STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, February 18, 2014

UWF yahimiza wanawake kushiriki Siku ya Wanawake Dunia


  MENEJA wa Tuzo ya Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Marafiki (UWF) Mariam Shamo akifafanua jambo mbele ya washindi wa tuzo hiyo wa mwaka juzi na jana pamoja na wanahabari kuhusiana na hafla yao wanayoitarajia kuifanya siku ya Familia 'Family Day' Machi 15 mwaka huu,ambayo imepangwa kufanyika ndani ya kiota kipya cha maraha na burudani Escape One Mikocheni jijini Dar, pembeni yake ni  Mdau mkubwa wa tuzo hizo na Mkurugenzi wa Benki ya Wanawake Tanzania Margareth Chacha.

Mjumbe wa Mradi wa Mwanamakuka (Mwanamakuka Awards) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania,Bi. Margareth Chacha akisisitiza jambo mbele ya washindi wa Mwanamakuka mwaka 2012 na 2013 alipokuwa akiongelea siku ya Familia  Duniani tarehe 15 mwezi ujao mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Wanawake Marafiki (Unit of Women Friends),Bi Maryam Shamo.
WASHINDI wa Tuzo ya Mwanamakuka mwaka 2012 na 2013 wakiwa pamoja wakati walipokutana na waratibu wa shindano hilo kwa ajili ya kujipanga na Siku ya Wanawake Duniani inayotarajiwa kufanyika mnamo Machi 8 na kufuatiwa na Family Day Machi 15 mwaka huu.
WANAWAKE nchini wamehamasishwa kushiriki Siku ya Wanawake Duniani itakayofanyika Machi 8, na kufuatiwa na Family Day Machi 15, mwaka huu jijini Dar es Salaam na kujadili masuala mbalimbali ya kumwezesha mwanamke.
Mjumbe wa mradi wa Mwanamakuka (Mwanamakuka Award) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania, Margareth Chacha, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki kuwa siku hiyo ni ya muhimu kwa wanawake kwa vile itawaleta pamoja na kujadili masuala mbalimbali.
“Tutakutana Siku ya Wanawake Duniani na kujadili namna bora zaidi ya kumuwezesha mwanamke kujiinua kiuchumi,” alisema.
Alisema benki yake inafadhili washindi wanawake wajasiriamali kupitia mradi huo na inafanya hivyo kwa ajili ya kumwinua mwanawake kupitia benki yao ya wanawake.
Alisema benki hiyo inataka kuona wanawake wengi wanaingia katika shughuli za kijasiriamali na pia imejipanga kutumia matawi yake nchini kupanua wigo wa zawadi ya Mwanamakuka.
Alisema mpaka sasa ni asilimia mbili tu ya wanawake wanaotumia huduma za kibenki kati ya asilimia nane ya Watanzania wote wanaotumia huduma hizo, na sasa wakati umefika kuongeza idadi ya wanawake.
“Hali hiyo ni ya kihistoria lakini kwa sasa wanawake tunashukuru hali imebadilika tunaweza kufanyakazi mbalimbali zikiwamo za biashara,”aliongeza.
Alisisitiza umuhimu wa wanawake kujiunga katika vikundi kwa ajili ya kupata mikopo kutoka katika benki yao kufanyia shughuli zao za kijasiriamali.
Naye Meneja wa mradi wa Mwanamakuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kituo cha Wanawake Marafiki (UWF),  Maryam Shamo, alisema Siku ya Wanawake Duniani kutakuwa na maonyesho ya kazi za kijasiriamali za wanawake na michezo mbalimbali.
“Siku hiyo washindi wa mwaka huu watapatiwa zawadi zao, na pia mshindi wa jumla wa mwaka 2012 na 2013 atapatiwa zawadi kati ya washindi kumi waliokwisha pata zawadi,'' alisema.
Alifafanua kuwa katika kusherehekea ya siku hiyo, watu wengi wamealikwa wakiwamo akinamama wajasiriamali na wanasiasa wanawake.
Kwa upande wake, mjasiriamali mkazi wa Dar es Salaam na mshindi wa nyuma wa mradi huo, Tatu Ngao, alisema alishinda Shilingi  milioni sita ambazo zimemwezesha kufanya biashara yake kwa ufanisi.
“Nilishinda kupitia biashara yangu ya kutengeneza keki...nimepanuka kwa kiwango cha kuridhisha hadi sasa,” alisema.
Zawadi ya Mwanamakuka ni mradi uliobuniwa na Kituo cha Wanawake Marafiki kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wanawake kwa ufadhili wa Benki ya Wanawake Tanzania na wadau wengine.

