STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, July 16, 2013

Waliokufa Darfur waagwa, JWTZ lakana ongezeko la vifoWAKATI miili ya wanajeshi saba wa Tanzania waliouwawa huko Darfur, Sudan wakiagwa kwa heshima nchini humo na kuanza mipango ya kurejeshwa nchini kwa ajili ya mazishji yake, Jeshi la Watanzania Tanzania, JWTZ, limekanusha taarifa za kuwepo kwa ongezeko la vifo vya askari wake.
Msemaji wa jeshi hilo. amenukuliwa hivi punde na Clouds FM kwamba hakuna askari mwingine aliyefariki japo alikiri mmoja wa majeruhi wa tukio hilo hali yake ni tete kiasi cha kuhamishwa hospitali aliyokuwa akipewa huduma na wenzake 9 na kupelekwa Khartoum kwa matibabu zaidi.
"Hatujui hizi taarifa zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii wanazipata wapi wakati sisi ndiyo wenye kuhusika na tukio, ila ukweli ni kwamba hakuna idadai iliyoongezeka ya vifo na jeshi halina sababu ya kuficha kitu," alisema Kanali Kapambala Mgawe Msemaji wa JWTZ.
Kanali Mgawe alisema hali za majeruhi wengine tisa zinaendelea vyema kiasi cha kuweza kutembea wenyewe japo mwenzao mmoja amehamishiwa Khartoum kwa matibabu zaidi na kuwataka watanzania wasiwe na hofu wala kuziamini taarifa hizo zinazoandikwa na kuwekwa kila muda katika mitandao hiyo.
"Watanzania hawana haja ya kuwa na hofu hali za askari wetu zinaendelea vyema japo mmoja hali yake siyo nzuri sana na kulazimika kuhamishiwa mjini Khartoum kwa matibabu zaidi na wenzake tisa tunashukuru kwani wanaendelea vyema," alisema.
Hapo chini ni baadhi ya picha za miili ya wanajeshi hao ikitolewa heshima na wanajeshi wenzao, sambamba na majeruhi waliolazwa baada ya tukio hilo la kushambuliwa na waasi wakati katika msafara wao wa kulinda amani katika jimbo hilo la Darfur.


The African Union – United Nations Mission in Darfur (UNAMID), held a memorial ceremony, in Nyala, the capital of South Darfur, to honor the seven fallen peacekeepers who lost their lives in the 13 July attack in South Darfur. The bodies are scheduled to be repatriated to Tanzania, the home country of the fallen peacekeepers. In addition to the seven killed, 17 military and police personnel were wounded, among them two female Police Advisors, all of whom are recovering from their injuries in UNAMID’s hospital in Nyala, South Darfur. Photo by Saidi Msonda, UNAMID.
 On 14 July 2013, following a 13 July attack in which seven military peacekeepers of the African Union - United Nations Mission in Darfur (UNAMID) were killed and 17 military and Police personnel wounded, among them two female Police Advisers, Joint Special Representative Mohamed Ibn Chambas visited the wounded peacekeepers at UNAMID’s hospital in Nyala to provide encouragement and support. Photos by Albert González Farran, UNAMID.


Casillas amkwamisha Kaseja kutua Mtibwa Sugar

http://api.ning.com/files/yP-BaUmjm1TVvubOvsoSqSDjHM5i*EFqxCiKIcJqP*Hp44nQRbrCsfGtyPFzTEVokJ7c7hN7dlExU4cM0Rphezsk191ETtnq/KASEJA.jpg?width=366
Juma Kaseja
http://www.ippmedia.com/media/picture/large/hussein%20sharrif%20%5C%27Casil.jpg
Hussein Sharrif 'Casillas'

