STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, June 11, 2013

MABONDIA WA JIJI DAR, MORO KUPAMBANA JUMAPILI 

KING CLASS MAWE 

Patrick  Kavako'Baunsa'





 

 

 

 

 

 

 

Bondia  Patrick Anthony Kavako 'Baunsa' wa Morogoro  ametamba kumsambalatisha Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mpambano wao wa raundi nane utakaofanyika siku ya jumapili june 16 katika ukumbi wa panandi panandi uliopo Ilala Bungoni Dar es salaam

Akizungumzia mchezo huo Kocha wa Kimataifa ambaye ni mratibu  wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa mpambano huo ni wa kukata na shoka ambao si wa kukosa kwani kila mmoja amejitahalisha kivyake hivyo wasubili tu siku ya mpambano huo

Unajua morogoro na Dar es salaam ni mahasimu katika michezo yote ukiangalia na sasa wamekutanishwa vijana katika masumbwi hivyo kila mmoja anaitaji ushindi ili ajiongezee rekodi yake kwani 'King Class Mawe' ato kubali kupigwa na Kavako ato kubali kabisa kupoteza mpambano wake kiraisi kwani na yeye anaitaji ajulikane katika ulimwengu wa masumbwi na kuiperekea sifa morogoro kama ilivyo kwa mabondia wengine wanao tamba mkoani hapo 
Mpambano huo ulioratibiwa na Kinyogoli Fondition kwa kushlikiana na PST itakuwa chachu kwa vijana kuendelea kuupenda na kuucheza mchezo huo unaopendwa na wengi nchini
mbali ya mpambano uho kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka bondia Abuu Mtambwe ataoneshana umwamba na Kassim Gamboo na Bondia mkongwe kabisa Yohana Robart atamenyana na Mussa Sunga
 
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini,Rajabu Mhamila ‘Super D’ ametoa DVD mpya 3 kwa ajili ya mafunzo ya mchezo wa ngumi ndani yake kukiwa na clips za mabondia  wanaofanya vizuri Tanzania kama Thomas Mashali vs Fransic Cheka na mambondia wengine mbalimbali

CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo zitakuwa chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi wakiwa wanangalia live mana DVD hizo zina maelekezo ya sheria mbalimbali ambazo zinatumika katika masumbwi

DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani kwingine ni GYM ya Amana iliyopo Ilala au unaweza kuwasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata DVD hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo

Mbali ya kupatikana katika maeneo hayo pia
 
katika mchezo mbalimbali ya masumbwi kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo
huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo katika CD na DVD
hizo ni ya Kalama Nyilawila ,Japhert Kaseba,Rashidi Matumla, Hassani Matumla,Thomas Mashali Dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na
Francis  Miyeyusho,Japhert Kaseba na Maneno Oswald, Said Mundi na King Class Mawe. 
 
 mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali 
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .

