STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 13, 2014

Demba Ba aibeba tena Chelsea, yashinda ugenini

Demba Ba of Chelsea celebrates after scoring against Swansea.
Demba Ba akimshukuru Mungu baada ya kuifungia Chelsea bao dhidi ya Swansea muda mfupi uliopita

Chelsea's Eden Hazard and Swansea's Jose Canas
BAO pekee lililofungwa na Demba Ba limeiwezesha Chelsea kuzidi kuisogelea Liverpool katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga Swansea City ikiwa kwao bao 1-0.
Msenegal huyo aliyeivusha Chelsea kwenye Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG aliyeanzishwa katika pambano hilo alitumbukiza wavuni bao hilo dhidi ya Swansea katika dakika ya 68 akimalizia kazi nzuri ya Nemanja Matic na kuwachambua mabeki wa Swansea kabla ya kufumua shuti kali lililoenda kimiani.
Wenyeji wa mchezo huowalijikuta wakicheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki wao Chico kutolewa mapema kwa kuonyeshwa kati ya pili ya njano dakika ya 16 ikiwa ni dakika mbili tangu aonyeshwe ya kwanza na kuifanya timu yake ipate pengo lililotumiwa vyema na vijana wa Jose Mourinho kuibuka na ushindi.
Ushindi huo wa Chelsea umeifanya ifikishe pointi 75, mbili pungufu na ilizonazo vinara wa ligi hiyo, Liverpool iliyoitia adabu Manchester City mapema leo katika pambano lililochezwa katika uwanja wa Anfield.

Buriani Mzee Muhidini Mwalimu Gurumo

Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka akimkabidhi Muhidi Gurumo fedha alizochangiwa kwa ajili ya matibabu wakati akiugua
MUHIDINI Mwalimu Gurumo (sio Maalim kama ilivyozoeleka kwa wengi) hatunaye baada ya kufariki dunia mchana wa leo baada ya kuteseka kwa muda mrefu na maradhi mchanganyiko.
Mkongwe huyo ambaye alitangaza kustaafu muziki Septemba mwaka jana baada ya kuitumikia fani hiyo kwa miaka karibu 55, amefariki akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Mzee huyo ameondoka huku akiwa bado anahitajika katika medani ya muziki kutokana na uzoefu wake katika fani hiyo aliyoianza akiwa na miaka 21 tu.
Mmiliki wa Blogu hii aliwahi kufanya mazungumzo na gwiji huyo wakati akijiuguza nyumbani kwake na kupata historia kamili ya fani yake ya muziki alipoanzia mpaka alipotangaza kustaafu ambapo nyota wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul 'Diamond' aliamua kumzawadia zawadi wa gari kufuatia kulalama kwamba kwa miaka yote 55 ya kufanya muziki hana cha kujivunia.
Hapo chini nimeamua kuiweka makala hiyo kama ilivyo ili umjue kwa undani mwanamuziki huyo ambaye ni vigumu kusahaulika kwa kipaji alichokuwa amejaliwa na namna alivyokuwa mstari wa mbele kutetea wanamuziki pamoja na kukumbatia utamaduni wa Kitanzania.
Taarifa ziliztufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa Mzee Gurumo atazikwa kesho majira ya saa 7 mchana kijijini kwake Masaki, Kisarawe mkoani Pwani na msiba kwa sasa upo Mabibo External.
***
Mzee Gurumo alikuwa mtu wa kujichanganya hapa akiwa na Nyosi El Saadat wa FM Academia
HUWEZI kuuzungumzia muziki wa Tanzania hasa miondoko ya dansi, bila kulitaja jina la Muhidin Mwalimu Gurumo (sio Maalim kama baadhi walivyozoea kumuita).
Hii ni kwa sababu mwanamuziki huyo mkongwe, maarufu kama 'Kamanda' au 'Mjomba', aliyewahi kutamba na kuziasisi bendi mbalimbali nchini ameutumia zaidi ya nusu ya umri wake katika mambo ya muziki, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika fani hiyo.
Gurumo alianza fani ya muziki katika bendi za mitaani miaka ya 1950 akipitia bendi moja baada ya nyingine hadi Msondo Ngoma, ingawa kwa siku za karibuni amekuwa hapandi jukwaani mara kwa mara kutokana na afya yake kutetereka kwa maradhi, hata hivyo aliendelea kuwa mhimili wa bendi hiyo.
Mzee Gurumo akitunukiwa tuzo maalum na Rais Jakaya Kikwete wakati wa uzinduzi wa TBC1 ya Tido Mhando

Gurumo (wa tatu toka kushoto) akiwa na wanamuziki wenzake wakongwe
Mzee Gurumo akionyesha ukali wake enzi za uhai wake
Gurumo akiwa nyumbani kwake kipindi akichanganya kwente maradhi yake
Mzee Gurumo akiwa uwani mwa nyumba yake iliyopo Mabibo mmiliki wa blogu alipomtembea nyumbani kwake mwaka 2012 na kutengeneza makala hii.
Mzee Gurumo akiwa na tuzo zake
Mzee Gurumo akiwa sebeleni kwake
Mzee Gurumo akiwa na mkewe kipenzi.
Mzee Gurumo akiwa na wanamuziki wenzake wa Msondo wakati maradhi yakichanganya mwilini mwake, lakini damu ya muziki haikumzuia kupanda jukwaani.
Mbali na mchango wake binafsi kama mwanamuziki, Gurumo mwenye umri wa miaka 71 amekuwa msaada mkubwa kwa wanamuziki waliowahi kuibuliwa naye au kufanya naye kazi kutokana na misimamo yake thabiti ya kulinda na kutetea haki za wanamuziki.
Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya naye kazi na Gurumo ni Shaaban Dede 'Super Motisha', Bennovilla Anthony, Hassan Rehani ‘Bitchuka’ na wengine kadhaa wakiwemo waliotangulia mbele ya haki kama Suleiman Mbwembwe na Tx Moshi William, wamewahi kukiri jambo hilo.
"Kama viongozi wa bendi wangekuwa kama Gurumo katika kupigania na kutetea haki za wasanii, naamini tungekuwa mbali mno, mjomba (jina jingine la utani la Gurumo) huwa hataki mchezo," aliwahi kusema Dede.
Wakati wa mahojiano maalum na yeye yaliyofanyika hivi karibuni nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam, Gurumo alisema kwamba kilichokuwa kikimsukuma kuwapigania wanamuziki wenzake na yeye mwenyewe ni dhamana ya uongozi na hali ya umaskini aliozaliwa nao.
"Unajua mimi nimezaliwa katika familia ya kimaskini na kimekulia kwenye umaskini, hivyo nafsi yangu huwa ngumu kumkandamiza maskini mwenzangu kwani naamini sio haki na dhambi kubwa kwa Mungu," alisema.
"Japo nilikuwa katika nafasi ya kufanya hila kwa kuegemea upande wa wamiliki wa bendi, ila kule kutambua kuwa uongozi niliopewa na wenzagu umetokana na imani  yao kwangu, ndio maana nilikuwa mkali kama pilipili kuwapigania wenzangu," aliongeza.
Gurumo, alisema hata alipokuwa akishawishiwa na baadhi ya wamiliki wa bendi ili kuwageuka wenzake ilimradi yeye aongezwe dau lolote analotaka, hakukubali kirahisi na  wakati mwingine kufikia kuamua kuhama iwapo dai lake halisikilizwi.
"Karibu bendi zote nilizopitia misimamo yangu ilikuwa hivyo na ikitokea uongozi ukawa mbishi  kukaidi madai ninayowasilisha kwao, huwa radhi kuondoka kama nilivyofanya OSS na kwingine," aliongeza.
Gurumo, alisema kutokana na misimamo hiyo mikali, alijikuta kila bendi aliyojiunga nayo wanamuziki wenzake humchangua kuwa kiongozi hadi sasa akielekea kustaafu fani hiyo kutokana na umri kumtupa mkono na maradhi yanayomsumbua kwa hivi sasa.
Alisema, tabia yake ya kutanguliza masilahi ya wanamuziki wenzake mbele kwa kiasi fulani yamechangia kushindwa kujijenga kimaisha kulinganisha na umaarufu wa jina lake na umri alioutumia katika fani hiyo ya muziki.
Gurumo, alisema katika umri wa zaidi ya miaka 40 aliyotumia katika muziki hana cha  kujivunia zaidi ya kujenga nyumba yenye vyumba 17 eneo la Mabibo, kujenga nyumba nyingine katika shamba lake lililopo kijijini kwao Masaki, Kisarawe, mkoani Pwani.
"Nyumba hii kama unavyoiona ambayo nimewapangisha watu na ninaendelea kuikarabati ndio pekee ya kujivunia, pia nina shamba nililojenga kibanda kingine huko Masaki, lakini kwa hadhi yangu nilipaswa kuwa mbali na hapa au vipi?" alisema Gurumo kwa kuhoji.
Alisema, kwa hadhi yake wala asingekuwa akipigana vikumbo na mashabiki wake kwenye daladala aendapo kwenye shughuli zake na hata kwenye kliniki ya matatizo yake kiafya, lakini hana jinsi kwa vile hana uwezo wa kumiliki hata gari ndogo ya kutembelea.
"Naamini wengine wanaweza wasiamini, lakini ukweli ni kwamba sijahi na wala sijui ni lini nitakuwa na usafari wangu binafsi, natamani lakini tatizo uwezo wa kifedha ndio tatizo, kama sio kujenga banda hili hapa Mabibo, sijui ingekuwaje," alisema.
Alisema, kinachomfanya awe katika maisha hayo licha ya umaarufu wake kimuziki,  Gurumo alisema mbali na kuthamini na kujali wengine, lakini ukweli ni kwamba enzi  akiutumikia muziki hakukuwa na masilahi ya kutosha kama wapatavyo vijana wa sasa.
"Huwa natamani miaka irudi nyuma na zama zile ziwe hivi sasa, ili nami niweze kunufaika na jasho langu katika muziki," alisema huku tabasamu la uchungu likimtoka usoni mwake.

