STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, March 9, 2014

Manchester City yatupwa nje FA Cup

James Perch
City wakitunguliwa bao
NDOTO za kocha Manuel Pellegrini kunyakua mataji manne kwa mpigo msimu huu katika michuano mbalimbali inayoshiriki klabu yake ya Manchester City imeanza kuyeyuka baada ya kung'olewa kwenye hatrua ya Robo Fainali na Wigan Athletic muda mfupu uliopita.
City ikiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Etihad, imejikuta ikinyukwa mabao 2-1 na Wigan na kushindwa kukutana na Arsenal kama wengi walivyokuwa wakitarajia na kuona ndoto za kocha huyo kutoa Chile zikitimia.
Mabao ya Jord Gomes kwa mkwaju wa penati dakika ya 27 na jingine la pili la dakika ya 47 lililofungwa na James Perch yalitosha kuizima wababe hao wa Manchester City licha ya Samir Nasir kufunga bao dakika ya 68 lililoshindwa kuisaidia timu yake.
Kwa ushindi huo sasa, Wigan inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza itaumana na Arsenal kwenye mechi ya Nusu Fainali, huku nusu fainali nyingine ikizikutanisha Hull City dhidi ya Sheffield United.

Ikulu yakana Rais kumtembelea mfungwa, yamtembelea Mkambara na wengine

D92A3630-1 (1)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten na Magic Radio FM Bwana Salum Mkambala aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa katika Hospitali ya Taifa muhimbili baada ya kuapata ajali na kujeruhiwa vibaya wiki iliyopita
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijulia hali Ofisa wa Habari tume ya Uchaguzi Bi.Margareth Chambiri aliyelazwa katika Tasisi ya MOI Hospitali ya Taifa Muhimbili.Bi.Chambiri aliwahi kufanya kazi katika Televisheni ya Taifa TBC.Picha na Freddy Maro-IKULU

Nusu Fainali FA ni Hull City vs Sheffield Utd, Arsenal vs Wigan (?)

USHINDI iliyopata jioni hii dhidi ya Sunderland imeifanya Hull City kukutana uso kwa uso na Sheffield United katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la FA, huku Arsenal wakisubiri mshindi kati ya Wigan Athletic inayoongoza mpaka sasa dhidi ya Manchester City katika hatua hiyo.
Kwa mujibu wa droo iliyotangazwa muda mfupi uliopita mechi za hatua hiyo zitacheza kati ya Aprili 12 na 13 kwenye uwanja wa Wembley jijini London.
Tumaini ya mashabiki wengi kutaka kuona nusu fainali ya aina yake kati ya Arsenal na Manchester City ni kama inapotea kwani mpaka sasa City wakiwa nyumbani wameshanyukwa mabao 2-1 na Wigan japo imesalia dakika 10 pambano hilo kumalizika, Samir Nasir alifunga bao la Man City baada ya muda mwingi Wigan kuongoza 2-0.
Iwapo City itashindwa kupenya hatua hiyo itafanya ndoto za kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini wa kuiwezesha timu hiyo kutwaa mataji manne msimu huu baada ya awali kunyakua Kombe la Ligi (Capital One) na Jumatano ana kibarua kigumu mbele ya Barcelona kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya awali kulala 2-0 nyumbani wiki mbili zilizopita.

CS Sfaxien, Cotonsport, AS Vita nazo zafuzu Afrika, Yanga ipo dimbani wakiwakimbiza Ahly Niyonzima nje

