STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, June 17, 2013

KONYAGI YAWAPIGA MSASA WABUNGE KUHUSU BIASHARA VIROBA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa, akionesha kinywaji cha Afrika Kusini kilichofungwa kwenye viroba kama ambavyo Konyagi inafanya hapa nchini.Vinywaji kama hivyo vipo karibu nchi nyingi Ulimwenguni.

 Meneja wa Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe akielezea jinsi vinywaji vyao vinavyochangia mapato ta serikali
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,Maji na Mifugo, Said Nkumba akichangia mada hiyo kwa kuviasa baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuandika habari za kudidimiza viwanda vya haba nchini. Kulia ni Idd Azzan Mbunge wa Kinondoni na Dunstan Kitandula ambaye ni Makamu Mwenyekiti was  Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
                               Bidhaa mbalimbali zikiwa zimfungwa kwenye viroba
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa () akifafanua jambo katika semina ya wajumbe wa Kamati mbili za Bunge za Uchumi,Viwanda na Biashara  pamoja na Kilimo,Maji na Mifugo kuhusu baadhi ya vyombo vya habari vyenye uhusiano na nchi jirani vinavyotumika kupiga vita viwanda vya ndani kikiwemo cha Konyagi. Semina hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Amos Makala, akichangia mada katika semina hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa TAMISEMI, Kassim Majaliwa na Said Nkumba.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, Dunstan Kitandula akichangia mada hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (kushoto) akimkabidhi jezi Idd Azzan kwa ajili ya timu ya Bunge iliyocheza na timu ya Konyagi kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma Jumamosi
 Mgwassa akikabidhi jezi ya timu ya Konyagi kwa Idd Azzan tayari kwa mtanange na timu ya Bunge
 Meneja Masoko wa Konyagi, Joseph Chibehe (kushoto) akimkabidhi W. Zuberi  msaada wa vyerehani, ambavyo alivipokea kwa niaba ya BNaibu Spika wa Bunge, Job Ndugai
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, George Mkuchika, akisalimiana na timu ya Bunge muda mfupi kabla ya pambano lao na timu ya Konyagi, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

 George Mkuchika akisalimiana na wachezaji wa timu ya Konyagi
 Wachezaji wa timu ya Bunge wakisalimiana na wachezaji wa Konyagi
 Kikosi cha timu ya Bunge kilichochuana na Konyagi
Kikosi cha timu ya Konyagi kilichomenyana na Timu ya Bunge

CCM yalaani tukio la mlipuko wa bomu Arusha wakiitupia lawama CHADEMA


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza  na waandishi wa habari leo mjini Dodoma.

CHAMA cha Mapinduzi, CCM kimetoa tamko la kulaani tukio la mlipuko wa bomu uliotokea kwenye mkutano wa CHADEMA, ambapo watu wawili walipoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na blog ya chama hicho ikimnukuu Katibu Mwenezi wake, Nape Nnauye, CCM imesema tukio hilo linasikitisha na tukio hilo huku ikiwatupia lawama viongozi wa CHADEMA kwa kulitumia tukio hilo kisiasa zaidi, huku wakiipongeza serikali.
Ripoti hiyo ya CCM isome mwenyewe hapo chini;
Itakumbukwa tarehe 16/06/2013 ilikuwa ni siku ya uchaguzi mdogo wa madiwani kwa baadhi ya kata nchini. Uchaguzi huo umefanyika kwenye kata ishirini na mbili (22)  kati ya kata ishirini na sita (26) zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi wazi.
 Matokeo tuliyoyapata toka kwenye maeneo yaliyofanya uchaguzi yanaonyesha kuwa kati ya kata 22 zilizofanya uchaguzi CCM tumeshinda kata 16 sawa na asilimia 72.72% na wenzetu wamechukua kata 6 zilizobaki sawa na asilimia 27.28%.


 Tunawashukuru sana kote walikoonyesha imani yao kubwa kwa Chama chetu kwa kutupa dhamana ya kuendelea kuwatumikia. CCM inawaahidi utumishi uliotukuka. Hata wale 27.28% walioamua kuwajaribu wenzetu, tunawatakia kila lakheri, kwani wametumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua wanaodhani watawasaidia kufikia malengo yao ya kimaendeleo. Uchaguzi kwenye kata hizi zote umeisha sasa tuwatumikie wananchi.
 Kata nne za jiji la Arusha hazikufanya uchaguzi baada ya kuahirishwa kufuatia tukio la kusikitisha la kulipuka kwa bomu kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema mjini Arusha tarehe 15/06/2013.