Naye mshindi wa pili wa mwaka jana , Leila Mwambungu alisema anashukuru mradi huo umemfanya apanuke kiakili katika ujasiriamali pamoja na kuweza kuwasaidia wanawake wenzake na kiu yake kubwa kuzidi kusonge mbele ili kuwa mfano kwa wengine.
"Nashukuru waandaji wa tuzo hii, shukrani zangu za pekee ziende kwa Mariam Shamo, Mama Margareth Chacha kwa namna wanavyowasaidia wanawake wenzao, najisikia furaha na fahari kuwa Mwanamakuka namba mbili wa mwaka 2013 na kiu yangu nifike mbali zaidi baada ya kuwezeshwa na mradi huu," alisema Leila. 


Yanga imepania, yamtuma Mkwasa Cairo kuifanyia ushushushu Al Ahly

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyhILGXEPzcg08Ou6VWhyphenhyphenGQ_bEGVRsjHkUwM-95WMFyKgoa3AmSEp0pQFl7LDHsP8AUvz0B1SdcA1_DqHCjiLzsmNFvGJVgE7hf4UYU6HgdkrfVXUq4_nOTvCDcVKeGrucIGKzxSSwSOHl/s640/Charles-Boniface-Mkwasa1.jpg
Charles Boniface Mkwasa aliyeondoka nchini leo mchana
Yanga watakaowavaa Al Ahly ya Misri Machi mwaka huu kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika
KATIKA kuhakikisha kwamba Wamisri hawaponi kwa vijana wa Jangwani, Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa 'Master' ameondoka nchini mchana wa leo kuelekea Cairo nchini Misri ili kwenda kuipeleleza Al Ahly katika mechi yake ya fainali ya Super Cup dhidi ya Cs Sfaxien ya Tunisia.
Mechi hiyo itachezwa Alhamisi na Mkwasa ataenda kuwafanyia ushushushu Al Ahly watakaovaana nao kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika mapema mwezi ujao.
Kwa mujibu wa tovuti ya klabu Yanga, imesema kuwa Mkwasa ataenda kushuhudia mchezo huo Super Cup inayozikutanisha Bingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika na wale wa Kombe la Shirikisho Afrika, mchezo utakaochezwa katika dimba la Cairo International Stadium.
Mkwasa ameondoka kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia Airline ambapo atapitia jijini Adis Ababa kabla ya kuunganisha kuelekea Cairo ambapo atatua Uwanja wa Ndege majira ya saa 7 usiku na kupokelewa na wenyeji kutoka ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Misri.
Kutokana na umuhimu wa mchezo huo Uongozi wa Young Africans kwa pamoja na Benchi la Ufundi walikaa na kukubaliana kuwa kocha msaidizi Mkwasa aende kushuhudia mchezo huo wa fainali ambao utaweza kusaidia kupata picha ya wapinzani Al Ahly ambao watacheza na Young Africans mwishoni mwa mwezi huu.
Lengo la safari ni kuweza kuwaona Al Ahly wanavyocheza katika mchezo huo wa fainali, pili ni kujua wanayocheza wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani na tatu ni kuijua timu nzima kiufundi inachezaje.
Kwa upande wake Kocha Mkwasa amesema anaamini ataitumia vizuri nafasi hiyo ya kuutazama mchezo wa Super Cup kwa kuwasoma wapinzani na pindi atakaporejea atasaidiana na kocha mkuu kuwaandaa vijana tayari kwa mchezo huo.
Mkwasa mara baada ya kuutazama mchezo huo dhidi ya CS SFaxien siku ya Alhamis jioni saa 11 kamili kwa saa za Afrika Mashariki atarejea nchini siku ya ijumaa n akuungana na kikosi kwa ajili ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Ruvu Shooting.
Al Ahly Mabingwa watetezi wa klabu Bingwa Barani Afrika watacheza na Young Africans Tarehe 1 Machi 2014 katika mchezo wa kwanza wa kuwania kuingia katika 16 bora kisha kurudiana jijini Cairo wiki moja baadae.
Rekodi inaonyesha kuwa Yanga haijawahi kuifunga achilia mbali kuitoa timu yoyote ya Afrika Kaskazini katika michuano ya kimataifa na safari hii wana jangwani wameapa ni lazima mzizi wa futina ukatwe kwa kuwaondosha na kuwavua taji Al Ahly katika mechi zao za raundi ya kwanza.

