STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 4, 2014

Mcongo wa Azam atimka kwao, Ghana, Mhaiti bado majaribuni

Kiungo Lofo Serge aliyetimkia kwao
Kiungo Joseph Peterson wa Haiti anayeendelea kujaribiwa
MABINGWA wa soka nchini, Azam wanaendelea kuwapima kwa mara ya mwisho wachezaji wawili wa kimataifa kutoka Haiti na Ghana, huku nyota mwingine wa DR Congo Lofo Serge akitimka kwao baada ya majaribio yake.
Wachezaji wanaoendelea kujaribiwa kabla ya kuamuliwa hatma yao ni kiungo Joseph Peterson wa Haiti na beki Ben Achaw kutoka Ghana, wakati Serge ambaye ni mshambuliaji akimaliza majaribio yake na kutimka.
Akizungumza na MICHARAZO, Meneja wa Azam, Jemedari Said alisema wachezaji wote wameonyesha viwango vya hali ya juu katika kusaka soka, ila hatma yao itaamuliwa na kocha Joseph Omog mwenye maamuzi ya mwisho.
Jemedari alisema Serge alitua nchini baada ya kutumiwa tiketi na uongozi wao na muda wake ulikuwa wa wiki moja, wakati wenzake walitua wenyewe nchini na watamalizia wiki yao ya pili kabla ya kuondoka.
"Serge alijaribiwa kwa wiki moja na kwa uzoefu na umaarufu wake siyo jambo la ajabu kumaliza mapema na hao wengine waliokuja wenyewe wanamalizia wiki yao ya mwisho kabla ya kocha kuamua hatma yao," alisema Jemedari.
Meneja huyo alisema kwa waliowashuhudia wachezaji hao wakati na kikosi cha Azam watakubaliana naye kwamba ni wachezaji wazuri, ila kocha ndiye atakayeamua iwapo kama watafaa uitumikia timu yao.
"Kama wataonekana wanavitu vya kuisaidia timu basi watafahamishwa hata wakiwa makwao, lakini kwa hakika karibu wote wanaonekana wazuri," alisema Jemedari nyota wa zamani wa kandanda nchini aliyetamba Majimaji-Songea.
Kabla ya kujaribiwa Azam Serge anayeichezea pia timu ya taifa ya nchi yake, aliwahi kutamba na timu za AS Paulino Kinshasa, TP Mazembe, AS Aviacao, Sagrada Esperança, AS Vita, FC Brussels na Maccabi Netanya.

MKAZI MWANZA AJIFUNGUA WATOTO WANNE

Watoto wa Tecra waliozaliwa wakiwa ni wanne huku mmojawapo ambaye hakufunuliwa uso akiwa amefariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa-Picha na Antony Sollo-Malunde1 blog-Mwanza 

 Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Proscovia Leopod akimhudumia bi Tecra baada ya kujifungua Picha na Antony Sollo-Malunde1 blog-Mwanza


Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Tecra Kazimili(24) mkazi wa Lubili katika wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza amjefungua watoto (4) kwa wakati mmoja huku mtoto mmoja wa kiume akifariki muda mfupi baada ya mama huyo kujifungua.
Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kushuhudia tukio hilo ambalo si la kawaida mama Tecra alisema hii ni mara yake ya nne kujifungua lakini ni mara yake ya kwanza kujifungua watoto wanne kwa wakati mmoja. 

Tecra ambaye amelazwa katika wodi ya wazazi katika Hospitari ya wilaya ya misungwi Mkoani Mwanza alisema anamshukuru Mungu kwa kumjalia Afya njema na kumuwezesha kujifungua watoto (4) pamoja na kwamba mmoja wa watoto hao amepoteza maisha muda mfupi baada ya kuzaliwa. 

“yote ni mipango ya mungu.”alisema Tecra

Tecra  aliongeza kuwa hiyo ni uzao wake wa nne lakini hana mtoto hata mmoja kutokana na watoto wake wote (3) kufariki wanapofikisha mwaka moja hadi mwaka mmoja na nusu kitendo kilichosababisha kufukuzwa na mume wake Mussa Masalu aliyekuwa anaishi naye baada ya kuona watoto wanafariki na kudaiwa kuwaua yeye mwenyewe jambo ambalo halina ukweli,alisema Tecra.

