STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 28, 2013

Breaking Newssss:Albert Mangwea afariki Afrika Kusini, inadaiwa kalishwa sumu

Albert Mangwea enzi za uhai wake
NYOTA wa nyimbo za Ghetto Langu, Mikasi, Nipe Deal na nyinginezo, Albert Mangwea 'Ngwair' amefariki dunia leo saa 9 alasiri akiwa nchini Afrika Kusini kwa kile kilichoelezwa huenda alilishwa sumu.
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Ngwair tangu alipolala usiku wa jana hakuweza kuamka na wenzake waliokuwa wameambatana nchini humo waliamua kumgongea na walipoingia ndani walimkuta katulia na kumkimbiza hospitali moja mjini Pretoria na kugundulika kuwa amefariki baada ya kupimwa na daktari aliyempokea hospitalini hapo.
Japo taarifa zingine zinasema kuwa Ngwair na msanii mwenzake alioenda nchini humo kufanya Show M to the P walijidunga 'unga' na kusababisha mkali huyo wa hip hop kuaga dunia na mwenzake kuwa taaban.
Tayari inaelezwa msiba wa msanii huyo umewekwa mjini Morogoro baada ya taarifa hizo kufika kwa mama yake anayeishi huko.
Mungu aiweze roho yake mahali pema na MICHARAZO inafuatilia zaidi taarifa hizo kujua ukweli.

Dekula Band kufanya makamuzi Little Nairobi




Dekula Kahanga 'Vumbi'

MKALI wa zamani wa bendi ya Orchestra Marquiz Original 'Wana Sendema', Alain Dekula Kahanga 'Vumbi' pamoja na kundi lake la Dekula Band wakiwa na wakali kama Lady Neema, Bobo Sukari na Yaya Sella wikiendi hii wataendelea na makamuzi yake nchini Sweden wanapoendelea na shughuli zao za muziki.
Vumbi aliiambia MICHARAZO kuwa Dekula Band 'Ngoma ya Kilo' watakamua burudani katika ukum,bi wa Lila Wien, maarufu kama Little Nairobi, wakiangusha ngoma mpya na za zamani mwanzo mwisho.
Maonyesho hayo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo Mei 31 na Juni Mosi na kusema mashabiki wa bendi hiyo na waliozoea ukumbi huo hawapaswi kuikosa burudani hiyo itakayoambatana na show kabambe pamoja na kukumbushiwa vibao vya zamani vilivyomfanya yeye wenzake kuwatamba nchini enzi zao.
Vumbi alisema wamepania kufanya mambo makubwa zaidi ya yaliyozoeleka kufanywa na bendi yake.

Tangazo lao linasomeka hivi;
"Wazee Wapewe" present's;
Lady Neema,Bobo Sukari & Yaya Sella
Dekula Band"Ngoma Ya Kilo"
Place: Lilla Wien"Little Nairobi"
Date: 31/may & 01/june/2013
Time: 21.00-01.00
Addr: Swedenborgsg.20
Pendel: Södra station
http://www.youtube.com/watch?v=T3KIYgRlyR0

Real Madrid wasisitiza Ronaldo hauzwi


http://img.thesun.co.uk/multimedia/archive/01623/ronni_1623771a.jpg
Cristiano Ronaldo

KLABU ya Real Madrid ya Hispania imesisitiza kuwa nyota wake, Cristiano Ronaldo hauzwi kwa vile bado  wanamtegemea mchezaji huyo kwa msimu ujao.
Nyota huyo wa Ureno mwenye miaka 28 amekuwa akitajwa kuwa yu mbioni kurejea klabu yake ya zamani wa Manchester United ya England pia akitajwa kunyatiwa na mabingwa wa Ufaransa, PSG.
Ronadlo alinukuliwa mwaka uliopita kuwa anajisikia huzuni kuwepo Bernabeu na kudai alikuwa anafikiria kuachana na klabu hiyo.
Lakini Rais wa Real, Florentino Perez alisema wanatumaini mshambuliaji huyo atasalia katika klabu yao na wana imani atakuwa miongoni mwa wachezaji wao kwa miaka kadhaa ijayo.
Perez alisema: Aliniambia katika kipindi cha majira ya joto alikuwa na huzuni na tulimueleza jinsi tukavyofanya kila linalowezekana kwa ajili yake mradi ajisikie poa.
"Sijui kama kuna ofa yoyote aliyopewa kutoka PSG. Nafikiri Cristiano ni mwansoka bora kabisa duniani," alisema Perez na kuongeza wangependa kuijenga Madrid kwa misimu kadhaa ikiwa na ubora wa hali ya juu sambamba na Ronaldo aliyedai wangependa kuendelea kuwa mchezaji anayelipwa vyema duniani.
Duru za soka zinasema kuwa Ronaldo yupo kwenye mipango ya kurejeshwa Old Trafford, kwa kile kinachoelezwa hafurahii maisha ya Madrid kwa namna mashabiki wanavyomchukulia licha ya kufanya kazi kubwa tangu atue katika klabu hiyo akitokea Manchester United.