http://www.africatopsports.com/wp-content/uploads/2013/09/CS_SFAXIEN_ONZE.jpg
CS Sfaxien waliyofuzu hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika
AS. VITA CLUB
AS Vita ya DR Congo
CS Sfaxien ikiwa nyumbani nchini Tunisia imeizamisha Dedebit ya Ethiopia kwa mabao 2-0 na kufuzu katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 4-1.
Katika mechi yao ya kwanza mjini Addis Ababa, Dedebit ilifungwa mabao 2-1.
Nayo timu ya Coton Spors ilifungwa bao 1-0 ugenini wiki iliyopita nchini Burundi leo ikiwa nyumbani imeifanyia mauaji ya kutisha Flambeau de l'Est kwa kuifumua mabao 5-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 6-1.
Mchezo mwingine uliochezwa DR Congo imeshuhudia AS Vita ikifuata nyayo za ndugu zao TP Mazembe kusonga mbele baada ya kuiondosha patupu Dyanamos ya Zambia kwa kuilaza bao 1-0.
Dynamos iliyolazimishwa suluhu katika mechi yao ya nyumbani ilishindwa kufurukuta kwa wenyeji hao na kujikuta wakilala 1-0 ugenini.
Yanga kwa sasa ipo dimba la Alexandria ikiumana na Al Ahly ambapo mpaka sasa hakuna timu iliyoona lango la wenzake na timu zimeenda mapumziko.
Kikosi cha Yanga kipo hivi;
Deo Munishi, Mbuyi Twite, Oscar Joshua, Nadir Cannavaro, Kelvin Yondani, Frank Dumayo, Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi. 

Juventus haishikiki Italia, Inter nayo yang'ara

Kwadwo Asamoa scores
Kwadwo Asamoah akiifungia Juventus bao pekee leo dhidi ya Fiorentina

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Italia (Seria A) Juventus imeendelea kutamba kwenye ligi hiyo baada ya jioni hii kuifumua Fiorentina kwa kuilaza bao 1-0, huku Inter Milan nayo ikichomoza na ushindi kama huo dhidi ya Torino.
Bao la dakika ya 42 lililofungwa na Mghana, Kwadwo Asamoah lilitosha kuwapa pointi tatu 'kibibi' cha Turin na kuongeza pengo la pointi na timu inayowafuata nyuma yao, Roma kwa pointi 14 ambayo itashuka .
Juve imefikisha pointi 72 wakati Roma itakayoshuka dimbani baadaye kuumana na Napoli ikiwa na pointi 58.
Katika mechi nyingine Inter Milan iliilaza Torino kwa 1-0, huku Lazio ikilala nyumbani kwa bao 1-0 dhidi ya Atalanta, Chievo ikishinda mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Genoa, Parma ikiifumua Hellas Verona mwaka 2-0 na Sampdoria ikishinda nyumbanio mabao 4-2 dhidi ya Livorno na Bologna na Sassuolo zikitoka suluhu.
Hull City, Sheffield Utd zaifuata Arsenal Nusu Fainali FA

Curtis Davies scores for Hull City
Hull City na Sunderland walipoumana leo
John Brayford
Huree tumefuzu mmoja wa wafungaji wa Sheffield Unitd akishangilia bao lake lililoivusha timu hiyo ya daraja la chini kutinga hatua hiyo ya Nusu Fainali tangu Wycombe Wanderers kufanya hivyo mwaka 2001.
TIMU ya Hull City imepata ushindi wa kishindo na kufuzu nusu fainali ya Kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1930 baada ya kuitambia Sunderland kwa mabao 3-0, huku Sheffeld United ikipenya hatua hiyo kuifuata Arsenal iliyotangulia jana kwa kuilaza Charlton Athletic kwa mabao 2-0.
Katika mechi ya kwanza Ryan Flynn aliifungia Sheffeld bao la kuongoza dakika ya 65 kabla ya dakika mbili baadaye John Brayford aliongeza la pili na kufuzu hatua hiyo baada ya miaka mingi, huku katika mechi ya pili Sunderland ilibanwa na wenyeji wao na kukubali kipigo hicho cha aibu na kuiondosha patupu.
Mabao ya Curts Davies katika dakika ya 68 kabla ya Meyler akaongeza la pili dakika ya 72 na Fryatt akafunga la tatu na kuihakikishia Hull City ikifuzu Nusu Fainali.
Mechi nyingine ya kuhitimisha robo fainali za michuano hiyo, Manchester City wenyewe wapo njiani sasa wakiumana na Wigan Athletic ambao wameshatangulia kupata mabao 2-0 ikiwa ni kipindi cha pili.

