STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 2, 2013

Paulinho atua Spurs, Adebayor akijiandaa kutoka

Adebayor
Paulinho
MSHAMBULIAJI Emmanuel Adebayor yupo mguu ndani mguu nje kuondoka katika klabu ya Tottenham Hotspur kuelekea timu ya Besiktas kupisha ujio wa kiungo toka  Brazili, Paulinho kutoka Corinthians kutoa kwa klabu hiyo ya London ya Kaskazini.
Inaelezwa kuwa Spurs imemnasa Paulinho kwa kitita cha pauni Milioni 17 na kwa sasa inaelekeza nguvu zake zaidi kwa Roberto Soldado wa klabu ya Valencia ya Hispania, ili kumnasa huku ikiwa mbioni kumuuza strika toka Togo, Adebayor kwa timu ya Uturuki Besiktas.
Kocha wa Spurs Andre Villas Boas anamhitaji Soldado ili kusaidia na wakali wengine wa timu yake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England mwezi ujao.
Inadaiwa kuwa Besiktas ipo tayari kutoa pauni Milioni 5 kumnyakua Adebayor mwenye miaka 29 ambaye alitua katika timu hiyo miaka miwili iliyopita na kulipwa mshahara wa pauni 80,000 kwa wiki kitu ambacho uongozi wa klabu hiyo unaona ni bora atimue zake kutokana na sheria mpya ya kodi nchini England.
Juu ya Soldado, Spurs imenukuliwa kuwa tayari kutoa kitita cha pauni milioni 15 wakati klabu hiyo ya Hispania imesisitiza kuwa bila pauni milioni 25 ambazo ni thamani ya mkali huyo inaweza kumkosa.
Rais wa Valencia, Amadeo Salvo Lillo alinukuloiwa akisema klabu yao inahitaji fedha kutatua matatizo kibao waliyonayo, lakini hawapo tayari kuwatoa wachezaji wao kwa bei chee.
Soldado, 28, amefunga jumla ya mabao 30 katika mechi 46 alizocheza kwa msimu uliopita na Spurs imejipanga kuhakikisha inamnyakua ili kuimarisha kikosi chao.

Sio kikapu tu hata soka najua! Obama akionyesha umahiri wake

IMEKUWA ikifahamika kuwa Rais wa Marekani Barack Obama ni mahiri katika mpira wa Kikapu na ndoto zake ilikuwa aje kucheza Ligi maarufu ya mchezao huo nchini mwake, NBA kabla ya upepo wa siasa haujamvuta na kumpeleka kuweka historia ya kuwa Rais wa kwanza mweusi nchini humo.
Hata hivyo kumbe sio kikapu tu hata soka analijua vyema kama pichani anavyoonekana akionyesha manjonjo yake mbele ya mwenyeji wake Rais Jakaye Kikwete ambaye naye ni mnazi mkubwa wa mchezop humo nchini na michezo kwa ujumla.
 
Rais Kikwete akimwangalia Obama wakati akipiga mpira danadana.OBAMA akionyesha uwezo wa kumiliki mpira kwa kupiga kichwa bila kutua chini wakati alipotembelea mitambo ya kufua umeme Ubungo jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuondoka nchini. 
Hapa akipiga danadana huku akishuhudiwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Mchungaji Mbeya afungwa miaka 30 kwa ubakaji

 MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi

   MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela
  Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
  Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
 Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini  baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30
 Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha
***********
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).
Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.
Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.
Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.
Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.
Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
Habari ,Picha na Mbeya yetu Blog 

Vital'O ya Burundi yairithi Yanga taji la Kagame 2013

Mabingwa wapya wa Kagame Cup, Vital'o wakishangilia taji lao

TIMU ya soka ya Vital'o ya Burundi jana ilifanikiwa kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa Kombe la Kagame wakiwarithi Yanga iliyokuwa bingwa mtetezi na kutokwenda kwenye michuano hiyo, baada ya kuilaza majirani zao APR ya Rwanda kwa mabao 2-0 katika mechi ya fainali.
Hilo ni taji la kwanza kwa timu hiyo katika historia ya michuano hiyo na ilifanikiwa kupata ushindi huo katika pambano kali lililochezwa kwenye uwanja wa El Fasher, Darfur nchini Sudan na kumaliza michuano hiyo bila kupoteza mechi yoyote.
Mabao ya washindi hao ambao waliing'oa timu nyingine ya Rwanda Rayon katika mechi ya nusu fainali yalitumbukizwa wavuni katika kipindi cha pili na Tambwe Amisi ambaye pia aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga mabao 6 kabla ya dakika tatu baadaye Christian Mbirizi kuongeza la pili na kuzima ndoto za wapinzani wao waliokuwa wakiwania taji la nne.
Wawakilishi wa Tanzania Simba, Falcon ya Zanzibar na waliokuwa watetezi wa taji hilo, Yanga hawakwenda katika michuano hiyo kwa hofu ya kutokuwepo amani na kufanya michuano hiyo kukosa msisimko japo yalichezwa na kumalizika salama bila tukio lolote kama ilivyokuwa ikitangazwa na wanasiasa wa Tanzania.

