STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 20, 2015

Kavumbagu wairejesha Azam kileleni

http://3.bp.blogspot.com/-GUs_A5ZoF20/VBW6DLRDmeI/AAAAAAABIv4/kJGIPp59iy4/s1600/HERM5672-1.JPG
Kikosi cha Azam
MABAO mawili kutoka kwa Mrundi, Didier Kavumbagu na jingine la Kipre Tchetche, limeiwezesha Azam kurejea kileleni katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara naada yua kutungua Kagera Sugar mabo 3-1.
Pambano hilo la kiporo lilichezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, na iliowachukua Azam dakika tatu kuandika bao kupitia kwa Kipre Tchetche kabla ya Kavumbangu kufunga bao la pili.
Kagera walipunguza idadi ya magoli kipindi cha pili kutipia Rashid Mandawa, lakini Kavumbagu alirejea tena nyavuni kuandika bao la tatu na lililokuwa la saba kwake msimu huu na kuipa ushindi muhimu mabingwa watetezi hao walifikisha pointi 20 baada ya mechi 10.
Azam imeiengua Mtibwa Sugar wenye pointi 17, ingawa wakata miwa hao wa Manungu wana mchezo mmoja mkononi na Jumamosi wanatarajiwa kuvaana na Ruvu Shooting uwanja wa Mabatini, wakati Azam watakuwa na kibarua kigumu jijini Dar dhidi ya Simba waliorejea upya kwenye ligi hiyo chini ya kocha Goran Kopunovic.

MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                                P   W    D    L    F    A   GD   Pts
01. Mtibwa Sugar     09  04  05  00  12  05  07   17
02. Azam                 10  06  02  02  14  07  07   20
03. JKT Ruvu           11  05  02  04   11   10  01  17
04. Yanga                09  04  03  02  11   07  04  15
05. Polisi Moro         11  03  06  02   09  08  01  15
06. Kagera Sugar     11  03  05  03   08  08  00  14
07. Coastal Union     10  03  04  03   09  08  01  13
08. Mgambo JKT       10  04  01  05   05  09  -4  13
09. Simba                09  02  06   01   09   07  02  12
10. Ruvu Shooting    11  03  03   05   05   08  -3  12
11. Mbeya City         09   03  02   04  04   06  -2   11
12. Stand Utd           11  02  05   04   07   13  -6  11
13. Ndanda Fc          11  03  01   07  10    16  -6  10
14. Prisons               10  01  05   04  06   08  -2   08
Wafungaji:
7- Didier Kavumbagu(Azam)
5- Ame Ali (Mtibwa), Rashid Mandawa (Kagera Sugar)
4-
Rama Salim (Coastal), Danny Mrwanda, Simon Msuva (Yanga) Samuel Kamuntu (JKT Ruvu)
3-
Ally Shomari, Emmanuel Okwi (Simba),  Jacob Massawe (Ndanda)

