STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 24, 2015

Breaking News: Waziri Prof Muhongo atangaza kujiuzulu

http://4.bp.blogspot.com/-oG045NjRdrE/UIZDJVmV3VI/AAAAAAAABsk/2-0pkmiqLWA/s1600/Prof.+Muhongo.jpg
Prof Muhongo aliyetangaza kuachia ngazi serikali asubuhi hii
HATIMAYE Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo leo ikiwa ni karibu mwezi mmoja tangu kuwepo kwa shinikizo la kumtaka ajiuzulu nafasi hiyo kutokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.
Prof Muhongo ni miongoni mwa waliotajwa katika kashfa hiyo, lakini hakuchukuliwa hatua zozote na Rais Jakaya Kikwete wakati akilihutubia taifa, huku aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka akiondolewa kwenye nafasi yake kutokana na sakata hilo.
Maamuzi ya kuachia ngazi kwa Prof Muhongo yametolewa mbele ya wanahabari aliokutana nao asubuhi jijini Dar es Salaam.
Pamoja na kueleza mafanikio yake ndani na nje ya nchi kupitia wizara hiyo na kujitaja kama mtu msafi ambaye ana doa lolote, waziri huyo alitangaza kuachia ngazi kwa madai ya kutafakari kwa kina, ingawa kabla ya hapo alishawahi kunukuliwa kwamba asingejiuzulu ng'o.
Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kuwa hatua hiyo imekuja baada ya shinikizo kubwa kutoka kwa wakubwa wake, ikizangatiwa heshima aliyonayo kama Profesa.
Kujiuzulu kwake kumekuwa wakati Katibu wake, Eliakim Maswi kutimuliwa kazini na Katibu Mkuu Kiongozi kutokana na sakata hilo, huku watendaji kadhaa umma wakiburuzwa mahakamani wakikabiliwa na kesi zinazohusiana na sakata hilo la Tegeta Escrow.

