STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, August 3, 2014

Jennifer Mgendi ajianda kumtoa Mama Mkwe

http://www.jennifermgendi.com/images/gallery/1361202026.JPG
Jennifer Mgendi katika pozi
MUIMBAJI nyota wa Nyimbo za Injili nchini ambaye pia ni muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi amekamilisha filamu yake mpya iitwayo 'Mama Mkwe' ambayo amewashirikisha wasanii kadhaa nyota wa filamu na miondoko ya Injili akiwamo Mussa Banzi na Bahati Bukuku.
Filamu hiyop inatarajiwa kuachiwa hadharani wakati wowote ndani ya mwezi huu na Jennifer amewataka mashabiki wa filamu wasiikose filamu hiyo kutokana na kubeba ujumbe mwanana wenye mafunzo makubwa kwa jamii.
Akizungumza na MICHARAZO, Jennifer alisema filamu hiyo iliyoongozwa na Mgeni Khamis na Chrissant Mhega wa Mega  Video Production imekamilika wiki iliyopita na sasa ipo katika maandalizi ya kuachiwa kwa sasa.
Jennifer anayetamba na albamu ya Hongera Yesu, alisema ndani ya filamu hiyo inayozungumzia mkasa wa mama mkwe anayemlilia mwanae wa kiume kumletea mjukuu na kuzua kizaazawa wamo pia Senga,Bi Bi Esther, Christine Matai, Husna Chobis. yeye (Mgendi)  na wengine ambao wameinoigesha vilivyo.
"Nimekamilisha filamu yangu mpya ya 'Mama Mkwe' ambayo nimeigiza mimi, Bahati (Bukuku) Christine Matai, Senga, Bi Esther, Mussa Banzi na wengine. Ni filamu yenye mafunzo makubwa kwa jamii na hasa mama wakwe wanaoingilia ndoa za watoto wao," alisema.
Kabla ya filamu hiyo, Jennifer amewahi kutamba na filamu kadhaa kama 'Chai ya Moto', 'Joto la Roho', 'Teke la Mama', na 'Pigo la Faraja'.

No comments:

Post a Comment