 CCM tunalaani tukio hilo la mlipuko wa bomu na matukio yanayofanana na hayo katika nchi yetu. Tunawapa pole wale wote walioathirika na tukio hilo. Ni vizuri serikali ikalichunguza swala hili kwa kutumia muda mfupi na kuhakikisha waliohusika wanapatikana na kuchukuliwa hatua zinazostahili.


 Pamoja na kulaani na kuitaka serikali kukomesha vitendo hivi nchini, ni wakati muafaka kwa vyama vya siasa nchini kujitazama upya kwani kuna kila dalili kuwa tukio hili kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari mhe. Mbowe Mwenyekiti wa Chadema Taifa kuwa ni la kupangwa, inawezekana limepangwa na Chadema wenyewe.
 Hali ya kisiasa jijini Arusha kuelekea uchaguzi huo ilikuwa wazi kuwa wana Arusha walishaamua kuzirudisha kata hizo nne kwa CCM, hasa baada ya kuchoshwa na maandamano na vurugu za kila siku jijini Arusha. Aidha kauli za kukata tamaa za viongozi wa Chadema na vitendo vyao ni dalili tosha kuwa tukio hili lilipangwa na Chadema wenyewe.


 CCM tunaendelea kusisitiza na kulaani juhudi za wenzetu kujaribu kujenga umaarufu wa chama chao juu ya damu za Watanzania. Juhudi hizi zinapaswa kulaaniwa na wazalendo wote ndani na nje ya nchi. Tukumbuke asiyekubali kushindwa, si mshindani. Si busara wala uungwana na ni kinyume na utu kutumia majanga ya kutengeneza kama mtaji wa kisiasa.
 Lakini CCM tunalaani pia kitendo cha viongozi wa Chadema kujaribu kutumia baadhi ya misiba na majeruhi wa tukio hili kisiasa na mwisho wa siku kwenda kuwatelekeza hospitali baadhi yao baada ya kuwaahidi kubeba gharama zote za matibabu na mazishi.Tunaipongeza serikali kwa kuingilia kati na kuwasaidia waathirika hawa na kuhakikisha wanapata huduma inayostahili.


 CCM inarudia kueleza masikitiko yake kwa waathirika wa tukio hili la kinyama na kikatili lisilostahili kuvumiliwa hata kidogo. Kama Chama tumeguswa sana na tukio hili pamoja na kulilaani, tunawasihi watanzania tushindane na kutofautiana bila kupigana na kuvunja tunu ya nchi yetu ya amani na utulivu. Katika demokrasia ya vyama vingi swala la kuvumiliana ni swala la msingi sana katika kufikia ukomavu wa demokrasia hiyo.


 Imetolewa;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa CCM Itikadi na Uenezi.
17/06/2013
 
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Ideology and Publicity Secretary

PRESIDENT KIKWETE TOURS SUNDERLAND FC 

President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and Chairman and owner of Sunderland Football Club Mr.Ellis Short pose with some students who study football skills at the club’s Academy of Light in Sunderland yestarday afternoon. The Club in collaboration with Symbion Power Tanzania Limited have agreed to build a state of the art football academy in Dar es Salaam at the request of President Kikwete. President Kikwete is London for a three days working visit.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete talks to pupils attending  some lessons on football skills AND HEALTH  at Sunderland’s Association Football Club Academy of Light in Sunderland yestarday afternoon.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with Sunderland’s Association Football Club  Chairman and owner Mr.Ellis Short at the Club’s Stadium of Light in Sunderland yestarday afternoon.
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his delegation pose with some students who attend football training at Sunderland’s  Association Football Club Stadium of Light Academy yestarday afternoon. Others in picture from left are Symbion’s Power Limited CEO Mr.Paul Hinks(left), Ilala member of parliament Hon. Musa Zungu(Second left), Minister for Information,Youth ,Culture and Sports Dr.Fenella Mukangara(fourth left) and Minister for Land and Human Settlement Prof.Anna Tibaijuka(right).
President  Dr.Jakaya Mrisho Kikwete unveils Sunderland’s Association Football plaque at the club’s Academy of Light yestarday afternoon when the President and his delegation toured the club. On the left, looking on, is the Club’s Chairman and Owner Ellis Short.(photo by Freddy Maro).

