STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 28, 2016

United? Mawe subiri mshtukizwe na Zlatan Ibrahimovic


http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2014/0605/fc_ibrahimovic_rh_1296x729.jpg&w=738&site=espnfcMSHAMBULIAJI wa KImataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amekuwa akihusishwa na kutaka kutua Manchester United ili kuungana na Kocha wake wa zamani, Jose Mourinho, lakini wakala wake wamesema klabu atakayojiunga nayo itashangaza wengi.
Wakala wa mchezaji huyo, Mino Raiola, alisema Straika huyo ambaye mkataba wake na PSG imeisha hakuna anayejua atatua wapi na hivyo mashabiki wasubiri kushtukizwa tu.
Nahodha huyo wa Sweden mwenye miaka 34, kwa sasa anaendelea na maandalizi ya kuiongoza timu yake katika michuano ya Fainali za Kombe la Ulaya itakayoanza Juni 10 nchini Ufaransa.
"Sidhani kama atajiunga na United, na wala hakuna anayelala Sweden kwa sasa hakuna anayejua kitakachotokea," alisema Raiola.
Wakala huyo alisema bila shaka mwisho wa yote watu watashangazwa na maamuzi ya mkali huyo kwa klabu atakayojiunga nayo kwa msimu ujao.
"Bado hatuajamua, lakini itashangaza wengi mwishowe. Watu wanazungumza kuhusu United, ila ukweli utafahamika tu na ndio maana hatusemi mengi kwa waandishi wasubiri waone wenyewe," alisema wakala huyo.

Mascherano, Higuain wajipa tumaini kwa Messi Copa America 2016

http://static.dnaindia.com/sites/default/files/styles/half/public/2016/05/28/465312-messi-injury.jpg?itok=WVjhADzW
Messi akisaidiwa kutoka uwanjani jana Ijumaa alipoumia katika mechi yao ya kirafiki dhidi ya Honduras
HOFU tupu. Kuumia kwa nyota wa Argentina, Lionel Messi kumezua hofu miongoni mwa wachezaji wa timu yake ya taifa inayojiandaa na fainali za michuano ya  Copa America zitakazoanza mwezi ujao nchini Marekani.
Javier Mascherano na Gonzalo Higuain kwa nyakati tofauti wamenukuliwa wakisema kuwa wana matumaini nahodha wao huyo, Lionel Messi atakuwa fiti kabla ya kuanza kwa fainali za Copa America 2016.
Messi aliumia jana Ijumaa katika mechi za kirafiki ya kimataifa dhidi ya Honduras na kusababisha hofu kubwa kwa wachezaji, mashabiki wa Argentina.
Mwanasoka huyo bora wa dunia, alitolewa Uwanjani baada ya kudondoka vibaya na kujiumiza mgongo na mbavu zake kwenye mjini San Juan waliposhinda bao 1-0.
Kocha Mkuu wa Argentina, Gerardo Martino alisema yu tayari kupokea taarifa zozote juu ya majeraha ya Messi, wakiwa wanakabiliwa na mchezo wa ufunguzi dhidi ya watetezi Chile Juni 6.
Hata hivyo mchezaji mwezake wa Barcelona Javier  Mascherano amesema anatumaini Messi atapona haraka na kurejesha Uwanja kwa ajili ya michezo ya Copa America.
Kauli kama hiyo ilitolewa pia na mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo wa Honduras, Gonzalo Hiuguain, alisema anaamini tatizo lililompata nyota wao halitakuwa kubwa kiasi cha kumkosa kwenye michuano hiyo migumu.

Spurs yakimbilia Wembley kwa Uefa Champion League ijayo

https://static.guim.co.uk/sys-images/Sport/Pix/columnists/2015/1/28/1422488355275/tottenham-010.jpgKLABU YA Tottenham Hotspur imetangaza kuwa itacheza mechi zake za Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani kwenye Uwanja wa Wembley.
Spurs ipo katika maandalizi ya kuukarabati Uwanja wao wa White Hart Lane, hivyo imeona ni vema mechi zake za UEFA ikacheza. katika Uwanja huo wa Taifa wa Uingereza wa Wembley.
Timu hiyo iliyomaliza Ligi Kuu ya England msimu huu kwa kushika nafasi ya tatu imethibitisha taarifa hizo leo Jumamosi kwa sababu ya upishaji wa matengenezo na upanuzi wa uwanja wao.

Chama cha Soka cha Uingereza (FA) kimewapa ofa pia timu hiyo kucheza mechi zao zote za Ligi Kuu za nyumbani na na zile michuano mingine ya makombe ya Uingereza kwenye Uwanja huo wa maarufu wa Wembley.

