STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 13, 2012

Mashali, Sebyala wapima uzito kuvaana kesho Friends Cornerupimwa uzito kesho


BONDIA Thomas Mashali wa Tanzania na Mganda Medi Sebyala wamepima uzito leo kwenye ukumbi uliopo Manzese jijini Dar es Salaam tayari kwa ajili ya pambano lao la ubingwa wa Afrika Mashariiki na Kati litakaofanyika Jumapili kwenye ukumbi wa Friend's Corner, Manzese jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao walipimwa uzito na afya hizo asubuhi ya leo tayari kwa pambano hilo lililoandaliwa na mratibu Regina Gwae chini ya TPBO.
Mbali na mabondia hao wengine waliopimwa leo ni  Abdul Awilo atakayepanda ulingoni kuchuana na Shedrack Juma, Selemani shaaban atakayechapana na Hamis Mohamed,  Jonas Segu atakayemkabili Ibrahim Class  na  Charles Mashali atakayevaana na Teacher Aaron.
Regina alisema maandalizi yote yamekamilika ikiwamo waamuzi wenye sifa za kuchezesha mapambano ya kimataifa anbao tayari wameshapatikana na mgeni rasmi katika pambano hilo atakuwa Kamanda wa  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela ambaye anatarajiwa kuambatana na wageni wengine maalum akiwamo Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mhe. Idd Azzan.
---

Kiemba akana kuziba pengo la Mafisango Simba

Amri Kiamba akishangilia bao moja ya mabao yake katika Ligi Kuu msimu huu

KIUNGO nyota wa Simba, Amri Kiemba, licha ya kuwashukuru mashabiki wa klabu hiyo kumfananisha na kiungo wa kimataifa wa timu hiyo Patrick Mafisango, aliyefariki kwa ajali ya gari Mei mwaka huu, amekiri hajaliziba pengo la kiungo huyo.
Akizungumza na MICHARAZOE muda mchache kabla ya kuondoka jijini na kikosi cha timu yake kuelekea Tanga kuwahi pambano lao dhidi ya Coastal Union, Kiemba alisema licha ya kuanza msimu kwa kung'ara, bado anajiona hajaliziba pengo la Mafisango hata kama watu wanaridhika na kiwango chake.
Kiemba, alisema ni vigumu pengo la kiungo huyo aliyefariki Mei 17 kuzibika kirahisi na kwa ukamilifu kutokana na uwezo na kipaji kikubwa alichokuwa nacho nyota huyo kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
"Nashukuru mashabiki kuridhika na juhudi zangu uwanjani kiasi cha kuona kama nimeziba pengo la Mafisango, ila ukweli ni vigumu pengo la kiungo huyo kuzibika kirahisi hata mie mwenyewe najiona sijaliziba hata kidogo, " alisema
Kiemba aliongeza, binafsi alikuwa akimkubali Mafisango kwa umahiri wake hivyo anajisikia vibaya kufananishwa naye japo anafurahia kuona mashabiki wanakikubali kiwango chake kwa mechi chache zilizoanza za msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kiungo huyo wa zamani wa Yanga, aliyeigomea Simba msimu uliopita kumtoa kwa mkopo kwenda kuichezea timu iliyokuja kushuka daraja ya Polisi Dodoma ameanza  msimu kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu akiifungia Simba mabao yaliyoiweka kileleni mwa msimamo huku mwenyewe akiongoza orodha ya wafungaji mpasa sasa.
Mchezaji huyo ameifungia Simba jumla ya mabao manne mpaka sasa, matatu akiyafunga katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Yanga waliotoka nao sare ya bao 1-1 na ile ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya JKT Oljoro, jingine alifunga walipilaza JKT Ruvu.

Mwisho

Miyeyusho, Nassib kuvaana Uhuru Day


MABONDIA wanaozidi kupanda chati nchini, Francis Miyeyusho na Nassib
Ramadhani wanatarajia kuvaana jijini Dar es Salaam siku ya Desemba 9 katika pambano la kuwania ubingwa wa Mabara unaotambuliwa na WB-Forum.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa PTA na limeandaliwa na promota Mohammed Bawazir wa kampuni ya Dar World Link chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST.
Hilo litakuwa pambano la kwanza kwa mabondia hao wenye rekodi ya kuwapiga wapinzani wao kukutana.
Akizungumza kwenye utambulisho wa mabondia hao, promota wa pambano hilo la uzani wa Bantam (kilo 53.5), Mohammed Bawazir, alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika ikiwemo kumalizana na mabondia hao.
Bawazir alisema ana imani litakuwa la aina yake kulingana na rekodi za mabondia hao.
Kwa mujibu wa rekodi za Miyeyusho mwenye umri wa miaka 32 amecheza jumla ya mapambano 44 akishinda michezo 32, 19 ikiwa ya KO amepigwa 10 na kutoka sare michezo miwili.
Kwa upande wa rekodi za Nassib inaonyesha amecheza mapambano 12 akishinda 10 na kupoteza mawili.
Kabla ya kuvaana na Miyeyusho bondia huyo anatarajiwa kuvaana na Mkenya Nick Otieno atakayepigana nae Novemba 30 kwenye pambano la kuwania ubingwa wa IBF Afrika na Ghuba ya Uajemi.

GOLDEN BUSH WALIPOPIMANA UBAVU NA WAHENGA FC UWANJA WA TP-SINZA


BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YA PAMBANO LA TIMU YA SOKA YA GOLDEN BUSH ILIYOKUWA IKIUNDWA NA NYOTA WA ZAMANI WA YANGA KAMA AKINA ALLY YUSUF 'TIGANA', ABDALLA MSHELI, WAZIR MAHADH 'MANDIETA' CHINI YA UNAHODHA WA ONESMO WAZIR 'TICOTICO' DHIDI YA WAHENGA FC ILIYOKUWA IKIONGOZWA NA MKONGWE MADARAKA SELEMAN 'MZEE WA KIMINYIO'.
Patashika dimbani kati ya Golden Bush na Wahenga FC

Onesmo Wazir 'Ticotico' wa Golden Bush (kushoto), akitafuta mbinu za kumpotoka China wa Wahenga Fc, huku mchezaji wenzake akiwa tayari kumsaidia.

Twende sasa kama 'Ronaldo'

Ticotico akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Wahenga Fc

China wa Wahenga Fc akiambaa na mpira dimbani katika mechi yao leo dhidi ya Golden Bush ambapo mpaka tunaondoka uwanjani matokeo yalikuwa bao 1-1. Wahenga wakitangulia kupata bao dakika ya 38 kupitia Moahmmed Ibrahim kabla ya Golden Bush kurejesha katika kipindi cha pili kupitia kwa Dau 'Messi'

China wa Wahenga akimtokea beki wa Golden Bush (14) huku wachezaji wengine wakiwa tayari kutoa msaada.

Machota wa Golden Bush akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Wahenga Fc