STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 3, 2014

KUMEKUCHA TAMASHA LA FILAMU LA DFF 2014

http://3.bp.blogspot.com/-V1BZ8KrjkOQ/UAlPDmkh4fI/AAAAAAAAABc/KXFPoOBEDYs/s640/lulu+1.jpg
Mabalozi wa mwaka jana wa DFF, Ray na Lulu katika pozi
TAMASHA kubwa la Filamu la Dar es Salaam maarufu kama Dar Filamu Festival (DFF) 2014 lipo njiani kufanyika likiwa na kauli mbiu isemayo "Filamu Zetu, Maisha Yetu".
Mratibu Mkuu wa tamasha hilo, Staford Kihore aliiambia MICHARAZO kuwa kila kitu kwa ajili ya tamasha hilo kipo tayari na kuanzia sasa utaratibu utatangazwa.
Kihore alisema tamasha lao limejikita katika kuhakikisha kazi za ndani ambazo zinazalishwa kwa wingi nchi zinapata fursa ya kutangazwa na kuingia katika majumba ya sinema sehemu ambayo ni biashara mpya na inayolipa haraka zaidi tofauti na Dvd na liliasisiwa mwaka jana na kufana.
"Dar Filamu Festival ni mkombozi wa mtayarishaji wa filamu Tanzania, lakini kitu kingine muhimu sana ni ukuzaji na kuitangaza Lugha ya Kiswahili ambayo ni biashara nyingine na alama ya filamu zetu," alisema.
Alisema ni fursa kwa watayarishaji kuwa tayari kupeleka filamu zao kwa ajili ya ushiriki wa tamasha hilo kubwa na la kimataifa, na ni sehemu ya kupata soko jipya kwani tamasha la mwaka huu litahusisha pia wageni kutoka nchi mbalimbali.
“Tamasha la mwaka jana lilifanikiwa sana kwani kwa mara ya kwanza tuliweza kuona filamu katika ubora mkubwa kuanzia sauti, picha na mambo mengine, mwaka huu tunakuja na kauli mbiu "Filamu Zetu, Maisha Yetu'" alisema Kihore.
Aliongeza kuwa, pia tamasha la DFF 2014 litaambatana na semina za utengenezaji wa filamu utoaji wa tuzo kwa filamu zilizofanya vizuri kwa mwaka wa 2013/2014 ikiwa ni katika hali ya kuwatia motisha watengenezaji wa filamu Bongo.
Alidokeza kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kutangaza mabalozi wa DFF 2014 baada ya mwaka kamati yao kuwateua  Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Vincent Kigosi 'Ray'.

No comments:

Post a Comment