APPT Maendeleo yaifagilia Rasimu ya Katiba



http://www.thisday.co.tz/media/picture/large/Peter%20Kuga%20Mziray-%20%20APPT%20Maendeleo.jpg
Rais wa APPT Maendeleo, Peter Kuga Mziray
WAKATI Watanzania wa kada mbalimbali wakiendelea kuchambua na kutafakari juu ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyozinduliwa hivi karibuni Chama cha African Progressive Party of Tanzania (APPT Maendeleo) kimeibuaka na kuwataka waipokee kwa mikono miwili kwani rasimu hiyo imekuja kutatua kero zao.
Kauli hiyo imetolewa na Rais Mtendaji wa APPT Maendeleo Peter Kuga Mziray wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii leo jijini Dar es Salaam.
Mziray alisema tangu rasimu hiyo izinduliwe rasmi 3/6/2013 kumekuwepo na mitazamo mbalimbali ya kuipongeza na kuipinga kwa baadhi ya watu ambao kimantiki wanaipinga  ni watu wenye  malengo yao ya kuwa Marais wa Tanzania jambo ambalo linaelekea kufa.
Alisema Watanzania hasa wale wa Bara wamekuwa na kilio cha miaka mingi cha kuhitaji uwepo wa Tanganyika kama ilivyo Zanzibar lakini hawakusika jambo ambalo kwa sasa limepatiwa muafaka na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Rais Mtendaji alisema mapendekezo ya Tume ni mazuri kwa asilimia kubwa kwani yamezingatia maoni ya watu wengi ambao walikuwa wakihitaji rasimu ya katiba iwe hivyo bila kuogopa vivuli vya baadhi ya watu ambao wamejionyesha dhahiri kutokubaliana nayo.
“Kimsingi naunga mkono mapendekezo ya Tume kwani yamezingatia mahitaji ya Watanzania wote wa Bara na Visiwani na pia yana nia ya kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kudumu bila mitafaruku,” alisema.
Alisema wapo watu wameibuka na kusema Serikali tatu zitakuwa ni kuongeza gharama kubwa kuziendesha jambo ambalo sio kweli kutokana na ukweli kuwa kila nchi itakuwa ikitumia rasilimali zilizopo katika upande wake na kuchangia Serikali ya Muungano ambayo haitakuwa kubwa.
Mziray alisema mapendekezo ya Tume yameaanisha mambo muhimu katika muungano ambayo yapo saba jambo ambalo ni ishara tosha kuwa hakukuwa na serikali kubwa kama inavyofikiriwa.
Mambo ayalitajwa kuhusika na muungano ni pamoja na katiba na mamlaka ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ulinzi na usalama wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, uraia na uahamiaji, sarafu na benki kuu, mambo ya nje, usajili wa vyama vya siasa na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo na kodi yatokanayo na mambo ya muungano.
Aidha alisema rasimu hiyo imeenda mbali pale ilipoweka wazi kuwa ili mgombea wa Urais atangazwe anapaswa kushinda kura ambazo zitampatia 50 ya kura zote, pamoja na wagombea wa Urais kupata haki ya kuenda mahakamani kupinga matokeo.
Rais Mtendaji huyo pia alisema kupunguzwa kwa madaraka na kuwajibishwa kwa wabunge ambao hawafanyi kazi katika majimbo yao ni jambo muhimu ambalo Tume inapaswa kupongezwa kutokana na umuhimu wake hasa ukizingatia kuwa baadhi ya wawakilishi wa wananchi wamekuwa wakiishi mijini zaidi.
Maziray alisema pamoja na mapendekezo hayo ya tume ni vema mabaraza ya katiba yakapendekeza adhabu ambazo zinaweza kutolewa kwa utoro unaofanywa na wabunge jambo ambalo linaweza kurejesha hadhi ya Bunge ambalo kila siku linaonekana lipo wazi.
Kwa upande mwingine Mziray ameiomba Serikali kuanza mchakato wa uwepo wa Katiba ya Tanganyika ili iweze kuendana na mchakato wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo litarahisisha uwepo kwa serikali hiyo.
Alisema bila kuwepo kwa Katiba ya Tanganyika itakuwa ngumu kutekeleza mapendekezo ya Tume ambayo yanahitaji kuwepo kwa Serikali tatu ambazo ni Tanganyika, Zanzibar na Tanzania.
Rais Mtendaji alisema mchakato huo hautakuwa na kazi ngumu kwani ukweli unaonyesha kuwa maoni mengi ambayo yapo katika rasimu na yalioachwa yalikuwa yanahusu serikali ya Tanganyika.

Vita ya Ally Choki, Asha Baraka yafika pabaya


MKURUGENZI wa Extra Bongo Ally Chocky ametoa kauli nzito kuhusu waajiri wake wa zamani, Asha Baraka na Baraka Msilwa.

Katika maongezi yake  Chocky alisema katika watu asiowapenda duniani ni Asha Baraka (Mkurugenzi wa ASET) na Baraka Msilwa (Mwenyekiti wa ASET). Asha Baraka na Baraka Msilwa ni mtu na kaka yake.

Kiongozi huyo wa Extra Bongo akaenda mbali zaidi kwa kusema: “Nikifa leo hii Asha Baraka na Baraka Msilwa wasije kwenye mazishi yangu, na kama watanitangulia wao na mimi sitakwenda kwenye mazishi yao.

“Nina uhakika leo hii nikipata matatizo au nikifa Asha na Msilwa watafurahi, sasa kuna haja gani ya watu kama hao kuja kwenye mazishi yangu.

“ASET ni kama simba wako tayari kukutafuna hadi macho, nimetafakari kwa muda mrefu sana nimevumilia mengi sana lakini nimeshindwa na sasa natamka rasmi, Nikifa wasinizike.”