KUKWAMA kwa kipa Hussein Sharrif 'Casillas' kujiunga na Fc Lupopo baada ya klabu yake ya Mtibwa kushindwa kuafikiana dau na timu hiyo ya DR Congo kumemfanya 'Tanzania One', Juma Kaseja kushindwa kutua Manungu kuichezea timu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu.
Kaseja aliyetemwa na Simba baada ya kuitumikia miaka karibu 10, alikuwa akitajwa kuwa mbioni kusajili wa Mtibwa, lakini Mkurugenzi wa klabu hiyo, Jamal Bayser aliiambia MICHARAZO muda mchache uliopita kuwa, mpango huo umekufa baada ya Casillas kukwama kutua Lupopo.
Casillas alifuzu majaribio katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya DR Congo na alikuwa katika maandalizi ya kuondoka kwenda kujiunga na timu hiyo wakati klabu hizo mbili zikifanya mazungumzo ya mwisho kuhusu dau la uhamisho wake.
Hata hivyo Bayser alisema kuwa  mazungumzo hayo ya Casillas kuhamia Lupopo yamekwama baada ya Wakongo kushindwa  kuafiki dau walilokuwa wakilitaka na hivyo kipa huyo atasalia Mtibwa kwa msimu ujao na kwa maana hiyo hawana mpango na kipa mpya.
Bayser alisema walikuwa na dhamira ya kumnyakua Kaseja iwapo mazungumzo baina yao na Lupopo yangeenda vyema kwa Casillas kuondoka, lakini kw ahali ilivyo wamesitisha mipango ya kumsajili Kaseja ambaye alimtaja kama kipa bora ambaye kila timu inatamani iwe naye.
"Mazungumzo yetu na Fc Lupopo juu ya kuwapa Casillas yamekwama na hivyo kipa huyo atasalia Mtibwa na kwa maana hiyo hatuna haja ya kumuongeza kipa yeyote mpya kama ambavyo tulikuwa tumepanga tukimfikiria Kaseja," alisema Bayser.
Bayser aliongeza pia klabu yao haina mpango wowote wa kusajili mchezaji kutoka nje ya nchi na badala yake wataendelea kuwaamini vijana wazawa kama walivyofanya msimu uliopita na kumaliza ligi wakiwa katika nafasi ya tano.
Kwa wiki moja sasa kulikuwa na tetesi kwamba huenda Kaseja aliyetemwa Simba angetua Mtibwa Sugar au Coastal Union, kabla ya Coastal kuweka bayana kuwa haina mpango naye.

Dereva wa Bodaboda afa, wengine wajeruhiwa katika ajali

e47f5cfc9fL 
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi, Handeni.
DEREVA mmoja wa Bodaboda amefariki dunia papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa kwenye ajali baada ya pikipiki mbili kugongana usukani kwa usukani huko kwenye eneo la Mzundu wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP Constantine Massawe, amemtaja Dereva huyo wa Bodaboda kuwa ni Ismail Mhando(30), mkazi wa Kabuku wilayani Handeni. Amesema kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mzundu wilayani Handeni mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo katika uchunguzi wa awali wa tukio hili Polisi walibaini kuwa imesababishwa na mwendo kasi kwa kila mmoja na kutokuwa makini barabarani.
 
Amesema marehemu Mhando akiendesha pikipiki yenye nambari za usajili T.256 AYM akitokea Kabuku kwenda Mzundu akiwa amempakia dada mmoja aitwaye Salama Bakari, aligongana na pikipiki nyingine iliyokuwa ikitokea Mzundu kwenda Kabuku yenye namba za usajili T.584 CCS. Alisema pikipiki hiyo ikiendeshwa na Sudi Nassoro ilikuwa imepakia abiria wawili maarufu kama mshikaki na ilikua ikitokea katika kijiji cha Mzundu kwenda Kabuku wilayani humo.
 
Kamanda Massawe amesema majeruhi wanne wa ajili hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Handeni kwa matibabu zaidi na hali zao amesema zinaendelea vizuri.
 
Kamanda Massawe ametoa wito kwa Madareva wote wa Bodaboda kuwa makini wanapokuwa barabarani na kujiepusha na upakiaji abiria zaiidi ya mmoja ili kuepuka matukio ya ajali zinazowahusisha watu wengi kwa wakati mmoja.
 
Amewataka kila mmoja wao kuwa mlinzi wa mwingine na kutoa taarifa pale wanapomuona mwenzao mmoja anavunja sheria na kutotii sheria bila ya shuruti ili achukuliwe hatua ili kuwanusuri wengine wanaofanya kazi zao vizuri.