OCODE yawaokoa wanafunzi 651 kukaa chini Chanika

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tungini, Chanika wakiyajaribu mawadati waliokabidhiwa na OCODE
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tungini, wakiyakalia madawati waliyokabidhiwa
Wakiwa haamini kama hawatakaa tena chini baada ya shule yao kupewa madawati 100
Wazazi wa Shule ya Msingi Tungini walikuwa mashuhuda wa makabidhiano hayo
Wanafunzi walishangilia na kupongeza kwa makofi
Afisa Elimu Shule za Msingi, Ilala, Elizabeth Thomas alitoa nasaha zake katika hafla ya makabidhiano ya madawati 217 kwa shule tatu za manisapaa yake toka kwa OCODE
Mratibu Mkuu wa OCODE, Jackson Joseph akisoma risala kuelezea asasi yao na misaada wanayotoa kwa jamii ya Watanzania katika nyanja ya elimu na uchumi
Akaikabidhi risala hiyo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Rogasian Seda aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo aliyekuwa awe mgeni rasmi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya OCODE, Vedasto Ngaiza naye akatoa nasaha zake kwa waalikwa
Mwenyekiti wa Bodi ya OCODE akakabidhi waraka wake kwa Mgeni Rasmi, Mchumi wa Manispaa ya Ilala aliye pia Kaimu Mkurugenzi, Rogasian Seda 
Kaimu Mkurugenzi wa Ilala, Rogasian Seda akimkabidhi cheti Mwalimu Mkuu wa Shule ya Tungini, Peter J Peter kuonyesha ishara ya kukabidhiwa msaada toka OCODE
Jamani madawati yenyewe ndiyo haya hapa kaimu Mkurugenzi wa Ilala (mwenye koti) na Afisa Elimu wakionyeshwa madawati na uongozi wa OCODE
Kaimu Mkurugenzi wa Ilala na Mwenyekiti wa Bodi ya OCODE wakishikana mkono kuonyesha ishara ya kukabidhiana madawati huku wakishuhudiwa na Mwalimu Mkuu wa Tungini, Peter J Peter (shati jeupe), Afisa Elimu (wa pili kushoto) na Mratibu wa OCODE, Jackson Joseph.
Wanafunzi wakayachangamkia kuyakalia kama ishara ya kuyapokea shuleni kwao
Mchumi wa Manispaa ya Ilala na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Rogasian Seda akitoa nasaha zake
Wanafunzi wakifuatilia kila tukio lililokuwa likiendelea katika hafla hiyo iliyofanyika Shule ya Msingi Tungini, Chanika jijini Dar es Salaam
Weweee hatukai tena chini ahsanteni OCODE, ahsanteni wazazi
Na Rahim Junior
WANAFUNZI zaidi ya 651 wa Shule za Msingi tatu za Tungini, Nzasa II na Msongola zilizopo Chanika, wilayani Ilala jiji la Dar es Salaam wameokolewa kukaa chini baada ya Asasi ya Maendeleo ya Jamii iitwayo Organization for Community Devlopment (OCODE) kuzikabidhi shule hizo msaada ya madawati 217 yenye thamani ya Sh. Milioni 21.
Aidha asasi hiyo imezisaidia kukarabati na kujenga majengo matatu ya madarasa yenye thamani ya Sh. Milioni 22 kwa Shule za Msingi Viwege na Msongola ambayo waliyakabidhi katika hafla zilizofanyika juzi na kushuhudiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, ambaye pia ni Mchumi wa Manispaa hiyo, Rogasian Seda aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa aliyekuwa awe mgeni rasmi wa hafla hiyo.
Msaada huo wa madawati na madarasa hayo ulikabidhiwa kwa wakuu wa Shule hizo juzi na kuhudhuria pia na Afisa Elimu wa Shule ya Msingi wilaya ya Ilala, Elizabeth Thomas ambaye aliushukuru uongozi wa OCODE kwa msaada huo na kutoa wito kwa asasi nyingine na wananchi kuendelea kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya elimu nchini na kuwafanya watoto wafurahie kwenda shuleni kwa sababu ya mazingira mazuri.
