STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, May 17, 2013

Golden Bush Veterani kushiriki Bonanza la Staki Shari J'piliKikosi cha Golden Bush Veterani
WAKATI wa kandanda la mavaterani jijini Dar es Salaam, Golden Bush imethibitisha kushiriki katika bonanza la klabu ya Staki Shari litakalofanyika siku ya Jumapili kwenye viwanja vya Staki Shari, Ukonga.
Kwa mujibu Msemaji wa Golden Bush Veterani, Onesmo Waziri 'Ticotico' alisema wanatarajiwa kushusha kikosi kamili katiika bonanza hilo ili kutoa dozi kwa wapinzani wao kama walivyofanya waliposhiriki wiki iliyopita'
Ifuatayo ni taarifa rasmi ya klabu hiyo ilitotumwa kwa MICHARAZO:

Tunapenda kuwafahamisha kwamba timu yenu ya Golden Bush imethibitisha kushiriki katika Bonanza ya tarehe 19/05/2013 litakalo fanyika katika viwanja vya Staki Shari. Golden Bush itakuja na kikosi kamili kama kinavyoonekana katika picha hapo chini.  Golden Bush itaingia uwanjani mnamo saa mbili kamili asubuhi tayari kutoa kipigo stahiki kwa timu yoyote itakayopambana na sisi. Waandaaji wa mashindano wanatambua ubora wa Golden bush itakoyokuwa ikiongozwa na nahodha wake Wisdom Ndlovu, hivyo tunategemea kupangiwa timu itakayoonyesha upinzani na kuleta burudani kwa mashabiki watakaokuja kushuhudia Bonanza hilo.

Tungependa kuwataarifu kwamba mchezaji wa zamani wa yanga na timu ya taifa ya Tanzania Salum Athuman Mbududu amesajiliwa rasmi baada ya kufuzu majaribio ya wiki moja, hivyo tunapenda kumtangaza kuwa kuanzia leo Salum Athuman atakuwa mchezaj halali wa Golden bush Veterans.

Imetolewa na msemaji wa timu
Onesmo Waziri "Ticotico"