STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 11, 2014

Ajali yachukua roho ya mmoja wengine wajeruhiwa

Gari la Hood likiwa limepinduka na majeruhi wakipigania uhai wao
Abiria wakiwa hawaamini kama wamenusurika kifo
AJALI zimeendelea kutikisa Tanzania, baada ya Basi la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za usajili T.488 AXV aina ya Scania kupata ajali mbaya leo asubuhi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na abiria wengine karibu 20 kujeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa tatu katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema  kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya mbele.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja kwa jina la Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri kuelekea jijini Mbeya.

Kamanda Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa Basi, Fadhili Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na Hospitali ya Rufaa mkoani Kilimanjaro, KCMC.

Kamanda Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku wengine 8 wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi.

No comments:

Post a Comment