STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 11, 2014

Maafande wa Polisi Moro yarejea tena Ligi Kuu


TIMU ya soka ya Polisi Moro imekuwa timu ya kwanza kurejea Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufanya vyema kweli Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) kundi B, huku ikiwa imesaliwa na mechi mbili mkononi kuhitimisha mechi zake.
Polisi walioshuka daraja msimu uliopita sambamba na timu za Toto Africans na African Lyon ambazo nazo zinapigana kurejea zikiwa katika makundi mawili tofauti.


Shaaban Dede bado amlilia Meddy Kitendawili

http://1.bp.blogspot.com/-cjdjW0iyNN0/TxQtbAxX1CI/AAAAAAAAUvc/JCJOdofxANw/s1600/Shaaban+Dede%252C+Msondo.JPG
Add caption

MTUNZI na muimbaji mahiri nchini, Shaaban Dede, amesema anaendelea kumkumbuka na kumlilia aliyekuwa 'swahiba' wake mkubwa, marehemu Mohammed Mpakanjia 'Meddy Kitendawili' aliyefariki karibu miaka mitano iliyopita.
Dede akizungumza na MICHARAZO, alisema licha ya ukaribu aliokuwa nao na marehemu Mpakanjia, lakini kukwama kwake kufanikisha mipango ya kufyatua albamu binafsi ya nyimbo zake za zamani humfanya amkumbuke zaidi.
Mwanamuziki huyo anayeiimbia Msondo Ngoma na aliyewahi kufanya kazi na bendi kama Mlimani Park, OSS na Bima Lee, alisema albamu hiyo ambayo ingekuwa na nyimbo sita na zingetolewa kwa mfuatano wa Vol, ilikuwa ifadhiliwe na Mpakanjia mipango iliyokuwa imeanza kabla ya swahiba wake huyo kukumbwa na mauti.
"Japo imepita miaka mitano takriban mitano sasa, bado  namkumbuka na kumlilia Meddy Kitendawili kwa mengio aliyonitendea na kuutendea muziki wa Tanzania. Ukiacha uswahiba wetu, pia kila nionapo nimeshindwa kufanikisha mipango ya kutoa albamu binafsi ya nyimbo zangu za zamani zilizotunga na kuimba katika bendi nilizopitia miaka ya nyuma naumia zaidi,"  alisema.
Dede alisema, hata hivyo anaendelea kupigana ili kufanikisha jambo hilo, hasa akisaka mfadhili mwingine wa kumpiga tafu.
Meddy Mpakanjia, aliyekuwa mume wa Mtangazaji na Mbunge maarufu wa Vijana, Amina Chipupa, alifariki Sept 14, 2009 miezi kadhaa tangu mkewe huyo kufariki wakati akiwa kwenye harakati za mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya.