Chocky ameorodhesha sababu nyingi sana za kufikia hatua hiyo lakini miongoni mwa sababu zake ni hizi tatu:

Kwanza kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari, pili Aset kukataa kurudisha pesa za Miraji Shakashia na tatu ni ASET kutothamini michango ya wasanii walioizalishia pesa nyingi.

Chocky ansema kitendo cha Aset kumpeleka mahakamani kumdai gari ambalo walimpa mwenyewe kilimkera sana.

“Mtu anapokupeleka mahakamani maana yake ni kwamba yupo tayari hata ufungwe, ukifungwa maana yake ni kila kitu kwenye maisha yako kinaharibika.

“Gari walinipa wenyewe na maandishi yapo kwamba nikimaliza mkataba wangu gari litakuwa la kwangu.

Lakini badala yake wakanigeuzia kibao na kwenda kunidai mahakamani kwamba nimeiba gari.

Kuhusu Shakashia, Chocky amesema mwanamuziki huyo alichukua shilingi milioni tano za Extra Bongo ili ajiunge nayo na akasaini mkataba wake.

“Lakini badala yake Shakashia akaingia mitini na pesa zetu, Aset wakasema watazirudisha wao na sasa wanakuja na hadithi mpya.

“Wanasema hawawezi kurudisha hizo pesa eti kwa vile wananidai, wanasahau kuwa mkataba wa Shakashia ni kati yeke na Extra Bongo na sio Ally Chocky.

“Hata kama kipo wanachonidai hiyo ni kati ya Chocky na Aset na haiingii akilini kuliingiza suala la Shakashia ndani yake.

“Huu ni utapeli na inatoa picha kuwa Aset walimtumia Shakashia kufanya utapeli huu, lakini wajue kuwa mwisho wa siku atakayeathirika ni Shakashia mwenyewe,” alisema Chocky.

Kuhusu kutothamini wasanii waliozalishia pesa nyingi kampuni, Chocky anasema wasanii walipota ASET na kuizalishia pesa hawana chochote walichopewa kulingana na thamani ya kile walichokizalisha. “Sio pesa tu bali hata heshima pia hakuna,” alifafanua Chocky.

Chocky akazama zaidi na kuwataja wakongwe kama Shem Karenga na Kasongo Mpinda ambao waliwahi kufanya kazi katika familia ya kina Asha Baraka kupitia bendi za MK Group na MK Beats.

“Wako wapi Kasongo Mpinda na Shem Karenga, Kasongo aliwatengenezea pesa nyingi kupitia MK Group “Ngoma za Magorofani” huku Shem Karenga  akiwatengenezea utajiri katika MK Beats “Tukunyema”.

“Lakini hebu tujiulize wako wapi hawa wazee na wana kipi cha kujivunia?” alihoji Chocky.
 
 Haikuishia hapo, tuliamua kumpigia Asha Baraka ambaye naye alikuwa na yake ya kujibu kuhusu  mapigo ya Chocky.

Asha Baraka amesema hayo ni mambo ya kike na kwamba kuzikana si tija.

Asha Baraka akasema: “Hata mimi sina mpango wa kwenda kwenye mazishi yake na yeye pia asije kwenye mazishi yangu.

“Hivi kuzikana ni nini? Wazazi wangu walifariki na Chocky hakuja kuzika, kilipungua nini? Halafu mi nikifa sitaona na yeye akifa sitaona kwahiyo hiyo siyo ishu, wamanyema wenzangu watatosha kunizika hata wasanii wote wasipokuja achilia mbali huyo Chocky.

“Nilimzikia wazazi wake na hakuliona hilo kwahiyo hata tusipozikana hakipungui kitu.

“Chokcy tunamdai gari na pesa shilingi milioni 13, kwenda mahakamani ni sehemu ya kudai haki na yeye kama anaona amedhulumiwa kuhusu pesa za Shakashia basi aende mahakamani.”

Asha Baraka alimtaka Chocky aelewe kuwa baadhi ya wasanii wa Twanga ni virusi na watammalizia pesa zake bure.

“Wako wasanii wamelelewa vizuri, wamefanyiwa mengi na Twanga na wanaelewa utu kwahiyo akijipendekeza kwao atapoteza pesa zake bure.

“Hao ni virusi wetu, wanatuletea taarifa zote za kila mtu anapotaka kuwachukua.


Asha Baraka amesema kama ni roho mbaya Chocky ndio anaoongoza kwa roho mbaya.