Kabla ya makabidhiano hayo, Mratibu wa OCODE, Jackson Joseph alifafanua mgawanyo wa madawati hayo kwa kueleza kuwa, Shule ya Msingi Tungini yenyewe imepata madawati 100,  wakati Nzasa II ilipewa madaewati 72 na Msongola ilipewa madawati 45, ambayo kwa jumla yake itawafanya wanafunzi 651 kwa maana ya kila dawati moja wanakaa wanafunzi watatu kuokolewa kukaa chini kutokana na msaada huo.
"Kwa hapa Tungini tunakabidhi madawati 100, lakini tayari tumeshapeleka madawati 72 katika shule ya Nzasa II na 45 Msongola ambapo kwa idadi hiyo ya madawati 217 tutakuwa tumewaokoa wanafunzi 651 kuketi chini kama ilivyokuwa mwanzoni kwa kuwafanya sasa wakae katika madawati na kusoma kwa utulivu," alisema Jackson.
Aliongeza kuwa asasi yao ambayo iliasisiwa mwaka 1992 na kusajiliwa serikali mwaka 2003 ilikabidhi pia madarasa mawili kwa Shule ya Viwege, moja wakilikarabati na jingine likiwa kipya wakishirikiana na wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo na jingine moja wamelikarabati katika Shule ya Msongola ambayo nao pia walikabidhiwa tayari kuwafanya wanafunzi wasome katika mazingira mazuri.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Rogasian Seda, licha ya kuishuruku na kuipongeza asasi ya OCODE pamoja na wazazi walioshiriki kuchangia michango mbalimbali ya shule zao, alisema bado manispaa hiyo ni tatizo sugu la madawati kwa shule zake.
Seda, alisema Ilala ina upungufu ya jumla ya madawati 12,000 na kwa bajeti ya mwaka huu wametenga kiasi cha madawati 2,100 tu hivyo kuwahimiza wazazi kuendelea kushirikiana na serikali na asasi za kijamii kama OCODE ili kupunguza tatizo hilo, huku akiwakumbusha wazazi na Kamati ya Shule za Ilala kulinda na kutunza vema misaada wanayopewa ili kuwaokoa watoto kukaa kwenye vumbi.
"Ni wajibu weenu kutunza misaada mnayopewa, wanafunzi tunzeni madawati yenu ili muendelee kuyakalia, msikubali yaharibike kwani mtataabika, kwa hakika Manispaa imefarijika kwa hili lililofanywa na OCOPDE na kuhimiza wengine kujitokeza," alisema Seda.
Kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Afisa Elimu wa Shule ya Msingi Manispaa ya Ilala, Elizabeth Thomas, alisema wamefurahishwa na juhudi ambazo zimekuwa zikifanyw ana OCODE na kuahidi kuwa nao bega kwa bega ili kuleta maendeleo ya elimu sawia na yale ya kiuchumi kwa wananchi wa manispaa hiyo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi wa OCODE, Vedasto Ngaiza aliweka bayana kuwa asasi yao haitaondoka Ilala mpaka ihakikishe tatizo la madawati katika shule za Ilala linaisha kama walivyoweza kufanya Temeke kwa kuzisaidia Shule 24 ambayo waliweka kambi kwa zaidi ya miaka 10.
Ngaiza alisema kitu cha muhimu wazazi na kamati za shule kuhakikisha hawageuzi madawati wanaoyopewa kuwa kuni baada ya kuharibika bali wayatunze na kuyakarabati ili yaweze kuwasaidia watoto.
Pia alisema mikakati ya OCODE ambayo tangu Januari mwaka jana imeanza kutekeleza programu mbili za miaka mitano katika manispaa ya Ilala moja ikiwa ni kusaidia kwenye masuala ya Elimu na nyingine kuwainua wananchi kiuchumi kupitia miradi mbalimbali, lakini pia wanafikiria kusaidia kuzijengea shule za manispaa hizo uzio kwa ajili ya kuwafanya wanafunzi wasome sehemu salama wao na vifaa vyao kama madawati.
"Kwa hali kama hii tunayoiona shule ikiwa haina uzio, ni rahisi misaada kama hii kuibwa na madarasa kuanza kutumiwa kwa mikutano ya nguvu za giza, hivyo OCODE tunafikiria pia kusaidia kujengwa kwa uzio ili wanafunzi na mali za shule ziwe salama," alisema Ngaiza na kuamsha vigelegele toka kwa walimu wa shule hiyo na wazazi waliohudhuria sherehe hizo za makabidhiano Tungini.

