STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 3, 2014

'Hii ndiyo dawa ya kuiepushia TZ aibu michezo ya kimataifa'

Mkurugenzi wa Joyland International School, Fredrick Otieno akihutubia wageni katika hafla iliyofanyika jana shuleni kwao Kigamboni.

Mkurugenzi wa Joyland International School, Fredrick Otieno akicheza muziki na wanafunzi wake
http://2.bp.blogspot.com/-OAIXB-JHlqE/U0AcWhXHzjI/AAAAAAAALEs/jMOqUKCPU2A/s1600/Joy12.JPG
Fredrick Otieno (kulia) akionyesha kipajo chake cha kucheza muziki akichuana na mmoja wa walimu wake
WAKATI mabondia wa Tanzania waliokuwa wakishiriki michezo ya Jumuiya ya Madola nchini Scotaland wakitarajiwa kuanza kurejea kesho kwa mafungu, imefichuliwa dawa ya kuiondolea aibu Tanzania katika michezo ya kimataifa.
Imeelezwa dawa pekee ya Tanzania kufanya vizuri michezo ya kimataifa ni kuwaandaa wachezaji tangu wangali wadogo wakiwa wamejengwa moyo wa kizalendo na ufahamu wa mchezo husika badala ya kukurupuka.
Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland na nyota wa zamani wa soka wa nchini Kenya, Fredrick Otieno, ndiye aliyefichua hayo wakati wa mahafali ya kwanza ya wanafunzi wa Chekechea shuleni kwao, Kigamboni jijini Dar.
Otieno aliyewahi kuichezea Gor Mahia, alisema ili Tanzania iweze kuja kutamba katika michuano ya kimataifa ni lazima ikubali kuwekeza michezo mashuleni na kuwaandaa vijana na siyo kutegemea miujiza.
Alisema amekuwa akijisikia aibu kila mara timu na wanamichezo wa Tanzania wakichemsha kwenye michuano ya kimataifa licha ya ahadi na mbwembwe nyingi na kuamini siasa zikiondolewa michezoni Tanzania itang'ara kimataifa.
"Hakluna njia ya mkato kuyaendea mafanikio katika michezo zaidi ya kuwekeza na kuwajengea misingi imara wenye vipaji tangu utotoni, na katika kuliunga hilo shule yetu inatarajia kuanzisha mtaala wa kimataifa ambao utahusisha poa masuala ya michezo," alisema Otieno.
Otieno alisema kama kila shule itakuwa na programu za michezo kama moja ya somo la darasani na wanafunzi wenye vipaji wakaanza kupikwa mapema ni wazi miaka michache ijayo Tanzania itakuwa na wanamichezo wenye kutisha.
"Zamani michezo ilipewa kipaumbele na kushuhudia Tanzania ikitoa nyota mbalimbali, siasa zilikuja kuua suala hilo. Sasa ni lazima tuamke na Joyland inataka kuonyesha mfano wa kuja kutoa nyota mbalimbali wa michezo watakaokuja kulisaidia taifa na nawahimiza wengine wafanye hivyo," alisema.
Alisema anajisikia aibu kusikia Tanzania imeenda Scotland na kuambulia patupu katika michezo ya Jumuiya ya Madola na kudai ni wakati wa serikali na wadau wa michezo kwa ujumla kujipanga kuifuta aibu hiyo siku za baadae.