Pamoja na hayo Tecra  anawaomba Watanzania wasamalia wema watakaoguswa wamsaidie kwa kuwa huyu aliyempa mimba hiyo si mumewe hivyo hana msaada wowote atakaopata wakati atakapokuwa anaendelea kuwalea watoto wake hao.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi Marco Mwita aliwaambia waandishi wa Habari kuwa tukio hili ni si la kawaida kutokea mara nyingi wakina mama wamekuwa wakijifungua watoto watatu na si wanne kama ilivyotokea kwa Tecra.

Wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi wameonyesha utendaji uliotukuka kwa namna ya kipekee jinsi waandishi walivyofika na kushuhudia namna walivyokuwa wakimhudumia Tecra ambapo mmoja wa wauguzi hao Proscovia Leopod 36 alikutwa akitoa huduma kwa upendo wa aina yake kwa kumsaidia Tecra mambo mbalimbali aliyopaswa kuyafahamu ili kuhakikisha watoto hao wanakaa salama.

Akifafanua Muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi  Proscovia Leopod alibainisha baadhi ya mambo aliyokuwa akimfundisha Tecra kuwa ni namna ya kuwanyonyesha watoto,kuwahudumia na kuwafunika shuka,na kumshauri ale chakula cha kutosha na bora ili aweze kupata maziwa mengi kwa ajili ya kuwanyonyesha watoto wake.

Pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu,wauguzi wa Hospitali hiyo wamesema kuwa,

“Tumefurahishwa na jinsi Mungu alivyotujalia moyo wa kujituma kufuatana na mazingira magumu ya utendaji wa kazi zetu,jambo hili siyo la mchezo tumehangaika na kutumia uwezo wetu wote tulio nao kuhakikisha Tecra anajifungua salama,tunaahidi kwa,tutamsaidia mama huyu kwa hali na mali mpaka hapo hali yake itakapotengemaa na kuruhusu arudi kwao.” Walisema wauguzi hao.

Bi Tecra hana msaada,na kama unaguswa basi piga simu namba 0768102438


Na Valence Robert

Huu ndiyo usajili wa timu za Ligi Kuu za England

Luke Shaw ametua Manchester United toka Southampton
Kipa David Ospina ametua Arsenal
Didier Drogba amerejea Chelsea
Fillipe Luis (mbele) amehamia Chelsea
http://static.goal.com/434100/434187_heroa.jpg
Alexis Sanchez ametua Arsenal toka Barcelona
Romelu Lukaku amehamia jumla Everton toka Chelsea
ARSENAL
WALIOSAJILIWA
Alexis Sanchez (Barcelona, £30m),
Calum Chambers (Southampton, £12m),
Mathieu Debuchy (Newcastle, £10m),
David Ospina (Nice, £3m)

WALIOONDOKA

Thomas Eisfeld (Fulham, ada haikutajwa),
Bacary Sagna (Manchester City, huru),
Lukasz Fabianski (Swansea, huru),
Nicklas Bendtner (ameruhusiwa),
Park Chu-young (ameruhusiwa),
Chuks Aneke (ameruhusiwa),
Daniel Boateng (ameruhusiwa),
Wellington Silva (Almeria, mkopo),
Carl Jenkinson (West Ham, mkopo)

ASTON VILLA

WALIOSAJILIWA
Philippe Senderos (Fulham, huru),
Joe Cole (West Ham, huru),
Tom Leggett (Southampton, ada haikutajwa),
Isaac Nehemie (Southampton, ada haikutajwa)
Kieran Richardson (Fulham, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA

Marc Albrighton (Leicester City, huru),
Nathan Delfouneso (Blackpool, huru),
Jordan Bowery (Rotherham, ada haikutajwa),
Nicklas Helenius (Aalborg, mkopo),
Yacouba Sylla (Kayseri Erciyesspor, mkopo)

BURNLEY

WALIOSAJILIWA
Lukas Jutkiewicz (Middlesbrough, £2.5m),
Michael Kightly (Stoke, ada haikutajwa),
Marvin Sordell (Bolton, huru),
Matt Gilks (Blackpool, huru),
Matt Taylor (West Ham, huru),
Steven Reid (West Brom, huru)

WALIOONDOKA

Chirs Baird (West Brom, huru),
Junior Stanislas (Bournemouth, huru),
David Edgar (Birmingham, huru),
Keith Treacy (ameruhusiwa),
Brian Stock (ameruhusiwa),
Nick Liversedge (ameruhusiwa)