Yanga vitani na Polisi Moro, Simba, Azam hapatoshi Taifa

Yanga kuendeleza sare au kuvunja mwiko Jamhuri
Polisi Moro kuvuna nini kwa Yanga leo?
Simba wataendeleza ubabe wao mbele ya Azam
Azam watakaojiuliza kwa Simba kesho Taifa

Mtibwa Sugar watakuwa wageni wa Ruvu Shooting
Ndanda Fc watakaokuwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar
BAADA ya kulazimishwa sare mbili mfululizo kiasi cha kuanza kupagawa, Yanga leo watakuwa uwanja wa ugenini Jamhuri, Morogoro kupambana na Polisi Moro katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga imekuwa na bahati mbaya na uwanja wa Jamhuri, hivyo pambano lao la leo watahitajika kupigana kiume ili kupata ushindi na pia kujiweka katika nafasi nzuri ya kuufukuzia ubingwa unaoshikiliwa na Azam ambao wapo kileleni mwa msimamo na watakaokuwa na kibarua kizito kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar kuvaana na Simba.
Yanga waliopo nafasi ya nne kwenye msimamo wakilingana pointi sawa na Polisi Moro, hawajaonja ushindi wowote tangu ligi itoke mapumziko.
Timu hiyo inayonolewa na kocha Hans van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa waliorejeshwa baada ya aliyekuwa kocha wao, Marcio Maximo kutimuliwa baada ya ligi kusimama Novemba 9, ilianza mechi zake kwa kupata sare ya 2-2 na Azam kabla ya kuambulia 0-0 katika mechi iliyojaa ubabe.
Kocha Pluijm atakuwa na kazi kubwa ya kuwazuia vijana wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Tanzania aliyetamba na timu za Yanga na Pan Africans, Mohammed Rishard 'Adolph' kutokana na ukweli Polisi waliorejea ligi kuu msimu huu wapo vema.
Yanga itashuka dimbani bila huduma za baadhi ya nyota wake ambao ni majeruhi akiwamo beki kiraka Mbuyi Twite.
Kivumbi cha ligi hiyo kitaendelea pia leo kwenye uwanja wa Mabatini kwa mchezo kati ya Ruvu Shooting dhidi ya Mtibwa Sugar, kabla ya kesho kushuhudiwa michezo kadhaa likiwamo la Azam na Simba ambazo zitaumna kwenye uwanja wa Taifa.
Simba walioshinda mechi zao mbili mfululizo wakitokea kunyakua Kombe la Mapinduzi, wameapa kuwatoa nishai Azam ambao wametoka kupata ushindi katika mechi mbili za ugenini dhidi ya Stand United na Kagera Sugar.
mechi nyingine za kesho zitakutanisha mahasimu wa jadi wa jijini Mbeya, Prisons dhidi ya Mbeya City mechi itakayochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Pia Kagera Sugar watakuwa nyumbani uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kuumana na Ndanda ya Mtwara, huku Stand itaialika Coastal Union uwanja wa Kambarage Shinyanga na Mgambo JKT itakuwa wageni wa JKT Ruvu pambano litakalochezwa uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Mpaka sasa msimamo unaaoonyesha Azam wanaongoza msimamo wakiwa na pointi 20 kutokana na mechi 10 wakifuatiwa na Mtibwa Sugar wenye pointi 17 kisha JKT Ruvu wenye pointi sawa na Mtibwa na kufautiwa na Yanga yenye pointi 15 sawa na Polisi Moro wanaowafuata nyuma yao.
Msimamo kamili wa Ligi hiyo mpaka sasa ni kama ifuatavyo;

1
Azam 106 2 2 147 20
2
Mtibwa Sugar 9 4 5 0 127 17
3
JKT Ruvu 11 5 2 4 111 17
4
Young Africans 9 4 3 2 114 15
5
Polisi Morogoro 11 3 6 2 91 15
6
Kagera Sugar 11 3 5 3 80 14
7
Coastal Union 10 3 4 3 91 13
8
Mgambo JKT 10 4 1 5 5-4 13
9
Simba 9 2 6 1 92 12
10
Ruvu Shooting 11 3 3 5 5-3 12
11
Mbeya City 9 3 2 4 4-2 11
12
Stand United 11 2 5 4 7-6 11
13
Ndanda 11 3 1 7 10-6 10
14
Prisons 10 1 5 4 6-2 8

Ronaldo ana miaka 10 kuichezea Real Madrid

http://senego.com/wp-content/uploads/2014/10/Ronaldo-et-Jorge-Mendes.jpg
Ronaldo na Mendes
http://estaticos.marca.com/imagenes/2013/10/29/en/football/real_madrid/1383080283_extras_mosaico_noticia_1_g_0.jpgWAKALA wa mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amedai kuwa mteja wake huo bado ana miaka 10 zaidi ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno mapema mwezi huu alinyakuwa tuzo yake ya tatu ya Ballon d’Or ikiwa ni ya pili toka atue Santiago Bernabeu lakini hivi karibuni amekaririwa akidai kuwa anafikiria kuhamia nchini Brazil kabla ya kutundika daruga zake.
Hata hivyo wakala huyo Jorge Mendes ana uhakika Ronaldo atamalizia soka lake akiwa Madrid huku akidai kuwa nyota huyo bado ana miaka 10 zaidi ya kucheza soka katika kiwango cha juu.
Mendes amesema ana uhakika Ronaldo atastaafu akiwa Madrid na umri wa miaka 38 au 39 kwasababu bado ana miaka mingi ya kucheza soka.
Mendes aliendelea kudai kuwa kikubwa kinachomfanya kuamini kwamba anaweza kufikia huko ni kutokana na jinsi anavyojiweka fiti mpaka kuwa mfano kwa wachezaji wenzake

