STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, May 28, 2013

Real Madrid wasisitiza Ronaldo hauzwi


http://img.thesun.co.uk/multimedia/archive/01623/ronni_1623771a.jpg
Cristiano Ronaldo

KLABU ya Real Madrid ya Hispania imesisitiza kuwa nyota wake, Cristiano Ronaldo hauzwi kwa vile bado  wanamtegemea mchezaji huyo kwa msimu ujao.
Nyota huyo wa Ureno mwenye miaka 28 amekuwa akitajwa kuwa yu mbioni kurejea klabu yake ya zamani wa Manchester United ya England pia akitajwa kunyatiwa na mabingwa wa Ufaransa, PSG.
Ronadlo alinukuliwa mwaka uliopita kuwa anajisikia huzuni kuwepo Bernabeu na kudai alikuwa anafikiria kuachana na klabu hiyo.
Lakini Rais wa Real, Florentino Perez alisema wanatumaini mshambuliaji huyo atasalia katika klabu yao na wana imani atakuwa miongoni mwa wachezaji wao kwa miaka kadhaa ijayo.
Perez alisema: Aliniambia katika kipindi cha majira ya joto alikuwa na huzuni na tulimueleza jinsi tukavyofanya kila linalowezekana kwa ajili yake mradi ajisikie poa.
"Sijui kama kuna ofa yoyote aliyopewa kutoka PSG. Nafikiri Cristiano ni mwansoka bora kabisa duniani," alisema Perez na kuongeza wangependa kuijenga Madrid kwa misimu kadhaa ikiwa na ubora wa hali ya juu sambamba na Ronaldo aliyedai wangependa kuendelea kuwa mchezaji anayelipwa vyema duniani.
Duru za soka zinasema kuwa Ronaldo yupo kwenye mipango ya kurejeshwa Old Trafford, kwa kile kinachoelezwa hafurahii maisha ya Madrid kwa namna mashabiki wanavyomchukulia licha ya kufanya kazi kubwa tangu atue katika klabu hiyo akitokea Manchester United.

No comments:

Post a Comment