CHELSEA

WALIOSAJILIWA
Cesc Fabregas (Barcelona, £30m),
Diego Costa (Atletico Mdrid, £32m),
Mario Pasalic (Hadjuk Split, ada haikutajwa),
Filipe Luis (Atletico, £16m),
Didier Drogba (Galatasaray, huru)

WALIOONDOKA

David Luiz (Paris Saint-Germain, £50m),
Romelu Lukaku (Everton, £28million),
Samuel Eto'o (ameruhusiwa),
Frank Lampard (New York City, huru),
Sam Hutchinson (Sheffield Wednesday, huru),
Mark Schwarzer (ameruhusiwa),
Henrique Hilario (ameruhusiwa),
Wallace (Vitesse Arnhem, mkopo),
Bertrand Traore (Vitesse Arnhem, mkopo)
Thorgan Hazard (Borussia Monchengladbach, mkopo),
Ashley Cole (Roma, £1.5m),
Demba Ba (Besiktas, £8m),
Mario Pasalic (Elche, mkopo)
Patrick van Aanholt (Sunderland, ada haikutajwa),
Ryan Bertrand (Southampton, mkopo),
Gael Kakuta (Rayo Vallecano, mkopo)

CRYSTAL PALACE

WALIOSAJILIWA
Chris Kettings (Blackpool, huru)
Fraizer Campbell (Cardiff, £800k)

WALIOONDOKA

Jonathan Parr (Ipswich, huru),
Dean Moxey (Bolton, huru),
Aaron Wilbraham (Bristol City, huru),
Kagisho Dikgacoi (Cardiff, huru),
Danny Gabbidon (ameruhusiwa),
Neil Alexander (ameruhusiwa),
Ibra Sekajja (ameruhusiwa),
Alex Wynter (Portsmouth, mkopo),
Kwesi Appiah (Cambridge, mkopo),
Jose Campana (Sampdoria, ada haikutajwa),
Jack Hunt (Nottingham Forest, mkopo)

EVERTON

WALIOSAJILIWA
Romelu Lukaku (Chelsea, £28m),
Gareth Barry (Manchester City, free)
Muhamed Besic (Ferencvaros, £4m)

WALIOONDOKA

Apostolos Vellios, (Lierse, huru)
Mason Springthorpe (ameruhusiwa)
Magaye Gueye (Millwall, huru)

HULL

WALIOSAJILIWA
Robert Snodgrass (Norwich, £8m),
Jake Livermore (Tottenham, £6m),
Tom Ince (Blackpool, free),
Harry Maguire (Sheffield United, £2.5m),
Andrew Robertson (Dundee United, £2.85m)

WALIOONDOKA

Matty Fryatt (Nottingham Forest, huru),
Cameron Stewart (Ipswich, huru),
Robert Koren (ameruhusiwa),
Abdoulaye Faye (ameruhusiwa),
Conor Henderson (Crawley, huru),
Dougie Wilson (released),
Conor Townsend (Dundee United, mkopo),
Joe Dudgeon (Barnsley, mkopo)

LEICESTER CITY

WALIOSAJILIWA
Matthew Upson (Brighton, huru),
Marc Albrighton (Aston Villa, huru),
Leonardo Ulloa (Brighton, £7m),
Ben Hamer (Charlton, huru),
Jack Barmby (Manchester United, huru),
Louis Rowley (Manchester United, huru)

WALIOONDOKA

Lloyd Dyer (Watford, huru),
Neil Danns (Bolton, huru),
Sean St Ledger (ameruhusiwa),
Zak Whitbread (Derby, huru),
Paul Gallagher (Preston, mkopo),
Marko Futacs (ameruhusiwa),
George Taft (Burton Albion, huru)

LIVERPOOL

WALIOSAJILIWA
Adam Lallana (Southampton, £23m),
Lazar Markovic (Benfica, £20m),
Emre Can (Bayer Leverkusen, £9.8m),
Rickie Lambert (Southampton, £4m)
Dejan Lovren (Southampton, £20m),
Divock Origi (Lille, £10m)

WALIOONDOKA

Luis Suarez (Barcelona, £75m),
Luis Alberto (Malaga, mkopo),
Iago Aspas (Sevilla, mkopo),
Andre Wisdom (West Brom, mkopo),
Divock Origi (Lille, mkopo)

MANCHESTER CITY

WALIOSAJILIWA
Fernando (Porto, £12m),
Bacary Sagna (Arsenal, free),
Willy Caballero (Malaga, £6m),
Bruno Zuculini (Racing Club, £1.5m)

