STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 5, 2013

Machini aibuka kumtetea Balotelli, adai hawatamfukuza

Kocha Mancini na Balotelli
MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini amesema atampa Mario Balotelli "nafasi nyingine 100 zaidi" za kujirekebisha baada ya kusisitiza kuwa malumbano yake na mshambuliaji huyo hayakuwa ni ngumi.
Picha zinaonyesha wawili hao wakitenganishwa wakati wa mazoezi yao ya jana.
Lakini Mancini alisema kuhusu tukio hilo kwamba kilichotokea na Muitalia mwenzake huyo: "Si ngumi, siyo kweli. Picha zinaelezea vibaya tukio.
"Nitampa nafasi nyingine 100 kama nadhani inawezekana akabadilika. Nampa nafasi nyingine, hakika, kwa sababu ana umri wa miaka 22 na anaweza kufanya makosa."
Tukio hilo jipya zaidi katika mfululizo wa matukio ya utata yanayomhusisha mshambuliaji huyo, limemuonyesha Balotelli katika picha akikunjana na kocha wake.
Picha zinaonyesha Mancini akimbwatukia mchezaji wake huyo, ambaye amefunga magoli matatu katika mechi 21 msimu huu.
Picha moja inawaonyesha wawili hao wakiangaliana uso kwa uso, nyingine Mancini akivuta jezi ya Balotelli, wakati katika picha nyingine mshambuliaji huyo anaonekana akivutwa pembeni na wafanyakazi wa uwanjani hapo.
Lakini Mancini amedai kwamba tukio hilo limekuzwa mno na kusisitiza kwamba Balotelli anahitaji klabuni hapo.
"Haikuwa mbaya," alifafanua. "Tulikuwa tunacheza mechi, Mario akampiga teke mwenzake nikamwambia 'nenda ndani (kwenye vyumba vya kuvalia), ondoka uwanjani'.
"Alisema 'hapana' hivyo nikamvuta shati lake na kumsukuma nje ya uwanja. Hicho ndicho kilichotokea. Hakuna cha zaidi."
"Mario yuko hivi lakini mtazamo wangu (kuhusu hatma yake) hautabadilika, hii siyo muhimu. Tatizo litakuwa yeye mwenyewe. Kama hatabadilika, kwake itakuwa ngumu sana huko baadaye, Kwake, si kwangu.
"Mario anaweza kubaki nami siku moja, mwezi mmoja, miaka mitano. Ana miaka 22. Anahitaji kubadilika. Tatizo lake ni yeye mwenyewe."
Alipoulizwa kama ni yeye ndiye aliyepandisha hasira katika tukio hilo, Mancini alijibu: "Hapana. Kwa sekunde mbili za kwanza, ndiyo, lakini baada ya sekunde tatu ama nne hakutaka kuondoka uwanjani. Kwangu alipaswa kuondoka."

BURIANI SAJUKI, NDIVYO ALIVYOZIKWA NA MAELFU JIJINI DAR

Hili ndilo kaburi ambalo Sajuki amezikwa  katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Januari 4, 2013.

Rais Kikwete naye alikuwepo katika kumzika Sajuki Januari 4, 2013.
Hallooo... hapa ndo tunakaribia kumzika mshkaji wetu Sajuki...!

Hapa ni maandaalizi ya mapeeema kabla jeneza la sugu halijaletwa na mwili wa msanii huyo kuzikwa Januari 4, 2013. Na mie nipishe nichukue ukumbusho wa kaburi la Sajuki...!Tafakuri makini kabla ya mazishi ya Sajuki  Januari 4, 2013.

Steve Nyerere mwenye kanzu mbele, Tino (nyuma ya Steve) na waombolezaji wengine wakitafakari kabla mwili kufikishwa kwenye makaburi ya Kisutu na kuzikwa jijini Dar es Salaam Januari 4, 2013.

Kwaheri jembe letu Sajuki... msanii Ray akitafakari kabla ya kuzikwa kwa Sajuki  Januari 4, 2013.

Tangulia mwana... sote tuko nyuma yako Sajuki! Jotti akitafakari kabla ya mazishi ya Sajuki  Januari 4, 2013.
Single Mtambalike 'Richie' (kushoto) naye aliibuka 'kisheikh' kumsindikiza Sajuki  Januari 4, 2013. 
Chuzi naye alikuwepo na mtoko wake wa Kisheikh


Kwaheri mwanangu Sajuki... msanii nyota wa filamu, Mzee Chillo naye alikuwapo kumzika Sajuki Januari 4, 2013.

Hivi ni kweli umeondoka Sajuki? Siamini!

