STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, March 4, 2014

Young Hassanally kuzindua Nyongo Mkaa na Ini

* Uzinduzi kufanyika Ijumaa Travertine Hotel
* Khadija Kopa, Jokha Kassim,Mwanahawa Ally ndani
Muimbaji Hassani Ally 'Young Hassanally'
Mwanahawa Ally naye atakuwepo ukumbini kumsindikiza Young Hassanally
Khadija Kopa (kushoto) naye atakuwepo Travertine Hotel
MALKIA wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, Mwanahawa Ally na Jokha Kassim wanatarajiwa kusindikiza uzinduzi wa albamu mpya binafsi ya muimbaji nyota wa muziki wa taarab nchini anayeliimbia kundi la King's Modern Taarab, Hassan Ally 'Young Hassanally'.
Uzinduzi huo wa albamu hiyo inayofahamika kwa jina la 'Nyongo Mkaa na Ini' utafanyika siku ya Ijumaa kwenye ukumbi wa hoteli maarufu iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MICHARAZO, Young Hassanally, alisema mbali na waimbaji hao mahiri nchini, pia uzinduzi huo utasindikizwa na kundi la King's Modern Taarab maarufu kama 'Wana Kijoka'.
Hassanally, alisema ameamua kuwashiriki wakali hao katika uzinduzi wake ili kuunogesha na kuwapa burudani mashabiki wa muziki wa mwambao.
"Siku ya Ijumaa natarajia kuzindua albamu yangu ya pili mpya iitwayo 'Nyongo Mkaa na Ini' ambapo nitasindikizwa na wakali wa muziki wa mwambao Afrika Mashariki na Kati, Al-hanisa Khadija Kopa, Mwanahawa Ally 'B52' na Jokha Kassim pia kundi langu la King's Modern litakuwapo ukumbini Magomeni kunisindikiza," alisema.
Hiyo ni albamu ya pili binafsi ya staa huyo baada ya awali kuzidnua albamu ya 'Aibu Yao Aibu Yetu' na  aliongeza kuwa maandalizi yote ya uzinduzi huo yamekamilika na kwa sasa kinachosubiriwa na siku ya uzinduzi huo ili mashabiki wapate burudani, huku akitaja viingilio ni Sh. 5000 tu kila kichwa.

Ridhiwani Kikwete kuitetea CCM-Chalinze, ambwaga Madega

Ridhiwani Kikwete (kulia)
Kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani lililoachwa wazi baada ya mbunge wake SAID BWANAMDOGO kufariki hivi karibuni Chama cha Mapinduzi kimefanya kura ya maoni ili kumpata mrithi wa Jimbo hilo atakayechuana na wagombea kutoka vyama vingine.

Katika kura hiyo ya maoni wagombea watatu wamejitokeza kuwania nafasi ya ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha CCM akiwemo mbunge wa zamani wa Jimbo hilo RAMADHAN MANENO, mwenyekiti wa zamani wa Yanga IMANI MADEGA na mdau mkubwa wa soka hapa nchini na mwanachama wa Yanga RIDHIWANI KIKWETE.
Baada ya kura kupigwa RIDHIWANI KIKWETE ndiye amepata Baraka za wanaCCM kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge kwa kumpa kura 758 huku IMANI MADEGA akishika nafasi ya pili kwa kupata kura 335 na RAMADHAN MANENO akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 206.
SHAFFIH DAUDA