WALIOONDOKA

Costel Pantilimon (Sunderland, huru),
Joleon Lescott (West Brom, huru)
Gareth Barry (Everton, huru),
Alex Nimely (ameruhusiwa),
Rony Lopes (Lille, mkopo),
Emyr Huws (Wigan, mkopo)

MANCHESTER UNITED

WALIOSAJILIWA
Luke Shaw (Southampton, £31.5m),
Ander Herrera (Athletic Bilbao, £29m),
Vanja Milinkovic (FK Vojvodina, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA

Alexander Buttner (Dinamo Moscow, £5.6m),
Rio Ferdinand (QPR, huru),
Nemanja Vidic (Inter Milan, huru),
Federico Macheda (Cardiff City, huru),
Jack Barmby (Leicester, huru),
Louis Rowley (Leicester, huru)
Ryan Giggs (amestaafu),
Patrice Evra (Juventus, £2.5m)
Bebe (Benfica, £2.4m)

NEWCASTLE

WALIOSAJILIWA
Remy Cabella (Montpellier, £12m),
Emmanuel Riviere (Monaco, £6m),
Siem de Jong (Ajax, £6m),
Daryl Janmaat (Feyenoord, £5m),
Ayoze Perez (Tenerife, £1.5m),
Jack Colback (Sunderland, huru)

WALIOONDOKA

Mathieu Debuchy (Arsenal, £10m),
James Tavernier (Wigan, ada haikutajwa,
Dan Gosling (Bournemouth, huru),
Shola Ameobi (ameruhusiwa),
Conor Newton (Rotherham, huru),
Michael Richardson (ameruhusiwa),
Sylvain Marveaux (Guingamp, mkopo)

QUEENS PARK RANGERS

WALIOSAJILIWA
Rio Ferdinand (Manchester United, huru),
Steven Caukler (Cardiff, £8m)

WALIOONDOKA

Tom Hitchcock (Mk Dons, huru),
Aaron Hughes (Brighton, huru)
Stephane Mbia (ameruhusiwa),
Andrew Johnson (ameruhusiwa),
Luke Young (ameruhusiwa),
Hogan Ephraim (ameruhusiwa),
Angelo Balanta (ameruhusiwa),
Yossi Benayoun (Maccabi Haifa, ada haikutajwa),
Esteban Granero (Real Sociedad, ada haikutajwa)

SOUTHAMPTON

WALIOSAJILIWA
Dusan Tadic (Twente, £10.3m),
Graziano Pelle (Feyenoord, £8m),
Ryan Bertrand (Chelsea, loan)

WALIOONDOKA

Luke Shaw (Manchester United, £31.5m),
Rickie Lambert (Liverpool, £4m),
Adam Lallana (Liverpool, £23m)
Guly do Prado (released),
Lee Barnard (Southend, huru),
Jonathan Forte (released),
Danny Fox (Nottingham Forest, huru),
Andy Robinson (Bolton, huru),
Tom Leggett (Aston Villa, ada haikutajwa),
Isaac Nehemie (Aston Villa, ada haikutajwa)
Dejan Lovren (Liverpool, £20m)
Calum Chambers (Arsenal, £12m)

STOKE CITY

WALIOSAJILIWA
Mame Biram Diouf (Hannover, huru),
Dionatan Teixeira (Banska Bystrica, ada haikutajwa),
Phil Bardsley (Sunderland, huru),
Steve Sidwell (Fulham, huru),
Bojan Krkic (Barcelona, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA

Michael Kightly (Burnley, ada haikutajwa),
Matthew Etherington (ada haikutajwa),
Juan Agudelo (ada haikutajwa)

SUNDERLAND

WALIOSAJILIWA
Billy Jones (West Brom, huru),
Jordi Gomez (Wigan, huru),
Costel Pantilimon (Manchester City, huru)
Patrick van Aanholt (Chelsea, ada haikutajwa)

WALIOONDOKA

Jack Colback (Newcastle, huru),
Craig Gardner (West Brom, huru),
Phil Bardsley (Stoke, huru),
Billy Knott (Bradford, huru)
Keiren Westwood (Sheffield Wednesday, huru),
Carlos Cuellar (ameruhusiwa),
Andrea Dossena (ameruhusiwa),
Louis Laing (ameruhusiwa),
Oscar Ustari (Newell's, huru),
David Vaughan (Nottingham Forest, huru),
John Egan (Gillingham, huru),
Ignacio Scocco (Newell's, £800,000)