Kifo mkweli ahadi! Fundi anusurika kifo licha ya kuchomwa chuma kichwani

Liu Fenghe akiwa hospitali na chuma kichwani
Picha ya X-ray ikionyesha jinsi chuma hicho kilivyoingia kichwani mwa bwana Liu. (Picha: HAP/Quirky China News/Rex)

FUNDI majengo Liu Fenghe wa nchini China, amenusurika kifo baada ya kuchomwa na chuma kichwani na kuzama inchi 8 ambazo ni sawa na sentimita 20.

Liu alikuwa akiongea na rafiki yake na kwa bahati mbaya alidondokewa na chuma hicho kilichomchoma kichwani.

Rafiki yake Liu aitwaye Zhang anasema:
"Ilikuwa ghafla. Kabla sijafanya chochote Liu alikuwa katika dimbwi la damu."Inadhaniwa kuwa chuma hicho kilidondoka kutoka ghorofa ya 25 ya jengo walilokuwemo mafundi hao mpaka kusababisha maafa hayo.
Madaktari walimfanyia upasuaji wa haraka katika hospitali iliyopo jimbo la Shanghe nchini China na kueleza kuwa Liu hayupo tena katika hatari japo bado haijajulikana ni lini ataweza kurudi kazini.

Fabregas azikata maini Arsenal, Man United

2013 cesc fabregas barcelona
Cesc Fabregas

SIKU moja tu baada ya klabu ya Manchester United kutangaza kuongeza dau ili kumnasa nahodha wa zamani wa mahasimu wao Arsenal, Cesc Fabregas, kiungo huyo ameikata maini timu hiyo.
Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Hispania anayeichezea Barcelona alikuwa chaguo la kwanza la David Moyes baada ya kumkosa Thiago Alcantara, pia alikuwa akiwindwa na klabu yake ya zamani. Hata hivyo  kocha wa Barcelona, Tito Vilanova amefichua kuwa,  aliongea na kiungo huyo na kumwambia kuwa kwamba anahitaji kuendelea kubaki Camp Nou.
Jana iliripotiwa kwamba United walituma ofa ya kwanza ya kiasi cha £25.9 million  kwa ajili ya kumsajili Fabregas, ambaye amefeli kupata nafasi katika kikosi cha kwanza tangu aliporudi akitokea Arsenal.
Lakini akiongea na waandishi wa habari leo mchana, Vilanova amesema wazi kwamba Fabregas bado anataka kubaki kwenye klabu yake hiyo ya utotoni, na hana mawazo ya kuondoka.
 "Ninafahamu kwamba tumepokea ofa kadhaa kutoka kwa vilabu tofauti. Niliongea na Cesc na ameniambia kwamba anataka kubaki.
"Cesc hana mawazo ya kuondoka kwenda klabu nyingine. Anajua ushindani ni mkubwa hapa na ana ndoto za kuendelea kuwa hapa na kufanikiwa.