Algeria yagongwa, Afrika Kusini huzuni, Mali, Ivory Coast kivumbi leo

Senegal's defender Kara Mbodji (right) celebrates after scoring the equaliser against South Africa
Kara Mbodji akishangilia bao la kusawazisha la Senegal dhidi ya Afrika Kusini
Gyan celebrates, while team-mate - Crystal Palace youngster Kwesi Appiah - is seen behind
Asamoah akishangilia bao pekee la Ghana dhidi ya Algeria
Tempers flared between Ghana and Algeria during the Africa Cup of Nations Group C match in Mongomo
Ubabe mtupu kati ya Algeria na Ghana
WAKATI timu ya Afrika Kusini ikijiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele kwenye kundi C la michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Ghana wenyewe wamezinduka na kuidunga 'vijogoo' wa Afrika, Algeria kwa kuichapa bao moja katika mechi za raundi ya pili ya kundi hilo.
Bafana Bafana walishindwa kulinda bao lao dhidi ya Senegal katika mechi iliyochezwa usiku wa jana na kuambulia pointi moja ikiwaacha wakiwa mkiani mwa msimamo wa kundi hilo la 'kifo'.
Afrika Kusini walioanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao 3-1 na Algeria, walitangulia kupata bao dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia kwa Oupa Manyisa kabla ya Senegal walioilaza Ghana kwenye mchezo wao wa kwanza kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Kara Mbodji.
Sare hiyo imeiweka Senegal kileleni mwa kundi hilo wakiwa na pointi nne wakifuatiwa na Algeria ambayo ilicharazwa bao 1-0 na Ghana iliyopo nafasi ya tatu kwa bao la dakika za jioni lililowekwa kimiani na nahodha wa Black Stars, Asamoah Gyan.
Kivumbi cha michuano hiyo kuhitimisha raundi ya pili kitaendelea leo kwa michezo ya kundi D ambapo Mali watavaana na Ivory Coast kabla ya Cameroon kujiuliza kwa Guinea. Timu zote nne katika mechi zao za awali waliambulia sare ya 1-1 na hivyo kulingana kwa kila kitu katika kundi hilo.

Nahodha wa Gabon akiri kuchemsha kwa Congo

http://www.africatopsports.com/wp-content/uploads/2014/12/aubagabon.jpg
Pierre Emerick Aubameyang
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang amekiri kuwa chini ya kiwango katika mchezo waliofugwa dhidi ya Congo Brazzaville ambao timu yake ililazwa bao 1-0.
Baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Burkina Faso katika mchezo wao wa ufunguzi Jumamosi iliyopita, Gabon walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo lakini mambo yalibadilika baada ya Congo kuwafunga bao 1-0.
Aubemeyang ambaye alikuwa nyota katika mchezo wao wa kwanza amekiri kuwa hakuwa katika kiwango chake katika mchezo dhidi ya Congo.
Nyota huyo anayekipiga katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani amesema walishindwa kutengeza na kutumia mchezo wao hali ambayo iliwafanya kuiga mchezo wa wapinzani jambo lililokuwa baya kwao. Hata hivyo, Aubameyang anaamini wanaweza kuamka katika mchezo wa mwisho na kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
Timu hiyo itashuka dimbani kesho dhidi ya wenyeji Guinea ya Ikweta katika pambano la kuamua timu zipi za kutinga robo fainali za zipi za kurudi makwao.
Katika kundi hilo Congo wanaongoza msimamo wakiwa na pointi nne wakifuatiwa na Gabon, kisha Guinea ya Ikweta yenye pointi 2 na inayoburuza mkia ni Burkina Faso yenye pointi moja.