Arsenal kusuka au kunyoa kwa Bavarian

Arsenal watashangilia leo Ujeruman kama hivi kwa Bavarians
 ARSENAL yenye morali baada ya kufanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Kombe la FA, usiku huu itakuwa ugenini nchini Ujerumani kujaribu kupenya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Bayern Munich.
Wakali hao wa London Kaskazini walitoka kuifumua Everton kwa mabao 4-1 katika mchezo wa Robo Fainali na leo itataka kuthibitisha kuwa msimu huu imepania angalau kuambuli mojawapo ya mataji ya ubingwa baada ya misimu karibu nane ikitoka patupu.
Ikiwa nyumba kwa mabao 2-0 ilipofumuliwa nyumbani na Bavarian, Arsenal itajarubuy kupambana na kuzika mzimu wa kutolewa kwenye 16 Bora kwa misimu karibu minne.
Msimu ulipita ni Bayern Munich iliyowakwamisha baada ya kuwatungua nyumbani kwao 3-1 kisha kupata ushindi Ujerumani kwa mabao 2-0 hata hivyo ikatoka kwa faida ya mabao ya ugenini, kitendo kilichomuudhi koca Arsene Wenger kiasi cha kulitaka Shirikisho la Ulaya, UEFA kuangalia upta sheria hiyo.
Arsenal imepewa nafasi kubwa ya kuitoa nishai Bayern kama ilivyofanya msimu uliopita, ila kazi ipo kwao kutokana na ubora na kiwango cha juu ilichonacho Bavarian kwa sasa, ikicheza mechi 16 na kufunga jumla ya mabao 26.
Wikiendi hii wakati Arsenal ikiigaragaza Everton, wenyewe waliichachafya  VfL Wolfsburg kwa mabao 6-1 ingawa kocha wake, Pep Guardiola amenukuliwa akiwahofia wapinzani wao na hasa kama wachezaji waop wataamua kuwaacha wamiliki mpira.
Kurejea katika kiwango kwa Mesut Ozil na majeruhi kadhaa katika kikosi cha Gunners kunawapa matumaioni makubwa mashabiki wa Arsenal kwamba leo watavunja mwiko wa kuishia 16t Bora kwa misimu minne mfululizo kwa kuing'oa Bayern Munich na kuivua taji la michuano hiyo.
Hata hivyuo Bayern wapo vyema na hasa baada ya kurejea kwa nyota wao, Frank Ribery aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu kumeiongezea chachu ya kuhakikisha wanatinga robo fainali na kuendeela kujipa matumaini ya kutetea taji hilo.
Mbali na mechi hiyo pia leo kuna mechi nyingine ambayo inaikutanishaAtletico Madrid itakayokuwa nyumbani kurejea na AC Milan ambayo walikubali kipigo nyumbani kwao katika mechi iliyopita ya kwanza.
Michezo mingine inatarajiwa kuchezwa kesho kwa pambano la kukata na mundu kati ya Barcelona itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Manchester City waliotota katika mechi ya kwanza kwa mabao 2-0 na pia wikiendi hii kujikuta wakitupwa nje kwenye michuano ya FA baada ya kuzabuliwa na watetezi wa taji hilo, Wigan Athletic kwa mabao 2-1.
Pia kesho PSG iliyopata ushindi mnono wa mabao 4-0 ugenini itaialika Bayer Leverkusen mjini Paris ili kuhitimisha nafasi yake ya kutinga robo fainali.

Msondo Ngoma wamaliza Suluhu

Baadhi ya watunzi na waimbaji wa albamu mpya ya Msondo Ngoma, Eddo Sanga na Juma Katundu
BENDI kongwe ya Msondo Ngoma hatimaye imekamilisha kurekodi nyimbo zake za albamu yao mpya iitwayo 'Suluhu' na ipo katika hatua ya mwisho kwa ajili ya kuziachia hewani kutuliza 'mzuka' wa mashabiki wake.
Akizungumza na MICHARAZO, mmoja wa viongozi na mwanamuziki wa bendi hiyo, Shaaban Dede 'Super Motisha' alisema Msondo imekamilisha kurekodi nyimbo hizo kwa mtayarishaji Malone Linje baada ya kipindi kirefu cha danadana juu ya suala hilo.
Dede ambaye ndiye mtunzi wa wimbo uliobeba jina la albamu hiyo, alisema nyimbo hizo zinahaririwa kwa sasa kabla ya kuanza kurushwa hewani na viongozi kujipanga kwa ajili ya uzinduzi wake.
'Tunashukuru kwa sasa tumeshamaliza kurekodi albamu yetu mpya, mashabiki waliokuwa na kiu ya muda mrefu sasa kiu hiyo imeisha kwani mambo yamekamilika nawakati wowote zitaachiwa hewani baada ya kuhaririwa," alisema.
Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni pamoja na 'Suluhu' alioutunga Dede, ' Lipi Jema' na 'Baba Kibene' za Eddo Sanga, 'Nadhiri ya Mapenzi' wa Juma Katundu, 'Kwa Mjomba Hakuna Urithi-Huruka Uvuruge na 'Machimbo' uliotungwa na bendi nzima.
Mara ya mwisho Msondo kutoa albamu ilikuwa miaka minne iliyopita walipoachia 'Huna Shukrani' ilikuja baada ya bendi hiyo kuzindua albamu yao ya 'Kicheko kwa Jirani' mwaka 2010.

Waamuzi wa soka kunolewa Dar

http://www.eatv.tv/media/picture/large/waamuzi(4).jpg
Baadhi ya waamuzi wakiwa uwanjani
WAAMUZI na waamuzi wasaidizi 22 wameteuliwa kushiriki semina na mtihani wa utimamu wa mwili kwa robo ya kwanza ya mwaka huu itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 14 hadi 16.

Semina hiyo inashirikisha waamuzi wote wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu (elite) kutoka Tanzania Bara za Zanzibar.