“Alikaa yeye na kamati yake yenye wakiwemo mpaka wafanyakazi wa umma na kuzoa wanamuziki wa Twanga”

Anawataja wasanii wa Twanga waliowahi kuchukuliwa na Extra Bongo ni pamoja na Ferguson, Rogart Hegga, Hosea, Otilya, Nyamwela, Danger Boy, Aisha Madinda, Maria Soloma, Subrina pamoja na Kanuti ambaye baadae alirudisha pesa zao na kubakia Twanga.

Asha Baraka anawataja wasanii wengine wenye damu ya Aset ambao wako Extra Bongo ni Ephraim Joshua, Martin Kibosho, Athanas, Banza Stone na yeye mwenyewe Chocky.

“Kwa mfumo huo utaona wazi kuwa Extra Bongo inapumua kwa nguvu ya Aset lakini sisi hatujasema kitu, kama ni kutoa kauli ya kutozikana basi sisi ndio tulipaswa kuwa wa kwanza,” alifafanua Asha.

“Tunajua pia kuwa Chocky alihusika kushawishi usajili wa Chaz Baba Mashujaa Band akiamini kuwa kwa kuondoka Chaz Twanga itakufa,” aliongeza

Asha Baraka amemtaka Chocky aonyeshe mfano wa namna ya kulea wasanii kwa kuwapa maisha mazuri wanamuziki waandamizi kama Banza na Rogart.

“Asiangalie mambo ya Aset, ajitazame yeye anaishi vipi na Banza anaishi vipi, badala ya kutoa milioni tano kumnunua Shakashia, angemnunulia japo Corola Banza au Rogart.

“Chocky aitishe mkutano wa waandishi wa habari halafu mimi na yeye twende na mikataba ya wasanii inayoonyesha mishahara na marupurupu tuone nani analea vizuri wasanii.

“Mimi nilifanya kazi Bima na sijajengewa nyumba wala kununuliwa gari, silalamiki kwa kuwa haikuwa sehemu ya makubaliano yetu.

“Kama Chocky anadhani muziki unalipa kiasi cha kumnunulia kila mtu gari na nyumba basi atuonyeshe mfano kupitia Extra Bongo.

“Kila baya linalomfika basi mchawi ni Aset, mbona mimi naumwa mguu na sijawahi kusema ni Chocky?

“Chocky akapime afya yake apate ukweli, tunajua rekodi ya sehemu alizopita, sasa asije akadondoka akasema ni Aset …akapime kwanza” alimaliza Asha Baraka.
 
MPEKUZI HURU

Bosi Masinde 'kulifufua' kundi la Shirikisho Msanii Afrika


Bosi Masinde katika pozi
MUIGIZAJI mkongwe aliyewahi kutamba na michezo ya kwenye runinga kupitia kituo cha ITV anayekimbiza kwa sasa kwenye filamu, Richard Mshanga 'Bosi Masinde' amesema anafikiria kulifufua upya kundi la Shirikisho Msanii Afrika baada yha kundi hilo kusambaratika kitambo.
Masinde, alisema wazo la kulirejesha upya kundi hilo katika 'uhai' baada ya kuzimika miaka kadhaa iliyopita inatokana na ushawishi anaopata kwa baadhi ya wasanii wenzake wa zamani pamoja na mashabiki ambao walikunwa na maigizo ya kundi hilo wakati likiwa kileleni.
Akizungumza na MICHARAZO, Masinde alisema Shirikisho Msanii Afrika halijafa kimoja, ila liligawanyika pande mbili mara baada ya yeye kujiweka kando na kulifanya kundi hilo lizimike tofauti na iliovyotamba enzi zake likitesa kituo cha ITV.
"Nimekuwa nikiombwa na baadhi ya wasanii nami nafikiria kama nirejeshe majeshi na kulifufua upya kundi hilo ambalo lifukuzana sambamba na Kaole Sanaa kama fitina hazijaingia na kuilisambaratisha," alisema Masinde.
Mshindi huyo wa tuzo ya Muigizaji Bora wa Mwaka wa ZIFF-2012, alisema anajihisi ana wajibu wa kuwarejeshea mashabiki wao burudani kama walivyoipata kupitia michezo kadhaa ilizotamba enzi zao kiasi cha kundi hilo kuwa 'gumzo' la jiji mbali na kuibua nyota kibao.
Enzi za kundi hilo lilitamba na michezo kama 'Tamu Chungu', 'Gumbizi', 'Hatia', 'Dumaza' na mingine huku likiwaibua mastaa wa sasa wa filamu nchini kama akina Amanda, Mama Kawele, Bakar Makuka, Aunty Ezekiel, Nyatawe na wengineo.