KUMEKUCHA TAMASHA LA FILAMU LA DFF 2014

http://3.bp.blogspot.com/-V1BZ8KrjkOQ/UAlPDmkh4fI/AAAAAAAAABc/KXFPoOBEDYs/s640/lulu+1.jpg
Mabalozi wa mwaka jana wa DFF, Ray na Lulu katika pozi
TAMASHA kubwa la Filamu la Dar es Salaam maarufu kama Dar Filamu Festival (DFF) 2014 lipo njiani kufanyika likiwa na kauli mbiu isemayo "Filamu Zetu, Maisha Yetu".
Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Staford Kihore aliiambia MICHARAZO kuwa kila kitu kwa ajili ya tamasha hilo kipo tayari na kuanzia sasa utaratibu utatangazwa.
Kihore alisema tamasha lao limejikita katika kuhakikisha kazi za ndani ambazo zinazalishwa kwa wingi nchi zinapata fursa ya kutangazwa na kuingia katika majumba ya sinema sehemu ambayo ni biashara mpya na inayolipa haraka zaidi tofauti na Dvd na liliasisiwa mwaka jana na kufana.
"Dar Filamu Festival ni mkombozi wa mtayarishaji wa filamu Tanzania, lakini kitu kingine muhimu sana ni ukuzaji na kuitangaza Lugha ya Kiswahili ambayo ni biashara nyingine na alama ya filamu zetu," alisema.
Alisema ni fursa kwa watayarishaji kuwa tayari kupeleka filamu zao kwa ajili ya ushiriki wa tamasha hilo kubwa na la kimataifa, na ni sehemu ya kupata soko jipya kwani tamasha la mwaka huu litahusisha pia wageni kutoka nchi mbalimbali.
“Tamasha la mwaka jana lilifanikiwa sana kwani kwa mara ya kwanza tuliweza kuona filamu katika ubora mkubwa kuanzia sauti, picha na mambo mengine, mwaka huu tunakuja na kauli mbiu "Filamu Zetu, Maisha Yetu'" alisema Kihore.
Aliongeza kuwa, pia tamasha la DFF 2014 litaambatana na semina za utengenezaji wa filamu utoaji wa tuzo kwa filamu zilizofanya vizuri kwa mwaka wa 2013/2014 ikiwa ni katika hali ya kuwatia motisha watengenezaji wa filamu Bongo.
Alidokeza kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutangaza mabalozi wa DFF 2014 baada ya mwaka kamati yao kuwateua  Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vincent Kigosi 'Ray'.

Tip Top Connection, TMK Wanaume wakumbushia Chama Kubwa

http://www.timesfm.co.tz/content/uploads/2014/7/10/cache/ww_full.JPG
Wakurugenzi wa makundi ya Top Top na TMK Wanaume Family, Said Fella na Babu Tale
http://3.bp.blogspot.com/-LsI64tMFQBg/T1wNxmujNBI/AAAAAAAAYbw/FWVqKaJwVR0/s400/19.JPG
Baadhi ya vichwa vya Tip Top
http://4.bp.blogspot.com/-W-dvzzBAMBc/Ue0Th2svlxI/AAAAAAAAQVQ/6WM5hJx_4NM/s640/b2b31624f03011e29c2822000a1fbe4c_7.jpg
Majembe ya TMK Wanaume Family
MAKUNDI maarufu ya muziki wa kizazi kipya nchini, Tip Top Connection na TMK Wanaume Family wameungana tena na kurekodi kati ya pamoja wakikumbushia enzi za kibao chao cha 'Chama Kubwa'.
Makundi hayo yanayoongozwa na wadau wakubwa wa muziki nchini Said Fella 'Mkubwa' na Hamis Tale 'Babu Tale' yamerekodi wimbo huo katika studio za Barning Records, japo mpaka sasa bado hawajaupa jina mpaka kwanza wajadiliane kuutafuta jina muafaka.
Akizungumza na MICHARAZO, mmoja wa wasanii wanaounda makundi hayo, Madee alisema wimbo huo unatarajiwa kuachiwa hewani mara baada ya kutungiwa jina na ni moja ya wimbo bomba.
"Baada ya kitamboi kirefu tangu tutoe Chama Kubwa, Tip Top Connection na TMK Wanaume Family tumeungana tena na kufyatua wimbo wa pamoja ambao bado hatujaupa jina mpaka sasa," alisema Madee.
Madee alisema wimbo huo umewashirikisha wasanii wa makundi hayo yote akiwamo yeye mwenyewe (Madee), Tundaman, Dogo Janja, Chege, Mheshimiwa Temba.
Msanii huyo aliongeza mara baada ya wimbo huo kuanza kurushwa hewani wataanza mchakato wa kurekodi video ya wimbo huo.

Madee kuweka shida zake videoni

http://4.bp.blogspot.com/_43Ui7xqwc_E/TIeMqUIJjVI/AAAAAAAAAA0/xFDGRaAVXwI/s1600/Mtu+mzima+Madee.jpg
Madee katika pozi
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Hamad Ally 'Madee' a.k.a Rais wa Manzese, anajianda kuanza kurekodi video ya wimbo wake mpya unaoendelea kutamba katika vituo vya redio uitwao Ni Sheeda'.
Akizungumza na MICHARAZO, Madee alisema ndani ya wiki mbili zijazo video ya wimbo huo itakuwa hewani kwani ameanza maandalizi ya kuirekodi.
Madee alisema video hiyo itarekodiwa na kampuni ya Next Level Production chini ya mtaalam Adam Juma na itafanyiwa katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.,
"Nipo katika maandalizi ya kurekodi video ya wimbo wangu mpya wa 'Ni Sheeda' (Ni Shida) kazi hiyo itafanywa na Adam Juma na huenda ikakamilika ndani ya wiki mbili kabla ya kuiachia hewani," alisema.
Madee alisema anaharakisha kutoa video hiyo kutokana na maombi ya mashabiki wengi wa muziki ambao wanataka kuona uhalisia wa wimbo huo ambao umekuwa gumzo kwa sasa nchini.
"Mashabiki wamekuwa wakiulizia mno juu ya video yake ndiyo maana nataka kuitoa mapema kabla ya kufanya mambo mengine," alisema Madee.
Mkali huyo anayeliongoza kundi la Tip Top Connection, kabla ya wimbo huo wa 'Ni Sheeda' Madee alitamba na nyimbo kama 'Pesa', 'Kazi yake Mola', 'Tema Mate', 'Pombe Yangu', Hip Hop Haiuzi na 'Yote Maisha'.

Jennifer Mgendi ajianda kumtoa Mama Mkwe

http://www.jennifermgendi.com/images/gallery/1361202026.JPG
Jennifer Mgendi katika pozi
MUIMBAJI nyota wa Nyimbo za Injili nchini ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi amekamilisha filamu yake mpya iitwayo 'Mama Mkwe' ambayo amewashirikisha wasanii kadhaa nyota wa filamu na miondoko ya Injili akiwamo Mussa Banzi na Bahati Bukuku.
Filamu hiyop inatarajiwa kuachiwa hadharani wakati wowote ndani ya mwezi huu na Jennifer amewataka mashabiki wa filamu wasiikose filamu hiyo kutokana na kubeba ujumbe mwanana wenye mafunzo makubwa kwa jamii.
Akizungumza na MICHARAZO, Jennifer alisema filamu hiyo iliyoongozwa na Mgeni Khamis na Chrissant Mhega wa Mega  Video Production imekamilika wiki iliyopita na sasa ipo katika maandalizi ya kuachiwa kwa sasa.
Jennifer anayetamba na albamu ya Hongera Yesu, alisema ndani ya filamu hiyo inayozungumzia mkasa wa mama mkwe anayemlilia mwanae wa kiume kumletea mjukuu na kuzua kizaazawa wamo pia Senga,Bi Bi Esther, Christine Matai, Husna Chobis. yeye (Mgendi)  na wengine ambao wameinoigesha vilivyo.
"Nimekamilisha filamu yangu mpya ya 'Mama Mkwe' ambayo nimeigiza mimi, Bahati (Bukuku) Christine Matai, Senga, Bi Esther, Mussa Banzi na wengine. Ni filamu yenye mafunzo makubwa kwa jamii na hasa mama wakwe wanaoingilia ndoa za watoto wao," alisema.
Kabla ya filamu hiyo, Jennifer amewahi kutamba na filamu kadhaa kama 'Chai ya Moto', 'Joto la Roho', 'Teke la Mama', na 'Pigo la Faraja'.