MJOMBA
Mkongwe huyo aliyejifunza muziki tangu akiwa Shule ya Msingi Sungwi, iliyopo Kisarawe akiimba na kupiga dramu katika bendi ya shule, alisema safari yake ya muziki kwa kiasi kikubwa ilichangiwa na mjomba wake aitwaye Seleman Sultan Wamikole.
Alisema mjomba wake aliyemchukua tangu akiwa mdogo baada ya baba yake mzazi  Mwalimu Mohammed Gurumo, kufariki na kumuacha katika maisha magumu na ndugu zake wakiwa na mama yao Mwazani Sultan aliyefariki mwaka 1981.
Alisema kutokana na hali ilivyokuwa nyumbani kwao, mjomba wake huyo alimchukua na kuja kuishi nae Dar es Salaam maeneo ya Ilala ambapo moja kwa moja alimwandikisha katika madrasa ambako alipata fursa ya kuimba kaswida.
Alisema kuwa baadaye alipata hamu ya muziki hasa kutokana na kuvutiwa na kazi za nyota wa wakati huo, Salum Abdallah 'SAY' na Luambo Luanzo Makiadi 'Franco'.
Alisema mjomba wake huyo akishirikiana na mama yake walitambua kiu kubwa aliyokuwa nayo katika sanaa ya muziki na hivyo wakamruhusu kujiunga jumla ambako alizidi kuiva na baadaye kufuatwa na bendi mbalimbali.
"Kwa kitendo nilichofanyiwa na mjomba kwa kunitunza, kunilea na kunisaidia katika harakati zangu za muziki, ilinifanya nimtungie wimbo maalum nilikuwa OSS miaka ya  1980, wimbo uliitwa 'Shukrani kwa Mjomba'," alisema Gurumo.
Alisema anaamini kama sio mjomba na mama yake ambaye hadi leo anamliza akikumbuka alivyofariki, huenda asingefikia mahala alipo sasa kimuziki.
Mtunzi na muimbaji huyo mahiri nchini, alisema licha ya kipaji cha kuzaliwa, lakini Salum Abdallah na Franco ni watu waliochangia kufika kwake hapo alipo kwani enzi zao walimvutia mno.
"Ni kweli kipaji cha muziki nimezaliwa nacho na kukirithi kutoka kwa mama yangu Mwazani aliyekuwa kiongozi wa kundi la ngoma, ila kuvutiwa na Salum Abdallah na Franco ni sababu ya mimi kufika hapa nilipo, niliwapenda mno wanamuziki hawa," alisema.

SAFARI
Gurumo alisema baada ya kujifunza muziki kwenye makundi mbalimbali ya mitaani,  mwaka 1959 ndipo alipoanza kutambulika rasmi baada ya kuchukuliwa na bendi ya  Kilimanjaro Chacha.
Alisema alijiunga na bendi hiyo kama muimbaji ingawa pia alikuwa anamudu kupiga  dramu chombo alichokuwa akikipiga katika bendi ya shule na ndani ya bendi hiyo ndipo alipotunga kibao chake cha kwamba kilichoitwa 'Wakati Nikiingia Bar'.
Hata hivyo Gurumo alisema hakukaa sana Kilimanjaro Chacha kwani mwaka 1962  alihama na kwenda kujiunga bendi ya Rufiji Jazz alipokutana na wakali kama Salum  Nonde, Mbarouk Khalfan na wengine.
Alisema alijiunga na bendi hiyo kutokana na kushawishiwa na safari ambayo Rufiji Jazz ilikuwa ikitarajia kufanya mkoani Arusha na pia maslahi, hata hivyo miezi michache baadaye aliiacha bendi hiyo na kuhamia Kilwa Jazz B mwaka 1963.
"Masiahi na ujana ndio ulionifanya niikache bendi ile na kutua Kilwa Jazz B, ambapo  kutokana na kipaji kikubwa cha uimbaji nilichokuwa nacho, uongozi wa Chama cha Wafanyakazi (NUTA) uliamua  kunichukua na kutua NUTA Jazz mwaka 1964," alisema.
Alisema kuwa alipotua NUTA alitunga kibao kilichokuja kumpa umaarufu cha kilichoitwa 'Mwangele', kikiwa na maana 'Mchumba' kwa lugha ya Kingoni na kisha kufuatiwa na nyimbo nyingine kadhaa.
"Kwa kweli idadi ya nyimbo nilizotunga nikiwa NUTA sizikumbuki kwa wingi wake, ila baadhi ni kama "Nimuokoe Nani', 'Kaka Seleman', 'Amina', Msondo Ngoma Na.1-4 na 'Maneno ya Nyerere'," alisema.
Gurumo alisema baada ya kuipandisha NUTA  iliyokuwa ikifahamika baadaye kwa jina la JUWATA, hasa alipowachukua wanamuziki nyota kama Bitchuka 'Stereo' na Said Mabera aliyekuwa akipuliza 'trumpet' katika bendi moja ya Arusha, Shirika la Teksi (TTTS) lilimfuata ili kuasisi bendi yao.
"TTTS walinifuata na kunieleza nia yao ya kutaka kuanzisha bendi na nikakubaliana nao ambapo walinilipa Sh 50,000, nikaondoka Juwata Jazz mwaka 1978 na kuasisi bendi ya Mlimani Park 'Sikinde' nikiwa na wanamuziki wenzangu wa Juwata na wengine kutoka Dar International," alisema.
Aliwataja baadhi ya waasisi wa bendi hiyo iliyokuja kufahamika kama DDC Mlimani Park kabla ya miaka mitatu iliyopita kurejea jina lake la awali baada ya kutemwa na mwajiri wao,  Shirika la Maendeleo mkoa wa Dar es Salaam, ni Hassani Bitchuka na marehemu Abel Baltazar aliotoka nao Juwata.
Wengine ni Joseph Mulenga 'Spoiler', Salum Machaku, Cosmas Chidumule, Hamis Juma  'Maalim Kinyasi', Ibrahim Mwinchande, Abdallah Gama na George Kessy kabla ya kuongezwa nguvu na akina Michael Enoch 'Teacher', Joseph Benard na Habib Jeff.