LUCY CHARLES NDIYE KISURA WA JIJI LA MWANZA


SHINDANO la kumsaka mrembo wa mkoa wa Mwanza kwa mwaka 2013, kiliteguliwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Lucy Charles, msomi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino kuwabwaga warembo wengine 13 waliojitokeza kuwania taji hilo.

Nyota ya mrembo huyo ilianza kuonekana mapema katika mavazi yote aliyovaa, lakini zaidi aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Yatch club baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.

Mshindi wa pili katika shindano hilo alikuwa Judith Josephat na mshindi wa tatu ni Suzan Ikombe.
Washindi hao watauwakilisha mkoa wa Mwanza katika shindano la kanda ya ziwa litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu.

MAREHEMU LANGA KILEO AAGWA LEO, AZIKWA JIONI HII




 Mwili wa marehemu langa ukiwa umeishafika nyumbani kwa ajili ya kuombewa na kuagwa 
 Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika kuuaga mwili wa Marehemu langa Nyumbani kwao
<

Mama na Baba wa Marehemu Langa wakiwa na uzuni wakati wa kuagwa kwa mwili wa marehemu Langa leo mchana
 Baadhi ya wananchi waliokuja kumuaga Marehemu Langa nyumbani kwao



 Baadhi ya marafiki na wapenzi wa marehemu Langa wakiwa katika makundi
Mara baada ya zoezi hilo la kuagwa kwa mwili wa Langa, msafara ulianza kuelekea makaburi ya Kinondoni ili kuuhifadhi katika nyuma yake ya milele ambapo muda huu ndiyo anazikwa.

Taifa Stars kuingia tena kambini Julai 4



Na Boniface Wambura
KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameiita tena kambini timu hiyo Julai 4 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inavunja kambi leo (Juni 17 mwaka huu) baada ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, kundi C Kanda ya Africa dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kim amesema wachezaji watakaoitwa kambin ni wote walioko kwenye timu hivi sasa isipokuwa Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaocheza mpira nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) katika klabu ya TP Mazembe Englebert.

Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Aishi Manula, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Mechi hiyo namba 37 dhidi ya Uganda (The Cranes) itachezwa jijini Dar es Salaa kati ya Julai 12 na 14 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika wiki mbili baadaye katika Uwanja wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Jiji la Kampala.

Epiq Open Mic kumekucha Dar

Vijana waliojitokeza wakiwa kwenye foleni. 
 Jopo la washauri likongozwa na Marco Chali (wa pili toka kulia), akifuatiwa na Dknob, Walter na mwisho kulia ni Godzila
 Mmoja wa vijana akiimba mbele ya washauri.
Mmoja wa wasichana akionyesha uwezo wake.

Vijana waliojitokeza wakijiandikisha.


NaMwandishi wetu


Baada ya kuzinduliwa kwa mafanikio wiki mbili zilizopita katika viwanja vya Mwembe Yanga, mamia ya vijana wamejitokeza mwishoni mwa wiki hili katika viwanja ya ofisi za Zantel kuhudhuria usaili wa Epiq Open Mic.
Huku ikiwa imebaki wiki kadhaa kabla ya kuanza kwa msimu mya wa Epiq BSS, Zantel kwa kushirikana na Marco Chali Foundation, wamezindua Epiq Open Mic ili kuwapa vijana nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Fursa hii, ya Epiq Open Mic, inawapa nafasi vijana wenye vipaji vya muziki fursa ya kusikilizwa na mtayarishaji wa muziki maarufu nchini, Marco Chali pamoja na jopo la wanamuziki kama Godzila na Dknob, ambao wanawashauri mambo kadhaa kuhusiana na muziki wao, na huku wale wenye vipaji zaidi wakipewa nafasi ya kurekodi na Marco Chali.
Akizungumzia Epiq Open Mic, Marco Chali anasema hii ni fursa ya vijana kujifunza misingi ya muziki, lakini pia kuweza kurekodiwa muziki wao.
‘Lengo la Epiq Open Mic ni kuwahamasisha vijana kushiriki katika kukuza vipaji vyao, kuongeza uelewa wa mambo ya muziki pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo katika muziki’ alisema Chali.
Marco Chali ambaye pia ni mtunzi na mwimbaji, ametayarisha nyimbo nyngi ambazo zimeshinda tuzo ndani na nje ya nchi za wasanii kama Ms. Trinity kutokea Jamaica, A.Y wa Tanzania, Prezzo wa Kenya, J Martins kutoka Nigeria na wengine wengi.
Kwa upande wake, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema kampuni ya Zantel inaaminini katika kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao.
‘Muziki ni ajira kwa vijana wengi, na kuamini hilo ndio maana kampuni ya Zantel imeamua kuwafikia vijana wote wenye vipaji na kuwapa nafasi ya kuonekana’ alisema Khan.

Stars, Tembo wa Ivory Coast zaingiza Mil 500



Na Boniface Wambura
MCHEZO wa mchujo wa Kombe la Dunia, Kundi C, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) uliochezwa jana (Juni 16 mwaka huu) umeingiza sh. 502,131,000 kutokana na watazamaji 57,203.

Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ziliuzwa kwa sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 76,596,254.24 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,809,104.

Asilimia 15 ya uwanja sh. 62,658,846.26, asilimia 20 ya gharama za mechi sh. 83,545,128.35 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 20,886,282.09.

Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 250,635,385.06 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,531,769.25 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Mechi iliyopita ya Stars dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) kwenye uwanja huo iliingiza sh. 226,546,000.

Rais Kikwete ashushtwa na shambulio la bomu Arusha

http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2013/03/rais-kikwete.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa taarifa za shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Arusha jioni ya leo, Jumamosi, Juni 15, 2013, tukio ambalo limesababisha vifo vya watu wawili na majeruhi ya Watanzania kadhaa.
Aidha, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa na ndugu wa wafiwa wote na pia ametuma pole nyingi kwa majeruhi ambao wameumizwa na kujeruhiwa katika tukio hilo ovu na katili.

Vile vile, Rais Kikwete amewatumia salamu za pole viongozi wa CHADEMA kufuatia tukio hilo la woga mkubwa na pia kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki za kuchunguza kwa haraka, kubaini, kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria wote waliohusika na tukio hilo, wawe watu wa ndani ya nchi ama nje ya nchi.
Katika salamu zake za rambirambi na za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Magesa Mulongo, Rais Kikwete amesema: “Nimepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa CHADEMA mjini Arusha jioni ya leo, tukio ambalo limesababisha vifo na majeruhi ya Watanzania wenzetu.”
Amesema Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Magesa Mulongo salamu zangu za rambirambi kufuatia vifo na pole nyingi kutokana na majeruhi katika tukio hilo na naomba kupitia kwako unifikishie salamu zangu za rambirambi kwa jamaa na ndugu wa wafiwa na pole nyingi sana kwa majeruhi.”
“Kadhalika naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kutokana na tukio hilo. Naomba uwajulishe kuwa uchungu wao ni uchungu wetu sote na msiba wao  ni msiba wetu pia. Nataka wajue kuwa tupo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi na huzuni mkubwa,” amesema Mheshimiwa Rais Kikwete.
Rais Kikwete amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Arusha: “Kadhalika, nimeviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za haraka kuwasaka wahusika, kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Aidha, nawataka viongozi wa Serikali ngazi ya kitaifa, Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arusha mjini kuhakikisha kuwa majeruhi wote wanapata matibabu ya haraka na huduma za tibabu stahiki.”
Aidha, Rais Kikwete ametoa wito maalum kwa wananchi akisema: “Kwa wananchi wenzangu, Watanzania wenzangu, napenda kutoa wito wa kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yao vizuri ili tuweze kuwabaini waovu waliofanya kitendo hiki.”
“ Natambua kuwa yatakuwepo maneno mengi na hisia mbali mbali zitakazojaribu kulielezea tukio hilio ovu na katili kwa njia mbali mbali. Nawasihi tujiepushe na kuchukua dhana na hisia zetu au maneno ya watu wengine kuwa ni ukweli wa tukio hili. Tujipe nafasi ya kutafakari vizuri na kufanya uamuzi ulio bora.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Mimi siamini kuwa Watanzania au wafuasi wa vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kufanyiana matendo ya unyama wa aina hii. Naamini kuwa hiki ni kitendo cha mtu ama watu wasioitakia mema nchi yetu, watu ambao wanatafuta kila sababu ya kupandikiza chuki miongoni mwa raia ama makundi ya raia, ili nchi yetu iingie kwenye machafuko makubwa.”
“Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, naomba tuzinduke,  ili tusiwape nafasi watu hawa waovu ya kuweza kutimiza malengo yao ya kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu kwa kuleta mifarakano baina yetu. Mungu Ibariki Tanzania, Munfu Ibariki Afrika.”