Steve Nyerere aja na Snake Kingdom

Hii ndiyo kazi mpya ya Steve Nyerere itakayosambazwa na Proin Promotions
MWENYEKITI wa Bongo Movie Unity (BMU), Steven Mengele 'Steve Nyerere' anajiandaa kuiachia hadharani filamu yake mpya kwa mwaka 2014 iitwayo 'Snake Kingdom'.
Akizungumza na MICHARAZO, Steve Nyerere alisema filamu hiyo ya kijamii ameigiza na wakali wenzake kama Chuchu Hans, Mayasa Mrisho, Cathy Rupia, Bi Terry 'Mama Nyamayao' na wengine.
Steve Nyerere alisema filamu hiyo ni ya aina yake na kuwataka mashabiki kujiandaa kupata uhondo mara itakapoachiwa mtaani hivi karibuni chini ya kampuni mpya na inayokuja kwa kasi katika kusambaza kazi za wasanii wa filamu nchini ya Proin Promotions.
Mchekeshaji huyo anayeigiza sauti za viongozi mashuhuri, alisema 'Snake Kingdom' ni filamu iliyozalishwa na kampuni yake iliyowahi kutoa filamu kama 'Mwalimu Nyerere', 'My President', 'My Son', 'Mke Mwema' na nyingine.

Huwezi kuamini! Kaole Sanaa Group 'lafufuka' na Kipusa

Issa Kipemba 'Kipemba' aliyepigana kuirejesha tena Kaole Sanaa
Mmoja wa waasisi wa Kaole Sanaa, Bi Chuma Suleiman 'Bi Hindu' aliyecheza igizo la 'Kipusa'
Unamkumbuka Mzee wa Mabreka? Swebe Santana naye ndani dah!
JANA niliwaacha na maswali mengi juu ya taarifa inayokuwa ikiuliza unalikumbuka kundi la Kaole Sanaa Group, kundi lililochangia kupatikana kwa asilimia kubwa ya mastaa wanaotamba kwenye Bongo Movie.
Kundi hilo lililoasisiwa na kuundwa na wasanii wakongwe wa maigizo waliotamba kupitia Radio Tanzania (RTD) na lililokuja kutamba na michezo yao ya kwenye runinga kupitia kituo cha ITV kabla ya kuhamisa TVT (sasa TBC1) lilikuwa kama 'limekufa' hasa baada ya mastaa wake kuhamia kwenye filamu.
Hata hivyo mmoja wa mastaa wake, Issa Kipemba na wenzake kadhaa walikaa chini na kutafakari ili kulirejesha tena kwa nguvu kundi hilo.
Vikao kadhaa vilivyowahusisha baadhi ya waasisi wake kama Chuma Suleiman 'Bi Hindu' na wengine hatimaye kundi hilo limeanza kurekodi igizo lao jipya kwa ajili ya kuwarejesha burudani mashabiki wake ambayo waliikosa kwa kipindi kirefu.
Igizo hilo ambalo hata hivyo bado halijafahamika litaonyeshwa katika kituo gani cha runinga kwa sasa nchini, utafahamika kwa jina la 'Kipusa' ambapo sehemu kubwa ya tamthilia hiyo imesharekodiwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MICHARAZO mmoja wa nyota wa kundi hilo Adam Malele 'Swebe Santana' alisema tamthilia hiyo imewashirikisha asilimia kubwa ya nyota za zamani wa kundi hilo.
Swebe aliwataja baadhi ya nyota hao akiwamo yeye ni pamoja na Rashid Mwinshehe 'Kingwendu', Issa Kipemba 'Kipemba', Abdallah Mkumbira 'Muhogo Mchungu' na Ndimbango Misayo 'Thea'.
"Pia igizo hilo limewashirikisha Khadija Yahya 'Davina', Bi. Star, Happiness Stancelaus ‘Nyamayao’, Mzee Chap Chapuo,Davina, Bi Star, Bi Hindu, Mama Nyamayao na wengine," alisema Swebe.
MICHARAZO ilikuwa wa kwanza kudokeza kuwepo kwa mipango ya kurejeshwa upya kwa kundi hilo baada ya kuwafumania Lango la Jiji wakifanya vikao na sasa imethibitika suala hilo ni kweli tupu.
Taarifa zaidi na wasifu wa washriki walioucheza mchezo huo MICHARAZO itaendelea kuwajuza kila mara.