JKT Ruvu yaifumua Mtibwa Sugar Chamazi

JKT Ruvu walioifumua Mtibwa leo
Mtibwa sugar iliyopoteza matumaini ya kuwnaia ubingwa na sasa kupigana kubakia katika ligi
TIMU ya Mtibwa Sugar imeendelea kuwa urojo baada ya kubamizwa na JKT Ruvu mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania, walishindwa kuwabana vijana wa Fred Felix Minziro na kupoteza mchezo huo ulioufanya uongozi wa Mtibwa kukiri kwamba mbio za ubingwa kwao ndiyo basi tena.
Nahodha Husseni Bunu aliifungia JKT Ruvu bao dakika ya 34 bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kusawazisha bao kupitia kiungo mkongwe, Vincent Barnabas katika dakika ya 70 kabla ya dakika tano baadaye Amos Mgisa kumaliza udhia kwa kuipatia JKT bao la pili./
Kwa ushindi huo JKT Ruvu imefanikiwa kufikisha pointi 25 licha ya kusalia kwenye nafasi ya 9 ikiwa nyuma ya Mtibwa waliolingana nao pointi ila wanatofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Al Ahli Benghazi yafuzu raundi ya pili Afrika

* Ndiyo ikayocheza na Yanga au Al Ahly
* TP Mazembe yapenya kwa kishindo 
* Raja Casablanca yatolewa kwa matuta
CAF Champions League | FIXTURES

Which clubs present your country?

Young Africans (Tanzania) v Al Ahly (Egypt)
Berekum Chelsea (Ghana) v Ahli Benghazi (Libya)
Gor Mahia (Kenya) v Esperance (Tunisia)
Enyimba (Nigeria) v AS Real (Mali)
Astres de Douala (Cameroon) v TP Mazembe (DR Congo)
B.Y.C (Liberia) v Sewe Sport (Cote d’Ivoire)
Dedebit (Ethiopia) v CS Sfaxien (Tunisia)
Horoya (Guinea) v Raja Casablanca (Morocco)
Flambeau de l’Est (Burundi) v Coton Sport (Cameroon)
Entente Setif (Algeria) v ASFA Yennenga (Burkina Faso)
Stade Malien (Mali) v El Hilal (Sudan)
AC Leopards (Congo) v Primeiro de Agosto (Angola)
Kaizer Chiefs (South Africa) v Liga Muçulmana (Mozambique)
Dynamos FC (Zimbabwe) v AS Vita Club (DR Congo)
Zamalek (Egypt) v Kabuscorp (Angola)
Nkana (Zambia) v Kampala City Council (Uganda) 

First leg: 28 February to 2 March 2014
Second leg: 7-9 March 2014
AL Ahli Benghazi ya Libya jioni hii imeifumua Berekum Chelsea ya Ghana kwa mabao 2-0 na kufuzu raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikisubiri mshindi kati ya Yanga ya Tanzania au Al Ahly ya Misri.
Ikiwa uwanja wa nyumbani Benghazi ilipata ushindi huo muhimu na kufanikiwa kufuzu raundi ya pili kwa jumla ya mabao 3-1 baada ya wiki iliyopita kulazimisha sare ya 1-1 ugenini.
Sasa timu hiyo itataka kujua itaumana na nani kati ya Yanga iliyopo ugenini kuwakabili mabingwa watetezi wa taji hili Al Ahly katika mechi inaytotarajiwa kucheza muda mfupi ujao mjini Alexandria, Misri.
Katika mechi ya kwanza Yanga ikiwa nyumbani jijini Dar es Salaam iliifumua Al Ahly kwa bao 1-0 na hivyo usiku huu itahitajika kupigania sare ya aina yoyote kuingia hatua hiyo ya pili na kukumbana na mwarabu mwingine.
Nao mabingwa wa zamani wa Afrika, TP Mazembe ikiwa nyumbani imepata ushindi wa kishindo baada ya kuicharaza Les Astres ya Cameroon mabao 3-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao  4-1 baada ya awali kulazimishwa sare ya 1-1 ugenini na wapinzani wao hao.
Nao vijogoo wa Morocco Raja Casablanca pamoja na kushinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Horoya ya Guinea imejikuta iking'oa raundi ya kwanza kwa kunyukwa kwa mikwaju ya penati 5-4.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Conakry, Raja walifungwa bao 1-0 na hivyo ushindi wa leo uliifanya kuwa sare ya 1-1 na kulazimishwa kupigiana penati na kushindwa na wapinzani wao. 