'Juventus? Hapana Dani Alves hajasaini bhana!'

http://static.pulse.ng/img/football/origs4099488/8810481433-w980-h640/danialves-cropped-nghtlocydwb61j2jec4boxnqp.jpgWAKALA wa beki kisiki wa Barcelona, Dani Alves amekanusha taarifa kuwa mteja wake amesaini mkataba wa awali na Juventus, japo amekiri kuwa mabingwa hao wa Italia na klabu nyingine zinamwinda mchezaji huyo. 
Vyombo vya habari nchini Hispania viliripoti juzi kuwa beki huyo wa Barcelona anatarajiwa kuondoka baada ya kutimukia timu hiyo kwa miaka nane na kwenda Turin kwa mkataba wa miaka mitatu. 
Hata hivyo, wakala wake ambaye pia amewahi kuwa mke wake, Dinorah Santa Ana da Silva alikanusha taarifa hizo akidai hazina ukweli wowote. 
Dinorah aliongeza kuwa hakuna klabu yoyote ambayo Alves aliyosaini nayo mpaka sasa kwani amehamishia nguvu zake zote katika timu ya taifa ya Brazil ambayo inakabiliwa na michuano ya Copa America inayotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao. 
Wakala huyo aliendelea kudokeza kuwa, ni kweli amekutana na Juventus lakini sio wao peke yao bali ameshakutana pia na klabu nyingine, ila hakuna dili lolote lililoafikiwa mpaka sasa.

Kocha Benitez akomaa na Newcastle United 'mchangani'

Benitez Akisaini Mkataba huo wa kumweka Newcastle United Miaka 3Wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari juu ya kuongeza Miaka 3 kuifundisha Klabu hiyo ya Newcastle UnitedKwenye Mkutano na Waandishi huko St. James Park
KOCHA Rapa Benitez amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kuendelea kuinoa Newcastle United licha ya klabu hiyo maarufu England kushuka daraja msimu huu.
Benitez alisaini mkataba huo baada ya mkataba wake wa muda mfupi wakati akipambana kuiokoa Newcastle isizame kumalizika. Kocha huyo ameahidi kuirejesha timu hiyo Ligi Kuu ya England akiamini alicheleweshwa kukabidhiwa timu wakati ikiwa na hali mbaya. VIjana hao wa Benitez walimaliza msimu kwa kutoa kipigo kitakatifu kwa Tottenham Hotspur na kuinyima nafasi ya kumaliza ikiwa ya pili na badala yake kuwaacha mahasimu wao wa London ya Kaskzini, Arsenal wakiibamba nafasi hiyo nyuma ya Leicester City walikuwa mabingwa wapya wa England.

Simba jeuri bwana, yamlipa Mosoti na kuwaokoa Wakimataifa

http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/musoti.jpg
Mosoti
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijkioCMLTxbWmSc7Or2shgbE674AVVOh8YREydnX4Y5pvner4ydWT610U0c1usyjR8IfbiAf_g6S3i-E4u_ylGIZCrsSr_-gUGX0_JaOfiXiQo9pb9KI0WWeEJyEj_SnYTR4TR7HnQCUGb/s1600/HANS+POPPE.jpg
Zakaria Hanspoppe
YAEPUSHA ugomvi. Klabu ya Simba imemaliza utata baada ya kumlipa chake, aliyekuwa beki wao wa kati, Mkenya Donald Mosoti na kujiepusha kushushwa daraja na pia kuikoa Tanzania isifungiwe na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).
Simba imemlipa Mosoti fedha zake za malimbikizo ya usajili na fidia nyingine zinazokaribia Sh Milioni 64.2 Mei 19 mwaka huu ikiwa ni wiki moja na ushei kabla ya siku ya mwisho waliyopewa na FIFA kabla ya kuchukuliwa hatua za kukiuka maamuzi ya Baraza la Usuluhishi la klabu Shirikisho hilo la Dunia.
Kabla ya Simba kulipa fedha hizo ambazo Mosoti amethibitisha kupata taarifa mapema wiki hii, Yanga kupitia Msemaji wake, Jerry Muro, ilitaka Simba iwapelekee nyaraka za deni inalodaiwa na Mosoti ili walipe kupitia Mamilioni ya fedha walizovuna kupitia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi.
Siku chache baada ya Muro kutoa kauli hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Zakaria Hans Poppe alisema klabu yao ina uwezo wa kulipa fedha hizo na isingehitaji msaada kutoka kokote.
Mosoti aliiburuza Simba FIFA kutokana na kuvunja mkataba wake wa kuichezea klabu hiyo kienyeji na hata ilipotolewa hukumu ya kumlipa Mkenya huyo, Simba ilipuuza ndipo mapema mwezi huu FIFA iliiagiza TFF kuilazimkisha Simba imlipe Mosoti ndani ya mwezi mmoja la sivyo Iishushe Daraja na yenyewe (TFF) itafungiwa kwa michuano ya kimataifa, jambo ambalo lingeizuia Yanga kucheza hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.