TFF/TWFA kutoa mafunzo maalum Siku ya Wanawake


Mwenyekiti wa TWFA, Linnah Mhando
KATIKA kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani na kudhamini mchango wa wanawake katika michezo Shirikisho la Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) ikishirikiana na TFF itaendesha mafunzo maalum.
Mwenyekiti wa TWFA, Linnah Mhando amesema shirikisho lake kupitia Kamati ya Wanawake ya mpira wa miguu kwa wanawake, wanatambua umuhimu wa siku ya wanawake duniani.
“Mpira wa miguu kwa wanawake ni moja ya michezo inayokuwa kwa kasi katika bara la Afrika na hata hapa nyumbani. Idadi ya wasichana wanoshiriki katika mpira wa miguu imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
Katika kusheherekea  siku ya wanawake duniani mwaka 2014. Sherehe rasmi zitafanyika katika mkoa wa Tanga
TFF /TWFA wanaamini kuwa ili kuwa na kiwango kizuri na maendeleo katika mpira wa miguu wanawake  ni lazima kuanza na vijana wadogo hivyo basi Shirikisho na chama cha mpira wa miguu Tanga limeandaa mafunzo kwa walimu wapatao 30 toka shule15 za mkoa wa Tanga.
Walimu hao watapatiwa mafunzo kwa siku mbili na tarehe 08/03/2014 kutakuwa na Tamasha la Grassroot litakalojumusha jumla ya wanafunzi wapatao 1000 toka shule husika.
Ni matumaini ya shirikisho kuwa mafunzo hayo na tamasha la grassroot litaleta mwamko wa mpira wa miguu katika mkoa wa Tanga na hamasa kwa watoto wa kike,wasichana na kina mama katika ushiriki wa mpira wa miguu wanawake.

TFF kuwaadhibu wawili Twiga Stars

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage. Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.
Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.
“TFF tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza,” imesema taarifa ya TFF.
Twiga Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.

Sikia hii! Mchungaji akataza waumini wake wasivae Ch**pi


UKISIKIA Mwisho wa Dunia haupo mbali ndiko huku, Mchungaji mmoja nchini Kenya amewapiga marufuku waumini wake wa kike kuvaa nguo za ndani waendapo kufnya ibada ndani ya kanisa analoliongoza ili wampokee YESU wakiwa huru.
Mchungaji huyo Mkenya amenukuliwa nchini mwake kuwa waumini wanapaswa kuwa huru kimwili na kiroho wakati a kumpokea Bwana hivyo wanapaswa kutovaa nguo za ndani.
Ebu soma taarifa hiyo hapo nchini uone maajabu ya mwisho wa dunia na wanaojifanya wachungaji wa Kondoo za BWANA.
KENYAN Pastor Orders Female Congregants To Attend Church Without Putting On Bras & Panties For Christ To Enter Their Lives 'Freely'

A Kenyan pastor has ordered his female congregants to go to the church 'free' - That
is without bras and panties for Christ to enter their
lives.

According to kenyan-post.com, Reverend Njohi of the Lord's Propeller Redemption Church in Nairobi reportedly advised female worshippers against
wearing any undergarments to the church, calling them ungodly.

In a meeting chaired by him, a law was passed banning the wearing of inner wears.

Njohi claims that when going to church, people need to be free in 'body' and 'spirit' to receive Christ.

He went ahead to warn members of dire consequences if they secretly put on their inner wears.

Mothers were also advised to do same and check their daughters when coming to church on Sundays so as to receive Christ too.

