STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 5, 2015

MATAJIRI WA ARSENAL 'FUNIKA BOVU' EPL

MMOJA wa wamiliki wa klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov ndiye anaongoza orodha ya mabilionea duniani ambao wanamiliki klabu za Ligi Kuu nchini Uingereza.
Usmanov ambaye anamiliki hisa asilimia 15 za klabu hiyo, anashilikilia nafasi ya 71 katika orodha za matajiri duniani ambazo zimetolewa na gazeti la Forbes mwaka huu.
Anayefuata ni bilionea wa klabu ya Queens Park Rangers-QPR Lakshmi Mittal anayeshika nafasi ya 82 kwa kuwa na utajiri unaokadiriwa kufikia paundi bilioni 8.8.
Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovic yuko katika nafasi ya 137 kwa akiwa na urajiri unaokadiriwa kufikia paundi bilioni 5.9 akifuatiwa na mmiliki mwingine wa Arsenal Stan Kroenke anayeshika nafasi ya 225 akiwa na urajiri unaofikia paundi bilioni 4.1.
Wengine ni mmiliki wa Tottenham Hotspurs Joe Lewis anayeshika nafasi ya 277 kwa utajiri wa paundi bilioni 3.5, Mike Ashley wa Newcastle nafasi ya 318 kwa utajiri wa paundi bilioni 3.2 na mmiliki wa Leicester City Vichai Srivaddhanaprabha anayeshika nafasi ya 714 akiwa na utajiri wa paundi bilioni 1.8.
Mmiliki wa Stoke City Denise Coates yuko katika nafasi ya 737 akimiliki utajiri wa paundi bilioni 1.6 akifuatiwa na mwanahisa wa Arsenal Farhad Moshiri anayeshika nafasi ya 894 huku tajiri wa Liverpool John Henry akifunga orodha ya 10 bora kwa kushinka nafasi ya 1190 katika orodha ya matajiri duniani.
Orodha kamili ipo hivi hapo chini:
Na.       JinaKlabuUtajiri
71Alisher UsmanovArsenal (15%)£9.4bn
82Lakshmi MittalQPR (33%)£8.8bn
137Roman AbramovichChelsea£5.9bn
225Stan KroenkeArsenal£4.1bn
277Joe LewisTottenham£3.5bn

318Mike AshleyNewcastle£3.2bn
714Vichai SrivaddhamaprabhaLeicester City£1.8bn
737Denise CoatesStoke City£1.6bn
894Farhad MoshiriArsnenal (15%)£1.4bn
1190John HenryLiverpool£1bn

HUYU NDIYE KIJANA TAJIRI KULIKO WOTE AFRIKA

* NI MTANZANIA, MBUNGE MOHAMMED DEWJI
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/07/Mohammed-Dewji.jpg
Mohammed Dewji kafunika Afrika
MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania ambaye pia ni  Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mohammed Dewji kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya mabilionea 29, akiwa tajiri kijana kuliko wote barani Afrika.
Jarida la Forbes la Marekani limemtaja Dewji (39), katika nafasi ya 24 ya matajiri wa Afrika akiwa na utajiri wa Dola 1.3 bilioni za Marekani (Sh2.34 trilioni) unaotokana na biashara mbalimbali anazozifanya kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises (Metl Group).“Dewji alibadilisha biashara aliyoanzisha baba yake kutoka uuzaji bidhaa na kuwa na viwanda vya Metl,” inasema sehemu ya habari inayomuhusu bilionea huyo Mtanzania .
“Alinunua viwanda vya nguo na mafuta vilivyokuwa vinamilikiwa na Serikali kwa bei ndogo na kuvifanya viwe na faida zaidi kwa kutumia mtindo wa kisasa wa menejimenti,” inaongeza ripoti hiyo.
Metl ina viwanda vya kutengeneza nguo na bidhaa nyingine za matumizi ya binadamu vikiwamo vyakula, sabuni na vinywaji. Pia ina mapato yanayozidi Dola 1.4 milioni za Marekani (Sh2.5 trilioni) kwa mwaka.
Katika kampuni hiyo, ambayo imekuwa na ushindani dhidi ya kampuni kubwa nyingine kama Said Salim Bakhresa, Dewji anamiliki asilimia 75 ya hisa zote.
Kwa mujibu wa tovuti yake, Metl inaendesha shughuli za uagizaji na usafirishaji bidhaa kutoka na kwenda nje, uzalishaji unaohusisha nguo, vinywaji na vyakula, usagaji nafaka, nishati na petroli na utengenezaji baiskeli.
Pia inahusika na huduma za simu, fedha, kilimo na pia ina kitengo cha kontena kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Dewji anashika nafasi mbili juu zaidi ya kada maarufu wa CCM na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Igunga, Aziz Rostam (50) aliyewekwa nafasi ya mwisho.
Rostam amefungana nafasi ya 26 na mabilionea wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu na Femi Otedola wenye utajiri wa Sh1.8 trilioni kila mmoja.
Orodha hiyo ya 29 bora inaoongozwa na bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote akiwa na utajiri wa Dola 15.7 bilioni za Marekani (Sh28.2 trilioni), kiwango ambacho ni mara moja na nusu ya bajeti ya Serikali ya Tanzania ya mwaka 2014/15.
Forbes linamtaja Rostam kuwa na utajiri wenye thamani ya Dola 1 bilioni za Marekani (Sh1.8 trilioni), kiwango ambacho kimebaki pasi na mabadiliko kutoka orodha ya mwaka jana. Rostam anamiliki asilimia 35 ya hisa katika kampuni ya huduma za simu za mkononi ya Vodacom.