AFC Leopards yatupwa nje Kombe la Shirikisho Afrika

Orange CAF Confederation Cup: SuperSport vs AFC Leopards clash
AFC Leopards

KLABU kongwe ya Kenya, AFC Leopards jioni hii imeyaaga mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Supersport ya Afrika Kusini.
Katika mechi hiyo ya marudiano iliyochezwa uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi Leopards imejikuta ikikwama kusonga mbele kwa Wasauzi baada ya wiki iliyopita kukubali kipigo cha mabao 2-0 ugenini na hivyo kung'olewa mashindanoni kwa jumla ya magoli 4-2.
Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao maara baada ya kipindi cha pili kuanza baada ya kufanikiwa kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nguvu sawa ya bila kufungana.
Bao hilo lilifungwa na dakika ya 48 kupitia James Situma, lakini wageni walisawazisha dakika ya 54 kupitia Thuso Phala kabla Supersport kuongeza la pili kupitia kwa Sameehg Doutie katika dakika ya 79 na kuwafanya Leopards kucharuka ili kuepuka kipigo cha nyumbani.
Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 90 wakati Allan Wanga kulisawazisha bao hilo na kufanya matokeo kuwa 2-2, matokeo ambayo hata hivyo hayakuwasaidia Wabaluya kusonga mbele dhidi ya wageni.
Katika mchezo mwingine wa michuano hiyo Bizertin ya Tunisia nayo ilifuzu raundi ya pili baada ya kuinyuka Desportivo Huila ya Angola kwa mabao 2-0.
Watunisia walikuwa nyumbani na ushindi huo umeifanya kutinga raundi nyingine kwa jumla ya mabao 3-0 baada ya wiki iliyopita kushinda 1-0 ugenini nchini Angola.

Simba yabanwa Mbeya, Prisons yaendeleza rekodi

Prisons
Simba
WEKUNDU wa Msimbazi imeendeleza rekodi mbaya ya kushindwa kuibuka na ushindi mjini Mbeya baada ya jioni hii kulazimishwa suluhu na Prisons-Mbeya katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba ambayo ilikuwa ikihitaji ushindi ili angalau kuendelea kuwepo kwenye mbio za kuwania ubingwa, ilishindwa kufurukuta katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine-Mbeya.
Ikiwa na nyota wake wote wakiwamo waliokuwa na timu ya taifa, Taifa Stars iliyokuwa Namibia kucheza mechi ya kirafiki na wenyeji wao, Simba haikuweka kuvunja mwiko wa Maafande hao wa Magereza ambao hawajapoteza mchezo wowote katika duru hili la pili la ligi.
Kwa sare hiyo Simba imeendelea kujiimarisha kwenye nafasi ya nne kwa kujikusanyia pointi 36 nyuma ya Yanga yenye pointi 38 ila ikiwa na michezo mitatu mkononi.
Prisons yenyewe imejiongeza pointi moja na kufikisha pointi 22 baada ya kucheza mechi ya 20.

Taifa Stars sasa kutumia jezi za Adidas


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kwamba kufuatia makubaliano hayo TFF ilipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars), zikiwemo jezi ambazo zilianza kutumika kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
Amesema vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.
“TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini,”amesema Malinzi.
Mwezi uliopita, Malinzi alikwenda makao makuu ya CAF, Cairo nchini Misri kujitambulisha baada ya kurithi kiti cha Leodegar Tenga Desemba mwaka jana na akiwa huko alikutana na Rais wa CAF, Issa Hayatou aliyeahidi kumpa sapoti kubwa.