Mtangazaji Benny Kinyaiya hakubaki nyuma kumsindikiza Sajuki  Januari 4, 2013.
Msanii Jimmy Mponda a.k.a Jimmy Master alikuwa akimuaga Sajuki kwa staili yake.
Mhe. Zitto Kabwe (wa pili kushoto) akitafakari jambo na wasanii na waombolezaji wengine katika makaburi ya Kisutu kabla ya kuzikwa kwa Sajuki  Januari 4, 2013.

Kwaheri kijana wangu....! Msanii nyota wa filamu, Mzee Magali (kulia) akionekana mwenye majonzi tele kabla ya kuzikwa kwa mwenzao Sajuki  Januari 4, 2013.  (Picha zote: Shafii Banzi)
Said Fella (kushoto) na Chege pia walikuwapon
Ni huzuni kubwa kwa kifo cha mpendwa wetu Sajuki... Mungu amlaze pema! Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi Azzan.
Hapa kabla ya kuwasili kwa mwili kwenye makaburi ya Kisutu  Januari 4, 2013.
RAIS Dk Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya msanii Juma Kilowoko 'Sajuki' aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya msanii huyo yalifanyika katika makaburi ya Kisutu na kuhudhuriwa na watu maarufu nchini wakiwemo viongozi wa Serikali, Wabunge, wanamichezo na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki.
Mwili wa Sajuki uliwasili makaburini katika gari maalum la kubebea wagonjwa saa 8:47 mchana, dakika tatu baada ya Rais Kikwete kuwasili na msafara wake.
Mwili huo uliingizwa kaburini saa 8:53 na baada ya hapo baba wa marehemu, Mzee Said Kilowoko alitupia udongo kwenye kaburi la mwanae na kufuatiwa na Rais Kikwete na kisha Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba na kufuatiwa na waombolezaji wengine.
Akiongea katika makaburi ya Kisutu, Dk. Kikwete alisema serikali inasikikitishwa na kifo cha msanii huyo kijana aliyekuwa na ndogo za kuendeleza tasnia ya filamu nchini na kuitaka familia kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha maombolezo.
Naye baba wa marehemu, Mzee Juma Kilowoko, aliishukuru serikali, wasanii na watanzania kwa ujumla kwa namna walivyoshiriki tangu kifo cha mwanaye kitokee mpaka walipompumzisha jana kwa heshima zote na kudai hana cha kuwalipa zaidi ya kulipwa na Allah SW.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa na wengineo wengi.
Sajuki alifariki dunia juzi asubuhi katika hospitali ya Muhimbili alipolazwa kwa matatizo ya upungufu wa damu.
Baadhi ya waombolezaji akiwemo Meneja wa kundi la TMK wanaume Family Said Fella,  Wanamuziki Banana Zoro na Kassim Mapili wamesema kifo cha Sajuki ni pigo sio tu kwa familia yake bali tasnia nzima ya sanaa nchini.
Wasanii mbalimbali pamoja na wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani walijitokeza katika mazishi ya msanii huyo, aliyeanza kufahamika mwaka 2005 alipojiunga Kaole kabla ya kuanza kujitegemea akizalisha filamu mbalimbali zilizompatia umaarufu mkubwa.
Marehemu Sajuki ameacha mke na mtoto watoto wawili.

SAJUKI ALIVYOPUMZISHWA KATIKA NYUMBA YAKE YA MILELE  Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni, wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.
Mwili wa Marehemu Sajuki ukipakiwa kwenye gari
Dua ikisomwa kabla ya kuondoka kwa Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo

Pamoja na mvua kubwa kunyesha haikuzuia watu kufika kwa aajili ya kuomboleza kifo cha Marehemu sajuki
Waombolezaji wakiwa wanajifunika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar
Mwili wa marehemu Sajuki ukiondoka nyumbani kuelekea makaburi ya Kisutu
 Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Sajuki katika makaburi ya Kisutu 
Wadau mabali mbali wakisubiria mwili wa Marehemu Sajuki, huku Profesa Jay akionekana kwa mbali miongoni mwa wanaousubiri mwili.
Umati wa watu ukiwa makaburini Kisutu Dar
 Mwili wa marehemu Sajuki ukiwasili katika makaburi ya Kisutu tayari kwa mazishi
 Rais Kikwete pia alihudhuria mazishi ya marehemu Sajuki
 Jeneza liliobeba mwili wa marehemu Sajuki
Hili ndilo kaburi alilo zikiwa Maehemu Sajuki
 Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
Msanii Z Anto akiswali juu ya kaburi la Marehemu Sajuki.
This is it! Hapa ndipo sajuki amelala! May his soul R.I.P

Inna Lillahi Wa Inna Ilayhi Raj'un

IMEHAMISHWA KUTOKA JESTINA GEORGE