MIUJIZA! Mtoto azaliwa na Tasibhi shingoni mwake

clip_image001KATIKA tukio la kustaajabisha, mtoto mmoja huko nchini Nigeria amezaliwa akiwa na tasbihi shingoni mwake na kuwashangaza wengi akiwemo wakunga waliomzalisha mama wa mtoto huyo.
Maelfu ya watu walifika hospitali binafsi ya uzazi kwenye jiji la Kotaworo eneo la Bida, iliyopo jimbo la Niger  Jumapili, kwa lengo la kwenda kumshuhudia mtoto wa kike aliyezaliwa akiwa amevaa Tasbihi inayotumika katika utajo wa Mwenyezi Mungu shingoni mwake.
Inaelezwa kwamba mama wa mtoto huyo ambaye ana miaka ya kati, Adijat, alikimbizwa hospitali karibu na nyumbani kwa  Mohammed Bello Masaba, mida wa saa 8 mchana na baada ya pilika za uzazi alifanikiwa kujifungua mtoto huyo.
Kwa mujibu wa mmiliki wa hospitali hiyo ya uzazi, Alhaji Abubakar Baiwa Shasha ambaye ndiye aliyesimamia zoezi hilo la kujifungua alisema; 
“Nilishtuka nilipoona mtoto anatoka akiwa na Tasbihi shingoni mwake, na wakati wa uzazi mtoto alizaliwa tasbihi hiyo ilikuwa nyeusi," alisema Shasha.
“Ila nilishangaa baada ya muda tasbihi hiyo ilibadilika na kuwa nyeupe huku kukiwa na watu wengine wamezunguka.”
“Mara baada ya habari hiyo kusambaa mjini, maelfu ya watu walifika kwenye hospitali hiyo ya uzazi huku wakisema “Allahu Akibar; Allahu Akibar (Mungu ni Mkubwa) huku wakifika na kumgusa mtoto huyo.”
Juhudi za kumpata Baba wa mtoto huyo aitwaye Isah, ambaye anatokea eneo la Loma ndani ya Jimbo la Kwara  zilishindikana baada ya kukataa kuongea na mtoa habari.
Mwanachuo mmoja wa Kiislamu, Malam Idiris Ndajiwo alisema, kuzaliwa kwa mtoto huyo akiwa na kitu kama hicho inaonyesha ukuu wa Allah (SW). Kuzaliwa kwa mtoto huyu leo, kwenye mji huu na eneo hili (Kutaworo) ni kitu kikubwa kwa Waislamu. Hii hakika inakuja kuonyesha kwamba Allah ndiye mwenye kupanga kwa lolote kutokea kwa yeyote kwenye ulimwengu huu.”

Pigo! Jaji Chipeta afariki dunia
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Buxton Chipeta enzi za uhai wake
HABARI zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania,Buxton Chipeta amefariki dunia muda mfupi uliopita.

Kwa mujibu wa mmoja wa wanafamilia, Jaji Chipeta alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kisukari ambapo ilifikia wakati akalazimika kukatwa vidole kadhaa vya miguuni.

Enzi za uhai wake, Jaji Chipeta aliweza kujijengea heshima katika kazi yake na kufikia kuwa mmoja wa majaji wanaoheshimika mno hapa nchini.
 

Pia Jaji Chipeta aliwahi kuwa miongoni mwa majaji wa Tume ya kurekebisha Sheria yeye akiongoza kanda ya Dar es Salaam.
 

MICHARAZO  inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao na kuwaombea kwa Allah Subhana Wataala kuwa na subira na uvumilivu kwa kuamini kuwa kila nafsi itaonja mauti na kurejea kwa aliyetuumba. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema.

Walimu Shule ya Msingi King'ongo wawalia wazazi, kisa utoro wa wanafunziUONGOZI wa Shule ya Msingi King'ongo, iliyopo Kata ya Saranga, wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, umelia na vitendo vya utoro uliokithiri kwa wanafunzi wanaosoma shule hiyo hasa wale wa darasa la saba na kuwaomba wazazi wa wanafunzi hao kuingilia kati kuwasaidia.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Flora Salila alitoa kilio hicho katika mkutano wa pamoja kati yao na wazazi wa wanafunzi wa darasa la saba uliofanyika juzi shuleni hapo.
Mwalimu Salila, alisema uongozi wao umekuwa katika wakati mgumu kutokana na vitendo vya utoro kwa wanafunzi na hasa wa darasa la saba, ambapo kuna wakati hufikia mpaka wanafunzi 58 kati ya 268 wa darasa hilo la saba kutoonekana shuleni.
Mwalimu huyo alisema vitendo hivyo huenda vinachangiwa na wazazi kutojenga utamaduni wa kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni na kuwapa wakati mgumu walimu ambao hujaribu kutatua tatizo hilo la utoro bila mafanikio kwa kukosa ushirikiano na wazazi.
"Lazima niwaeleze ukweli kuwa, utoro ni tatizo sugu shuleni kwetu hasa hawa wa darasa la saba kwa mfano karibu wanafunzi 58 miongoni mwa 268 wa darasa hilo hawakuwepo shuleni wakati wa upigaji wa picha za maandalizi ya mitihani, hii siyo jambo zuri, wazazi tusaidieni," alisema.
Aliongeza kwa jumla ya wanafunzi 1762 waliopo shuleni hapo kwa siku watoto kati ya 100-200 huwa hawafiki shuleni na kuhoji wazazi wenye watoto hao wanafanya nini katika kuwasaidia walimu kuwaondoa watoto katika vitendo hivyo vinavyochangia kudumaza taaluma.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King'ongo,  Demetrius Mapesi alisema ni lazima wazazi washirikiane na walimu kutatua utoro shuleni hapo iwapio wanataka shule yao iendelee kushika nafasi ya pili katika Kata ya Saranga.
Mapesi alisema wazazi wamekuwa wakishindwa kufuatilia nyendo za watoto wao na kuishia kuwatumia lawama walimu pale watoto wao wanapofanya vibaya kwenye mitihani wakati jukumu hilo ni la lazima kwao kabla ya walimu kufuatia hasa wanapokuwa shuleni.
"Wazazi badilikeni, kutofuatilia nyendo za watoto wenu ndiyo chanzo cha kuharibika kwa vijana, dunia ya sasa imeharibika na haiaminiki, ukijifanya upe bize na kazi ujue unazalisha watoto machangudoa, vibaka na hata mashoga, mtakuja kumlaumu nani," alihoji Mapesi.

Mwisho

Polisi Dar wawanasa watuhumiwa wa ujambazi, mbakaji

wanachuo walipoandama baada ya tukio la kuvamiwa na kupigwa risasi kwa wenzao na majambazi waliokamtwa na jeshi l polisi

WATU wanne wanaodaiwa kuwa majambazi wamenaswa na Jeshi la Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na tukio la ujambazi lililotokea Juni 21, mwaka huu, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), katika eneo la bweni la Yombo One.
Aidha mtu mwingine anayedaiwa kumlewesha kwa dawa za kulevya kisha kumbaka kabla ya kumpora mfanyabiashara nyumbani kwake naye katiwa mbaroni na jeshi hilo baada ya kuendesha msako dhidi yake.
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Ally Mlege, alisema watuhumiwa wanne waliohusika na tukio la Chuo Kikuu,  walikamatwa na jeshi hilo Julai 8, mwaka huu, kwenye kituo cha Daladala Ubungo.
Kamanda Mlege, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata watu hao wakiwa na silaha aina ya SMG ikiwa na risasi moja, laptop mbili aina ya Toshiba, simu aina ya Samsung, panga moja na nyundo.
Alisema baada ya mahojiano, majambazi hayo yalikiri kuhusika katika tukio la unyang’anyi lililotokea UDSM.
Afande Mlege, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Dolisera Gerald (22), Leonard Mathias (21), Leonard Leopard (32), Gerald Moses (23), ambao licha ya kukiri kuhusika katika tukio hilo pia  walikiri kuhusika katika matukio mbalimbali ya kihalifu sehemu tofauti jijini.
Wakati huo huo Kamanda Mlege alisema jeshi hilo limemtia mbaroni mkazi wa Kimara, jijini Dar es Salaam, Ezekiel Matiti (35), kwa tuhuma za kumlewesha dawa za kulevya mkazi wa Makongo Juu, jijini humo, Aida Kiangi.
Kwa mujibu wa Mlege baada ya mtuhumiwa kumlewesha Aida, alimpeleka nyumbani kwake (Makongo Juu) na kumuingiza ndani na kumbaka na kisha kumuibia runinga, pamoja na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. milioni nane.
Aidha aliongeza kuwa, katika tukio lingine, polisi inawashikilia Michael Pascal (35), Donald Joseph (43), Kulwa Adamson (43), na Ally Akiri (41),  na watuhumiwa wengine watano, kwa tuhuma za kuhusika katika tukio la kurushiana risasi na askari polisi eneo la Kunduchi Mtongani.

