STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, October 13, 2012

Miyeyusho, Nassib kuvaana Uhuru Day


MABONDIA wanaozidi kupanda chati nchini, Francis Miyeyusho na Nassib
Ramadhani wanatarajia kuvaana jijini Dar es Salaam siku ya Desemba 9 katika pambano la kuwania ubingwa wa Mabara unaotambuliwa na WB-Forum.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa PTA na limeandaliwa na promota Mohammed Bawazir wa kampuni ya Dar World Link chini ya usimamizi wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Tanzania, PST.
Hilo litakuwa pambano la kwanza kwa mabondia hao wenye rekodi ya kuwapiga wapinzani wao kukutana.
Akizungumza kwenye utambulisho wa mabondia hao, promota wa pambano hilo la uzani wa Bantam (kilo 53.5), Mohammed Bawazir, alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika ikiwemo kumalizana na mabondia hao.
Bawazir alisema ana imani litakuwa la aina yake kulingana na rekodi za mabondia hao.
Kwa mujibu wa rekodi za Miyeyusho mwenye umri wa miaka 32 amecheza jumla ya mapambano 44 akishinda michezo 32, 19 ikiwa ya KO amepigwa 10 na kutoka sare michezo miwili.
Kwa upande wa rekodi za Nassib inaonyesha amecheza mapambano 12 akishinda 10 na kupoteza mawili.
Kabla ya kuvaana na Miyeyusho bondia huyo anatarajiwa kuvaana na Mkenya Nick Otieno atakayepigana nae Novemba 30 kwenye pambano la kuwania ubingwa wa IBF Afrika na Ghuba ya Uajemi.

No comments:

Post a Comment