Waamuzi hao ni Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama (Iringa), Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya) na Jonesia Rukyaa (Bukoba).

Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza Kinduli (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).

Wakufunzi wa semina hiyo ambao wanatambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Joan Minja na Riziki Majala.

Mawakala wa wachezaji kutahiniwa April 3

MTIHANI kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Aprili 3 mwaka huu saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA). Kwa wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni maswali kutoka FIFA wakati nyingine ni kutoka TFF.
Tanzania ina mawakala watatu tu wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally Saleh, John Ndumbaro na Mehdi Remtulla.

Babi apewa unahodha Malaysia

Photo: Thamani.yangu na uwezo .wangu na nithamu yangu ndio inayonifanya .nipewe ukepten..ndani ya nchi na nje ya .nchi..nawatakia kila la heri YANGA..
Babi (kushoto-mbele) akiwa na kitambaa cha unahodha
KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nchini Malaysia, Abdi Kassim 'Babi' ameteuliwa kuwa nahodha wa timu ya UiTM inayoshiriki Ligi Kuu ya nchi hiyo.

Babi alipewa unahodha huo wiki iliyopita alipoingoza timu hiyo katika mchezo dhidi ya 'vibonde' wa ligi hiyo Perlis na kupoteza mchezo huo wa ugenini kwa kulala mabao 2-1.

Kiungo huyo wa zamani wa Taifa Stars, aliiambia MICHARAZO kuwa nidhamu na kiwango bora cha soka alichokionyesha tangu atue katika timu hiyo ndicho kilichofanya apewe cheo hicho na kusema anamshukuru Mungu.

"Ninajisikia fahari kupewa cheo hicho baada ya viongozi na wachezaji kuridhika na uwezo wangu uwanjani na nidhamu kubwa niliyonayo ni furaha kwangu hasa ikizingatiwa nipo ughaibuni," alisema Babi.

Kuhusu mechi yao ya Ijumaa, Babi alisema walifungwa kimchezo katika pambano hilo la ugenini lililochezwa kwenye uwanja wa Darul Aman mjini Alor Setar, likiwa pambano lao la tatu mfululizo kupoteza. Wako katika nafasi ya tisa wakiwa na pointi nne tu.

"Tumefungwa kimchezo na kwa muda kulikuwa na mgogoro wa kiuongozi ambao kwa sasa umeisha na tunajipanga kwa mechi yetu ya Ijumaa hii tutakayocheza nyumbani," alisema Babi, nahodha wa zamani wa Yanga.


UiTM itaumana na DRB-Hicom katika mechi ambayo Babi ametamba kwamba timu yake wataibuka na ushindi katika mechi hiyo itakayochezwa uwanja wa Mini UiTM, katika mji wa Shan Alam.

Babi aliyewahi kuzichezea pia Mtibwa Sugar, Azam na KMKM kabla ya kutimkia Malaysia alikosaini mkataba wa mwaka mmoja, alisema ligi ya nchi hiyo ni ngumu na imejaa ushindani tofauti na alivyofikiria mwanzoni.

Ajali yachukua roho ya mmoja wengine wajeruhiwa

Gari la Hood likiwa limepinduka na majeruhi wakipigania uhai wao
Abiria wakiwa hawaamini kama wamenusurika kifo
AJALI zimeendelea kutikisa Tanzania, baada ya Basi la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za usajili T.488 AXV aina ya Scania kupata ajali mbaya leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na abiria wengine karibu 20 kujeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa tatu katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema  kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya mbele.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja kwa jina la Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.

Kamanda Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa Basi, Fadhili Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na Hospitali ya Rufaa mkoani Kilimanjaro, KCMC.

Kamanda Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku wengine 8 wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Ratiba ya VPL yapanguliwa tena

Na Boniface Wambura
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya Aprili 27 mwaka huu. 
Marekebisho hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa, Taifa Stars, kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza raundi ya awali Mei mwaka huu.
Kutokana na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi 26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam.
Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa).
Raundi ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs Mtibwa (Mkwakwani), Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam Complex).
Machi 29 mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs Ruvu Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino (Azam Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi ya 24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal vs Mgambo (Mkwakwani), Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi), Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT Ruvu (Taifa).
Aprili 12 mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini), Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya City vs Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Raundi ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi), Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro), JKT Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa).