STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 30, 2013

David Mwantika amrithi Kelvin Yondani Taifa Stars, kocha Kim Poulsen amuita kikosini

Beki David Mwantika (kulia) aliyeitwa Taifa Stars kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani
Na Boniface Wambura
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza kwenye kikosi chake beki wa Azam, David Mwantika kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.

Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kelvin Yondani ambaye ni majeruhi. 

Mbali na Yondani Stars ina wachezaji majeruhi watatu ambao kocha Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ni waweze kushughulikia matibabu yao. 

Wachezaji hao ni Athuman Idd 'Chuji' , Shomari Kapombe na John Bocco 'Adebayor'.

Taifa Stars imeingia kambini jana (Agosti 29 mwaka huu) na imeanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. 

Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.

TFF, AZAM MEDIA ZASAINI MKATABA WA BIL. 5.5/-

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).

Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. 

Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.

Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.

Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.

Gervinho achekelea kuhama Arsenal

http://u.goal.com/310700/310729_heroa.jpg
MSHAMBULIAJI wa Ivory Coast, Gervinho (26) amebainisha kwamba alifurahi sana kuondoka Arsenal.
Nyota huyo amesema alikuwa na maisha magumu London Kaskazini na kwamba ilipotokea ofa ya kuondoka aliichangamkia haraka.
Gervinho alishuka kiwango na akashindwa kuonyesha makali yake Arsenal baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa paundi milioni 10.8 akitokea Lille mwaka 2011.
Alikamilisha uhamisho wake wa kutua Roma mapema katika kipindi hiki cha usajili chini ya kocha wake wa zamani wa Ufaransa, Rudi Garcia na amesema atatisha chini ya kocha huyo.
Nyota huyo aliyesajiliwa kwa paundi milioni 8 alisema: "Ilikuwa ni faraja kubwa kwangu kuchezea Arsenal, lakini baada ya miaka miwili ya kupanda na kushuka ilikuwa ni wakati mwafaka wa mabadiliko.
"(Arsene) Wenger, nadhani ni kocha mkubwa. Ni mtu ambaye namheshimu sana na nina furaha kubwa kupata fursa ya kucheza katika timu yake. Nadhani washambuliaji wanahitaji kuaminiwa na kocha wao na kupewa muda mwingi wa kucheza. Nilitamani nami iwe hivyo. Lakini ukurasa huo umepita mambo yamebadilika. Naweka akiliyangu yote Roma.
"Roma ni timu kubwa yenye kocha mkubwa. Sikujiuliza kukubali ofa yao.
"Daima nina mahusiano mazuri na Garcia - amekuwa akinijengea kujiamiani daima, na alikuwa ndiye kocha wa kwanza kunichezesha kwenye wingi.
"Nataka kuonyesha naweza kuisaidia timu. Siko katika hali nzuri kimwili kwa sasa, lakini Garcia ananifahamu vyema, nina kazi ya kufanya ili niwe fiti tena."
(Talksport)

Diamond nouma, amzawadia Mzee Gurumo gari...wengine mpo...!

Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
Show.
Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

STAA wa nyimbo za 'Kesho', 'Nataka Kulewa', 'Mawazo' na vingine, Naseeb Abdul ameonyesha mfano kwa wadau wa muziki nchini baada ya kumzawadiwa gari mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi aliyetangaza kustaafu, Muhidini Gurumo.
Diamond alimkabidhi Gurumo gari hilo kuonyesha kujali na kuthamini mchango wa mwanamuziki huyo, baada ya hivi karibuni kunukuliwa 'akilia' kwamba kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa mwanamuziki anastaafu akiwa hana hata baiskeli.
Alichokifanya Diamond ni jambo la kupongezwa na kuigwa na wadau wengine wa muziki kama alivyowahi kunukuliwa mwenyewe (Gurumo) kwamba angependa ale jasho na kupewa pongezi zake angali hai badala ya watu kumsubiri afe ndipo watu wajitokeze kumwagia sifa na kujifanya kumuenzi wakati akiwa hao walimtelekeza.
MICHARAZO inakupa pongezi Diamond na tunawaomba wengine wamsadie mkongwe huyo ambaye amestaafu siyo kwa sababu ya kuishiwa kimuziki, bali hali yake ya kiafya akisumbuliwa na maradhi na wenye kutaka kumchangia watume fedha kwa njia ya TiGO Pesa katika simu yake ya mkononi 0655-401383.