Stars watua salama Ethiopia waanza kujifua

Wachezaji wa Stars katika suti kabla ya kwenda Ethiopia
Na Boniface Wambura, Addis Ababa
Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.

Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis.

Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0.

Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.

Wakongo wanne wajitokeza kuomba kazi Msimbazi


Wachezaji wa Simba wakijifua

Tutamvutia tu Kibadeni! Ndivyo wachezaji wapya wanaoomba kazi Mismbazi wakijifua kabla ya kuangaliwa na kocha Kibadeni

Kibadeni akiwahakiki wachezaji wapya walijitokeza kujaribiwa

Andika majina yako kamili: Kibadeni akiwaandikisha majina wachezaji

Add caption

Wachezaji wapya wakijifua

Mtacheza hivi: Kocha msaidizi, Seleman Matola kizungumza na wachezaji wapya waliojitokeza kujaribiwa huku King KIbadeni (wa pili kulia) akisikiliza kwa makini


Wachezaji wa Simba U20 na wapya wakipimana ubavu leo uwanja wa Kinesi

Wachezaji wa Simba wakionyeshana kazi mazoezini leo asubuhi

Matola akitetea jambo na wanahabari

Mimi ndio Matola Bwana! Kocha wa U20 Seleman Matola akimueleza jambo Mahmoud Zubeiry mwenye miwani,  huku Saleh Ally akicheka kando yao

Wachezaji wapya wa Simba wakipashga moto uwanja wa Kinesi
WACHEZAJI wanne kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DR Congo), wakiwamo watatu wanaokipiga AS Vita wamejitokeza kuomba kibarua cha kuichezea Simba kwa msimu ujao ambao asubuhi ya leo walikuwa wakijaribiwa na kocha mpya wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni 'King Mputa'.
Pia katika majaribio hayo wapo wachezaji wengine kadhaa akiwamo Mtanzania aliyekuwa akiichezea timu ya Ferreviario de Nampula ya Msumbuji, Miembeni Zanzibar na wachezaji wengine chipukizi kutoka jijini Dar katika klabu za Fc Boom ya Ilala, Buza Sports na Mbagala Scaret Academy.

Wachezaji kutoka Kongo wakiwamo washambuliaji watatu ni pamoja na Joe Fils kutoka Le Verez Club, Fabian Tshayaz, Fabrice Balou na Patrick Milambo wote wa AS Vita.
Wengine waliojitokeza kuomba 'kazi' Msimbazi ni Ramadhani Kipicha kutoka klabu ya Buza, Adeyun Saleh wa Miembeni Zanzibar, Mohammed Abdallah aliyekuwa anacheza Ferreviario De Nampula ya Msumbiji, Shaaban Kondo wa Mbagala Scalet Academy na Shaaban Said wa Fc Boom ya Ilala.
Wachezaji hao walisema wamejitokeza kuomba nafasi ya kufanya kazi Msimbazi kwa kuamini wanaweza licha ya kudai jukumu la kupima uwezo wao lipo mikononi mwa makocha wao, King Kibadeni, Jamhuri Kihwelu 'Julio', Seleman Matola na wote waliopo kwenye benchi la ufundi la timu hiyo.

Wakati wa maharibio hayo wachezaji wao walipewa muongozo na kocha wa timu ya vijana, Seleman Matola kabla ya Kibadeni kuzungumza nao huku wakishuhudiwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala aliyefika mapema uwanja wa Kinesi kwa ajili ya kuona kazi zinaendeleaje.

King Kibadeni atua rasmi Msimbazi na mikwara, Julio achekelea


Kocha Abdallah Kibadeni akizungumza na baadhi ya wachezaji wapya walijitokeza kujaribiwa Simba

King Kibadeni (wapili kulia) akiteta na Amri Said wakati walipokuwa wakizungumza na wachezaji waliojitokeza kuwania kusajiliwa Simba ambao jana walipimwa na kocha huyo.

Kocha Abdallah Kibadeni (kulia) akiwa na wasaidizi wake, Jamhuri Kihwelu 'Julio' na Seleman Matola wakiwa kwenye  mazoezi ya timu hiyo asubuhi ya leo katika uwanja wa Kinesi.

Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala akiteta na makocha wa timu yao, Abdallah KIbadeni (kulia) Jamhuri Kihwelu 'Julio' na Seleman Matola.

Kocha msaidizi, Seleman Matola akigawa jezi kwa wachezaji waliojitokeza kutaka kusajiliwa Simba asubuhi ya leo kwenye uwanja wa Kinesi.

Wachezaji wa kikosi cha Simba B wakijifua kabla ya kuwapima wachezaji wapya wanaowania kujiunga na Simba
KOCHA maarufu aliyewahi kuwa nyota wa Simba na Taifa Stars, Abdallah Kibadeni, ameanza rasmi kazi ya kuinoa timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Mfaransa, Patrick Liewig aliyetimuliwa.
Kibadeni maarufu kama 'King Mputa' ametua Simba ikiwa ni mara yake ya nne akitokea Kagera Sugar aliyoinoa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja katika Ligi Kuu Tanzania Bara iliyomalizika hivi karibuni na kuifikisha timu hiyo kwenye 'Nne Bora'
Kocha huyo alianza kazi asubuhi ya leokwenye uwanja wa Kinesi, Ubungo jijini Dar es Salaam kwa kuwajaribu wachezaji wapya waliojitokeza kuwania kusajiliwa Simba wakiwemo Wakongo wanne na mmoja kutoka Msumbiji.
Kibadeni alisema amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa Simba na kwamba malengo yake ni kuhakikisha Simba inafika mbali katika ligi ya nyumbani na kimataifa kama ilivyo desturi yake.
Kocha huyo aliyewahi kuifikisha Simba kwenye fainali za michuano ya CAF mwaka 1993 na kufungwa mabao 2-0 na Stella Abidjan, alisema kitu cha muhimu angependa apewa muda ndani ya kikosi hicho kufanya kazi zake.
"Nimetua rasmi Simba kwa mkataba wa miaka miwili na matarajio yangu ni kuifikisha mbali, ingawa watarajie lolote kwa michuano ya Kagame kwa muda uliopo wa maandalizi, lakini kwa ligi wasiwe na shaka," alisema.
Aliongeza anachopenda kwa uongozi wake ni kumpa nafasi ya kufanya kazi bila kuingiliwa, ili hata mwisho wa  siku iwe rahisi kwao kumbana.
"Hakuna jambo ambalo silipendi kama kuingiliwa kazi, kila mtu atekeleze majukumu yake kwa maana benchi ya ufundi tuachwe tuifanye kazi na wataona nini tutakachokifanya kwani najiamini naweza," alisema Kibadeni.
Kuhusu wachezaji waliosimamishwa na uongozi wa tuhuma za utovu wa nidhamu, Kibadeni alisema hawana nafasi kwake kwa madai siku zote yeye amekuwa muumini wa suala la nidhamu kwa wachezaji.
"Kama viongozi waliwasimamisha kwa utovu wa nidhamu, kwangu pia hawana nafasi ili wasije wakaniharibia kazi, nitafanya kazi na wachezaji wote walio tayari kuitumikia Simba kwa hali na mali ili ifike mbali," alisema.
Kocha huyo anayeanza rasmi kuinoa timu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika nchini Sudan, aliusisitizia uongozi umpe ushirikiano katika utekelezaji wa programu zake kama walivyokuwa wakifanya kwa makocha wa kigeni.
"Nikipewa ushirikiano na kutekelezewa kila ambalo nahitaji kwa maandalizi na programu ya timu naamini Simba itatisha msimu ujao, ikizingatiwa nalijua soka la Tanzania na wasaidizi nilionao ni watu wanaojua soka," alisema.
Kwa upande wa makocha wasaidizi waliompokea Kibadeni, Jamhuri Kihwelu 'Julio', Seleman Matola na Amri Said walisema wamefurahi ujio wa mwalimu huyo aliyewahi kuwanoa enzi za uchezaji na kuamini benchi la ufundi sasa limekamilika na Simba itatisha.
"Simba ijayo itatisha, nani asiyemjue Super Coach, King Kibadeni, ebu piga picha huku King, hapa Julio aaah Simba itatakata tuombe Mungu, ila tumefurahi mno kurejeshwa kwa Kibadeni Msimbazi," alisema Julio.