Hivi ndivyo mahafali ya kwanza ya Pre Primary Joyland yalivyofana

Mgeni Rasmi wa Mahafali hayo Bi Bushra Malik Regional Development Manager wa Edexcel akizungumza kwenye shughuli hiyo zilizofanyika jana Kigamboni, Dar es Salaam
Mmoja wa wahitimu wa kozi ya Kiingereza inayotolewa bure shuleni Joyland akipokea cheti chake toka kwa Bi Bushra Malik

Mmoja ya wanafunzi waliofanya vyema katika mitihani akipewa zawadi yake na mmoja wa wageni waalikwa wa hafla hizo
Mwanafuzi Ansilath Kwariko akilia kwa furaha wakati akijiandaa kupokea zawadi yake
Madogo kwa kuimba hawajambo
Wahitimu wa Pre Primary wakiongozwa na mwalimu wao kuingia eneo la tukio
Sisi tunajua kuimba
Mkurugenzi wa Joyland International School, Fredrick Otieno akisaini mkataba wa kurushwa kwa vipindi vya shule yake na kituo cha Channel Ten huku akishuhudiwa na mwakilishi wa Idara ya Masoko ya kituo hicho

Saini hapa.....Tutakurusha hewani mpaka basi! Mwakilishi wa Channel Ten akimuangalia Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland akisaini mkataba walioingia baina yao kwa mujibu wa taarifa zilizotangazwa kwenye hafla hiyo jana.
Wanafunzi wa Grade 5 wakitumbuiza

Siyo kuhitimu tu hata kuimba nasi tunajua
Mkurugenzi wa Joyland, Fredrick Otieno  akionyesha ufundi wa kucheza akichuana na wanafunzi wake

Yebhaa! Mnacheza hivi bhana!
Full Vipaji Joyland International School
Hongera kwa kumaliza kozi!
Msosi nao ulikuwapo kuwafariji wahitimu

Kadhalika vinjwaji navyo viliburudisha makoo ya watoto

Tupo makini na watoto wenu, tunawaangalia vya kutosha kuhakikisha wapo salama
Mkurugenzi wa Joyland International School, Fredrick Otieno akizungumza kwenye hafla hiyo
WAZAZI na walezi nchini wamehimizwa kuwapatia elimu watoto wao ili kuwajengea msingi imara wa maisha yao kwa kuwa, elimu ni hazina isiyoweza kuharibika au kuibwa na yeyote.
Aidha wazazi na walezi pia wamekumbushwa kujenga utamaduni wa kuwa na mahusiano mazuri baina yao na walimu wanaosoma watoto wao sambamba na kufuatilia nyendo za watoto wao ili kulinda wasiharibike.
Wito huo ulitolewa juzi na Mkurugenzi wa Shule ya Kimataifa ya Joyland, Fredrick Otieno wakati akizungumza na wazazi na walezi waliohudhuria mahafali ya kwanza ya wahitimu wa Chekechea wa shule hiyo.
Otieno alisema elimu ndiyo msingi wa kila kitu kwa maisha ya binadamu, hivyo wazazi wajenge utamaduni wa kuwa wepesi kuwasomesha watoto wao ili kuwajengea msingi mzuri wa mustakabali wa maisha yao ya ukubwani.
Alisema wapo baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wepesi kuwanunulia watoto wao vitu vyenye thamani, lakini wanakuwa wagumu kuwalipia watoto ada au kuwapatia elimu bora bila kujua kama wanawaharibia maisha yao ya ukubwani ambayo hujengwa na elimu bora ya utotoni.
"Dunia ya sasa imebadilika, bila elimu ni kazi bure hivyo wazazi na walezi wakubali kujinyima mradi kuwapatia watoto wao elimu bora itakayowasaidia maisha yao ya ukubwani," alisema.
Alidokeza katika kuhakikisha shule yao inaendelea kuwapatia watoto elimu bora wanatarajia kuanzisha mtaala wa kimataifa utakaoenda sambamba na ule wa taifa ambao kwa sasa unafundishwa katika shule hiyo.
Nao wageni rasmi wa mahafali hayo, Bushra Maliki na Mchungaji Albert Okanga katika hotuba zao waliwaasa wazazi kujenga uhusiano mzuri na walimu ili kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na malezi mazuri kwa maisha yao ya baadae.
Bushra ambaye ni Meneja Maendeleo wa Edexcel tawi la Tanzania, alisema amejitolea kushirikiana na uongozi wa shule hiyo ya Joyland ili kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa ngazi ya kimataifa kwa lengo la kuinua elimu nchini na kusaidia watoto wa Tanzania kupata elimu inayostahiki katika dunia ya sasa.
Mchungaji Okanga kwa upande wake alisisitiza kwa kusema ni wazazi wanakijita katika kuwapa watoto huduma vipaumbele kwa ajili ya kuwajengea msingi imara wa maisha kuliko kuwastarehesha, sambamba na kuwa karibu na watoto wao kuwasikiliza kujua matatizo waliyonayo na kuwasaidia kwa haraka.
Katika mahafali hayo wanafunzi waliofanya vizuri mbali na wale wahitimu wa Pre Primary walizawadiwa sambamba na wahitimu wa mafunzo ya lugha ya Kiingereza yanayotolewa bure shuleni hapo kwa lengo la kusaidia ufahamu wa lugha hiyo ya kigeni.