SWANSEA

WALIOSAJILIWA
Marvin Emnes (Middlesbrough, £1.5m),
Bafetimbi Gomis (Lyon, huru),
Lukasz Fabianski (Arsenal, huru),
Stephen Kingsley (Falkirk, ada haikutajwa),
Gylfi Sigurdsson (Tottenham, ada haikutajwa)
Jefferson Montero (Monarcas Morelia, £4m)

WALIOONDOKA

Leroy Lita (ameruhusiwa),
David Ngog (ameruhusiwa),
Daniel Alfei (Northampton, mkopo),
Jernade Meade (ameruhusiwa),
Darnel Situ (ameruhusiwa),
Michu (Napoli, mkopo),
Ben Davies (Tottenham, £10m)
Michel Vorm (Tottenham, £5m)
Alejandro Pozuelo (Rayo Vallecano, ada haikutajwa)

TOTTENHAM

WALIOSAJILIWA
Ben Davies (Swansea, ada haikutajwa)
Michel Vorm (Swansea, £5m)

WALIOONDOKA

Jake Livermore (Hull, £6m),
Heurelho Gomes (Watford, huru),
Cameron Lancaster (ameruhusiwa),
Alex Pritchard (Brentford, mkopo),
Gylfi Sigurdsson (Swansea, mkopo)

WEST BROMWICH ALBION

WALIOSAJILIWA
Brown Ideye (Dynamo Kiev, £10m),
Craig Gardner (Sunderland, huru),
Joleon Lescott (Manchester City, huru),
Chris Baird (Burnley, huru),
Sebastien Pocognoli (Hannover 96, ada haikutajwa),
Andre Wisdom (Liverpool, mkopo)

WALIOONDOKA

Liam Ridgewell (Portland Timbers, huru),
Billy Jones (Sunderland, huru),
Steven Reid (Burnley, huru),
Cameron Gayle (Shrewsbury, huru),
Diego Lugano (ameruhusiwa),
Zoltan Gera (ameruhusiwa),
Scott Allan (ameruhusiwa),
Nicolas Anelka (ameruhusiwa),
George Thorne (Derby County, ada haikutajwa)

WEST HAM

WALIOSAJILIWA
Enner Valencia (Pachuca, £12m),
Cheikhou Kouyate (Anderlecht, £7m),
Mauro Zarate (Velez Sarsfield, ada haikutajwa),
Aaron Cresswell (Ipswich, ada haikutajwa),
Diego Poyet (Charlton, ada haikutajwa),
Carl Jenkinson (Arsenal, huru)

WALIOONDOKA

Joe Cole (Aston Villa, huru),
Matt Taylor (Burnley, huru),
Stephen Henderson (Charlton, huru),
Jack Collison (ameruhusiwa),
George McCartney (ameruhusiwa),
Callum Driver (ameruhusiwa),
Jordan Spence (ameruhusiwa),

Isike Samuel: Wasanii tuache wivu wa kijinga tusonge mbele

MUIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini, Isike Samwel amesema tabia za wivu, utengano na kutopendana miongoni mwa wasanii ndiko kunakofanya waendelee kulizwa na maharamia kwa kuwaibia kazi zao na kushindwa kusonga mbele.
Hivyo akawataka wasanii kubadilika na kupendana, kushirikiana na kusaidiana bila kujali uzoefu, umaarufu au uwezo wa kiuchumi walionao kwa vile wote wanasafiri katika 'jahazi' moja.
Akizungumza na MICHARAZO, Isike alisema gurudumu la fani ya sanaa hasa ya uigizaji imekuwa ikishindwa kusonga mbele kutokana na wasanii kutopendana na kuoneana kijicho pale mwenzao anapofanya vyema.
Isike alisema hivyo ni wajibu wasanii kubadilika kwani umoja, mshikamano na upendo itasaidia kuwafanya wawe kitu kimoja na kusaidia kupambana na watu wanaowanyonya na kuwaibia kazi zao wanazozitolea jasho kuziandaa.
"Bila umoja, upendo na ushirikiano ni vigumu fani yetu kusonga mbele, wasanii tumekuwa hatupendani wenyewe kwa wenyewe na watu wanaoneana wivu wa kijinga ambao unazorotesha maendeleo ya fani hiyo kwa ujumla," alisema.
Mkali huyo anayejiandaa kutoa filamu yake mpya iitwayo 'Naiogopa Kesho' kupitia kampuni binafsi ya Classic Vision alisema pia wasanii wazoefu wasiogope kuwapiga tafu chipukizi kwa hofu ya kufunikwa kwani hata wao waklisaidia na kupewa nafasi ndiyo maana wapo hapo walipo.