Duh, Vibaka Nouma kweli wamliza Ally Choki

Ally Choki 'Mzee wa Ambulance' aliyelizwa na vibaka
AMA kweli kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani. Mkurugenzi wa bendi ya muziki wa dansi Extra Bongo Next Level 'Kamarade' 'wazee wa Kimbembe' Ally Choki alijikuta akimwaga machozi baada ya watu wanaodhaniwa kuwa vibaka kujipenyeza wakati wa uzinduzi wa albamu ya 'Mtenda Akitendewa' Februari 22 mwaka huu na kumuibia saa ya silva yenye thamani ya dola 300 sawa na sh.500,000.
Extra Bongo ilizindua albamu hiyo ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki na wadau wa muziki wa dansi ambapo Choki aliingia ukumbini akiwa ndani ya gari la kubeba wagonjwa 'Ambulance' na kulakiwa juu kwa juu.
Choki, alieleza, tukio la kuibiwa lilimkuta wakati akishuka kwenye ambulance ambapo ndani ya kundi la mashabiki waliompokea kulikuwepo na vibaka waliofanikwa kumvua saa hiyo pasipo yeye kujitambua.
"Kwa kweli saa yangu inaniuma sana nililetewa zawadi na rafiki yangu kutoka Qatar lakini ndo hivyo vibaka wameniingiza mjini alisema Choki kwa masikitiko na kuongeza.
"Wakati nimepanda jukwaani ndiyo nikashtukia nimelambwa saa, bahati nzuri simu na vitu vyangu vingine vya thamani nilikuwa nimeviacha kwa mlinzi wangu vinginevyo hali maumivu yangekuwa makali zaidi ya hivi.
Tukio la Choki kuibiwa linakumbusha tukio jingine lililowahi kutokea miaka kadhaa nyuma kwa aliyekuwa rapa wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) Papii Kocha 'Mtoto wa Mfalme' kuporwa cheni na vibaka akiwa jukwaani wakati wa uzinduzi wa moja ya albamu za bendi hiyo katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.
Aidha Choki alisema atatoa zawadi ya sh.300,000 kwa mtu yoyote atakayeweza kufanikisha kupatikana kwa saa hiyo huku akitaka aliyeiba kumrejeshea kiroho safi na atampatia kiasi hicho cha fedha pasipo kufikishwa kwenye vyombo vya dola.
"Nimeamua kutoa zawadi kwa atakayewezesha niipate saa yangu au kwa aliyechukua kuirudisha kwangu, hii ni sababu nilikuwa naipenda sana alieleza.

Samuel Sitta ndiye Mwenyekiti wa Bunge la Katiba

  CCM waridhia awanie uenyekiti Bunge la Katiba
  Samia Hassan Suluhu kuwania umakamu
Mhe Samuel Sitta
WAJUMBE wa Bunge Maalumu la Katiba wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamemaliza ‘mnyukano’ wa muda mrefu wa vigogo wa kuwania uenyekiti wa kudumu wa Bunge hilo, baada ya kutoa baraka zote kwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kugombea nafasi hiyo.

Wakati Waziri Sitta akipewa baraka hizo na wajumbe hao kupitia Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM, Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, ameripotiwa kuamua kutogombea nafasi hiyo.

Pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu, amepitishwa na kamati hiyo kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo kutokea Zanzibar.

NIPASHE lilimtafuta Sitta jana kueleza kupitishwa na chama chake, lakini alisema kuwa hakuwa kwenye mkutano huo hadi mwisho. “Niliingia kwenye kikao na kutoka mapema, sijui kama uamuzi huo umefikiwa,” alisema.

Vyanzo mbalimbali vya NIPASHE kutoka ndani ya kikao hicho vinaeleza kuwa, uamuzi wa kamati hiyo ulifikiwa baada ya kuwaita viongozi hao na kuwahoji kwa nyakati tofauti iwapo wana nia ya kugombea nafasi hizo au la.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Waziri Sitta na Waziri Suluhu, walipitishwa kwa kauli moja kuwania nafasi hizo, baada ya kamati hiyo kujiridhisha kwamba, wamekidhi sifa.

Mbali na Sitta, Suluhu na Chenge, chanzo hicho kilieleza kuwa mwingine, ambaye aliitwa na kuhojiwa na kamati hiyo ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, aliyefahamika kwa majina la Mwajuma Mgeni, ambaye hata hivyo, naye kama Chenge aliamua kutogombea nafasi hiyo.

Kabla ya kamati hiyo kutoa baraka hizo, kiongozi pekee aliyejitokeza hadharani na kutangaza azma ya kuwania nafasi hiyo ni Sitta pekee.

Sitta alisema anataka kuwania nafasi hiyo ili apate fursa ya kutimiza kwa vitendo ndoto ya Rais Jakaya Kikwete ya kuhakikisha Tanzania inapata katiba bora.

