STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, November 10, 2014

Maelfu wajitokeza kuuaga mwili wa Amigolas, azikwa Kisutu leo

Mwili wa marehemu Amigolas ukiwasilia nyumbani kwake Mburahati-Mianzini
Amigolas akikaribishwa kuiaga mara ya mwisho nyumba yake ya duniani
Sheikh akihirimia kwa ajili ya swala la maiti
Mwili wa Amigolas ukiswaliwa
Ukitolewa uwanjani kupelekwa kwenye Ambulance ili kupelekwa kuzikwa makaburi ya Kisutu

Dah! Inahuzunisha mno!
Waombolezaji wakiubeba mwili wa Amigolas ukiwa ndani ya jeneza kupelekwa kuzikwa

Kila mtu alitaka kumpa mkono wa buriani
baadhi ya waombolezaji
Choki alishindwa kujikaza na kuangusha kilio!
Luiza Mbutu akihojiwa na wanahabari kueleza kifo cha Amigolas kilivyomgusa
Waombolezaji
Wadau wa muziki waliofika kumsindikiza mwanamuziki Amigolas
Hata hawa walikuwapo
Choki alitia huruma alipoliona jeneza la mwili wa Amigolas!
Wanamuziki wenzake walikuja pia kumuaga
Hata hawa nao walikuwapo kumuaga Amigolas

Ally Choki akiangusha kilio
Steve Nyerere akiwa na huzuni huku James Chirwa akiwa pemebeni yake Kushoto
jeneza la Amigolas likiondolewa nyumbani ili kwenda kuzikwa
Chalz Baba naye alikuwapo
Kila mmoja alitaka kumsindikiza Amigolas
Jenezala Amigolas likiingizwa kwenye Ambulance
mwili ukiingizwa kwenye gari ili kwenda kuzikwa
Jeneza lenye mwili wa Amigolas ukiwa kwenye gari
baadhi ya waombolezaji wakiwa hawaamini kama ndiyo wanaagana na Amigolas na kutoweza kumuona tena milele
Ambulance yernye mwili wa Amigolas likijiandaa kuondoka
Safari inaanza kuelekea makaburini

Dah Amigolas akipelekwa makaburi ya Kisutu kuzikwa
Kama utani vile kwa hakika sisi ni wa Allah na Kwake Tutarejea!
Msafara ukisimama kupakia waombolezaji wengine
Kaburi alimohifadhiwa Amigolas
Dua ya mwisho mwisho kwenye makaburi ya Kisutu baada ya mwili wa Amigolas kuzikwa
MAELFU ya waombolezaji wakiwamo wanamuziki, wanasoka soka na waigizaji wa filamu wamejumuika pamoja kuusindikiza mwili ya Mwanamuziki wa zamani wa bendi za African Stars 'Twanga Pepeta' na Ruvu Stars, Khamis Kayumbu 'Amigolas' aliyefariki usiku wa kuamkia jana na kuzikwa leo jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki huyo alifariki akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhumbili akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo na aliagwa rasmi na mamia ya watu mapema leo nyumbani kwao Mburahati kabla ya kupelekwa makaburi ya Kisutu.
Miongoni mwa waliojitokeza kuusindikiza mwili wa Amigolas ambayo uliwasili nyumbani hapo ukitokea hospitalini majira ya saa 6:45 na kuswaliwa saa 8:30 kabla ya kupelekwa makaburi ya Kisutu Robo Saa baadaye ni 'bosi' wake wa zamani, Asha Baraka 'Iron Lady', Ally Choki, Said Mabela na Mwenyekiti wa Shirika la Wasanii Tanzania (SHIWATA).
Pia walikuwamo Mwinjuma Muumin,  Mafumu Bilal aliyeasisi pamoja bendi ya Twanga Pepeta, na waigizaji Steve Nyerere, Jacob Stephen 'JB', Mrisho Zimbwe 'Tito', wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, Fm Academia, waimbaji wenzake wa Twanga Pepeta na Ruvu Stars mwanasoka wa zamani James Chirwa na wadau wengine wa muziki akiwamo Juma Mbizo.
Baadhi ya wanamuziki waliozungumza na MICHARAZO kabla ya mwili wa Amigolas kwenda kuzikwa walisema kifo cha muimbaji huyo ni pebngo kubwa kwa tasnia ya muziki na sanaa kwa ujumla kwani alikuwa na mchango mkubwa.
"Kwangu binafsi ni pigo kubwa, alikuwa msaada katika kufika nilipo, hakuwa mchoyo wa kutoa ujuzi wake kwa wasanii chipukizi," alisema Dodo Rama aliyeimba naye Twanga Pepeta.
Juma Mbizo alisema kifo cha Amigolas ni pengo kubwa kwani linaongeza idadi ya wanamuziki wa ukweli wanaoondoka na kuacha nafasi ambazo hajui wa kuziziba kwani vijana wengi kwa sasa wanakimbilia muziki wa kizazi kipya na hawataki kuwa wanamuziki.
"Kwa hakika ni pengo, kariba ya akina Amigolas inazidi kupungua na kuacha mapengo ambayo hakuna wa kuyaziba...inauma ila kwa kuwa ni kazi ya Mungu hakuna cha kulaumu ila kumuombea kila la heri katika safari yake ya Ahera," alisema Mbizo.
Ally Choki alishindwa kuzungumza kutokana na kuzidiwa na kilio cha uchungu cha kumpoteza mtu aliyefanya kazi kwa muda mrefu na aliyekuwa zaidi ya rafiki yake.
"Siwezi kuzungumza, inatia simanzi...ina huzunisha kumpoteza rafiki kipenzi, mwanamuziki mwenzangu na...naa  ..." Choki alishindwa kuendelea na kuangusha kilio cha uchungu.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka na Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu walisema kwa nyakati tofauti, msiba huo umewagusa kwa sehemu kubwa kwani Amigolas alikuwa ni zaidi ya mwanamuziki na mtu mwenye mchango mkubwa wa mafanikio ya Twanga Pepeta aliyoifanyia kazi kwa zaidi ya miaka 10 kabla ya hivi karibuni kujiondoa kuanzisha Super Stars na baadaye kwenda Ruvu Stars.
Super Nyamwela na Rama Mhoza Pentagone kwa upande wao walisema tasnia ya muziki uimepata pigo kubwa kutokana na mchango wa mwanamuziki huyo na kumtakia kila la heri katika safari yake ya Ahera kwani ni njia ya kila mmoja.
Amigolas aliyeanza fani ya muziki mwanzoni mwa miaka ya 1990 bendi yake ya kwanza ikiwa Bicco Stars kabla ya kupita Chezimba Band na baadaye kujiunga na Twanga Pepeta mwaka 1997.
Hadi nakumbwa na mauti alikuwa Kiongozi na muimbaji wa bendi ya Ruvu Stars akisaidiana na Rogert Hegga, Jojo Jumanne, Victor Mkambi na Khadija Mnoga 'Kimobitel'.
Marehemu ameacha mke na watoto wanne, wakike watatu na mmoja wa kiume.
MICHARAZO Inawapa pole wote walioguswa kwa namna moja au nyingine na msiba huo wa Amigolas hususani familia, ndugu, jamaa, rafiki, wanamuziki wenzake na wadau wote wa sanaa Tanzania. Kwa Hakika Kila Nafsi Itaonja Mauti na 'Sisi ni wa Allah na Kwake Tutarejea' Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Khamis Kayumbu 'Amigolas' Mahala Pema Peponi Akimghufria madhambi yake Inshalllah!