‘KASSIM WA KUTUMIA’
Alisema ndani ya Sikinde, kama kawaida aliendelea kutamba na utunzi wa nyimbo zilizotwaa umaarufu mkubwa ukiwemo wa 'Kassim' uliokuwa na sehemu mbili.
Gurumo alisema kibao hicho ni tukio la kweli lililomhusu rafiki yake aitwaye Kassim aliyekuwa akifanya kazi katika kampuni ya mizigo uwanja wa ndege (DAHACO), ambaye alikuwa akisifika enzi hizo kwa ulevi na kusahau familia yake.
"Huu wimbo nilimtungia rafiki yangu ambaye alikuwa akiendekeza starehe kupita kiasi na kila nilipokuwa nikimsihi apunguze,  alikuwa akinitaka nimuimbe ndipo ataacha ulevi," alisema.
Alisema kuwa baada ya hapo, ndipo alipoamua kutunga 'Kassim namba 1', ambapo mwenyewe (Kassim) alikuwa akijisikia fahari, ingawa hakuacha ulevi hadi alipopatwa matatizo kazini na kuchacha ambapo kidogo aliacha pombe na yeye kumtungia Kassim Na.2'.
Gurumo alisema mpaka sasa hajui kama jamaa yake huyo aliacha pombe na pia hajui kama yu hai au la kwa vile ni miaka mingi imepita bila kuonana naYe.
"Sijui kama yu hai au la, ila nyimbo zile zilimhusu yeye katika kumkataza anasa ingawa pia nilikuwa natoa ujumbe kwa jamii," alisema.
Mkali huyo ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Simba, akiwa ni mmoja wa wanachama wake tangu mwaka 1972 na pia anayeishabikia Manchester United ya Uingereza, alisema alikaa na Mlimani Park hadi mwaka 1985 alipojiunga na safari Sound (OSS) akiwa na Bitchuka.
Alisema alipotua OSS aliwakuta baadhi ya wanamuziki wake ambao wengi wao walitokea Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) wakilala chini na kuushinikiza kuwanunulia vitanda kama anataka aifanyie kazi bendi hiyo.
Alisema kuwa kwa bahati nzuri, uongozi ulimsikiliza  na kuwanunulia wanamuziki wote vitanda kama alivyotaka na kuanza kufanya kazi ikiwemo kubadili mtindo wa bendi hiyo wa 'Dukuduku Yee' na kuwa 'Ndekule'.
Gurumo alifichua kuwa mitindo yote aliyoasisi katika bendi za NUTA Jazz, Mlimani Park na OSS ya 'Msondo Ngoma', 'Sikinde Ngoma ya Ukae na 'Ndekule' ni ngoma ya asili ya kabila lake la Kizaramo ambazo mama yake alikuwa akiimba na kuzicheza enzi zake.
Alisema jambo hilo la kutumia ngoma za makabila ya kabila lake, ndilo ambalo hata wanamuziki nyota wa nchi za Kongo na mataifa mengine ya Afrika Magharibi wamekuwa wakifanya na kuutangaza muziki wao kimataifa tofauti na ilivyo nchini.
"Hata Wakongo na wanamuziki wa kimataifa kutoka nchi kama Senegal, Cameroon, Nigeria na Chad wamekuwa wakibuni muziki wao kwa kutumia ngoma za makabila yao, bahati mbaya vijana wengi wameshindwa kuumiza vichwa nao kubuni kazi zao na kuishia kunakili kazi za wenzao bila kujua wanawasaidia kuwatangazia, kwa kulikwepa hilo ndio maana nilikuwa nakubuni miondoko ya kabila langu la Kizaramo," alisema.
Gurumo, alisema sio jambo baya wanamuziki wa Tanzania kuiga kazi za wenzao, kitu alichodai ni vigumu kukikwepa, lakini alidai ni vema kama wangekuwa wakibuni vionjo vitakavyowatofautisha na wanamuziki hao wanaowaiga.
Alisema kwa muono wake ukiondoa Msondo na Sikinde zinazopiga muziki unaotambulika kama dansi la Tanzania, karibu bendi zote zinapiga muziki kwa kuwaiga wakongo, hata kwa zile bendi ambazo zilikuwa zikiaminika kuwa ni kilelezo rahisi kuitambulisha Tanzania kimataifa.

ULEVI
Gurumo hafichi kitu juu ya ujana wake kwa kueleza mbali na 'ubitozi' aliokuwa nao, pia alikuwa 'gangwe' enzi zake na pia aligeuzwa mtumwa wa pombe kutokana na kuwa mlevi aliyepitiliza.
Alisema, alikuwa anakata kilaji isivyo kawaida jambo ambalo lilikuwa likimfanya akorofishane na mama yake mzazi aliyetishia kumuachia 'laana' kama angeendelea kuendekeza ulevi.
"Kwa wanaonijua sidhani kama hili ni jipya, nilikuwa mlevi haswaa, kiasi mama alishindwa kunivumilia na kutishia kuniachia laana kama nisingesikilia wito wake wa kuachana na pombe," alisema.
Alisema, baada ya kushindana na 'shetani' kwa muda mrefu akikorofishana hata na mkewe, Pili bint Said Kitwana, hatimaye aliachana na ulevi mwaka 1982, miezi michache tangu mama yake mzazi kufariki.
"Ilikuwa ni kazi ngumu kuachana na pombe, lakini kwa heshima ya mama niliacha, pia shinikizo la mke wangu kipenzi ambaye ninampenda na kumsifia kwa uvumilivu wake, niliacha miezi michache baada ya mama kufariki na hadi leo situmii hiyo kitu," alisema.
Gurumo, alisema binafsi anajutia masuala ya ulevi akidai ni kati ya mambo yaliyochangia kumkosesha kufanya mambo ya maendeleo pamoja na kuihatarisha ndoa yake, kama mkewe asingekumvumilia kwa miaka 20 tangu walipooana mwaka 1962.
"Naamini ulevi uliopitiliza kwa hakika ni mbaya kama vijana wa sasa mnavyosema kwamba 'ulevi ni noma', nusura ndoa yangu ivunjike kwa ajili ya kuendekeza hii kitu, hata nilipotangaza kuachana na pombe si mke wangu wala marafiki zangu waliokuwa wakiamini hadi walipoona siku zikienda bila kupiga kilaji," alisema Gurumo.
Gurumo alisema hakuna kitu anachofurahia maishani mwake kama siku alipooana na mkewe, aliyezaa nae watoto wanne, Mariam aliyemzaa mwaka 1981,  Mwalimu, 28, Omar na Mwazani pamoja na alipoachana na pombe.
"Hivyo ndivyo vinavyonifurahisha hadi leo, nilipomuoa mke wangu na nilipoacha pombe, ila kwa huzuni ni kifo cha mama yangu, huwezi kuamini hadi leo huwa nikikumbuka natokwa machozi kwa namna mama alivyokuwa anikipenda na tulivyokuwa tunapendana na kuishi kwa upendo na furaha," alisema.
Gurumo, alisema maisha yake yamekuwa mikononi mwa mama yake kutokana na baba yake kufariki mwaka 1948 wakati akiwa na miaka nane tu, ndio maana amekuwa akimkumbuka kila mara marehemu mama yake.