'Ningeshangaa kama Yanga isingeenda Kagame'

http://2.bp.blogspot.com/-Ul1OP5Db9mM/UylVVoPJMCI/AAAAAAAArtc/6PetAMhfYOI/s1600/mzazi.JPG
KOCHA za zamani wa klabu ya Yanga, Kennedy Mwaisabula amesema angeishangaa sana Yanga kama isingekubali kwenda kushiriki michuano ya Kombe la Kagame ambayo inatarajiwa katikati ya wiki.
Mwaisabula alisema michuano hiyo ina faida kubwa kwa Yanga hivyo kama isingeenda Kigali-Rwanda kuishiriki angeiona timu ya ajabu.
Kocha huyo alisema alibaki njia panda juu ya tetesi zilizokuwa zikidai kuwa, Yanga isingeenda Kigali kwa vile haikuwa imepewa taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Alisema kama Yanga itaitumia vyema michuano ya Kagame itawasaidia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ilisogezwa mbele kwa ajili yao ili ishiriki vyema michuano hiyo.
"Yanga ipo chini ya kocha mpya, Marcio Maximo na ina wachezaji kadhaa wapya ilikuwa ina haki zaidi ya kushiriki michuano hiyo kuliko msimamo wao wa awali," alisema.
Alisema hata hivyo amefurahishwa na maamuzi ya mwisho yaliyotolewa na uongozi wa Yanga kuhusu kwenda Kigali akiamini itakuwa kipimo kizuri kwa kocha na Wabrazil, Andrey Coutinho na Genilson Santos ‘Jaja’ .
Yanga iliyopangwa kundi A na timu za Rayon Sport ya Rwanda, KMKM ya Zanzibar na Atlabara ya Sudani Kusini itaanza kibarua cha kuwania taji hilo iliyotwaa mara tano kuumana na wenyeji Rayon.

Taifa Stars kufanya maajabu Maputo Leo

http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/05/DSC_457511.jpgLICHA ya Taifa Stars kuwa na pambano gumu leo mjini Maputo, Msumbiji itakaporudiana na wenyeji wao, Mambas baadhi ya nyota wa timu hiyo wametamba kufanya maajabu.
Stars ambayo imekuwa ikinyanyaswa na Mambas inahitaji ushindi wowote ili kupenya hatua ya makundi ya kuwania kucheza Fainali za AFCON-2015 zitakazochezwa Morocco.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa wiki mbili zilizopita, Stars ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dakika za mwishoni na kujiweka katika wakati mgumu kwa mechi hiyo ya ugenini.
Hata hivyo baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wametamba kabla ya kuelekea Maputo kwamba watafanya maajabu ambayo wengi hawayatarajii kwa kuing'oa Mamba kwao.
Nahodha wa Stars, Nadir Haroub 'Cannavaro', kipa Deo Munishi 'Dida' na John Bocco kwa nyakati tofauti walisema kuwa wana ari kubwa ya kulipigania taifa leo Maputo.
"Ni kweli mechi yetu itakuwa ngumu kwa vile tutakuwa ugenini, ila tumejipanga kuhakikisha tunaivusha Stars hatua ya makundi na Inshallah mtuombee," alisema Cannavaro.
Cannavaro alisema wachezaji wamezingatia maelekezo ya kocha Mart Nooij baada ya kufanya uzembe katika mechi iliyopita ambapo Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-1 hadi dakika ya 87 kabla ya wageni Msumbiji klusawazisha.
Dida kwa upande wake alisema kila mchezaji wa Stars anajua wajibu wake kwa siku ya leo Jumapili mjini Maputo na amewaomba watanzania waungane nao kwa dua njema.
Msumbiji imekuwa na zali la kuikwamisha Stars kila inapokutana katika hatua kama hiyo ya kuwania kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Mara ya kwanza waliwazuia kwenda fainali za Ghana za mwaka 2008 na mwaka jana ilirudia tena na kuwafanya mashabiki wa soka kuamini Stars leo ina kazi ngumu Maputo.
Kama Stars itapenya kwa Mambas, itaangukia katika kundi F ambalo litakuwa na timu za Zambia, Niger na Cape Verde ili kuanza kusaka tiketi ya kwenda Morocco mwakani.