Prof Muhongo kujiuzulu uwaziri?

http://api.ning.com/files/17StHKe5zK7HSUrKU-HhrOv-dPDLCOp2bhaxh8P5xjEfQfYciwmCCausbIfHnM2VPo24wYqptCTGEAzK0unqbx4qNxHqFmZe/profmuhongo.JPG
Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo
HABARI zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo ambaye amekuwa akisakamwa kutokana na sakata za uchotwaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow anazungumza na wanahabari asubuhi hii.
Taarifa hizo hazijaweka bayana Prof Muhongo atazungumza kitu gani, lakini inadhaniwa huenda akatangaza kuachia ngazi katika nafasi hiyo kutokana na shinikizo kubwa lililopo ndani na nje ya serikali na chama chake cha CCM.
Hata hivyo kwa namna Waziri huyo alivyo ng'ang'ari inadaiwa huenda akatoa ufafanuzi juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake na kutakiwa kujiuzulu, japo Rais Jakaya Kikwete katika hutoba yake alisema amemweka kipioro Waziri huyo aliyetajwa kama 'Dalali' katika sakata zima la Escrow kwa mujibu wa ripoti ya PEC inayoongozwa na Mwenyeki wake, Zitto Kabwe.
MKICHARAZO itawaletea taarifa kamili juu ya mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam.

Wenger afichua sababu za kutomsajili di Maria

http://i2.mirror.co.uk/incoming/article4465324.ece/alternates/s2197/Angel-di-Maria-of-Manchester-United.jpg
MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ametaka kanuni za kutoa kibali cha kufanya kazi kwa ajili ya wachezaji ambao hawamo kwenye Umoja wa Ulaya zifutwe.
Wenger anajaribu kumsajili Gabriel Paulista kutoka Villarreal ambaye atahitaji kibali cha uidhinisho toka nchini kwake sababu hajawahi kulitumikia taifa lake.
Kocha huyo amekosoa mpango wa mapendekezo ya kupunguza idadi ya wachezaji toka mashirikisho yasiyo ya Umoja wa Ulaya katika Ligi Kuu Uingereza msimu ujao.
Kwa sasa kibali cha kufanyia kazi kwa nchi zisizo Umoja wa Ulaya kinahitaji mchezaji awe anatoka katika nchi zilizo ndani ya nafasi 70 za viwango vya FIFA na awe amecheza kwa asilimia 75 katika timu ya taifa ndani ya miaka miwili.
Chama cha Soka cha Uingereza kinataka kupunguza idadi ya wachezaji wasiokua wenyeji wa Umoja wa Ulaya kufikia asilimia 50 kwenye ligi.
Lakini Wenger anadhani kuondoa kanuni itakuwa bora zaidi kwa ajili ya wachezaji chipukizi wa nchi hiyo. Wenger amesema alitaka kumsajili winga wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria wakati akiwa na umri wa miaka 17 lakini kibali cha kazi kikaleta shida.