Hussein Javu airuka kimanga Yanga, asisitiza yeye bado wa Mtibwa

Hussein Javu
MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar, Hussein Javu ameiruka kimanga klabu ya Yanga kuhusu mipango yao ya kutaka kumsajili kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Javu alisema hajawahi kufanya mazungumzo na kiongozi yeyote wa Yanga na kushangazwa na taarifa kwamba yupo njiani kutua Jangwani akitokea Mtibwa.
Akizungumza na MICHARAZO, Javu alisema mpaka sasa yeye ni mchezaji wa Mtibwa Sugar na angependa kuendelea kuichezea klabu hiyo kwa misimu mingine na hajui wanaomzushia kwamba anajiandaa kuhamia Yanga.
"Sijajua hizi taarifa zinatoka wapi, sijazungumza na kiongozi yeyote wa Yanga kuhusu suala la kuhamia Jangwani, lakini naona naandikwa kuhusu mipango hiyo wengine wakidai nimteoa masharti ya kutaka nyumba na gari," alisema.
Alisema anashukuru kupata nafasi ya kuzungumza na MICHARAZOna kuweka bayana suala hilo ili isije akaeleweka vibaya kwa viongozi na wachezaji wenzake.
Alipoulizwa yupo tayari kutoka Mtibwa Sugar, Javu alisema hajafikiria kwa sasa ila alisema kama kweli kuna klabu inayomhitaji ni lazima izungumze naye pamoja na viongozi wake na wakiafikiana atakuwa na maamuzi sahihi.
"Soka ni ajira yangu, pamoja na kwamba napenda kucheza Mtibwa, kama itatokea klabu yoyote itakayokuwa inanihitaji ikazungumza nami au viongozi wangu naweza kuhama, lakini siyo kwa kuzushiwa kama sasa," alisema Javu.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa na bahati za kuzitungua Simba na Yanga kila timu hizo zikikutana na Mtibwa Sugar, alisema ingekuwa vyema vyombo vya habari zinaposikia fununu zozote hasa kipindi hiki cha usajili kikafanya jitihada za kuzungumza na wahusika badala ya kuandika tu na kuharibiana.
Javu amekuwa akihusishwa na mioango ya kutua Yanga kwa nia ya kuimarisha kikosi cha timu hiyo baada ya washambuliaji waliopo sasa baadhi yao kushindwa kung'ara kwenye msimu uliopita.

Wawakilishi wa Tanzania Big Brother The Chase hawa hapa

Nando

Feza Kessy
MASHINDANO ya Big Brother Africa ‘Big Brother-The Chase’ yamezinduliwa rasmi juzi nchini Afrika Kusini.
Mashindano hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya nane mwaka huu, yanashirikisha jumla ya watu 24 kutoka katika nchi 14 za Afrika.
Washiriki hao wanatarajiwa kukaa ndani ya nyumba hiyo kwa muda wa siku 90 ambapo wataanza kuchujwa kuanzia mwishoni mwa wiki hii.
Tanzania inawakilishwa na Feza Kessy pamoja na Ammy Nando ambapo mshindi wa mwaka huu ataondoka na kitita cha dola za Kimarekani 300,000.
Akizungumza Dar es Salaam juzi wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Habari wa Dstv Tanzania Barbara Kambogi, alisema kuwa pamoja na kuwa msimu huu Ligi mbalimbali zimeshamalizika hivyo mashabiki wengi watapata burudani kupitia katika shindano hilo.
Alisema kuwa mashindano hayo yanaonyeshwa moja kwa moja na Dstv kupitia chaneli 197 na 198 ambapo mashabiki kutoka nchi 50 watapata fursa ya kuyaangalia.
Pia Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Airtel ambao pia ni wadhamini wa mashindano hayo kwa mwaka huu Bw, Levi Nyakundi alisema kuwa mashindano hayo yanazidi kupata umaarufu kutokana na kila mwaka kuwa tofauti.
Aliongeza kuwa wateja wa Airtel wananafasi ya kulipia huduma ya DSTV kwa kupitia huduma ya Airtel kwa kupiga *150*60# kwa urahisi wakiwa nyumbani au sehemu zao za kazi.
“Airtel Money itasaidia sana wateja wetu kuokoa muda wao wa kazi pale wanapolipia huduma ya DSTV wakati wowote wakati wa msimu huu wa Big Brother, mashabiki hawana budi kuwapigia kura washiriki wanaoiwakilisha Tanzania ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi,” alisema Nyakundi.
“Mashindano ya mwaka huu yanaonekana kuwa tofauti na yaliyopita hivyo tunatarajia kupata burudani nzuri na hivyo mashabiki wawapigie kura Watanzania ili wafanye vizuri” alisema.
Katika uzinduzi huo kulikuwa na burudani zilizotolewa na wasanii kutoka Afrika Kusini Mafikizolo pamoja na Stela Mwangi wa Kenya.