Machava yapeta RCL, kipute cha raundi ya 3 wikiendi hii


Na Boniface Wambura
MICHEZO ya kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zitachezwa Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) wakati za marudiano zitachezwa Jumatano ya Juni 19 mwaka huu.

Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Juni 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za michezo iliyopita na kufanya uamuzi mbalimbali ikiwemo mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars na Machava FC ambayo haikuchezwa.

Machava FC ambayo ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Moshi kwa mabao 2-0 inaendelea katika hatua ya tatu kwa vile haikuhusika katika kukwamisha mchezo wa marudiano uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kiliuhamishia mchezo huo kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa kinyume na maelekezo ya Kamati ya Mashindano ya TFF. Kamati katika kikao chake cha awali iliekeleza kuwa mechi zote za RCL zitachezwa makao makuu ya mikoa isipokuwa kwa Morogoro ambapo timu ya Techfort FC iliruhusiwa kutumia Uwanja wa CCM Mkamba mjini Ifakara.

Hivyo timu nane zilizofuzu kucheza raundi hiyo ni Friends Rangers ya Dar es Salaam, Kariakoo ya Lindi, Katavi Warriors ya Katavi, Kimondo SC ya Mbeya, Machava ya Kilimanjaro, Njombe Mji ya Njombe, Polisi Jamii ya Mara na Stand United FC ya Shinyanga.

Wakati timu nyingine zimefuzu kwa kushinda mechi zao za raundi ya mbili, Njombe Mji imeingia hatua hiyo kwa kuwa timu yenye uwiano mdogo wa kufungwa (best looser) katika hatua ya pili.

Katika hatua hiyo mechi ni ifuatavyo; Kariakoo vs Friends Rangers, Machava FC vs Stand United FC, Polisi Jamii vs Katavi Warriors, na Kimondo SC vs Njombe Mji. Timu zilizoanza kutajwa ndizo zinazoanzia nyumbani.

Vilevile Kamati ya Mashindano imeagiza Kamishna wa mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars vs Machava FC, Mwijage Rugakingira wa Tanga ambaye alikwenda Uwanja wa Mgambo badala ya Uwanja wa Jamhuri kinyume na maelekezo ya TFF aondolewe kwenye orodha ya makamishna.

Pia waamuzi wa mechi hiyo ambao nao walikwenda Mpwapwa badala ya Dodoma Mjini wamepelekwa Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kutokana na tukio hilo.

Kamati ya Mashindano imekumbusha kuwa RCL ni mashindano yanayosimamiwa na TFF, hivyo maelekezo yoyote kuhusiana na mashindano hayo pia yatatoka TFF na si mahali pengine popote. Hivyo, msimamizi wa kituoa hana mamlaka ya kubadili uwanja.

Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.

PARTY YA LADY JAYDEE 'ANACONDA' IJUMAA HII SI YA KUKOSA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjzSsnvfgzuiBzhvHAdJtj8JnKhjDIlp_mjeidbuAC2oLPoUAJsBO5WWkH2NAAC3LvI41jBB_cOBUuoOWCo1PVHKxiIIEQLtxWNwtFt9M5W7bZ9jxlLzb9NAErM32e1Z_DaPD-Jn3upqoE/s1600/Jaydee+Balance.jpg

Waaljeria kuzihukumu Stars, Ivory Coast

Kocha Kim Poulsen akiwoanyesha kwa vitendo wachezaji wa Stars

Na Boniface Wambura

SHIRIKISHO la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Algeria kuchezesha mechi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayofanyika Jumapili saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kundi C kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil wataongozwa na Charef Mehdi Abid atakayepuliza filimbi. Atasaidiwa na Hamza Hammou na Bouabdallah Omari wakati mezani atakuwa Sofiane Bousseter.

Abdi na wezake wanatarajiwa kutua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir. Mtathmini wa waamuzi ni Athanase Nkubito kutoka Rwanda ambaye atatua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya RwandAir.

Kamishna wa mechi hiyo ni Bernard Mfubusa kutoka nchini Burundi ambapo atawasili nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Maofisa wote hao wa mechi hiyo watarejea makwao Jumatatu (Juni 17 mwaka huu).