STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 20, 2010

Ligi ya TFF Kilosa kuanza mwezi ujao


LIGI ya Soka ya TFF Wilaya ya Kilosa, inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi ujao ambapo fomu za ushiriki wa ligi hiyo zitaanza kutolewa Septemba 15 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Kilosa, KIDFA-Kilosa, Anthony Malipula, alisema ligi yao inatarajiwa kushirikisha timu zaidi ya 20 kati ya klabu zote 57 zilizosajiliwa wilayani humo.
Malipula, alisema fomu hizo za usajili zitakaponza kutolewa klabu zitalazimika kulipa ada ya Sh 30000 badala ya 50000 iliyowekwa kwa lengo la kutoa nafasi klabu nyingi zaidi kujitokeza tofauti na msimu uliopita.
"Ligi yetu ya TFF inatarajiwa kuanza mwishoni mwa Septemba kwenye Uwanja wa Halmashauri ya Kilosa na fomu zitaanza kutolewa Septemba 15 kwa gharama ya Sh. 30,000 badala ya 50,000." alisema.
Katibu huyo alisema ligi yao ya msimu uliopita ilishirikisha timu 18 ambapo klabu ya Mvumi Stars ndio walioibuka mabingwa na kuiwakilisha wilaya yao katika Ligi ya TFF Mkoa wa Morogoro na kuishia kushika nafasi ya pili kwenye kundi lao na kukwama kwenda kushiriki Ligi ya TFF ngazi ya Taifa iliyomalizika hivi karibuni.

Mwisho