BITCHUKA
Gurumo anayekula vyakula vyote halali na vyenye manufaa kwa afya yake na kunywa juisi na soda, alisema hakuna tukio lisilofutika kichwani mwake kama siku alipoamua kumsimamisha kazi 'swahiba' wake, Hassani Rehani Bitchuka.
Alisema, alifanya uamuzi huo aliouita kuwa mgumu kuwahi kukutana nao maishani kama mwanamuziki mwaka 2005, baada ya Bitchuka kugoma kushiriki kwenye onyesho la pamoja kati ya Msondo Ngoma na African Stars 'Twanga Pepeta'.
"Bitchuka aligoma kushiriki onyesho hilo kwa madai asingeweza kufanya onyesho na watoto, kitu ambacho kiliwaudhi wanamuziki wenzake na wote waliniangalia mimi kama kiongozi wao nitafanya nini kwa kosa alilofanya 'swahiba' wangu ambaye tumekuwa katika 'udugu' tangu nilipomchukua toka Arusha mwaka 1973," alisema.
Alisema, hata hivyo alilazimika kusimama kidete kama kiongozi kwa kuweka kando 'uswahiba' wake kwa Bitchuka, ili kuinusuru Msondo na kuitisha kikao nilichotangaza kumtimua kundini, jambo ambalo anadai hadi leo humpa tabu kubwa kutokana na uhusiano aliokuwa nao na Bitchuka kwa mjda mrefu.
"Kwa kweli jinamizi la tukio lile hadi leo huniwewesesha, lakini tayari nilishazungumza na Bitchuka na kunielewa, pia unajua wakati mwingine ukiwa kiongozi unapaswa kufanya maamuzi magumu bila kutarajiwa," alisema.
Alipoulizwa juu ya msanii gani kwa sasa anayemuona kama ndiye mrithi atakayeendeleza gurudumu la muziki wa dansi nchini, Gurumo bila kificho alimtaja Husseni Jumbe mmiliki wa bendi ya Talent.
"Kwangu namuona Jumbe kama ndiye tumaini pekee la maendeleo ya muziki wa dansi kutokana na kipaji kikubwa alichonacho akitunga, kuimba, kupanga muziki na kujaliwa sauti ya kipekee," alisema.
Kuhusu muziki wa kizazi kipya, alisema upo juu kwa vile unatangazwa mno na vyombo vya habari, ila haoni kama ni muziki wenye nguvu unaoweza kuufunika muziki wa dansi.
"Promo ndio inayoubeba muziki huu, kitu kinachowalemaza wasanii wake kushindwa kuwa wabunifu na kujiona wamefika mbali, wakati wana kazi kubwa hususani ya kujifunza kupiga ala mbalimbali ili wapige muziki wao utakaokubalika kimataifa tofauti na sasa wakitegemea kila kitu kifanywe studio," alisema.
Hata hivyo alikiri wanaoufanya muziki huo na taarabu wamekuwa na mafanikio makubwa kimaisha kwa vile soko limewapokea vema, jambo ambalo hata yeye hupata wivu akifikiria anapowaona vijana wakiendesha magari wakati yeye akitembea kwa miguu licha ya muda mrefu aliotumia kwenye fani hiyo ya muziki.

SWAHIBA WA JK
Gurumo, alisema fani yake ya muziki imemsaidia kufahamiana na wengi wakiwemo viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, huku akimtaja Rais Jakaya Kikwete kwamba ni mmoja wa viongozi 'rafiki' zake.
Alisema, urafiki huo ndio anaoamini ulimfanya Rais Kikwete kuvunja shughuli zake na kumtembelea hospitalini kumjulia hali alipolazwa kwa mara ya kwanza kutokana na maradhi yanayomsumbua.
Gurumo, alisema kitendo cha Rais Kikwete kuacha kazi zake kwendsa kumjulia hali na kumsaidia katika matibabu yake kumemfariji mno, kwa vile katika kulazwa kwake na hata sasa akiendelea kujiuguza nyumbani hakuna kiongozi yeyote wa serikali wakiwemo wa Wizara wa Habari na Utamaduni, kuwahi kwenda kumjulia hali.
"Huwezi amini ni yeye na mkewe, Mama Salma ndio waliokuja kunijulia hali hospitalini, akianza mwenyewe kisha mkewe kitu ambacho kinanifariji hadi leo nikiamini Rais Kikwete anatujali na kututhamini wasanii," alisema.
Aliongeza kuwa, ukiondoa kufarijika kwake kutembelewa hospitalini na Rais Kikwete na mkewe, Mama Salma, pia kitendo kilichofanya na Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka cha kuandaa onyesho maalum kwa ajili ya kumchangia ni kitu ambacho kitabaki kichwani mwake na kumpongeza mwanamama huyo maaraufu kama 'Iron Lady'.
"Kwa kweli sikutarajia kama Asha Baraka angeweza kufanya kitendo kile ambacho ni wazi ninaonyesha ni jinsi gani anavyothamini na kujali mchango katika muziki. Nadhani watu wengine wanapaswa kuiga mfano wake, ni mtu ambaye ameonyesha mapenzi kwangu na kujali mchango wangu katika muziki, namshukuru na kumpongeza," alisema.
Gurumo, anayechizishwa na rangi nyekundu na nyeupe na ambaye anapenda kutumia muda wake za ziada kujishughulisha na mambo ya Kilimo kwenye shamba lake lililopo Masaki, alisema katika maisha yake kisanii amewahi kupata tuzo mbili tu zote za mwaka 2008.
Alisema tuzo hizo ni ile ya Kili Music Award kama Mwanamuiki Mkongwe na ile ya Hall of Fame, huku aliyekuwa mdau mkubwa wa muziki nchini aliyekuwa akifanya shughuli zake Umangani, Is'haka Kibene alimtengenezea na kumpa tuzo maalum kumtambua kama 'Kamanda wa Muziki wa Tanzania.

UBUNIFU
Gurumo, aliyeanza kuonekana tena kwenye jukwaa la bendi yake ya  Msondo baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa kutokana na kulazwa hospitalini, alisema muziki wa Tanzania umepiga hatua kubwa kimaendeleo, ingawa alikiri kwamba kukosekana kwa ubunifu miongoni mwa wananamuziki na wasanii wake ni tatizo linaloukwaza usitambe nje.
Alisema, hata muziki wa kizazi kipya (bongofleva) ambao umekuwa ukitajwa kama wenye maendeleo makubwa kwa wasanii wake, alisema unashindwa kutamba kimataifa kwa sababu wasanii hao hawaumizi vichwa kubuni vitu vipya.
Mkongwe huyo alisema tatizo la wasanii kupenda kuiga kazi za wenzao wa nje na kuzifanya zao kwa kuziimba kiswahili, ndilo linalowafanya wasitambe kimataifa na kutaka kuwepo kwa mabadiliko kuanzia sasa.
Alisema suala la kuiga kazi za nje halijaanza sasa, bali kitamboi kirefu akikiri hata wao (wakongwe) walikuwa wakifanya hivyo, ila alisema ubunifu wa ziada ndio uliowafanya waonekane mahiri katika soko la kimataifa.
"Kuiga ni jambo lisilokwepeka, lakini ni wajibu wa wasanii wa sasa kuumiza vichwa na kubuni vitu vipya ambavyo vitawatofautisha na wanaowaiga. Sio Bongofleva wala dansi kote wamelemaa kwa kuiga kazi za wenzao," alisema.
Alisema cha ajabu hata bendi za zamani ukiondoa Msondo Ngoma na Mlimani Park, zote hushindana kupiga muziki wa kikongo bila kujua wanasaidia kuutangaza muziki wa nchi hiyo na kuzidumaza bendi zao tofauti na Msondo na Sikinde.
Aliongeza anahisi bendi hizo zimeamua kuingia kwenye mkumbo huo kutokana na upepo wa soko ulivyo, japo alisema kimezifanya bendi husika zisiwasisimue mashabiki wake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