Cheki picha za ajali ya basi la iliyoua watu Arusha



 Muonekano wa basi la Hood kwenda Mbeya baada ya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha asubuhi ya leo.


 Wananchi wakiwa wamekusanyika baada ya basi la Hood kwenda Mbeya baada ya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha.


 Muonekano wa Hiace hiyo kwa mbele baada ya ajali.







Watu 5 wamekufa baada ya basi la Hood kwenda Mbeya kugongana na Hiace eneo la Kilala, Arusha asubuhi ya leo, wengi wajeruhiwa.

Lampard atua Manchester City kwa mkopo, Pellegrini athibitisha

KOCHA wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa kiungo wa zamani wa Chelsea, Frank Lampard keshokutwa ataanza mazoezi na wachezaji wa Manchester City kwenye uwanja wa Carrington kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo.
Pellegrini alisema kuwa Lampard atakuwa mchezaji muhimu kwenye mechi za ligi kuu na ligi ya mabingwa mpaka atakapoondoka kwenda Marekani mwezi Januari mwakani.
City imewasili nyumbani kutoka Marekani ilipokuwa katika maandalizi ya ligi na kucheza mechi kadhaa za kimataifa maalum kabla ya jana jumapili kupoteza nafasi ya kucheza fainali ya michuano hiyo kwa kufungwa kwa penati ikiwa ni mecxhi yao ya pili katika siku nne kupoteza kwa mikwaju ya penati.
Baada ya mechi, Pellegrini kwa mara ya kwanza alizungumzia kumsajili Frank kwa mkopo na kusema maamuzi ya kumchukua kiungo huyo wa kimataifa wa England mwenye miaka 36 ni kumfanya awe fiti kabla ya kuanza kuichezea klabu yake ya New York City mwakani.
Lampard alijiunga na New York City akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Chelsea.
Pellegrini alisema: "Kuanzia jumatano ijayo ataanza kufanya kazi na timu na atacheza mpaka januari na tutaona baada ya hapo".
"‘Kwa wakati huu atafanya kazi na kikosi na atakuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi. Atapambana kusaka nafasi"
"Anajua tuna timu nzuri, tuna wachezaji wengi katika nafasi yake na yeye ameongezeka. Tuna mechi nyingi sana hususani za ligi ya mabingwa, kwahiyo ni mtu muhimu sana kwa timu".

Simba wam-delete Wambura na wenzake jumla Msimbazi

Michael Wambura
Mwenyekiti wa Simba, Evance Aveva
ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Soka ya Simba uliofanyika mwezi Juni mwaka huu, Michael Wambura, pamoja na wanachama wengine 70 jana walifutwa rasmi uanachama wa klabu hiyo kutokana na hatua ya kufungua kesi kwenye mahakama za kawaida jambo ambalo ni kinyume na katiba.
Maamuzi ya kumfuta uanachama Wambura pamoja na wanachama wengine yalifikiwa kwa pamoja jana katika Mkutano Mkuu wa mwaka uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wanachama 860 waliokutana jana hawakutaka agenda hiyo ya 12 ijadiliwe na badala yake wakisema kwa sauti kwamba wanachama hao wafutwe mara moja.
Agenda hiyo ya kuwajadili wanachama hao ambao awali walisimamishwa na Kamati ya Utendaji ilianza kujadiliwa saa 6:33 mchana na ilipofika saa 6:49 mchana Aveva alitangaza kwamba wanachama hao 71 wamefutwa uanachama wao kutokana na kwenda kinyume na ibara ya 55 ya Katiba ya Simba.
Kabla ya kutoa maamuzi hayo, Aveva alisema alipokea maoni mbalimbali kutoka kwa wanachama na aliamua kumtumia mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Ramesh Patel, ili akutane na wanachama hao kwa ajili ya kupata suluhu.
Aveva alisema wanachama hao walielezwa na Patel kwamba wanatakiwa kwanza wafute kesi waliyoifungua Juni 23, mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam na kwamba walikataa na hakuna kati yao ambaye alijitokeza kukanusha kuhusika na uvunjwaji huo wa katiba.
"Natangaza rasmi watu wote 71 sio wanachama wa Simba Sports Club kuanzia leo (jana)", alisema Aveva na kumaliza agenda hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na wanachama waliohudhuria mkutano huo.
Rais huyo alisema kwamba wanachama walikosea kwa kupinga bila kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Fifa.
NIPASHE lilipomtafuta Wambura jana ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT sasa TFF,  kuelezea maamuzi hayo yaliyochukuliwa na mkutano mkuu wa wanachama, alisema "siwezi kuzungumza lolote kwa sasa hadi nitakapopewa barua ya kufahamishwa kufutwa uanachama."