Yanga tupeni raha Watanzania, funga Ahly leo

 
ROHO zikiwadunda baadhi ya mashabiki wa kandanda nchini kuhuisiana na pambano la marudiano baina ya Yanga na Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha msaidizi wa mabingwa hao watetezi wa Tanzania, Charles Mkwasa amesisitiza timu yao haitapaki basi badala yake itashambulia mwanzo-mwisho.
Yanga inavaana na Alhy wiki moja baada ya kuwadonyoa bao 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo katika mechi ya leo Jangwani wanahitaji sare yoyote ili kufuzu hatua ya 16 Bora.
Mechi hiyo inachezwa kwenye uwanja wa Mexx, mjini Alexandria badala ya Cairo kama ilivyokuwa ikifahamika awali, kitu kinachoelezwa kama hila za wapinzani wao kutaka kuwachanganya akili kabla ya mechi hiyo itakayochezwa majina ya saa 2 usiku kwa hapa kwetu na itaonyeshwa live kupitia mtandao wa Yanga.
Kocha Msidizi wa Yanga, Mkwasa alisema mchezo wa leo utakuwa mgumu kutokana na Yanga kuwafunga wenyeji wao 1-0 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam na kudai itakuwa kosa kama Yanga itaingia uwanjani na mkakati wa kujihami.
 Badala yake kocha huyo alisema Yanga itashambulia huku ikiwa makini kwenye ulinzi, ili kuhakikisha inailiza tena Ahly nyumbani kwao na kuweka rekodi Afrika.
"Naamini hawa jamaa watacheza mchezo wa kutushambulia ili kupata goli la mapema," alisema Mkwasa.
"Tunalifahamu hilo lakini ili kuwapa wakati mgumu ni lazima tumiliki mpira na kuwashambulia muda wote na kutowapa nafasi ya kupanga mashambulizi."
Aidha, Mkwasa alisema katika mikanda ya hivi karibuni waliyoiangalia Al Ahly imeonekana kuwa inatumia zaidi mawinga na mabeki wa pembeni kupiga krosi katika mashambulizi yake lakini wamejipanga kudhibiti mchezo huo.
Mkwasa alisema kila mchezaji wa Yanga yupo kwenye hali nzuri kimchezo na wapo tayari kwa mpambano wa leo.
"Unajua ushindi wa nyumbani umewapa wachezaji hali ya kujiamini," alisema. "Wapo tayari kwa mchezo na kwa kweli kama tutafanikiwa kufanya tulichokipanga kwenye mazoezi yetu, ni wazi tutasonga mbele kwenye mashindano haya."
Akizungumzia kikosi cha leo, Mkwasa alisema kupanga ni kazi ya kocha mkuu, Hans van Pluijm. Hata hivyo alisema hakitabadilika sana kulinganisha na mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita.
Kwenye mchezo huo ambao goli pekee lilifungwa na naodha Nadir Haroub 'Canavaro' kikosi kilichoanza kilikuwa:
Deogratias Munishi 'Dida', Oscar Joshua, Mbuyu Twite, Canavaro, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa, Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi.
Katika mchezo wa leo, Yanga ina anasa ya hata kutofungwa si zaidi ya bao 1-0 na ikasonga mbele angalau kwa njia ya matuta
MICHARAZO MITUPU na watanzania kwa ujumla inaitakia kila la heri Yanga katika mechi hiyo ya leo ili kuweza kufanya vyema na kuwapa furaha mashabiki wa soka ambao wamechoka kuona timu zao zikiwa wasindikizaji katika michuano ya kimataifa.
Yanga ndiyo tiumu pekee ya Tanzania kusalia kwenye michuano hiyo mwaka huu baada ya Azam, KMKM na Chuoni za Zanzibar kung';olewa kwenye mechi ra awali za michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika.

Atletico Madrid yashinda ugenini na kuiporomosha Barca

Villa akipongezwa na wachezaji wenzake
MABAO mawili ya David Villa usiku wa kuamkia leo yaliiwezesha Atletico Madrid kurejea nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania na kuiporomosha Fc Barcelona hadi nafasi ya tatu baada ya kuinyuka  Celta Vigo ikiwa kwao kwa mabao 2-0.
Villa alifunga mabao hayo ndani ya dakika mbili dakika ya 62 na 64 na kuiwezesha timu yake iliyocheza bila 'muuaji' wake Diego Costa anayetumikia kadi nyekundu kufikisha p[ointi 64 kulingana na Real Madrid ambayo ina mchezo mmoja mkononi ambao itaucheza leo.
Timu hizo zinatofautiana uwiano wa mabao Madrid ikiizidi Atletico mabao matano tu na kuitangulia watetezi wa ligi hiyo Barcelona ambao jana walichezea kichapo cha bao 1-0 toka kwa Real Vallodolid kwa pointi moja kwani yenyewe ina pointi 63.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo  Jumapili, Grenada ilijipatia ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya wageniu wao Villarreal.
Kipute cha ligi hiyo kitaendelea tena leo kwa michezo kadhaa ambayo inaweza kuiongeza pengo la pointi baina ya vinara Real Madrid dhidi ya wapinzani wake waliopo ndani ya Tatu Bora.AC MIlan bado mwaka wa tabu Italia yanyukwa tena