STAND UNITED YAIKATIA RUFANI KANEMBWA JKT

Vurugu  za mechi ya awali baina ya Stand Utd na Kanembwa JKT

TIMU ya soka ya Stand United ya Shinyanga imekata rufani Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikipinga Kanembwa JKT ya Kigoma kuchezesha wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo kwenye mechi ya kiporo iliyozikutanisha timu hizo.
Mechi hiyo namba 22 ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ilichezwa juzi (Februari 16 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo Kanembwa JKT iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Katika rufani yake, Stand United inadai kwenye mechi hiyo Kanembwa JKT ilichezesha wachezaji wanane waliosajiliwa katika dirisha kidogo kinyume na maelekezo kutoka TFF kwa timu hizo kuwa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha dogo hawawezi kucheza mechi hiyo.
Wachezaji wanaodaiwa kusajiliwa dirisha dogo na kucheza mechi hiyo ni Hamidu Juma, Ibrahim Shaban Issa, Joseph Mlary, Lucas Charles Karanga, Raji Ismail, Salvatory Kulia Raphael, Seif Ibrahim Zaid na Yonathan David Sabugowiga.
Dirisha dogo lilifunguliwa Novemba 15 na kufungwa Desemba 15 mwaka jana, hivyo Stand United katika rufani yake inaombwa ipewe pointi tatu na mabao matatu kwa Kanembwa JKT kuchezesha wachezaji wasiostahili.
Awali mechi hiyo ilichezwa Novemba 2 mwaka jana Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, na kuvunjwa na mwamuzi dakika ya 87 baada ya Kanembwa JKT kugomea pigo la penalti dhidi yao.

Twiga Stars kurudiana na Zambia Machi 2

 Na Boniface Wambura
MECHI ya pili ya raundi ya kwanza kuwania Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) kati ya Tanzania (Twiga Stars) na Zambia (Shepolopolo) itachezwa Machi 2 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

Twiga Stars tayari imeingia kambini kujiandaa kwa mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili jioni. Twiga Stars chini ya Kocha Rogasian Kaijage inafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Karume ambao ni wa nyasi za bandia kama ulivyo ule wa Azam Complex.

Shepolopolo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.

Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuiondoa Shepolopolo itacheza na mshindi wa mechi kati ya Botswana na Zimbabwe. Zimbabwe ilishinda mechi ya kwanza ugenini.

Wachezaji wa Twiga Stars waliopo kambini ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya na Fatuma Mustafa.
Wengine ni, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Flora Kayanda, Happiness Mwaipaja, Maimuna Mkane, Mwajuma Abdallah, Mwapewa Mtumwa, Pulkeria Charaji, Sherida Boniface, Sophia Mwasikili, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.

Wa3 waombewa ITC kucheza Thailand, Ujerumani



WACHEZAJI watatu wanaocheza mpira wa miguu nchini Tanzania wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili wakacheze katika nchi za Thailand na Ujerumani.



Mchezaji Khamis Mroki Jamal aliyekuwa na timu ya Daraja la Kwanza ya Polisi Dar es Salaam ameombewa ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Thailand (FAT) ili akajiunge na Kabinburi ya nchini humo.



Said Ali Nassor aliyekuwa akichezea FC Turkey ya Zanzibar na Samuel Chuonyo wameombewa na ITC na Chama cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) kwa ajili ya kujiunga na klabu ya VfB Eichstatt.



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zote zitakapokamilika ikiwemo ridhaa ya klabu zao za hapa Tanzania itatoa ITC hizo.

Wadanganyifu TFF washtakiwa Kamati ya Maadili

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewalalamikia wana familia watano wa mpira wa miguu kwa Kamati ya Maadili kuhusiana na udanganyifu katika mtihani wa utimamu wa mwili wa waamuzi na usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi.

Riziki Majala na Army Sentimea ambao ni wakufunzi wa waamuzi, na Oden Mbaga na Samwel Mpenzu ambao ni waamuzi wanadaiwa kughushi nyaraka kuhalalisha mtihani huo kinyume cha taratibu.

Naye Sabri Mtulla analalamikiwa na TFF kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi lolote juu ya usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.

Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo.

CCM yawaonya vikali Lowassa na wenzake


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTt29nQDhgvo4aSwRstqcg9niRSVdsUPKCplQaZqwKxhMtoltV8TO3YuTwgV7VyC54dDsO4Hwl5onj7IXeagLMkN9ReHe73OIfKg6nNThzTzD5rSEcLu9xrW1u-a6p0VjLxg_itDR65gC-/s1600/nec13.jpg
Kati ya tarehe 13/02/2014  na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama.



Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013.



Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:-



1.            Ndg. Frederick Sumaye

2.            Ndugu Edward Lowasa

3.            Ndugu Bernard Membe

4.            Ndugu Stephen Wassira

5.            Ndugu January Makamba

6.            Ndugu William Ngeleja



Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza adhabu.  Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika.



Kwa ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-



1.        Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).



2.       Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.  Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo.

 

Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi.



Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni:-



“Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.”



Kamati Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama.



Aidha, Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu za Chama.




Imetolewa na:-




Nape Moses Nnauye,

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,

ITIKADI NA UENEZI,

18/02/2014

KUMEKUCHA KILI MUSIC AWARDS 2014


Mwaka 2009, wazo jipya lilizaliwa. Wazo la kuwa na tuzo zitakazopatikana kwa mchakato wa wazi utakaotokana na mapendekezo ya watu wenyewe ya kuchagua mastaa wa michezo, muziki, filamu au vipindi na watangazaji wanaopendwa zaidi. Wazo hilo liliendelea kuboreshwa na mwaka huu (2014), limeiva na liko tayari kutoka kwenye hatua ya wazo la kichwani, na kuwa tukio lenyewe.

"Nilizisajili na kuanzisha mwaka 2009 ila kutokana na mipango na malengo ya kampuni niliamua kuziweka kwanza hadi sasa," anasema Mwenyekiti wa Bongo5 Media Group, Luca Neghesti.

"Sasa hivi tumeshuhudia ukuaji katika tasnia mbalimbali na tumeona ni wakati muafaka wa kuwatunuku wale wanaopendwa na wananchi, kuwapatia tuzo pamoja na zawadi ya fedha taslimu milioni 1" ameongeza.

Tofauti na tuzo zingine, tuzo za watu hazitafuti ubora bali zinalenga wanaopendwa zaidi na tuzo hizi hazitajikita katika tasnia moja peke yake.

Kwa kuanzia, tuzo hizi zitatolewa katika tasnia ya burudani inayojumuisha filamu na muziki. Pia zitaiangazia sekta ya utangazaji kwa kuwatunuku watangazaji na vipindi vinavyopendwa zaidi na watu nchini huku pia mwanamichezo bora (soka, basketball, ndondi na michezo mingine) naye akipewa nafasi.

Tuzo za watu si tuzo za vijana peke yake, zipo kuwakilisha watu wa rika zote.

Tofauti nyingine kubwa ni kuwa tuzo za watu zitalenga kuwatunuku watu kutokana na umaarufu ama kupendwa kwao na si ubora. "Tuzo hizi hazileti ushindani na tuzo zingine kwasababu hazilengi tasnia moja tu," anafafanua Neghesti.

"Tanzania imesifiwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na tuzo hizi zinalenga kujumuika na tuzo zingine kuhakikisha watanzania wanaopendwa na kufanya vizuri wanatambuliwa."

Upigaji kura unaanza wiki hii katika vipengele 11 ambapo wananchi wenyewe watachagua majina ya washiriki watakaoshindana kwenye vipengele hivyo. Awamu ya kwanza ya upigaji kura itafungwa baada ya wiki mbili kutoka siku ya kwanza ya upigaji kura na majina ya watu watano waliotajwa zaidi kutoka kwenye kila kipengele watachaguliwa kama watajwa wa mwisho.

Kuanzia hapo, upigaji kura wa wananchi utajikita tu katika orodha ya majina hayo matano kwenye kila kipengele kinachoshindaniwa. Wiki moja baada ya majina ya washiriki kutangazwa, mchujo wa kwanza utafanyika katika kila kipengele na mtu mmoja ataondolewa.

Wiki moja baadaye, mchujo wa pili utafanyika na kuwabakiza washiriki watatu kwenye ila kipengele.

Washiriki wote 33 (watatu katika kila kipengele) waliosalia baada ya kufanyika mchujo wa mwisho, watakuwa wageni wa heshima kwenye utoaji wa tuzo hizo, utakaofanyika wiki moja baada ya mchujo huo wa mwisho.

Katika hafla hiyo, washindi watatangazwa na kila mshindi atapokea zawadi ya fedha taslimu, shilingi 1,000,000 za Kitanzania pamoja na tuzo ya thamani iliyotengenezwa kwa mkono kutoka kwenye mali ghafi asili za Kitanzania.

Tuzo za watu mwaka 2014 zitajumuisha vipengele 11 ambavyo ni pamoja na:

1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW1 na jina' kwenda 15678)
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW2 na jina' kwenda 15678)
3. MTANGAZAJI WA TV ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW3 na jina' kwenda 15678)
4. KIPINDI CHA TV KINACHOPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW4 na jina' kwenda 15678)
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW5 na jina' kwenda 15678)
6. MWANAMUZIKI WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW6 na jina' kwenda 15678)
7. MWANAMUZIKI WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW7 na jina' kwenda 15678)
8. WIMBO UNAOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW8 na jina' kwenda 15678)
9. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIUME ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW9 na jina' kwenda 15678)
10. MUIGIZAJI WA FILAMU WA KIKE ANAYEPENDWA (tuma SMS yenye 'TZW10 na jina' kwenda 15678)
11. FILAMU INAYOPENDWA (2013) (tuma SMS yenye 'TZW11 na jina' kwenda 15678) JINSI YA YA KUPIGA KURA

Mchakato wa kupendekeza majina ya washiriki katika tuzo hizi utafanyika kwa njia kuu mbili. Ya kwanza ni kwa kutumia tovuti ya tuzo hizi ambayo ni www.tuzozetu.com ambapo utakutana na hatua rahisi ya kupendekeza na kutaja majina katika vipengele vyote 11. Jinsi ya kupiga kura, bofya palipoandikwa Piga Kura na ufuate hatua rahisi kabisa ambayo haikuhitaji kujiandikisha jina wala email yako.

Njia ya pili ni kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu ambapo utaandika neno ‘Tuzo’ kwenda namba 15678. Ukishafanya hivyo utaletewa Menu yenye vipengele vyote 11 vikiwa na code number zake. Kutaja ama kupendekeza jina, tuma code husika na jina kwenye namba hiyo hiyo; kwa mfano Justin Bieber. Gharama ya sms ni ile ile inayotozwa sms ya kawaida.

ROBO FAINALI YA FA HAIMTISHI KOCHA EVERTON

DROO ya mechi za Robo fainali ya michuano ya Kombe la FA Englabnd imetoka na kuonyesha timu gani itakutana na nani katika hatua hiyo baada ya kufuzu mwishoni mwa wiki.
Arsenal walioing'oa Liverpool wenyewe wataanzia nyumbani dhidi ya Everton iliyoitambia Swansea City kwa kuilaza mabao 3-1.
Hata hivyo kocha wa timu hiyo ya  Everton, Roberto Martinez amesisitiza kuwa hawana cha kuogopa watakaposafiri kwenda Emirates kuivaa Arsenal .
Martinez alisema: "Wakati wa upangaji wa ratiba mara zote unatumai kuangukia nyumbani, lakini hilo halijalishi – kama unahitaji kutwaa kombe siku zote lazima ujiandae kukutana na yeyote. Tutahitaji kuwa katika kiwango chetu bora lakini ni kitu ambacho tunahitaji kukitazama."
Kutinga katika hatua hiyo ni hatua nzuri kwa kocha Arsene Wenger ambaye kwa muda mrefu hajashuhudia klabu yake ikinyakua taji lolote ambapo kesho itakuwa vitani barani Ulaya kuumana na watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ili kuona kama inaweza kunyakua matji matatu kwa mpigo.
Arsenal ipo katika nafasi nzuri ya ubingwa wa Ligi Kuu ya England ikiongoza kwa sasa mbele ya Chelsea, Manchester City na Liverpool.
Mbali na mechi ya Toffee's na Gunners, pia robo fainali ya FA inaonyesha Brighton & Hove Albion itaumana ama Hull City v Sunderland, Sheffield United v Sheffield Wednesday au Charlton Athletic na  Manchester City dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo Wigan Athletic.