KUSTAAFU
Gurumo, alisema hana muda mrefu kabla ya kutangaza kustaafu fani ya muziki kutokana na hali yake ya kiafya na umri mkubwa alionao akitaka kuwapisha wanamuziki wenye damnu changa kuendelea gurudumu la fani hiyo.
Alisema, ingawa hajajua ni lini atafanya hivyo ila hadhani kama utamalizika mwaka huu wa 2012 kabla ya kutimiza azma hiyo na kudai atakapostaafu atajikita kwenye kuwasaidia vijana chipukizi.
Gurumo, alisema mipango yake ni kuanzisha chuo cha muziki anachotaka kukijenga Masaki, Kisarawe iwapo atapata mtu wa kumsaidia kufanikisha hilo kwa lengo la kutaka kuendeleza vipaji na kuudumisha muziki wa Tanzania.
"Sina muda mrefu kabla ya kustaafu rasmi muziki, sitajiweka kando kabisa na ndoto zangu ni kutaka kujenga chuo cha muziki katika shamba langu lililopo Masaki, lakini natatizwa na hali ya kiuchumi, hivyo kama serikali au mtu yeyote mwenye uwezo kifedha akinisaidia nitafurahi kwa vile nataka kuendeleza muziki wetu," alisema.
Alisema, anaamini vijana wanapaswa kujifunza mengi kutoka kwake na kwa wakongwe wengine ili kuufanya muziki wa Tanzania uendelea kudumu hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kidunia.

FAMILIA
Muhidini Mwalimu Gurumo, alizaliwa mnamo mwaka 1940 katika kijiji cha Masaki, Kisarawe akiwa ni mtoto wa pili kati ya watatu wa mzee Mwalimu Mohammed Gurumo.
Baba yake alifariki wakati Gurumo akiwa na miaka nane tu na hivyo maisha yake ya utotoni kuwa chini ya mama yake mzazi kabla ya kuchukuliwa na mjomba wake aliyemsaidia kuingia kwennye muziki.
Gurumo, alifanikiwa kufunga ndoa na mkewe, Pili bint Said Kitwana na kubahatika kuzaa nae watoto wanne, ambapo ni mmoja tu aitwae Mariam ndiye aliyerithi kipaji chake cha muziki akiimba kundi moja la taarabu lililopo Temeke.
Mkongwe huyo anayemtaja Said Mabera 'Dokta' kama mmoja wa wanamuziki viongozi anayemzimia, alisema katika maisha yake ya ndoa hakuna anachokifurahia kama kudumu kwa ndoa yake na mkewe ambayo imetimiza miaka 50 mwaka huu.
Alisema, kama sio uvumilivu wa mkewe, huenda ndoa hiyo ingevunjika kitambo kutokana na ukweli ukiondoa ulevi na kazi yake ya sanaa, pia ukorofi aliokuwa nao uliochangiwa na ujana ni kati ya mambo yaliyotaka kuivunja ndoa yake.
"Sio siri najivunia kuwa na mke mvumilivu kama huyu, kuna mambo niliyomfanyia kwa muda mrefu ndani ya ndoa yetu, lakini alinivumilia hadi leo tukiingia mwaka wa 50 tangu tuoane mwaka 1962," alisema.
Aliongeza, kuwa anaamini ndoa yao ilikuwa mipango ya Mungu ndio maana wamedumu na kuzeeka pamoja wakiwa ndio kwanza wanapendana kama wameoana jana, jambo ambalo linamfanya kila mara kumshukuru Mungu.

MKEWE
Pili Bint Said Kitwana, alikiri kwamba ndani ya uhusiano wa kimapenzi hadi kuja kuoana na Gurumo alipitia katika misukosuko mingi, lakini anashukuru Mungu alijaliwa uvumilivu na kuidumisha hadi leo.
Mama huyo alisema ugomvi wake mkubwa na mumewe ilikuwa ni tabia yake ya ulevi, hali iliyomfanya mara kwa mara kukwaruzana nae akimsihi aache.
Alisema, kuna wakati mumewe alikuwa akiondoka nyumbani Ijumaa kwenda kwenye maonyesho na asionekane hadi Jumatatu akiletwa na rafiki zake akiwa 'bwii', kitu kilichokuwa kikimuuma.
"Tatizo kubwa baina yangu na Gurumo ilikuwa suala la ulevi, hata alipokuja kuacha sikuamini," alisema.
Aliongeza, jingine ni tabia ya kuwa na 'kuchakachua nje', na kumfanya aumie roho hasa wanawake zake wa nje kumfuata na kumtukana na hata wakati mwingine kutaka kupigana nao hasa anapoamua kuambatana nae kwenye maonyesho.
Alisema, ukiondoa matatizo hayo, Gurumo ni mume bora, mpole, mkarimu  na baba anayejali familia mwenye mapenzi ya dhati, ndio maana aliamua kumvumilia hadi leo na kutoa wito kwa wanandoa wengine kuvumiliana katika ndoa zao ili kuzifanya zidumu kama ilivyo kwao.
Pia, alisema kitu kinachomfurahisha kwa Gurumo ni tabia ya kutochagua chakula cha kula, akidai hula chakula chochote isipokuwa 'kitimoto'.
Mama huyo alisema kwa namna mumewe alivyojitolea ndani ya taifa hili kupitia fani yake ya muziki ni vema serikali ikamkumbuka kwa kumsaidia angali akiwa hai, badala ya kusubiri aje afe ndipo wajitokeze kumwagia sifa lukuki.
"Naiomba serikali imsaidie mzee huyu, huwa naumia roho tunapokuwa tukipelekana klinini jinsi abiria ndani ya daladala wanavyotushangaa, najua ni kutokana na jina kubwa la Gurumo na hali aliyonayo kimaisha," alisema.
Aliongeza, ingelikuwa ni amri yake angependa kuona Gurumo akipumzika masuala ya muziki baada ya kuutumikia kwa zaidi ya miaka 50.

Mwisho

Vita ya kushuka daraja nouma


Mgambo JKT
Ashanti United
BAADA ya Azam kupata ushindi wa mabao 2-1 na kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara bila kupoteza mchezo wowote, huku Yanga ikishinda mjini Arusha kwa idadi kama hiyo, vita kwa sasa ipo kwa timu zilizopo mkiani, baada ya Mgambo JKT leo kulazimishwa suluhu kwenye uwanja wa Mkwakwani na Kagera Sugar na kuwafanya wasipumue vyema.
Sare hiyo imeifanya timu hiyo kufikisha pointi 26 moja zaidi ya timu za Ashanti United iliyoinyoa Simba jijini Dar es Salaam na Prisons iliyoishusha daraja Rhino Rangers mjini Mbeya jana kwa kuilaza mabao 4-3 ambazo kila moja ina pointi 25 baada ya mechi 25 kwa kila timu.
Timu mojawapo kati ya hizo zitaungana na Rhino Rangers na Oljoro JKT iliteremsha leo kurudi Ligi Daraja la Kwanza na Mabingwa watetezi Yanga kwa kufungwa 2-1 kuzipisha timu za Polisi Moro, Ndanda Fc ya Mtwara na Stand United ya Shinyanga zilizopanda Ligi Kuu kwa msimu ujao.
Mechi za Jumamosi hasa inayozikutanisha AShanti United na Prisons mjini Morogoro ndiyo inayosubiriwa kwa hamu kuona inakuwaje kwa timu hizo zilizorejea ligi kuu kwa misimu miwili tofauti.
Pia kama Simba itaendelea kutoa takrima kwa wapinzani wake kuna uwezekano ikajikuta ikitolewa kwenye nafasi ya nne iliyoikalia kwa muda mrefu kutokana na Kagera Sugar na Ruvu Shooting kuonekana kuinyemelea nafasi hiyo nyuma yao.
Hapa chini ni msimamo kamili baada ya mechi za leo za ligi hiyo;

                            P     W      D     L     F      A         D      Pts
1.Azam              25     17     8     0     50     15     +35     59    
2.Yanga              25     16     7     2     60     18     +42     55    
3.Mbeya City    25     12     10   3     32     20     +12     46    
4.Simba             25      9      10    6     40     26     +16     37    
5.Kagera Sugar 25      8      11    6     22     20     +2       35    
6.Ruvu Shooting25     9      8      8     26     32      -6       35    
7.Ruvu Stars     25     10     1     14     23     39     -16     31
8.Mtibwa Sugar25      7      9       9      29     30     -1      30
9.Coastal Union25     6      11     8      16     19     -3      29
10.JKT Mgambo25    6       8     11     18     34     -16    26    
11.Prisons          25     5     10    10     25     33     -8      25    
12.Ashanti Utd   25     6     7      12     20     38     -18    25    
13.JKT Oljoro    25     3     9     13     18     36     -18     18    
14.Rhino Rangers25    3     7     15     18     37     -19     16    

Inter Milan yaifumua Sampdoria x4 Italia

INTER Milan ikiwa ugenini jioni hii imeifumua timu ya Sampdoria kwa mabao 4-0, huku Napoli ikitoa kichapo cha mabao 4-2 dhidi ya wageni wao Lazio waliowafuata nyumbani kwao.
Mabingwa hao wa zamani wa Ulaya walianza kuisulubu Sampdoria dakika ya 13 baada ya Mauro Icardi kufunga bao la kuongoza akimalizia kazi ya Rodrigo Palacio bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili wageni walicharuka na kuwapeleka puta wenyeji wao kwa kufunga mabao mengine matatu kupitia kwa Walter Samuel dakika ya 60 kabla ya Icardi kuongeza jingine na Palacio kumalizia udhia dakika ya 79.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo ya Seria A, Livorno ilikung'utwa nyumbani na Chievo kwa kufungwa mabao 4-2, Hellas Verona nayo kama ndugu zao wa Chievo walilala nyumbani kwa mabao 5-3.
Torino wakiwa nyumbani kwao waliifumua Genoa kwa mabao 2-1 na Napoli wakaikaribisha Lazio kwa kipigo cha mabao 4-2.

Azam yaivua Yanga ubingwa bila kupoteza

*Yaifumua Mbeya City 2-1, Bocco shujaa
*Yanga yaishusha Oljoro kwa hasira

Mabingwa wapya wa kandanda Tanzania 2013-2014 Azam Fc
HISTORIA imeandikwa nchini baada ya Azam kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifumua Mbeya City nyumbani kwao kwa mabao 2-1.
Azam imekuwa klabu ya tisa kutwaa taji hilo baada ya kufanikiwa kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote 13 zilizopo kwenye ligi hiyo ya msimu wa 2-13-2014.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya Azam walitangulia kupata bao lililofungwa na Gaudence Mwaikimba lililodumu hadi wakati wa mapumziko kabla ya Mbeya City kuchomoa kipindi cha pili kupitia kwa Mwageni Yeya.
John Bocco 'Adebayor', alitumbukiza mpira kimiani na kuipa Azam ushindi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na kutwaa taji kabla ya ligi hiyo haijamalizika wiki ijayo wakiwavua ubingwa Yanga.
Yanga yenyewe ilikuwa jijini Arusha kuvaana na Oljoro JKT na kumalizia hasira zao kwa kuishusha daraja maafande hao kwa kuwalaza mabao 2-1, huku Simba ikikubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa dhidi ya Ashanti United inayopigana kuepuka kushuka daraja kwa bao la Mohammed Nampaka aliyefunga katika dakika ya 17.
Nayo Mtibwa Sugar ikiwa uwanja wa nyumbani ikafungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting Stars bao lililofungwa na Elias Maguli huku Mtibwa wakipoteza penati.
Nayo Kagera Sugar ilisafiri hadi Tanga kuumana na Mgambo JKT na kumaliza mechi hiyo kwa kutoka suluhu ya bila kufungana na kuwafanya Wana Nkurukumbi kufikisha pointi 35 sawa na ilizonazo Ruvu Shooting japo wenyewe wanaendelea kubaki nafasi ya tano nyuma ya Simba yenye pointi 37.

Liverpool yaikwanyua Man City 3-2

Philippe Coutinho scores Liverppol's winner against Manchester City
Coutinho akiifungia Liverpool bao la ushindi dhidi ya Manchester City
UZEMBE uliofanywa na Nahodha Vincent Kompany umeiwezesha Liverpool kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 na kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England.
Nahodha huyo alishindwa kuondosha vyema mpira uliokuwa umeelekezwa lango mwake katika dakika ya 78 wakati matokeo yakiwa 2-2 na Philippe Coutinho kuukwamisha kimiani.
Liverpool waliwaendesha puta wageni wao kwa kutangulia kufunga mabao mawili ya haraka moja likifungwa na Raheem Sterling dakika ya sita akimalizia pasi ya Luis Suárez kabla ya Martin Skrtel kuongeza la pili akimalizia kazi ya Steven Gerrard dakika ya 26.
Mabao hayo yalidumu hadi wakati wa mapumziko kabla ya kipindi cha pili mabadiliko yaliyofanywa na kocha Manuel Pellegrini kumuingiza James Milner ilibadilika na kurejesha mabao hayo.
David Silva alifunga bao la kwanza dakika ya 57 akimalizia krosi pasi ya Milner kabla ya mchezaji huyo kufumua shuti kali dakika ya 63 na kumgonga Glen Johnson na kumpoteza maboya kipa wake na kufanya matokeo kuwa 2-2 bla ya Coutinho kuwapa uongozi Liver na kuwafanya wafikishe pointi 77 baada ya mechi 34.
Manchester City waliokuwa wakihitaji angalau sare kuweza kuweka hai matumaini ya kunyakua taji hilo, wakisaliwa na pointi 70 baada ya kucheza mechi 32.
Muda mfupi ujao Chelsea watakuwa ugenini kuumana na Swansea City katika mechi nyingine ya ligi hiyo ya England.
Katika mchezo huo Liverpool ilimpoteza Jordan Henderson alionyeshwa kadi nyekundu dakika chache kabla ya pambano hilo kumalizika.

