STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, January 5, 2013

BURIANI SAJUKI, NDIVYO ALIVYOZIKWA NA MAELFU JIJINI DAR

Hili ndilo kaburi ambalo Sajuki amezikwa  katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Januari 4, 2013.

Rais Kikwete naye alikuwepo katika kumzika Sajuki Januari 4, 2013.
Hallooo... hapa ndo tunakaribia kumzika mshkaji wetu Sajuki...!

Hapa ni maandaalizi ya mapeeema kabla jeneza la sugu halijaletwa na mwili wa msanii huyo kuzikwa Januari 4, 2013. 



Na mie nipishe nichukue ukumbusho wa kaburi la Sajuki...!



Tafakuri makini kabla ya mazishi ya Sajuki  Januari 4, 2013.

Steve Nyerere mwenye kanzu mbele, Tino (nyuma ya Steve) na waombolezaji wengine wakitafakari kabla mwili kufikishwa kwenye makaburi ya Kisutu na kuzikwa jijini Dar es Salaam Januari 4, 2013.

Kwaheri jembe letu Sajuki... msanii Ray akitafakari kabla ya kuzikwa kwa Sajuki  Januari 4, 2013.

Tangulia mwana... sote tuko nyuma yako Sajuki! Jotti akitafakari kabla ya mazishi ya Sajuki  Januari 4, 2013.
Single Mtambalike 'Richie' (kushoto) naye aliibuka 'kisheikh' kumsindikiza Sajuki  Januari 4, 2013. 
Chuzi naye alikuwepo na mtoko wake wa Kisheikh


Kwaheri mwanangu Sajuki... msanii nyota wa filamu, Mzee Chillo naye alikuwapo kumzika Sajuki Januari 4, 2013.

Hivi ni kweli umeondoka Sajuki? Siamini!

Mtangazaji Benny Kinyaiya hakubaki nyuma kumsindikiza Sajuki  Januari 4, 2013.
Msanii Jimmy Mponda a.k.a Jimmy Master alikuwa akimuaga Sajuki kwa staili yake.
Mhe. Zitto Kabwe (wa pili kushoto) akitafakari jambo na wasanii na waombolezaji wengine katika makaburi ya Kisutu kabla ya kuzikwa kwa Sajuki  Januari 4, 2013.

Kwaheri kijana wangu....! Msanii nyota wa filamu, Mzee Magali (kulia) akionekana mwenye majonzi tele kabla ya kuzikwa kwa mwenzao Sajuki  Januari 4, 2013.  (Picha zote: Shafii Banzi)
Said Fella (kushoto) na Chege pia walikuwapon
Ni huzuni kubwa kwa kifo cha mpendwa wetu Sajuki... Mungu amlaze pema! Mbunge wa Kinondoni, Mhe. Iddi Azzan.




Hapa kabla ya kuwasili kwa mwili kwenye makaburi ya Kisutu  Januari 4, 2013.








RAIS Dk Jakaya Kikwete jana aliongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya msanii Juma Kilowoko 'Sajuki' aliyefariki juzi jijini Dar es Salaam.
Mazishi ya msanii huyo yalifanyika katika makaburi ya Kisutu na kuhudhuriwa na watu maarufu nchini wakiwemo viongozi wa Serikali, Wabunge, wanamichezo na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki.
Mwili wa Sajuki uliwasili makaburini katika gari maalum la kubebea wagonjwa saa 8:47 mchana, dakika tatu baada ya Rais Kikwete kuwasili na msafara wake.
Mwili huo uliingizwa kaburini saa 8:53 na baada ya hapo baba wa marehemu, Mzee Said Kilowoko alitupia udongo kwenye kaburi la mwanae na kufuatiwa na Rais Kikwete na kisha Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba na kufuatiwa na waombolezaji wengine.
Akiongea katika makaburi ya Kisutu, Dk. Kikwete alisema serikali inasikikitishwa na kifo cha msanii huyo kijana aliyekuwa na ndogo za kuendeleza tasnia ya filamu nchini na kuitaka familia kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha maombolezo.
Naye baba wa marehemu, Mzee Juma Kilowoko, aliishukuru serikali, wasanii na watanzania kwa ujumla kwa namna walivyoshiriki tangu kifo cha mwanaye kitokee mpaka walipompumzisha jana kwa heshima zote na kudai hana cha kuwalipa zaidi ya kulipwa na Allah SW.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa na wengineo wengi.
Sajuki alifariki dunia juzi asubuhi katika hospitali ya Muhimbili alipolazwa kwa matatizo ya upungufu wa damu.
Baadhi ya waombolezaji akiwemo Meneja wa kundi la TMK wanaume Family Said Fella,  Wanamuziki Banana Zoro na Kassim Mapili wamesema kifo cha Sajuki ni pigo sio tu kwa familia yake bali tasnia nzima ya sanaa nchini.
Wasanii mbalimbali pamoja na wachezaji wa mpira wa miguu wa zamani walijitokeza katika mazishi ya msanii huyo, aliyeanza kufahamika mwaka 2005 alipojiunga Kaole kabla ya kuanza kujitegemea akizalisha filamu mbalimbali zilizompatia umaarufu mkubwa.
Marehemu Sajuki ameacha mke na mtoto watoto wawili.

No comments:

Post a Comment