NABII HUYU KIBOKO! AWATUNDIKA MIMBA MADEMU ZAIDI YA 20


Wanawake na mabinti waliopewa mimba na nabii/mchungaji huyo.

HABARI kutoka Nigeria zinaripoti kuwa wanawake zaidi ya 20 wakiwemo wake za watu na mabinti wamepachikwa mimba na mtu anayejifanya 'Nabii' ambaye aliwadanganya kuwa aliambiwa na Roho Mtakatifu kufanya nao mapenzi.
 
 Nabii huyo alifahamika kwa jina la Timothy Ngwu ambaye ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Vineyard Ministry of the Holy Trinity huko Enugu tayari anashikiliwa na jeshi la polisi la jimbo hilo kwa kosa la kuwalazimisha kufanya nao mapenzi na wanawake hao.

Mchungaji huyo amedai anatii wito wake wa kinabii na kiroho alioitiwa na kufanya sawa na mapenzi ya Mungu kwa kuwapa mimba yeyote yule aliyechaguliwa na kuwekwa wazi na Roho mtakatifu bila kujali kama mwanamke huyo ameolewa ama la alisema msemaji wa jeshi la polisi Enegu kamanda Ebere Amaraizu akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kudai kwamba mwanamke akijifungua mtoto hubakia kwenye huduma hiyo na mzazi wake.

Taarifa kutoka kwa familia za mchungaji huyo zinasema mkewe aitwaye Veronica Ngwu ambaye alichoshwa na tabia ya mumewe hasa alipompa ujauzito mdogo wake na kuamua kumripoti Polisi. 
 
Kwa upande wa kaka wa mtuhumiwa ambaye hakutaka jina lake lifahamike ameiambia Vanguard report kwamba amekuwa akimuonya kaka yake juu ya tabia yake kwa muda mrefu lakini hakutaka kusikiliza, amesema gadhabu ya Mungu imeshuka juu ya kaka yake.


"Ngoja niwaambie hasira ya Mungu imemshukia kaka yangu tumekuwa tukimuonya kila siku kuacha alichokuwa akifanya amejaza boma letu kwa kuzaa watoto bila uangalifu na kutuambia tunamuonea wivu kwasababu anafanya maagizo ya Mungu" alisema kaka mtu.
 
Aliongeza "kwamba angalia majengo yote ya kanisa ameyageuza kuwa ya kwake kwa jina la huduma yake, alimfukuza mkewe wa ndoa waliyezaa naye watoto watatu na kuanza kuwajaza mimba wake za watu na mabinti wadogo, we angalia boma lote limejaa watoto wa jinsia zote alilalamika kaka huyo"

Aidha kaka huyo amesema waumini wote wa kanisa la kaka yake ni wapumbavu kwa sababu mwanamke hawezi kumuacha mumewe na kwenda na mwanaume mwingine kwa kisingizio cha kwenda kumuabudu Mungu na kufanya zinaa, na kudai hawezi kujiingiza katika tatizo hilo, "Vero amefungua msaada kwa wamama hao ngoja wayamalize na polisi ila nataka huduma hii ifungwe kabisa" alisema

Ngwu ameiambia NaiJ kwamba kaka yake ana wake wapatao watano na watoto 13 pamoja na wake za watu kwa madai ya kufuata mapenzi ya Mungu. 
 