Tanzia! Mzee Gurumo Hatunaye

Mzee Gurumo enzi za uhai wake
TASNIA ya muziki nchini imepata pigo baada ya muasisi wa miondoko ya Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae na Ndekule, Muhidini Mwalimu Gurumo kufariki dunia mchana huu.
Mkongwe huyo aliyestaafu shughuli za muziki katikati ya mwaka jana kutokana na kusumbuliwa na maradhi pamoja na uzee baada ya kuutumikia muziki kwa miaka zaidi ya 50.
Taarifa zilizotufikia zinasema mkongwe huyo ambaye atakumbukwa kwa mchango wake katika muziki kwa kuasisi bendi za NUTA Jazz (Msondo Ngoma Band kwa sasa) Mlimani Park alifariki saa 9 mchana.
Inaelezwa kuwa Mzee Gurumo aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo alianguka wakati akielekea msalani katika hospitali hiyo na madaktari walijaribu kumpa tiba kutokana na hali yake kuwa mbaya na hatimaye mauti kumkuta.
Taarifa zaidi zitawajia kadri tutakavyokuwa tumezipata kwa usahihi ikiwa kujua mazishi ya gwiji hilo ambalo litakumbukwa na wanamuziki wengi nchini kutokana na tabia yake ya kutetea masilhai ya wasanii kiasi cha kutibuana na wamiliki wa bendi alizowahi kufanyia kazi.
MICHARAZO inaungana na familia, ndugu na jamaa za marehemu Mzee Gurumo pamoja na wadau wote wa muziki katika msiba huu mzito. Kwa hakika kila Nafsi itaonja Nafsi, yeye katangulia sisi tu nyuma yake.

Parma chupuchupu kwa Bologna

http://www1.pictures.zimbio.com/gi/Manolo+Gabbiadini+Bologna+FC+v+Parma+FC+Serie+lHGeErY1Sgpl.jpg
LIGI Kuu ya Italia Seria A imezidi kushika kasi wakati Parma ikiwa ugenini ikilazimika kupigana na kusawazisha bao dhidi ya vibonde, Bologna na kuambulia pointi moja kwa kutoka sare ya bao 1-1.
Bao la dakika ya 79 lililofungwa na Raffaele Palladino liliisaidia kuikoa Parma kuaibika kwa Bologna walioonekena kuelekea kushinda katika mechi hiyo.
Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya 44 kupitia kwa Nicolo  Cherubin akimalizia kati pande la Mgiriki Lazaros Christodoulopoulos.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo zilizochezwa jana Sassuolo na Cagliari zilitoshana nguvu ya kutoka sare ya 1-1, huku Roma ikitamba nyumbani dhidi ya Atalanta kwa kuikandika mabao 3-1.
Ligi hiyo itaendelea tena leo nchini huyo kwa michezo kadhaa; ambapo  Livorno itaumana na Chievo, Hellas Verona itaikaribisha Fiorentina, huku Torino wakiialika Genoa wakati Sampdoria itaumana na Inter Milan, huku Napili na Lazio zenyewe zitapimana ubavu na AC Milan itaikaribisha Catania.

Sevilla yazidi kujisongesha La Liga

http://www.number1sport.es/wp-content/uploads/2012/01/Imagen-231.pngKLABU ya Sevilla imezidi kujiweka katia nafasi nzuri ya kufuzu Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya hivi punde kupata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya wenyeji wao Real Betis katika mfululizo wa Ligi ya Hispania.
Mabao mawili yaliyofungwa na Kelvin Gameiro moja likiwa na mkwaju wa penati yaliiwezesha Sevilla wanaojiandaa kuvaana na Valencia kwenye mechi ya Nusu Fainali ya Ligi Ndogo ya Ulaya kufikisha jumla ya pointi 56 ikisalia katika nafasi ya tano nyuma ya Athletic Bilbao.
Gamerio alifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 33 na kuongeza la pili kipindi cha pili kwenye dakika ya 82 kumalizia kazi ya Diogo Figueiras.
Kivumbi cha ligi hiyo kitaendelea jioni hii kwa michezo mitatu ambapo Valencia itakuwa nyumbani kuikaribisha Elche, huku Getafe itavaana na vinara wa Ligi hiyo Atletico Madrid itakayowavuata kwao na Espaniol itaikaribisha Rayo Vallecano.

Newz Alert! Makamu wa Rais, Kova wanusurika kufa Dar

MAKAMU wa Rais Dk Gharib Mohammed Bilal p[amoja na Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli wamenusurika kufa katika ajali ya Helikopta wakati wakiwa kwenye ukaguzi wa uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua kubwa katika Jiji la Dsm.
Dk Mohamed Gharib Bilal, Dk.John Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar, Meck Sadiki na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum mkoa wa Dar es Salam Suleiman Kova na maafisa 11 waliokuwa kwenye helikopta hiyo  walinusurika kufa katika ajali hiyo iliyookea leo  Jijini Dsm.

walionusurika ni

1. Makamu wa Rais, Dr. Bilal

2. Mkuu wa mkoa wa Dar, Sadik

3. Mkuu wa polisi Kanda Maalum, Kova

Wamepata majeraha kidogo walikuwa wakikaguwa athari za mvua jijini.

Azam ndiyo habari ya mjini kwa sasa

Azam Fc inayosubiriwa kuingiz kwenye rekodi ya kuwa klabu cha tisa kunyakua taji la Ligi Kuu Tanzania Bara tangu mwaka 1965
KLABU ya Azam kama itafanikiwa kutwaa taji la ubingwa leo jijini Mbeya kwa kuilaza wenyeji wao Mbeya City, itaweka rekodi ya kuwa klabu ya tisa kunyakua taji hilo nchini tangu mwaka 1965.
Azam yenye pointi 56 ikiwa imecheza michezo 24, ina asilimia kubwa ya kutangazwa kuwa bingwa wa msimu huu, licha ya watetezi Yanga watakaokuwa jijini Arusha jioni hii kuivaa Oljoro JKT kuendelea kuwapa presha ikiwa na pointi 52.
Azam iliyoshika nafasi ya pili misimu miwili mfululizo nyuma ya Simba na Azam, safari hii hakuna kinachoonekana kuweza kuizuia kunyakua ubingwa huo ikizingatiwa kuwa inasaka pointi tatu tu kati ya mechi mbili zilizosalia ukiwamo wa leo na ule wa kufungia msimu dhidi ya JKT Ruvu utakaochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi.
Ukiondoa Yanga na Simba walionyakua mataji mara nyingi, Azam itaingia kwenye orodha ya walionyakua ubingwa huo ikifuata nyayo za Cosmopolitan iliyofanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1967.
Baada ya Cosmo walifuata Mseto ya Morogoro waliofanya hivyo mwaka 1975, kisha Pan Africans iliyoweka rekodi mwaka 1982, ikafuata Tukuyu Stars iliyonyakua mwaka 1986 na kufuatiwa na Wagosi wa Kaya, Coastal Union mwaka 1988.
Klabu ya Mtibwa Sugar ilikuja kuweka rekodi ya kunyakua taji hilo la Ligi Kuu misimu mizili mfululizo mwaka 1999 na 2000 kabla ya Simba na Yanga kupokezana taji hilo tangu hapo hadi msimu huu ambapo inaelekea wazi Azam wanaingia kwenye orodha hiyo.
Tusubiri baada ya dakika 90 za mechi za mfululizo wa ligi hiyo zinazochezwa leo kwenye viwanja vitano tofauti kujua kama Azam itaweka rekodi hiyo ya kuwa timu ya tisa kunyakua taji hilo na kuisimamisha Yanga inayoshikilia kwa sasa likiwa ni taji la 24, ikiongoza orodha ya klabu zilizonyakua mara nyingi ikifuatiwa na Simba ilitwaa mara 18.
Orodha kamili ya Mabingwa wa Ligi Kuu tangu 1965-
    1965 Sunderland (Simba)
    1966 Sunderland
    1967 Cosmopolitan
    1968 Yanga
    1969 Yanga
    1970 Yanga
    1971 Yanga
    1972 Yanga
    1973 Simba
    1974 Yanga
    1975 Mseto
    1976 Simba
    1977 Simba
    1978 Simba
    1979 Simba
    1980 Simba
    1981 Yanga
    1982 Pan Africans
    1983 Yanga
    1984 Simba
    1985 Yanga
    1986 Tukuyu Stars
    1987 Yanga
    1988 Coastal Union
    1989 Yanga
    1990 Simba
    1991 Yanga
    1992 Yanga
    1993 Yanga
    1994 Simba
    1995 Simba
    1996 Yanga
    1997 Yanga
    1998 Yanga
    1999 Mtibwa Sugar
    2000 Mtibwa Sugar
    2001 Simba
    2002 Yanga
    2003 Simba
    2004 Simba
    2005 Yanga
    2006 Yanga
    2007 Simba
    2007/08 Yanga
    2000-09 Yanga
    2009-10 Simba SC
    2010-11 Yanga
    2011-12 Simba SC
    2012-13 Yanga
    2013-14  ???

