STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 20, 2015

Jennifer Mgendi kweli Sura Sio Roho, Goliati amchelewesha

BAADA ya kusumbua sokoni na filamu ya Mama Mkwe, muimbaji nyota wa muziki wa Injili na muigizaji wa filamu, Jennifer Mgendi yupo katika maandalizi ya kutengeneza filamu mpya iitwayo 'Sura Sio Roho' ambayo itawashirikisha wakali kadhaa wa fani hiyo nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, Jennifer anayetamba kwa sasa na wimbo wa 'Wema ni Akiba' alisema filamu hiyo mpya inatarajiwa k
"Kwa sasa nipo katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza kurekodi filamu yangu mpya itakayofahamika kwa jina la 'Sura Sio Roho' ambayo itawashirikisha wakali wanaotamba kwenye fani ya muziki wa Injili na filamu nchini," alisema Jennifer.
Mkali huyo ambaye anajiandaa kuitoa hadharani albamu yake mpya ya 'Wema ni Akiba' itakayokuwa na nyimbo nane, alisema filamu hiyo itaingia sokoni kabla ya sikukuu ya Pasaka inayotarajiwa kusherehekewa baadaye mwaka huu.
Kabla ya 'Mama Mkwe', Jennifer Mgendi alitamba na filamu kadhaa zikiwamo 'Teke la Mama', na 'Chai ya Moto'.
urekodiwa ikiwashirikisha wasanii kama mchekeshaji maarufu Senga, Mussa Banzi, Bahati Bukuku, Bi Eshter, yeye mwenyewe (Jennifer) na wengine.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo alifichua sababu ya kukwama kwa albamu yake mpya  iitwayo 'Wema ni Akiba' na kudai imetokana na kutakakuongeza wimbo mwingine mpya utakaokuwa wa nane.
Jennifer aliutaja wimbo huo ulioichelewesha albamu hiyo ni  'Goliati', lakini akaahidi albamu hiyo itakuwa mtaani kabla ya kumalizika kwa mwezi huu wa Januari kwa sababu mambo yanaenda vema.
"Albamu yangu ya nane iitwayo 'Wema ni Akiba' imekwama kutokana kwa sababu nilikuwa namalizia wimbo mwingine wa nyongeza uitwao 'Goliati', nilikuwa nataka kuwapa burudani zaidi mashabiki wangu, nikaona nyimbo saba kama ni chache mno kwao, lakini sasa wajiandae kuipokea wakati wowote," alisema.
Jennifer alisema mara baada ya albamu hiyo upande wa 'audio' kuingia sokoni ataanza mchakato wa kutengeneza video yake ambayo amepanga kuitoa Juni mwaka huu kabla ya kuitengenezea filamu ambayo amepanga kuitoa mwezi Septemba.
"Video ya Wema ni Akiba itatoka Juni wakati filamu yenye jina kama hilo itakufuata mwezi Septemba na kazi yangu ya mwisho kwa mwaka huu wa 2015 nimepanga kutoa filamu iitwayo 'Goliati'," alisema.
Jennifer anayetamba na albamu ya 'Hongera Yesu' alisema ameiweka ratiba yake hadharani kwa kazi alizopanga kuzitoa mwaka huu ili mashabiki wake wajue kitu gani kitafuata baaada ya kingine kutoka kwake kwa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment