Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi, Handeni.
DEREVA
mmoja wa Bodaboda amefariki dunia papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa
kwenye ajali baada ya pikipiki mbili kugongana usukani kwa usukani huko
kwenye eneo la Mzundu wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP Constantine Massawe, amemtaja Dereva huyo
wa Bodaboda kuwa ni Ismail Mhando(30), mkazi wa Kabuku wilayani Handeni. Amesema
kuwa ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Mzundu wilayani Handeni
mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo katika uchunguzi wa awali wa tukio
hili Polisi walibaini kuwa imesababishwa na mwendo kasi kwa kila mmoja
na kutokuwa makini barabarani.
Amesema
marehemu Mhando akiendesha pikipiki yenye nambari za usajili T.256 AYM
akitokea Kabuku kwenda Mzundu akiwa amempakia dada mmoja aitwaye Salama
Bakari, aligongana na pikipiki nyingine iliyokuwa ikitokea Mzundu kwenda
Kabuku yenye namba za usajili T.584 CCS. Alisema
pikipiki hiyo ikiendeshwa na Sudi Nassoro ilikuwa imepakia abiria
wawili maarufu kama mshikaki na ilikua ikitokea katika kijiji cha Mzundu
kwenda Kabuku wilayani humo.
Kamanda
Massawe amesema majeruhi wanne wa ajili hiyo wamelazwa katika Hospitali
ya Wilaya ya Handeni kwa matibabu zaidi na hali zao amesema zinaendelea
vizuri.
Kamanda
Massawe ametoa wito kwa Madareva wote wa Bodaboda kuwa makini
wanapokuwa barabarani na kujiepusha na upakiaji abiria zaiidi ya mmoja
ili kuepuka matukio ya ajali zinazowahusisha watu wengi kwa wakati
mmoja.
Amewataka
kila mmoja wao kuwa mlinzi wa mwingine na kutoa taarifa pale
wanapomuona mwenzao mmoja anavunja sheria na kutotii sheria bila ya
shuruti ili achukuliwe hatua ili kuwanusuri wengine wanaofanya kazi zao
vizuri.
No comments:
Post a Comment