Di Natale alipowatungua Milan jana
KLABU ya AC Milan imeendelea kusuasusa kwenye Ligi Kuu ya Italia Seria A baada ya jana usiku kudonyolewa bao 1-0 ugenini na Udinese na kuzidi kuiweka katika wakati mgumu hata kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.
Bao pekee lililoizamisha Milan iliyomweka benchi mshambuliaji wake nyota, Mario Balotelli na kumuingiza kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Robinho, liliwekwa kimiani na Antonio di Natalie katika dakika ya 67 akimaliza kazi nzuri ya Bruo Fernandes.
Kwa kipigo hicho Milan imeendelea kusalia na pointi 35, ikiwa ni kama nusu ya pointi ilizonazo vinara na watetezi wa ligi hiyom Juventus yenye pointi 69 na inayotarajiwa kushuka dimbani leo kukamilisha mchezo wake wa 27.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana Catania na Cargliari zilitoka sare ya kufungana bao 1-1.

Simba katika mtihani mgumu Mbeya leo

Simba
Wenyeji Prisons
SIMBA ambayo haijashinda katika mechi nne mfululizo, inatakiwa kuifunga Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine leo ili kubakiza hai matumaini yake ya kutokosa mara mbili mfululizo kwa mara ya kwanza, moja ya nafasi mbili za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya Bara.
Simba ambayo ilishika nafasi ya tatu msimu uliopita nyuma ya Yanga na viongozi wa ligi kuu msimu huu Azam, ipo hatarini kukosa tena moja ya nafasi mbili za juu kutokana na kuachwa na Azam kwa tofauti ya pointi tano zikiwa zimebakiwa mechi sita.
Wekundu wa Msimbazi pia wameachwa kwa tofauti ya pointi tatu na Yanga ambayo ina mechi tatu mkononi katika nafasi ya pili. Azam ina mechi mbili za ziada.
Hivyo ni ushindi tu ambao utaendeleza ndoto ya Simba ya kucheza angalau Kombe la Shirikisho la klabu za Afrika mwakani, lakini inakutana na Prisons ambayo imeshinda mechi tatu mfululizo zilizopita. 
Kocha wa Prisons, David Mwamaja alinukuliwa toka Mbeya akisema kuwa amekiandaa vyema kikosi chake kuhakikisha kinaibuka na ushindi dhidi ya Simba ili kiendelee kusalia kwenye ligi kuu msimu ujao.
Licha ya kutopoteza mchezo wowote katika mechi sita za duru la pili, Prisons ipo pointi nne tu juu ya janga la kushuka daraja na ushindi dhidi ya Simba leo utaisaidia kupiga hatua kubwa katika kutimiza lengo la klabu na Mwamaja.
“Tunaiheshimu Simba kwa sababu ni klabu kongwe nchini lakini hatuiogopi na kamwe wasitarajie mteremko katika mechi yetu ya kesho (leo).," alisema Mwamaja.
"Tunazihitaji pointi tatu muhimu dhidi yao ili tujiweke sehemu nzuri katika msimamo wa ligi.”
Naye Zdravko Logarusic, kocha mkuu wa Simba, alisema ana matumaini makubwa ya kushinda mechi ya leo.
Alisema kuifunga Prisons ni sehemu ya mikakati ya kushinda mechi zao zote sita zilizobaki ili kuwa katika nafasi za juu kadri iwezekanavyo katika msimamo wa ligi hiyo.
Mechi nyingine itakayopigwa leo ni kati ya JKT Ruvu itakayoikaribisha Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Chamazi ikiwakosa wachezaji wake kadhaa akiwamo Mussa Mgosi na Salvatory Ntebe walioadhibiwa na TFF