Imeelezwa kuwa wajumbe kadhaa walipendekeza jina la Sitta lipitishwe pasipo kuwapo mgombea mwingine, kwa maelezo kuwa wana-CCM wengine waliokuwa wanatajwa, wanaonekana kutokuwa na uwezo wa kulimudu Bunge hilo.

“Tumetoka kwenye kikao cha wajumbe wa CCM na kwa namna ya pekee, imekubalika kwamba Sitta ndiye anayefaa kwa uenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,” kilieleza chanzo kimojawapo kwa sharti la kutokutajwa jina lake gazetini.

“Kama chama kimeonyesha imani yake kwa Sitta, na kwa mujibu wa Sheria, Makamu wake anatakiwa kutoka Zanzibar ambapo jina la Samia Suluhu limepitishwa ndani kwa wajumbe wa CCM,” kilieleza chanzo hicho.

Sitta amekuwa akitajwa ndani na nje ya Bunge Maalum la Katiba, kwamba anafaa kuchukua nafasi hiyo kutokana na rekodi nzuri aliyoiacha alipokuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

ZENGWE LA SERIKALI TATU
Hata hivyo, waliokuwa wanampinga Sitta waliibua hoja kwamba mwanasiasa huyo mkongwe, amekuwa na mwelekeo wa kutaka kuwapo kwa serikali tatu, hoja aliyoipinga mara kadhaa akisema uamuzi wowote kuhusu hatima ya Katiba Mpya na hususani mfumo wa utawala utakavyokuwa, vitaamriwa na Watanzania.

HAKUNA MARIDHIANO
Katika hatua nyingine, matumaini ya kufikia maridhiano yatakayowezesha kupatikana kwa katiba mpya, yamezidi kufifia.

Hiyo ni baada ya wajumbe wa Bunge hilo kutoka vyama vya upinzani na makundi ya kijamii na wale wanaotoka CCM kuendelea kuvutana kuhusu utaratibu utakaotumiwa kupata uamuzi katika vikao vya Bunge hilo.

Katika mvutano huo, wajumbe wa CCM wanataka utaratibu utakaotumiwa kupata uamuzi katika vikao vya Bunge hilo uwe wa kura ya wazi, huku wale wanaotoka katika vyama vya upinzani na wa baadhi wanaotoka katika makundi ya kijamii wakitaka utumike wa kura ya siri.

Msimamo wa wajumbe kutoka vyama vya upinzani na makundi ya kijamii, ulifikiwa kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kikao chake kilichofanyika juzi.

Chanzo chetu kutoka ndani ya kikao cha wajumbe wa CCM zinaeleza kuwa baadhi ya wajumbe walilalamikia kile walichokiita mjadala wa Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalumu kuachwa kuhodhiwa na wapinzani bungeni.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, baadhi ya wajumbe katika kikao hicho walitoa mfano wakisema uundwaji wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalumu, ambao walidai kuwa imeachiwa kuhodhiwa na wapinzani.

Mbunge huyo alieleza pia kuwa wajumbe wengine katika kikao hicho walidai kwamba hata Rasimu ya Kanuni ya Bunge Maalumu ya Mwaka 2014 zimetungwa kwa kuwabeba wapinzani.

Alieleza kuwa kuwa baadhi ya wajumbe katika mjadala huo, walitaka kumjua waliyemuita “mchawi” aliyesababisha hali hiyo.

MKAKATI WA KUTEKA BUNGE
Mtoa taarifa wetu alieleza kuwa baada ya majadiliano yaliyochukua takriban saa sita, hatimaye kikao kilifikia maamuzi mbalimbali, ikiwamo namna wajumbe watahakikisha utaratibu wa kupata uamuzi katika Bunge hilo kwa kura ya siri unadhibitiwa.

Alieleza kuwa jambo lingine, ambalo lilitolewa uamuzi na kikao hicho, linahusu namna ya kumdhibiti mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho.

Chanzo hicho kilisema udhibiti huo utalenga zaidi katika maelekezo yoyote yatakayotolewa na mwenyekiti huyo wakati wa kusimamia mjadala wa rasimu ya kanuni hizo hadi azimio la kuzipitisha litakapotolewa na Bunge hilo.