MABADILIKO YA KATIBA
Wanachama wa klabu hiyo pia walifanya mabadiliko kadhaa katika baadhi ya vipengele vya katiba ikiwamo ibara ya 5 inayoainisha aina ya wanachama kwa kuteua wanachama wa heshima ambao waliitumikia Simba kwa muda mrefu na kutoa mchango mkubwa.
Ibara ya 18 sasa inasomeka kuwa wadhamini wa klabu watakuwa wanne na ndiyo wamiliki na wadhibiti wa mali zote za klabu zinazohamishika na zisizohamishika. Pia mkutano mkuu ndiyo utakuwa na mamlaka ya kumuondoa mdhamini kutoka kwenye wadhifa huo baada ya kupata taarifa kutoka katika Kamati ya Utendaji.
Kipengele kingine kilichofanyiwa marekebisho ni cha ibara ya 22 ambacho kinaelezea Mkutano Mkuu wa dharura sasa kinasema kuwa wanachama wasiopungua 1000 waliojiorodhesha ndiyo wanaweza kuomba mkutano huo kwa maandishi na Kamati ya Utendaji itatakiwa kuitisha mkutano ndani ya siku 30 baada ya kuwasilisha ombi.
Ibara ya 25 (8) (111) inayompa nguvu rais wa klabu kuteua wajumbe wengine watano wa Kamati ya Utendaji ambao anaweza kuwabadilisha kwa kadri anavyoona inafaa ilipitishwa lakini baadhi ya wanachama walikuwa wakiipinga kwa madai kwamba itafanya kiongozi huyo wa juu kuwa dikteta.
Wanachama hao pi walitoa ridhaa ya kuundwa kwa Kamati ya Maadili (ibara ya 40) huku ibara ya 42 ikieleza kwamba kutaundwa Kamati ya Nidhamu ya Simba ambayo Mwenyekiti na Makamu wake lazima wawe na taaluma ya sheria.
Mkutano huo uliamua kwamba kila tawi litaendelea kuwa na wanachama kuanzia 50 na wasiozidi 250 na kukataa idadi ya tawi moja kuundwa na wanachama 500 kwa kuhofia 'mapinduzi'.

SITTA, MO WAULA SIMBA
Rais huyo aliyechaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Juni 29, mwaka huu pia aliwatangaza wadhamini wapya wa klabu hiyo kuwa ni pamoja na Samwel Sitta, Patel, Hassan Dalali na Adam Mgoyi.
Aveva pia aliwatangaza wanachama wengine wanne ambao watakuwa ni walezi wa Simba kuwa ni aliyekuwa mfadhili wa klabu hiyo, Mohammed Dewji 'Mo', Naibu Waziri Wizara ya Maji, Amos Makalla , Jaji, Thomas Mihayo na Zacharia Hanspoppe.
Wadhamini na walezi hao walithibitishwa na mkutano huo na watatambuliwa kwa muda wa miaka minne.

NIPASHE

Ligi ya wanawake Dar kuanza Agosti 28

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi18rX9xD35fNe7sEatYXVlGC5N3kSwbk9mXkU2mRjmrbN47__02bzOL9rdGPuJ38cYQFWp_mNmtz0P5wM3cy1brDiJZh5qAZscl9N3Ld9QlevvNQlROe21kwK6qmSoSplekcOY7eXmxfQ/s1600/MADEM.JPG 
LIGI ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam inatarajiwa kuanza Agosti 28 mwaka huu katika viwanja vya  Benjamin Mkapa, Bandari na Makurumla.

Ofisa Habari wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Mohamed Mharizo alisema kuwa ligi hiyo ni moja ya mkakati wao wa kuimarisha mchezo ili uweze kuwa na hamasa kwa wanawake.