MAP yaandaa maonyesho kuelekea siku ya Sickle Cell Duniani

WAKATI Dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya ugonjwa wa Sickle Cell mnamo Juni 19, imefahamika kuwa Tanzania ina madaktari wanne tu wa kutibu ugonjwa huo kitu alichodai huenda ndiyo sababu ya ongezeko la ugonjwa huo ambapo Tanzania inashika nafasi nne duniani kwa sasa.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Motion Arts Production (MAP), Honeymoon Aljabri, ndiye aliyefichua hato juzi alipokuwa akieleza maandalizi yao ya kufanya maonyesho ya michoro itakayoonyesha rasilimali za nchi Tanzania pamoja na kujadiliana na wadau mbalimbali juu ya ugonjwa huo.
Maonyesho hayo ya uchoraji yanaanza leo katika Jumba la Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam.
Aljabir alisema takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na wagonjwa wengi wa Sickle Cell hivyo ni wakati muafaka kwa kila mtu kujitokeza kusaidia kukabiliana na ugonjwa huo.
Alisema ni kitu cha ajabu kwamba pamoja na ugonjwa huo kuwa tishio lakini nchi ina madaktari wanne tu ambao alidai hawatoshi kukabiliana na ugonjwa huo.
“Siku ya Jumatano ni siku ya Sickle Cell Duniani, tumeona ni vyema kuwaeleza Watanzania wakatambua kuwa nchi yao ina waathirika wengi wa ugonjwa huo ikishika nafasi ya nne duniani, lakini ikiwa na idadi ndogo ya madaktari kwa sasa wakiwa ni wanne tu kwa nchi nzima, idadi ambayo haitoshi," alisema.
Mwasisi huyo wa MAP  pamoja na kutumia maonyesho hayo pia tunatarajia kufanya matembezi ya kilometa tano mwezi Septemba ambao ni mwezi uliopangwa duniani kote kuwa mwezi wa kupata elimu kuhusu ugonjwa huu wa Sickle Cell.
Aljabri alisema katika matembezi hayo tunatarajia kuchangia damu pamoja na shughuli nyingine mbalimbali za kijamii ili kuweza kuwasaidia waathirika wa ugonjwa huo hapa nchini,pamoja na juhudi zetu hizo malengo ya  kudumu ni kufungua kituo cha taarifa ambacho kitasaidia watu wenye Sicle Cell  kupata taarifa juu ya maradhi hayo na hupatikanaji wa huduma zake.
Mkurugenzi huyo alisema mwaka huu wataendesha kampeni hiyo katika mkoa wa Dar es Salaam pekee ila matarajio yao ni kuhakikisha kuwa kwa miaka ijayo wanafika kwenye mikoa yote nchini.

Langa Kileo kuzikwa leo, wengi wamlilia

Langa Kileo enzi za uhai wake
WAKATI mwili wa msanii wa kizazi kipya, Langa Kileo, aliyefariki Juni 13 ukitarajiwa kuagwa na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam, wasanii wenzake na watu mbalimbali maarufu wametoa salamu zao za pole wakionyesha kuguswa na vifo mfululizo vya wasanii nchini.
Baadhi ya wasanii na mastaa hao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii wamesema kifo cha Langa ni kama kutoneshwa kidonda cha msiba wa Albeert Mangweha aliyefariki Mei 28 nchini Afrika Kusini na kuzikwa Juni 6 mjini Morogoro.
Wasanii kama Hammer Q, Nikki Mbishi, Joh Makini ambaye naye alikuwa akisumbuliwa na malaria, Fina Mango, Teddy Kalonga, MwanaFA wamelezea kusikitishwa na kifo cha Langa na kumtakia mapumziko mema.
Teddy Kalonga aliandika katika ukurasa wake wa facebook akihoji inakuwaje watu wengi wanakufa wakiwa vijana wadogo katika zama hizi, huku Joh Makini akiweka bayana kwamba hatatoa kazi yake yoyote mpya ili awaomboleze wasanii wenzake waliotangulia mbele ya haki.
Fina Mango yeye alitoa pole kwa baba na mama Langa Kileo na kuwataka kuwa na uvumilivu na subira katika kipindi hiki cha msiba wa mtoto hukuywao aliyemtakia safari njema huko aendako.
Langa Kileo alifariki jioni ya Alhamisi iliyopita baada ya kuugua ghafla na kukimbizwa Muhimbili na anatarajiwa kuagwa leo saa 7 kabla ya kuzikwa baadaye kwenye makaburi ya Kinondoni, huku msiba wa Ngwair na muigizaji Taji Khamis 'Kashi' ukiwa bado haijasahaulika baada ya kufululizana.