STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, December 3, 2013

Dk Asha-Rose Migiro aula, awa Mbunge

Dr. Asha-rose Migiro 
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.
Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

Wasauzi kuifuata Tanzanite Alhamis


KIKOSI cha Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 dhidi ya Tanzania (Tanzanite) kinatua nchini Alhamisi (Desemba 5 mwaka huu).

Afrika Kusini ambayo itafikia hoteli ya Sapphire itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) itatua saa 8 kamili mchana kwa ndege ya South Africa Airways.

Mechi hiyo itachezeshwa na refa Nabikko Ssemambo kutoka Uganda wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Gebreyohanis Trhas kutoka Ethiopia. Waamuzi wengine ambao pia wanatoka Uganda ni Nakitto Nkumbi na Irene Namubiru.

Kamishna wa mechi hiyo ni John Muinjo kutoka Namibia. Muinjo pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Namibia (NFA) na mjumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Viingilio katika mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) kuanzia saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange, sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.

Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.

Aboubakar Mlawa aula UVCCM awa kamanda Kisarawe

Kamanda wa  Mpya wa umoja wa Vijana CCM wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Aboubakary Mlawa akisimikwa kuwa Kamanda wakati wa sherehe maalum iliyofanyika katika makao makuu ya ccm Wilayani Kisarawe hii ni moja ya njia ya  kuhamasisha katika utekelezaji wa ilani ya chama kwa vijana akiwa ameshika mkuki na ungo pamoja na kigoda cha asili
Mbunge wa jimbo la Kisarawe  Suleiman Jaffo m akiteta jambo na kamanda mpya wa Vijana Wilayani Kisarawe Aboubakary Mlawa kulia mara baada ya kuapishwa kuwa Kamanda mpya wa Vijana katika wilaya hiyo huku akiwashukuru vijana wa wilaya hiyo kwa ushirikiano waliompa kwa kumchagua kuwa kamanda huku akitoa maelezo yake kwamba umoja ni nguvu tutatekeleza ilani ya chama vijana ndio ngao yetu kwa Taifa hili.
Kamanda wa Vijana UVCCM wilaya ya Kisarawe Aboubakary Mlawa akiapa kuwa kamanda wa vijana kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia novemba 28 mwaka huu,nyuma kulia ni mwenyekiti wa UVCCM taifa Mh Sadifa Hamisi na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Mh Habib Nyundo wakishuhudia.

Kivumbi cha Kawambwa Cup kuanza rasmi kesho Bagamoyo

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjMGF2vNfT2sP-JfQ9GM5IgSYh0Zm4Lm1ZWlxhKbi8LOulbpyI5xezNnOhI7J4M3C7YMjHisVPcBPQkdNf5fSw-Ygj9J_qO5aIAM8pDE9pz5YAoxIkqGoRji3vBhPRsmTpV0i6uH2U8X_M/s400/1.jpg
FAINALI za mashindano ya soka katika Jimbo la Bagamoyo maarufu 'Kombe la Kawambwa' zitaanza rasmi kesho kwenye viwanja vinne vya Mwanakalenge, Vigwaza, Karege na Magereza - Kigongoni mjini humo.
Timu 16 zimetinga hatua hiyo ya fainali kati ya 72 zilizoshiriki mashindano hayo ngazi ya kata huku Majengo Stars wakitwaa ubingwa wa Ngao ya Hisani baada ya kuwafunga kwa matuta mabingwa watetezi, Beach Boys FC katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano hayo uliochezwa kwenye Uwanja wa Mwanakalenge mjini Bagamoyo juzi.
Akizungumza katika ufunguzi wa mashandano hayo makubwa mjini humo, ambayo mwaka huu yanafanyika kwa mara ya nane tangu yaanzishwe 2006, Mkuu wa Wilaya hiyo, Ahmed Kipozi alisema mashindano hayo yatarejesha heshima ya soka katika wilaya hiyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla kwa vile yatazalisha vijana wengi wenye vipaji.
Mjumbe wa Kamati ya Mashindano hayo, Masau Bwire alisema Dk. Shukuru Kawambwa, ambaye ni Mbunge wa jimbo hilo (CCM) na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi tayari ameshagawa jezi seti moja, mipira na fedha za usafiri wakati wa mashindano kwa kila timu inayoshiriki fainali hizo mwaka huu.
Bwire, ambaye pia ni msemaji wa kamati hiyo, alizitaja baadhi ya timu zilizoingia katika hatua hiyo kuwa ni pamoja na Majengo Stars, Bongororo FC na Maji Coast za kata ya Magomeni.
Kata ya Dunda itawakilishwa na Beach Boys FC na Mwambao FC wakati Muungano FC na Buyuni FC zitaiwakilisha Kata ya Vigwaza huku Vijana Stars na Balack Rhino FC zikitoka Kata ya Zinga.
Timu nyingine na kata zinakotoka kwenywe mabano ni Tungutungu FC, Kegere United FC na Udindivu FC (Kegere), Kongo FC na Yombo FC (Yombo).

Yaya Toure ndiye Mchezahi Bora Afrika wa BBC

KIUNGO nyota wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure amechaguliwa kuwa mchezaji bora Afrika wa tuzo ya BBC 2013.
Toure amenyakua tuzo hiyo akiipokea toka kwa Mzambia Christopher Katongo aliyeinyakua mwaka jana.
Kiungo huyo ametwaa tuzo hiyo kwa kuwapiku Pierre-Emerick Aubameyang, Victor Moses, John Mikel Obi na Jonathan Pitroipa .
KUTOKA KUSHOTO; AUBAMEYANG, PITROIPA, OBI, MOSES NA YAYA.
Yaya mwenye miaka 30, ameiambia BBC kuwa: “Nimeteuliwa kwa miaka minne bila ya kushinda, safari hii ni mara ya tano na nimeshinda, ni kitu cha aina yake.”
 “Nina furaha kubwa kufanikiwa kushinda tuzo hii kubwa na ninatoa shukurani zangu kwa waandaaji.

"Najua kuna wachezaji wengi bora barani Afrika mfano kama Aubameyang, Pitroipa, Mikel, Moses, Salomon Kalou, Gervinho na wengine wengi lakini leo nimeshinda.”

Yaya pia alilisifia bara la Afrika kwa kuendelea kuzalisha vipaji na mpira wake kuendelea kupiga hatua.

Buku tu kuziona Tanzanite, Sauzi Afrika

Tanzanite
MASHABIKI watakaoshuhudia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini watalipa kiingilio cha sh. 1,000.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano hiyo itachezwa Jumamosi (Desemba 7 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Kiingilio cha sh. 1,000 ni kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na orange. Viingilio vingine kwa mechi hiyo vitakuwa sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A watalipa sh. 10,000.
Tanzanite chini ya Kocha Rogasian Kaijage inaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na ule wa Taifa kujiandaa kwa mechi hiyo. Kambi ya Tanzanite hivi sasa imehamia Msimbazi Hotel kutoka Ruvu mkoani Pwani.