Ratiba ya mechi zijazo

Jan 24, 2015 
Azam vs Simba 
Kagera Sugar vs Ndanda
Stand Utd vs Coastal Union 

Polisi Moro vs Yanga

Mbeya City vs Prisons
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar 

Jan 25, 2015JKT Ruvu vs Mgambo JKT

Chelsea, Liverpool hapatoshi leo Nusu Fainali Capital One

Gerrard (left) celebrates as Chelsea captain John terry looks distraught in the 2006 FA Cup semi-final
manahodha wa Liverpool, Steven Gerrerd na John Terry wa Chelsea watazibeba vipi timu zao kwenye mechi ya Capital One Cup leo?
Jose Mourinho (right) holds the ball under his shoulder and Rodgers looks on during the match last April
Makocha Brendan Rodgers na Jose Mourinho watavuna nini?
ZOTE zikiwa zimetoka kupata ushindi muhimu viwanja vya ugenini kwenye mechi za Ligi Kuu ya England mwishoni mwa wiki, klabu za Chelsea na Liverpool leo zitakuwa vitani kwenye pambano la Nusu Fainali ya Kombe la Ligi (Capital One Cup).
Liverpool iliyotoka kuitoa nishai Aston Villa kwa kuicharaza mabao 2-0 siku ya Jumamosi, itakuwa uwanja wa Anfield kuikaribisha Chelsea walioitoa nishai Swansea City kwa kuifumua mabao 5-0 kwenye uwanja wa ugenini pia.
Pambano hilo litakalochezeshwa na mwamuzi Martin Atkinson, litazikutanisha timu hizo ambazo zilikutana Novemba 8 mwaka jana kwenye mechi ya ligi kwenye dimba hilo na wenyeji LIverpool kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka wa wageni wao Chelsea.
Kocha  Jose Mourinho ana rekodi nzuri dhidi ya Liverpool, lakini hiyo haimpi jeuri ya kulidharau pambano hilo kama alivyonukuliwa mwenyewe akidai wanaenda Anfield kwa ajili ya kuska ushindi kujiweka pazuri kabla ya mechi ya marudiano wiki ijayoStanford Bridge.
Kwa mujibu wa rekodi zilizopo Jose Mourinho ameiongoza Chelsea dhidi ya Liverpool katika mechi 19 akishinda 10 na kupata sare michezo minne na kupoteza mitano.
Chelsea imefika kwenye hatua hiyo baada ya kuichapa timu ya Derby Count kwa mabao 3-1 wakati LIverpool iliing'oa AFC Bournemouth pia kwa magoli 3-1 na zitarudiana Jumanne ijayo.
Mechi nyingine ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Ligi itazikutanisha timu za Tottenham Hotspur dhidi ya Sheffield United mchezo utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa White HartLane nyumbani kwa Spurs kabla ya timu hizo kurudiana Jumatano ijayo nyumbani kwa Sheffield United.

Ghana, Wasauzi wafa AFCON, leo zamu ya Ivory Coast, Cameroon

Algeria wakishangilia ushindi wao dhidi ya Bafana Bafana
Substitute Sow (right), who plays his club football for Fenerbahce, slotted past Ghana keeper Brimah Razak
Senegal walivyokuwa wakiiadhibu Ghana katika mechi ya kundi C
WAKATI timu za Senegal na Algeria wakianza vyema mechi zao za Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika , AFCON inayoendelea nchini Guinea ya Ikweta kwa kuzitandika timu za Ghana na Afrika Kusini, vigogo vingine vya soka Afrika, Ivory Coast na Cameroon zenyewe zitakuwa dimbani leo kujaribu bahati yao.
Ivory Coast na Cameroon zilizopo kundi D zitacheza mechi zao za kwanza za kukamilisha raundi ya kwanza ya makundi kwa kupepetana na Guinea na Mali katika mechi zitakazochezwa usiku wa leo katika mji wa Malabo.
Tembo wa Afrika, Ivory Coast wataanza kibarua chao mapema kwa kuumana na Guinea kabla ya Cameroon kuivaa Mali katika pambano la usiku.
Timu hizo zilizofanya vema kwenye mechi zao za kuwania kufuzu fainali hizo zitakuwa zikihitaji ushindi katika mechi zao ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya 'vigogo' wenzao Ghana usiku wa jana kutolewa nishai na Senegal kwa kucharazwa mabao 2-1 huku Afrika Kusini ambao walifuzu fainali hizo bila kupoteza mchezo wowote katika kundi lake lililokuwa na mabingwa watetezi Nigeria waliokwama kwenda Guinea ya Ikweta ilinyukwa mabao 3-1 katika mechi za kundi la kifo la C.
Gervinho, Wilfried Bony wanatarajiwa kuiongoza Ivory Coast katika pambano la mapema usiku, ili kuibeba timu yao ambayo iliukosa mwaka 2012 michuano hiyo ilipofanyika katika nchi ya Guinea ya Ikweta iliyoshirikiana na Gabon kuziandaa fainali hizo zilizotwaliwa taji na Chipolopolo ya Zambia.
Mpaka sasa raundi ya kwanza ya makundi ikitarajiwa kukamilisha leo, ni timu tatu tu zilizoweza kupata ushindi katika mechi zao za awali, wakiwamo Gabon waliowatoa nishai Burkina Faso katika mechi za kundi A ambazo zitashuka tena dimbani kesho kwa mechi za pili ambapo wenyeji waliolazimishwa sare tya 1-1 na Jamhuri ya Kongo watavaana na Burkina Faso na vinara wa kundi hilo Gabon itaumana na Kongo.