Kilisema kuwa maamuzi hayo pia yalipinga ushauri uliotolewa na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, wakati akichangia mjadala wa rasimu ya kanuni hizo wiki iliyopita, kwamba ushauri huo hauna maslahi na chama.

Chanzo hicho kilieleza kuwa kikao hicho pia kilipitisha maamuzi ya kujengwa mazingira ya kuahirishwa makusudi kikao cha Bunge cha jana asubuhi, kama ilivyotokea.

Kilieleza kuwa uamuzi huo ulipitishwa ili kuwapa fursa wajumbe wa CCM kuifanya marekebisho rasimu ya kanuni hizo kama wanavyotaka.

NDIYO DHIDI YA SIRI

Chanzo hicho kilieleza pia kuwa uamuzi mwingine uliofikiwa na kikao hicho ulitaka lazima mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo ahakikishe upitishaji wa vifungu vya rasimu ya kanuni hizo unafanyika kwa kura za wajumbe kupaza sauti za ndiyo au hapana.
 

Katibu wa wajumbe wa CCM, Jenista Mhagama, hakupatikana jana kuzungumzia yaliyojiri katika kikao chao cha juzi na hata alipopigiwa, simu yake ilikuwa inaita bila majibu.
 
CHANZO: NIPASHE

Inatisha jamaa afukua kaburi na mwanamke akiwa uchi

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzMYECCwkRKCFGbps0HoMYnLTH_Qnj1FT7Lc8nRmd6SQUU_iopPLSDtZrhMxlJqwdEv1hBiLOV3Fs1G4dPx8oHT59kcCtTbMznrMoHiZBiLDy-JI7LOQzK-Fx1WsVNz5jA8b1Zw9jA7npz/s1600/4680222.jpg
MKAZI wa kijiji cha Ikola  Wilaya ya Mpanda Mkoa  wa Katavi  Richard  Clavery  34 amefikishwa  Mahakamani  katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kujituhuma za kufanya vitendo vya ushirikina  wa kufukua kaburi la mwanamke aliyekufa.
Mtuhumiwa  alifikishwa kizimbani hapo Februari   25 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa   na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka  Godfrey  Luzabila
Mwendesha mashitaka alidai  Mahakamani hapo kuwa  mtuhumiwa  alitenda kosa hilo hapo Februali   18 mwaka huu majira ya saa nne usiku nyumbani kwa  Lenada  Sakafu
Mwendesha mashitaka   Luzabila  aliiambia mahakama kuwa siku  hiyo ya tukio  mtuhumiwa alifika nyumbani kwa Lenana  Sakafu  na kufukua  maiti ya mdogo wake na Lenada  aitwaye Tabu Omera  ambae alikuwa amefarii  siku tatu kabla ya tukio  hili
Aliendelea kuieleza Mahakama   siku hiyo  Lenada  alikuwa nyumbani  kwake pamoja na   majirani na ndugu  zake wakiendelea kuomboleza msiba  ghafla alitokea  mtoto wake aitwaye  Brandina  na kuwaeleza  kuwa ameona mtu nje akifukua kaburi la marehemu   ambae alikuwa amezikiwa  kwenye eneo la nyumba yao
Alieleza ndipo watu hao walipoamua kutoka nje   na kumkuta  mtuhumiwa  Richard  Clavery   akifukua kaburi  hilo huku akiwa  amevua nguo zake zote  ambazo alikuwa amezitundika kwenye msalaba  wa kaburi  hilo  na walipomsemesha mtuhumiwa  alijifanya kupandisha majini
Mtuhumiwa  baada ya kusomewa mashitaka  alikana   na Hakimu Mkazi Mfawidhi  Chiganga Ntengwa aliharisha kesi hiyo hadi hapo machi 6 na mtehumiwa alipelekwa rumande  baada ya kushindwa kutimiza masharti ya mdhamana ambapo alitakiwa adhaminiwe na mtu mmoja kwa  dhamana ya shilingi milioni  moja