Alizitaja timu zitakazoshiriki ligi hiyo kuwa ni Mburahati Queens, Evergreen Queens, Sayari, Real Tanzanite, Uzuri Queens,  Simba Queens,  BYC Queens, JKT Queens,  Lulu Queens,  Mchangani Sisters, TMK Queens, Msimamo Queens na Mikocheni Queens.

“Kwa kweli ligi ya wanawake nayo ni muhimu kama ilivyo kwa wanaume, lengo letu ni kuona wanawake wanakuwa na ligi yao na sisi tunaona hili ni jambo zuri ambalo litasaidia kupata wachezaji wa timu ya taifa (Twiga Stars).

Mharizo aliyaomba makampuni na taasisi mbalimbali kujitokeza kudhamini ligi hiyo ili iweze kuleta ushindani kwa timu shiriki.

Stars si Riziki AFCON, kama kawa yanyukwa na Msumbiji

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/07/taifa.jpgUTEJA wa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) mbele ya Msumbiji umeendelea baada ya kutolewa katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa wenyeji Msumbiji (Mambas) katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Zimpeto mjini Maputo.
Kwa ushindi huo, Mambas wamesonga mbele katika mashindano hayo kwa kutinga hatua ya makundi baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-3 baada ya awali kutoka sare ya 2-2 katika mechi iliyochezwa Julai 20, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mambas walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa mbele kwa bao 1-0 lililofungwa na Josemar sekunde chache kabla timu hizo hazijaenda mapumziko.
Mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Samata, aliisawazishia timu yake bao la kwanza katika dakika ya 77 na kuufanya mchezo huo uzidi kuwa mgumu kwa pande zote mbili.
Dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho kupulizwa na mwamuzi, Dennis Batte kutoka Uganda, Domingues alizima ndoto za Taifa Stars kutinga hatua ya makundi baada ya kuipatia Mambas bao la pili na la ushindi.
Stars ilikuwa hivi; Deogratius Munishi ‘Dida’, Said Mourad, Shomary Kapombe, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Erasto Nyoni, Thomas Ulimwengu, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Mbwana Samata na Khamis Mcha ‘Vialli’.
Katika benchi waliwapo Aishi Manula, Aggrey Morris, Oscar Joshua, Haroun Chanongo, Mrisho Ngassa, Simon Msuva na Amri Kiemba.
Baada ya kushindwa kutinga hatua ya makundi, Tanzania ikiwa chini ya kocha huyo, Mholanzi Mart Nooij, itasubiri kucheza mashindano ya Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki huku ikiwa watazamaji kwenye fainali zijazo za Afcon zitakazochezwa nchini Morocco mwakani.
Wakati huo huo mjini Kigali juzi timu ya soka ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) juzi Jumamosi ilifanikiwa kusonga mbele katika mashindano hayo ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuiondoa Congo kwa njia ya penalti 4-3 baada ya matokeo ya jumla kuwa 4-4.
Amavubi juzi ilipata ushindi wa mabao 2-0 ikiwa nyumbani wakati Congo nayo ilipata ushindi wa aina hiyo ilipokuwa nyumbani na kusababisha mechi hiyo kutinga hatua ya matuta.
Nyota wa mechi ya juzi mjini Kigali alikuwa ni kipa wa Amavubi, Jean Luc ‘Bakame’ Ndayishimiye, ambaye alidaka penalti tatu za Congo zilizopigwa na Ferebory Dore, Mael Francis Lepicier na Herman Lakolop wakati Delvin Chansel Ndinga, Silver Mbousi Ganvoula na Thierry Koulossa Bifouma walifunga.
Kwa upande wa Amavubi waliopata ni Jimmy Mbaraga, James Tubane, Emery Bayisenge na Patrick Sibomana wakati Haruna Niyonzima aligongesha mwamba na ile ya Meddy Kagere ilidakwa na kipa wa Congo, Chasel Mohikola Massa.
Amavubi sasa itaungana na mabingwa watetezi wa michuano hiyo Nigeria, Afrika Kusini na Sudan kwenye Kundi A.
Harambee Stars ya Kenya jana ikiwa nyumbani ililazimishwa suluhu na Lesotho hivyo kuyaaga mashindano hayo kufuatia kichapo cha bao 1-0 ilichopata ugenini wiki mbili zilizopita.