Louis Van Gal awacharukia mashabiki Man Utd

http://www.oslobodjenje.ba/portal/images/articles/louis-van-gaal-od-srijede-novi-trener-manchester-uniteda_1399028363.jpg
Kocha Louis Van Gaal
KOCHA wa klabu ya Manchester United, Louis Van Gaal amesisitiza kuwa hakubadili mfumo wa kiuchezaji katika mchezo dhidi ya Queens park Rangers kutokana na malalamiko ya mashabiki.
Mashetani Wekundu hao walianza na mfumo wa kuchezesha mabeki watatu nyuma ilishindwa kuonyesha makeke mpaka walipobadilisha na kuanza kucheza 4-4-2 baada ya mashabiki kupaza sauti zao kutoka jukwaani ndipo matunda yalipoanza kuonekana.
Lakini Van Gaal amesema kubadili mfumo ilikuwa mipango yake ya kiufundi katika mchezo huo hivyo kwamba amesikiliza mashabiki walichokisema sio kweli.
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa United ina mashabiki zaidi ya milioni 600 hivyo hadhani kama ataweza kuchukua maoni ya kila mshabiki. Van Gaal amesema kazi yake ni kuangalia, kuwasiliana, kuchambua na kuona makosa yanayofanywa na wachezaji wake wakiwa uwanjani na sio kusikiliza mashabiki wanasemaje.
Mashabiki hao wa Manchester City pia walionyeshwa kushangaza na kocha wao kumcheza Angel di Maria kama mshambuliaji na Wayne Rooney kucheza kama kiungo huku beki Jonas akiachiwa kupiga mipira ya kona.

Jennifer Mgendi kweli Sura Sio Roho, Goliati amchelewesha

BAADA ya kusumbua sokoni na filamu ya Mama Mkwe, muimbaji nyota wa muziki wa Injili na muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi yupo katika maandalizi ya kutengeneza filamu mpya iitwayo 'Sura Sio Roho' ambayo itawashirikisha wakali kadhaa wa fani hiyo nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, Jennifer anayetamba kwa sasa na wimbo wa 'Wema ni Akiba' alisema filamu hiyo mpya inatarajiwa k
"Kwa sasa nipo katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kurekodi filamu yangu mpya itakayofahamika kwa jina la 'Sura Sio Roho' ambayo itawashirikisha wakali wanaotamba kwenye fani ya muziki wa Injili na filamu nchini," alisema Jennifer.
Mkali huyo ambaye anajiandaa kuitoa hadharani albamu yake mpya ya 'Wema ni Akiba' itakayokuwa na nyimbo nane, alisema filamu hiyo itaingia sokoni kabla ya sikukuu ya Pasaka inayotarajiwa kusherehekewa baadaye mwaka huu.
Kabla ya 'Mama Mkwe', Jennifer Mgendi alitamba na filamu kadhaa zikiwamo 'Teke la Mama', na 'Chai ya Moto'.
urekodiwa ikiwashirikisha wasanii kama mchekeshaji maarufu Senga, Mussa Banzi, Bahati Bukuku, Bi Eshter, yeye mwenyewe (Jennifer) na wengine.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alifichua sababu ya kukwama kwa albamu yake mpya  iitwayo 'Wema ni Akiba' na kudai imetokana na kutakakuongeza wimbo mwingine mpya utakaokuwa wa nane.
Jennifer aliutaja wimbo huo ulioichelewesha albamu hiyo ni  'Goliati', lakini akaahidi albamu hiyo itakuwa mtaani kabla ya kumalizika kwa mwezi huu wa Januari kwa sababu mambo yanaenda vema.
"Albamu yangu ya nane iitwayo 'Wema ni Akiba' imekwama kutokana kwa sababu nilikuwa namalizia wimbo mwingine wa nyongeza uitwao 'Goliati', nilikuwa nataka kuwapa burudani zaidi mashabiki wangu, nikaona nyimbo saba kama ni chache mno kwao, lakini sasa wajiandae kuipokea wakati wowote," alisema.
Jennifer alisema mara baada ya albamu hiyo upande wa 'audio' kuingia sokoni ataanza mchakato wa kutengeneza video yake ambayo amepanga kuitoa Juni mwaka huu kabla ya kuitengenezea filamu ambayo amepanga kuitoa mwezi Septemba.
"Video ya Wema ni Akiba itatoka Juni wakati filamu yenye jina kama hilo itakufuata mwezi Septemba na kazi yangu ya mwisho kwa mwaka huu wa 2015 nimepanga kutoa filamu iitwayo 'Goliati'," alisema.
Jennifer anayetamba na albamu ya 'Hongera Yesu' alisema ameiweka ratiba yake hadharani kwa kazi alizopanga kuzitoa mwaka huu ili mashabiki wake wajue kitu gani kitafuata baaada ya kingine kutoka kwake kwa mwaka 2015.

Kichupa kipya cha Avril ft Ommy Dimpoz-Hello baby