STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 16, 2014

DUA ZOTE KWA AZAM LEO MSUMBIJI

Azam wakijifua uwanja wa Ferroviario de Beira utakaotumiwa kwa mechi yao na wenyeji wao leo
KLABU ya Azam inatarajiwa kushuka dimbani leo mjini Beira kurudiana na wenyeji wao Ferroviario de Beira katika pambano la raundi ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Wawakilishi hao wanahitaji dua za kila Mtanzania ili kuweza kuvuka hatua hiyo mbele ya wenyeji wao hao ambao siyo wa kubezwa kwa jinsi walivyoonyesha kandanda lao wiki iliyopita walipolala 1-0.
Azam inahitaji sare ya aina yoyote ili kusonga mbele, lakini siyo kazi rahisi licha ya kwamba kikosi kamili cha timu hiyo kipo tayari kwa vita ugenini.
Watanzania wangependa kuona Azam ikifuzu kama ilivyokuwa jana kwa Yanga katika Ligi ya Mabingwa kwa sababu tayari Chuoni ya Zanzibar imeshaaga Kombe la Shirikisho na leo KMKM haina hakika ya kuing'oa Dedebit ya Ethiopia kwenye Ligi ya Mabingwa.
Azam inayonolewa na kocha Joseph Omog ipo katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo, lakini dua za heri za watanzania ni muhimu kuwaongezea nguvu na kuinyoa Ferroviario de Beira waliotamba kulipa kisasi nyumbani na kuindosha wawakilishi wetu.