STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 20, 2015

Chelsea, Liverpool hapatoshi leo Nusu Fainali Capital One

Gerrard (left) celebrates as Chelsea captain John terry looks distraught in the 2006 FA Cup semi-final
manahodha wa Liverpool, Steven Gerrerd na John Terry wa Chelsea watazibeba vipi timu zao kwenye mechi ya Capital One Cup leo?
Jose Mourinho (right) holds the ball under his shoulder and Rodgers looks on during the match last April
Makocha Brendan Rodgers na Jose Mourinho watavuna nini?
ZOTE zikiwa zimetoka kupata ushindi muhimu viwanja vya ugenini kwenye mechi za Ligi Kuu ya England mwishoni mwa wiki, klabu za Chelsea na Liverpool leo zitakuwa vitani kwenye pambano la Nusu Fainali ya Kombe la Ligi (Capital One Cup).
Liverpool iliyotoka kuitoa nishai Aston Villa kwa kuicharaza mabao 2-0 siku ya Jumamosi, itakuwa uwanja wa Anfield kuikaribisha Chelsea walioitoa nishai Swansea City kwa kuifumua mabao 5-0 kwenye uwanja wa ugenini pia.
Pambano hilo litakalochezeshwa na mwamuzi Martin Atkinson, litazikutanisha timu hizo ambazo zilikutana Novemba 8 mwaka jana kwenye mechi ya ligi kwenye dimba hilo na wenyeji LIverpool kukubali kichapo cha mabao 2-1 toka wa wageni wao Chelsea.
Kocha  Jose Mourinho ana rekodi nzuri dhidi ya Liverpool, lakini hiyo haimpi jeuri ya kulidharau pambano hilo kama alivyonukuliwa mwenyewe akidai wanaenda Anfield kwa ajili ya kuska ushindi kujiweka pazuri kabla ya mechi ya marudiano wiki ijayoStanford Bridge.
Kwa mujibu wa rekodi zilizopo Jose Mourinho ameiongoza Chelsea dhidi ya Liverpool katika mechi 19 akishinda 10 na kupata sare michezo minne na kupoteza mitano.
Chelsea imefika kwenye hatua hiyo baada ya kuichapa timu ya Derby Count kwa mabao 3-1 wakati LIverpool iliing'oa AFC Bournemouth pia kwa magoli 3-1 na zitarudiana Jumanne ijayo.
Mechi nyingine ya nusu fainali ya michuano hiyo ya Kombe la Ligi itazikutanisha timu za Tottenham Hotspur dhidi ya Sheffield United mchezo utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa White HartLane nyumbani kwa Spurs kabla ya timu hizo kurudiana Jumatano ijayo nyumbani kwa Sheffield United.

No comments:

Post a Comment