Kaondoka Obama tumebaki na BushRais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura na Mama Salma Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Wageni wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU 

Masoko Veterani yatangulia Fainali za Jimbo Cup- Kilwa

 
Kikosi cha Masoko Veterani kilichotangulia fainali za Jimbo Cup Kilwa Kusini
TIMU ya soka ya Masoko Veterani imefanikiwa kutinga fainali za michuano ya kuwania Ubingwa wa Jimbo la Kilwa Kusini 'Mbunge Cup' kwa kuidonyoa Kilwa Kisiwani kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa jioni ya jana kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari, Kilwa mkoani Lindi.
Bao hilo lililotimiza ahadi ya kocha wa Masoko Veterani, Abdallah Ahmad kwamba wangeilaza timu hiyo ya nyumbani kwao, lilitupiwa kimiani kwa kichwa na Said Mohammed aiyemalizia kazi nzuri iliyofanywa na Salum Teru.
Kocha huyo aliahidi mara baada ya timu yake kutinga hatua ya nusu fainali kwamba wangeinyuka Kisiwan anakotokea yeye na kutinga fainali ili kutimiza lengo la kuibuka mabingwa wa michuano hiyo iliyoandaliwa na kudhaminiwa na Mbunge wa Kilwa Kusini maarufu kama Bwege.
Katika pambano hilo la jana lililokuwa lenye upinzani na kosa kosa karibu muda wote, Masoko Veterani iliwakosa nyota wake kadhaa kama Shaaban Kassali na Yusuph Polisi waliopumzishwa na kocha wao ili kuwa tayari kwa mechi ya fainali itakayochezwa Jumamosi kati yao na mshindi wa mechi ya leo ya nusu fainali ya pili.
Nusu fainali hiyo ya pili itazikutanisha timu za Fresh Nigger dhidi ya Transpoters ambapo wadau wa soka wanaofuatilia michuano hiyo wametabiri litakuwa pambano kali zaidi ya lile la jana.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo, kocha msaidizi wa Masoko, Cool Mudi, aliwaomba mashabiki wa timu yao kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wa fainali akiamini kwamba hakuna cha kuwazuia kutawazwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo iliyoshirikia timu zaidi ya 10 kabla ya kufika hapo ilipo.

Obama amaliza ziara yake Bongo aacha gumzo

RAIS Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana....

Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo....

Tunapenda  kuungana na  Rais Jakaya  Kikwete na  watanzania  wote  wapenda amani katika  kumshukuru Rais wa Marekani Barack Obama kwa  kuichagua  Tanzania...

Pia tunawapongeza  watanzania  wote kwa kuonyesha umoja  wetu na hata  kuzika itikadi zetu za kisiasa   na   hata  kupelekea  TV zaidi ya 1000 duniani na radio zaidi ya  3000 duniani  kuitazama  Tanzania.

Timu ya Kikapu ya UDSM ikijifua

BAADHI ya wachezaji wa timu ya kikapu ya Chuo Kikuu UDSM wakijifua kwa mazoezi kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Chuo Kikuu Mlimani-Dar es Salaam.

Njemba yaumbuka Sabasaba kwa kukwapua simu

KIBAKA ALIEIBA SIMU KATIKA BANDA LA VETA SIMU YA STAFFUWA VETA LEO
KIBAKA AMBAYE ALISHIRIKIANANA MWENZAKE KUIBA SIMULEO
KIBAKA ALIEIBA SIMU NAKUFANIKIWA KUKIMBIA LAKINI ALIBAMBWA LEO
AFISA WA NSSF AKITOA KITABUWATU MBALIMBALI WALIOTEMBELEABANDA HILOLEO
WASANIIWAKUNDI LA TOTI WAKIPOKEA VITABU KUTOKA KWA AFISA WA NSSF LEO
AKIONYESA BAADHI YUA VIKOMBE WALIVYOSHINDA
AFISA WA NSSF WAKIWAFAHAMISHA WATU MBALIMBALI WALIOFIKAKWENYE BANDA HILO LEO
KIKUNDI CHA SACCOS WALIOPATA KUPITIA NSSF
KIKUNDI CHA SACCOSICHA NSSF AMBAOWAMEFANIKIWA KUPAT MKOPO KUPITIA SACOSI WAKIWA NA DUKA LAO
KIKUNDI CHA TOTI
THEOPITA MICHAEL KUTOKA VETA  HOTEL NA UTALII KUTOKANJIRO ARUSHA AKIMUONYESHA MKURUGENZIMKUU WA VETA ZEBADISH MOSH KULIA CHUPA YA WINE INAYOTENGENEZWA NJIRO ARUSHA LEO
MKURUGENZI MKUU WA VETA ZEBADISH MOSH KUSHOTOAKIANGALI BAADHI NGUA ZINAZOTENGENEZWA PUGUKATIKA KIWANDA CHA TMBE KULIA NI ANGELA SAMUEL

Wanariadhaa Wa Dar wakijifua tayari kwa mashindanoBaadhi ya wanariadhaa wa jijini Dar es Salaam wakijifua kwenye viwanja vya Chuo Kikuu kujiandaa na mashindano mbalimbali.