Serikali yalaani ubaguzi aliofanyiwa Tambwe mechi ya Ruvu

Amissi Tambwe (wa Tano toka Kulia) akichuana kwenye mechi yao na Ruvu Shooting ambapo alilalamika kubaguliwa na kukabwa na George Assey (wa kwanza kulia) katika pambano lililoisha kwa sare ya 0-0
WIZARA ya Habari Utamaduni na Michezo imeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutoa adhabu kwa timu ya Ruvu Shooting kutokana na kitendo cha ubaguzi kilichofanywa na wachezaji wa timu hiyo dhidi ya mshambuliaji wa Yanga kutoka nchini Rwanda, Amissi Tambwe.
Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii, Naibu Waziri wa Habari, Juma Nkamia amesema kuwa TFF isikae kimya kutokana na matamshi ya udhalilishaji juu ya Tambwe na kuiagiza TFF kuchukua hatua za kinidhamu haraka iwapo itathidibitika mshambuliaji huyo alitolewa maneno hayo ya udhalilishaji ili iwe fundisho kwa wengine.
"Hakuna nchi yoyote duniani inayopenda vitendo vya ubaguzi, kitendo ambacho upendi kufanyiwa usimfanyie mwenzie, nimesikia malalamiko ya Tambwe kama ni kweli Ruvu Shooting wamemuita mkimbiza wajue sio kitu kizuri tena wale ni jeshi, nadhani wanajua madhara ya vita.
"Wenzetu Burundi hawakupenda kuingia vitani, hakuna nchi yoyote inayopenda kuwa vitani, vita ni mbaya hata hapa inaweza kutokea, ni jambo la kumshukuru Mungu mpaka leo mna amani, uwezi kujua mtu unayemwambia ameumia kiasi gani na hiyo vita ni ndugu wangapi au marafiki wangapi amewapoteza sio kitu kizuri, naiagiza TFF ishugulikie suala hili kwa kuchukua hatua za haraka."alisisitiza Nkamia.
Kauli ya Nkamia imekuja siku moja baada ya Tambwe kulalamikia kitendo cha kuitwa mkimbizi na wachezaji wa Ruvu Shooting wakiongozwa na George Michael ikiwa ni pamoja na kumkaba nusura wamtoe roho.
"Maneno makali waliyonitamkia yananiuma sana roho hadi sasa, wameniita mkimbizi, eti nimekimbia vita nyumbani Burundi, vita hata hapa inaweza kutokea, hakuna anayependa mabaya kama hayo yatokee, kumwambia mtu haujui kapoteza ndugu wangapi, si sahihi kabisa, cha kushangaza wale ni wanajeshi lakini hawaonyeshi kuwa wanajua athari za vita." kauli iliyotolewa na Tambwe jana.
Hata hivyo Chama cha Waamuzi nchini (FRAT), kimetangaza kumfungia mwamuzi wa kati wa mchezo huo Mohamed Theofil, huku ikiwaweka kwenye uchunguzi waamuzi wasaidizi Michael Mkongwa na Yusuf Sekile.
Mwenyekiti wa FRAT, Salum Chama aliiambia Globu ya Jamii kuwa wamefikia uamuzi wa kumsimamisha Theofil baada ya ripoti ya Kamisaa kuonyesha kuna mapungufu yaliyofanywa na mwamuzi huyo ambaye katika mchezo huo uliomalizika kwa suluhu, alishindwa kumudu mchezo kutokana na rafu za mara kwa mara kitendo kilicholazimu mpira kusimama kila dakika.
"Ripoti ya kamisaa imeonyesha kuna udhaifu mkubwa uliofanywa na mwamuzi, kamati yangu imemfungia kupisha uchunguzi, na bado tunaendelea na uchunguzi pia kwa waamuzi wasaidizi, kikao cha kamati yangu kitakaa Februari 6 kuwajadili na kuangalia adhabu stahiki itakayofaa.
"Kitendo kinacholalamikiwa sana ni kile cha Tambwe, na ni kweli kila mtu ameona, hata kama ripoti ya kamisaa isingesema tungechukua hatua kwa sababu wapo viongozi wa TFF walioona, tunachunguza ripoti ya mechi asesa, kamisaa,"alisema Chama.
Hata hivyo, Chama alisema kuwa hawafanyi kazi kwa shinikizo la Yanga ambao waliwapa mpaka Jumamosi wawe wameshatoa adhabu kwa waamuzi wa mchezo wao na Ruvu Shooting la sivyo watagomea Ligi.
Kwa hisani ya Michuzi blog

Real Madrid yamnasa Lucas Silva toka Cruzeiro

http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2014/0923/soc_g_silva_1296x1296.jpg&w=1500&h=1500&scale=crop&site=espnfcKLABU ya Real Madrid imefanikiwa kumnaza beki wa kati wa timu ya Cruzeiro ya Brazil, Lucas Silva.
Awali klabu ya Cruzeiro iliweka bayana kuwa mchezaji huyo mchezaji wao huyo alikuwa akikaribia kutua Real Madrid.
Makamu wa Rais wa klabu hiyo, Marcio Rodriguez amedai kuwa uhamisho wa Lucas Silva kwenda Real Madrid umeshafikia hatua nzuri ya makubaliano.
Kwa kipindi kirefu Madrid iliyo chini Carlo Ancelotti imekuwa ikimfukuzia kiungo huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 21.
Rodriguez amesema uhamisho wa Silva tayari umekamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni Madrid wenyewe kutangaza rasmi.
Rodriguez aliendelea kudai kuwa hawata pata tabu kutafuta mbadala wake kwani kuna wachezaji wengi ambao wako tayari kupandishwa.
Hata hivyo imefahamika kuwa Madrid imeafiki kunyakua mchezaji huyo na kwa sasa ni mali tayari kuanza kupiga mzigo Santiago Bernabeu.