Hussein Javu atamani soka la kulipwa

Hussein Javu (kulia) akikabana na Aggrey Morris wa Azam katika moja ya mechi za igi Kuu

MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya Mtibwa Sugar, Hussein Javu amesema anatamani kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchini bila kujali kama ni Afrika au barani Ulaya, ili kutimiza ndoto zake za tangu utotoni.
Javu, aliye katika kikosi cha pili cha taifa 'Young Taifa Stars' alisema ipo mipango anaiweka sawa ili kutimiza ndoto hizo za kucheza soka la kulipwa akiwa tayari kutua kokote hata kama ni nchi jirani za Kenya, DR Congo au Msumbiji.
Alisema kwa sasa anamsikilizia wakala wake kuona mipango hiyo inakwendaje, ingawa alisisitiza kuwa bado ana mkataba wa kuitumikia timu yake ya Mtibwa hadi mwakani.
Mshambuliaji huyo ambaye amekuwa wakitajwa kama miongoni mwa wachezaji wapya wa Yanga, ingawa mwenyewe anakanusha kuwa hajasaini kokote zaidi na kujitambua kama mchezaji wa Mtibwa kulingana na mkataba aliokuwa nao na klabu hiyo aliyojiunga nayo tangu mwaka 2007 katika kikosi cha vijana, alisema kiu ya kucheza soka la kulipwa ni kubwa kiasi cha kutoelezeka.
"Hakuna kitu ninachokitamani na kulilia kama kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, kuna mipango inafanywa lakini siwezi kuiweka wazi kwa sasa kwa vile ni mapema, ila nitafarijika sana kama nitaenda hata Kenya tu," alisema.
Javu anayemhofia dimbani beki wa zamani wa Simba aliyehamia Coastal Union Juma Nyosso, alisema kiu yake ya kucheza nje ya nchi imeongezeka baada ya kuona mafanikio ya wachezaji wenzake wa timu ya taifa, Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na watanzania wengine wanaocheza soka hilo barani Afrika katika nchi za DR Congo, Kenya, Msumbiji na Angola.
Pia aliweka bayana kwamba mbali na kiu ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi, pia angependa kuichezea timu mojawapo kubwa nchini kati ya Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikimuwinda ili kumsajili.

Maugo, Mwakyembe kutimka J4 ijayo kwenda Urusi

Mada Maugo
MABONDIA machachari wa Ngumi za Kulipwa nchini, Mada Maugo na Benson Mwakyembe wanatarajia kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Russia kwa ajili mapambano yao ya kimataifa dhiddi ya wenyeji wao itakayochezwa mwishoni mwa mwezi huu.
Rais wa TPBO-Limited, Yasin Abdallah 'Ustaadh', aliiambia MICHARAZO mabondia hao wataondoka Julai 23, ambapo Maugo ataenda kupigana na Movsur Yusupov na Mwakyembe ataonyeshana kazi na Apti Ustarkhanov kwenye michezo itakayochezwa kwenye ukumbi wa Trade &Intertainment uliopo mji wa Kasiysk, nchini Russia.
Ustaadh alisema watanzania hao watapigana na Warusi hao katika michezo ya kilo 75 (Super Middle Weight) itakayokuwa na raundi nane kila mmoja.
Rais huyo wa TPBO alisema mpinzani wa Maugo rekodi yake inaonyesha kuwa amecheza mapambano matatu na yote ameshindwa moja likiwa kwa KO wakati mpinzani wa Mwakyemba amecheza mechi mbili na kushinda moja na mwingine kupigwa.
"Pamoja na rekodi ndogo za wapinzani wao, lakini ikumbukwe kuwa mabondia wa Russia na kwingineko Ulaya huwa hawachezi ngumi za kulipwa bila kucheza ngumi za ridhaa na kufikia hatua ya kushiriki michuano ya Olimpiki kwa maana hiyo Maugo na Mwakyembe wakitarajiwe wepesi Russia," alisema Ustaadh.
Ustaadh aliongeza kuwa tayari mabondia hao wa Tanzania wameshaombewa visa za kwenda nchini humo gharama zote zikilipwa na TPBO-Limited na wataondoka nchini wakiongoza na wakala wao kutoka Kenya, Thomas Mutua atakayeondokea Kenya na kukutana na mabondia hao Dubai.