Amedai hajawahi kufanya mapenzi na wake za watu ila amefanya hivyo endapo waume zao wamekubaliana na ombi la Roho mtakatifu. Calista Omeje na Assumpta Odo ni wanawake ambao waliawaacha waume zao ili kuishi na nabii huyo kwakuwa ilikuwa ni upako wa kinabii wa mchungaji huyo.

Calista ambaye ana watoto 10 na mumewe alipewa mimba na mchungaji huyo ila mtoto alikufa, amesema mwanamke huyo alimkabidhi mchungaji huyo binti yake huku Odo naye amesema mchungaji huyo amempa mimba yeye na binti yake.
Chanzo  Wilfredasuqu

Fainali Kombe la Mfalme Hispania ni Barcelona vs Atletico Bilbao

Barcelona celebrate
Neymar akipongezwa na Messi baada ya kufunga huku Suarez akiwajongelea kwa furaha
Lionel Messi
Messi akiwajibika
KLABU za Barcelona na Athletic Bilbao zinatarajiwa kuvaana kwenye pambano la Fainali za Kombe la Mfalme (Copa del Rey) litakalochezwa Mei 30.
Timu hizo zimefuzu hatua hiyo baada ya kufanikiwa kushinda mechi zao za marudiano ya Nusu fainali ya michuano hiyo, Barcelona wakiichapa wenyeji wao Villarreal kwa mabao 3-1. Mabao hayo yaliwekwa kimiani na Neymar aliyefunga mawili na jingine la Luis Suarez.
Ushindi huo umeifanya vijana hao wa Luis Enrique kupenya kwa jumla ya mabao 6-2, kwani katika pambano lililochezwa Febaru 11 walishinda idadi kama hiyo.
Wapinzani wao Athletic Bilbao ikaisasambua Espanyol mabao 2-0 na kusonga mbel kwa jumla ya mabao 3-1 kwani katika pambano lao la awali walishindwa kutambiana kwa kutoka sare ya 1-1.

GHARIKA! MVUA ZAUA WATU 42, WENGINE 96 WAJERUHIWA

http://2.bp.blogspot.com/-JMObZ1QCDyQ/VPdFGS9KTxI/AAAAAAABpEo/1d4hUD9R3vQ/s1600/kahama%2B1.jpg
Moja ya nyumba iliyoporomoshwa na mvua zinazoendelea kunyesha
Na Mwandishi Wetu, Kahama
ZAIDI ya watu 40 wameripotiwa kufariki mjini Kahama, Shinyanga kutokana na mvua kubwa huku wengine wapatao 96 wameripotiwa kujeruhiwa na kupoteza makazi.
Aidha mikoa ya Kilimanjaro, Morogoro, Pwani na Tabora mvua kama hizo zenye kuambatana na upepo mkali zimeleta uharibifu mkubwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) imeonya huenda mvua hizo za mawe zikaendelea kunyesha mfululizo na watu wawe na tahadhari.
Awali iliripotiwa kuwa 39 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 69 wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. 
Taarifa hizo zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa.
 Bw. Mpesya amesema hadi majira ya asubuhi walikuwa wamefanikiwa kupata miili ya watu 39 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa matibabu zaidi. 
Mkuu huyo wa Wilaya amesema nyumba nyingi zimeanguka na zoezi la kutafuta watu waliojeruhiwa au kupoteza maisha bado linaendelea kwa kasi.
Hata hivyo idadi ya waliopoteza maisha na waliojeruhiwa ilizidi kuongezeka kadri shughuli za uokozi ilipokuwa inaendelea na kuleta simanzi kubwa kwa taifa.