Kocha Herve Renard alamba shavu Tembo wa Ivory Coast


KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia, Mfaransa Herve Renard ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ivory Cost.
Renard aliyeipa taji Zambia katika Fainali za Afrika za mwaka 2012 kwa kuilaza Ivory Coast amenyakuliwa na vinara hao wa Afrika kurithi nafasi ya Sabri Lamouchi aliyejiuzulu baada ya nchi hiyo kutolewa katika hatua ya makundi ya Fainali za Dunia 2014.
Renard mwenye miaka 45 alichaguliwa miongoni mwa majina matatu ya mwisho yaliyowajumuisha kocha wa zamani wa Sporting na Benfica, Jose Manuel De Jesus kutoka nchini Ureno na Frederic Antonetti, kocha wa zamani wa timu ya Rennes ya Ufaransa.
Beki huyo wa zamani, aliyeiongoza Zambia kupata ushindi dhidi ya Ivory Coast kwenye mechi ya fainali ya mataifa ya Afrika mwaka 2012 nchini Gabon, amepewa kazi ya kuhakikisha Tembo hao wanafuzu fainali za AFCON 2015 nchini Morocco.
Rais wa chama cha soka nchini Ivory Coast alisema Renard ndiye mwenye mpango mzuri kwa nchi hiyo, na hata mshahara wake aliotaja unalipika, hivyo ndiye aliyestahili.
Renard anakabiliwa na changamoto ya kuitengeneza timu upya baada ya wachezaji wengi kutupwa na umri.
Pia mashabiki na vyombo vya habari vimekuwa vikiiponda timu hiyo, hivyo ni kazi kwake kuiweka sawa.
Kocha huyu amesaini mkataba wa miaka mwiwi ambao unaweza kuongezwa kama atafanya vizuri,na hii kwa mujibu wa rais wa chama cha soka nchini Ivory Coast, Augustin Sidy Diallo.

Kilichomponza Lukaku Chelsea hadharani

http://i1.liverpoolecho.co.uk/incoming/article6554287.ece/alternates/s615b/3366398.jpg
LICHA ya Romelu Lukaku kuwa mfungaji mzuri, mwenye kasi na umri mdogo wa miaka 21 tu, kocha Jose Mourinho alipoteza mapenzi dhidi yake saa 72 tu baada ya kukosa penalti wakati wa kupigiana "matuta" katika fainali ya European Super Cup dhidi ya Bayern Munich Septemba mwaka jana.
Kisha Desemba mwaka jana Mourinho akasema: "Romelu Lukaku anapenda kuongea. Ni kijana mdogo anayependa sana kuongea. Lakini jambo ambalo halisemi ni kwa nini ameenda Everton kwa mkopo.
"Hilo ndilo jambo pekee ambalo hasemi. Na mara ya mwisho nilipowasiliana naye nilimwambia hilo hilo. Ni jambo ambalo alipaswa kulisema, sababu kwanini hayuko na Chelsea na yuko Everton."
Lukaku ameuzwa rasmi kwa Everton kwa paundi milioni 28, ada ya uhamisho ambayo imevunja rekodi ya klabu hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Mbelgiji mwenzake Marouane Fellaini aliyenunuliwa kwa paundi milioni 15, na amesaini mkataba wa miaka mitano.