fadhil Mkinda wa Dar.
"NI burudani isiyopaswa kukoswa na mashabiki wa mchezo wa ngumi kwani mabondia wote watakaoumana ni wenye viwango na wanaoujua mchezo huo," alisema Rutta.

Azam nouma yanasa udhamini wa miaka miwili NMB

 
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Azam wameingia mkataba wa miaka miwili na Benki ya NMB  jana
Kwa mujibu wa Mweyekiti wa Azam Said Mohamed alisema mkataba huo utakuwa ikiisadia timu hiyo mambo mbalimbali ikiwemo vifaa vya michezo kama Jezi, Viatu na nauli ya kusafiria wakati wa mechi za mikoani.
“Udhamini wetu na NMB utakuwa  ukihusisha vifaa vyote vya michezo ikiwemo Jezi, Viatu na vifaa vingine na hatuwezi kusema gharama yake kwa sababu ni makubaliano yetu sisi na NMB ,” alisema Mohamed.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Mark Wiessing alisema mafanikio ya Azam FC pamoja na uongozi bora ndivyo vilivyo wavutia kuingia nao mkataba huo ambao anaamini utakuwa na manufaa kwa pande zote mbili.
Hiyo siyo mara ya kwanza kwa NMB kujiingiza katika udhamini wa michezo mara ya kwanza iliwahi kuidhamini timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,mwaka 2007 hadi 2010 na imekuwa ikitoa mchango katika kuendeleza soka la vijana nchini.