Aibu! Watanzania 443 wanaswa na dawa za kulevya ughaibuni

http://api.ning.com/files/NWvFMlVPFcx5SxCYa4RDXr0NMMnq6gRcpSfjyInB*mxa*WWMz0x1MendQbi7EkT588mJKfgz3DjGsbaCvcR6Q0AgTJ03rTXA/Pipi.jpg
Baadhi ya dawa zilizowahi kunaswa nchini
http://api.ning.com/files/NGHxxVgVd17fuWKh*v1l7*4NyFc2GYTkLp2o69tup7nXuo4nQgBPU2OuQ-it1jCnSiXwKCGVj6KQ*c8ylkYzAyOgRGizDiJb/IMG_0532.jpgBIASHARA ya Dawa za Kulevya bado ni kizungumkuti kwa taifa la Tanzania, kwa raia wake wapatao 443 kunaswa katika mataifa mbalimbali duniani.
Hata hivyio ni angalau udhibiti juu ya biashara hiyo nchini imeanza kuonekana kwa kunaswa kwa 'unga' upatao tani 2.3 (kilo 2300).
Imeelezwa kuwa Tanzania imefanikiwa kudhibiti zaidi ya tani 2.3 za dawa za kulevya zilizokamatwa na vikosi vya wanamaji huku za zaidi ya watanzania 443 wamekamatwa katika nchi mbalimbali duniani wakihusishwa na usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya. 
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ripoti ya dawa za kulevya ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Kudhibiti Dawa za Kulevya na Makosa ya Jinai (UNODC) Mwakilishi kutoka Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Tanzania Bw. January Ngisi amesema tatizo la dawa za kulevya katika ukanda wa Afrika Mashariki bado ni kubwa na kueleza kwa kushirikiana na vyombo vya dola wameridhia mikataba ya kupunguza upatikanaji wa dawa za kulevya.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bi. Stela Vuzo amesema ripoti hiyo imeitaka serikali kuwasaidia watoto wasijingize katika matumzi ya dawa za kulevya ambazo zimekuwa na madhara makubwa ikiwemo athari za kiafya na iwekwe mikakati itakayotokomeza uingizwaji na utumiaji wa dawa za kulevya nchini.

Arsenal, Chelsea, Man U zatamba ugenini, Liverpool moto chini!

Adrian dives in vain as Hazard's header sails past the Spanish shot stopper and into the back of West Ham's net
Hazard akiifungia Chelsea bao pekee dhidi ya West Ham
Sanchez celebrates doubling Arsenal's lead mid way through the second half at Loftus Road
Sanchez wa Arsenal akishangilia bao la pili alilolifunga yeye wakati wakiizamisha QPR
David Silva shoots the ball past Leicester goalkeeper Mark Schwarzer to give Manchester City the lead just before half-time
Silva akiwatungua Leichester City
Ashley Young fires home the winner for Manchester United to earn his side a valuable three points at Newcastle 
Ashley Young akifunga bao la 'jioni' kuipa ushindi murua Manchester City ugenini dhidi ya Newcastle Utd
MABAO mawili kupitia kwa Olivier Giroud na Alexis Sanchez yameiwezesha Arsenal kuikomalia nafasi ya tatu, huku Chelsea wakijiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya zote kupata ushindi katika mechi zao zilizochezwa usiku wa jana.
Arsenal ikiwa uwanja wa ugenini nyumbani kwa QPR ilipata mabao hayo katika kipindi cha pili na kuizamisha wenyeji wao kwa mabao 2-1, huku Chelsea nao wakipata ushindi ugenini mwa West Ham United kwa bao 1-0 bao lililofungwa Eden Hazard akimalizia kazi ya Ramires.
Katika pambano la Arsenal na QPR, Giroud alianza kuifungia timu yake bao dakika ya 64 kabla ya dakika nne baadaye Sanchez kuongeza la pili na wenyeji kuja kupata la kufutia machozi dakika ya 82 kupitia kwa Charlie Austin.
Kwa ushindi iliyopata Chelsea imeifanya mabingwa hao wa Kombe la Ligi kufikisha pointi 63, huku wapinzani wao wakisaliwa na pointi 39 na kukamata nafasi ya 10 huku Arsenal wakiwafukuzia mabingwa watetezi Manchester City waliopo nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 54.
City wenyewe alipata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Leicester City na kuwqafanya wafikishe pointi 58 baada ya kushuka dimbani mara 28. Mabao ya washindi yaliwekwa kimiani na David Silva na James Milner.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Liverpool ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Burnley, Manchester United ikiwa ugenini ilipata ushindi muhimu wa bao 1-0 mbele ya Newcastle United, huku Stoke City ikiitambia Everton kwa kuilaza mabao 2-0 na Tottenham Hotspur ilipata ushindi mujarabu kwenye uwanja wake wa nyumbani wa White Hart Lane kwa kuilaza Swansea City kwa mabao 3-2.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena keshokutwa kwa pambano moja tu kati ya QPR dhidi ya Spurs na timu nyingine zitakuwa kwenye majukumu ya Kombe la FA kabla ya ligi hiyo kuendelea wikiendi ijayo ya Machi 14 na 15.