Newz Alert! Ruvu Darajani hakupitiki magari yakwama

Msururu Mkubwa wa Magari barabara ya Chalinze Mlandizi  Eneo la Ruvu Darajani,Hali hii anatokana na Mvua Zinazozidi Kunyesha hali iliyopelekea Maji kujaa na Kukatiza Juu ya Barabara,Kwa usalama magari yote yamesimama kusubiri hali kutengemaa.
Maji yaliojaa pande zote za Barabara ya Morogoro chalinze Eneo la Ruvu darajani muda huu.Maji ni Mengi Mto haujulikano unapoanzia na kuishia maji yamejaa pande zote za barabara,Magari yamesimama na hakuna Gari linalovuka daraja la Ruvu kwa sasa.



PICHA NA JF

Mwanamke atafunwa na Simba akifanya mapenzi vichakani


MWANAMKE mmoja ametafunwa na simba hadi kufa wakati alipokuwa akifanya mapenzi na rafiki yake wa kiume nje nchini Zimbabwe, iliripotiwa jana.

Sharai Mawera alifariki juzi baada ya simba huyo alipomshambulia ghafla wakati akifurahia kitendo hicho cha kufanya mapenzi na mpenzi wake ambaye hakutajwa kwenye kichaka.

Tovuti moja nchini humo iliripoti kwamba mnyama huyo aliwashambulia wapenzi hao kwenye eneo lililojitenga katika kichaka hicho kilicho karibu na kaskazini mwa mji wa Kariba.

Rafiki wa kiume wa Sharai, ambaye hakutajwa, inaaminika aliruka na kutimua mbio akiwa uchi wakati simba huyo alipowashambulia ghafla.

Chanzo cha habari kimoja kimeieleza tovuti hiyo kwamba mwanamke huyo alifariki dunia katika eneo la tukio.

Alisema: "Kwa bahati mbaya mwanamke aliraruriwa hadi kufa na simba huyo, lakini rafiki yake wa kiume alifanikiwa kujiokoa akiwa uchi."

Rafiki wa wapenzi hao alieleza Sharai alikuwa akifanya shughuli zake kwenye soko moja mjini humo na kwamba mpenzi wake alikuwa mvuvi.

Rafiki huyo alisema: "Ni mvuvi na kila mara alikuwa akikutana mahali hapo na rafiki yake wa kike, ambaye kwa sasa ni marehemu.

"Wawili hao walikuwa wakirukaruka wakati tukio hilo lilipotokea.

Simba huyo alitokea kwa nyuma yao na kuwarukia.

"Mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka kabla ya kusimama mbali ambako aliweza kushuhudia mwenzi wake alivyokuwa akishambuliwa.

"Baadaye ndipo akatimua mbio kuelekea barabarani kuomba msaada."

Tovuti hiyo iliripoti kwamba mtu huyo aliyekuwa amejawa hofu alifanikiwa kutoa taarifa.

Polisi wa mji huo na askari wenye silaha kutoka Mamlaka ya Hifadhi na Udhibiti Wanyamapori ya Zimbabwe walikimbia kuelekea eneo la tukio.

Chanzo hicho kilisema: "Askari na maofisa walifikia eneo la tukio na kufyatua risasi moja kabla ya kufika eneo husika.

"Mwanamke huyo alikuwa tayari ameshauawa. Alikuwa na mikwaruzo ya damu mwili mzima. Shingo yake na tumbo vilikuwa vimetafunwa."

Walenga shabaha walianzisha msako wa simba huyo kufuatia janga hilo, huku kukiwa na taarifa kwamba mnyama huyo anawezekana kuwa ameua mkazi wa eneo hilo ambaye alitoweka mwishoni mwa wiki.

Mabaki ya mwili wa marehemu yalipatikana juzi katika mpaka wa mji huo, ambao uko karibu na Mto Zambezi.

Polisi wanaamini mtu huyo, ambaye hakutajwa jina, aliliwa na simba wakati akielekea nyumbani kutoka klabu moja ya usiku.

Gazeti la serikali la The Helard liliripoti kwamba maofisa wanaamini taarifa kwamba mwanamke huyo aliyeuawa juzi alikuwa ameng'atwa kuliko kuliwa wakieleza kwamba simba huyo huyo anawezekana kuwa alihusika na mashambulio yote mawili.

Gazeti hilo liliongeza: "Wakazi wa mji huo kwa sasa wanaishi kwa hofu huku simba wakirandaranda kwa kujiamini kufuatia ukweli kwamba bado hawajakamatwa."
EDDY

Manny Pacquiao amshinda Timothyu Bradley kwa pointi


 Bondia Manny Pacquaio kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Timothy Bradley wakati wa mpambano wao uliofanyika leo alfajili manny pac alishinda kwa point
Bondia Timothy Bradley kushoto akipambana na Manny Pacquiao wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa WBO welterweight champion uliofanyika alfajili ya leo katika ukumbi wa MGM Grand in Las Vegas, Nevada. USA  Paquaio alishinda kwa pointi katika mchezo uho wa marudiano
Bondia Manny Pacquaio kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Timothy Bradley wakati wa mpambano wao uliofanyika leo alfajili manny pac alishinda kwa point
Bondia Timothy Bradley kushoto akipambana na Manny Pacquiao wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa WBO welterweight champion uliofanyika alfajili ya leo katika ukumbi wa MGM Grand in Las Vegas, Nevada. USA  Paquaio alishinda kwa pointi katika mchezo uho wa marudiano

Picha nyingine za athari za mvua za Dar



VIONGOZI WAZIRI WA UJENZI JOIHN MAGUFULI  WA PILI KUSHOTO MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM MECK SADIK KAMANDA WA KANDA MAALUM SULEIMAN KOVA PAMOJA NA MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE RIDHIWAN KIKWETE LEO WALIPOFIKA KUKAGUA DARAJA LILILOBOMOKA NA MVUA LEO

DARAJA LA MTO MPIJI LIMEBOKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA Add caption KUNYESHA  NCHI NZIMA DARAJA HILO NI KIUNGO MUHIMU KWA WAKAZI WA BAGAMOYO NA DARES SALAAM WAKAZI HAOKWA LEO WAMEPATA USUNBUFU WA KURUDI IMELAZIMIKA KUPITIA KIBAHA NA KUPITIAMPIJI HADI BAGAMOYO 

DARAJA

DARAJA LA MTO MPIJI LIMEBOKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA Add caption KUNYESHA  NCHI NZIMA DARAJA HILO NI KIUNGO MUHIMU KWA WAKAZI WA BAGAMOYO NA DARES SALAAM WAKAZI HAOKWA LEO WAMEPATA USUNBUFU WA KURUDI IMELAZIMIKA KUPITIA KIBAHA NA KUPITIAMPIJI HADI BAGAMOYO 

WAKAZI WA BASI HAYA ENEO LA TEGETA WAKIPITA KWENYE MAJI YA MVUA WAKIVUKA


DARAJA LA MTO MPIJI LIMEBOKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA Add caption
 KUNYESHA  NCHI NZIMA DARAJA HILO NI KIUNGO MUHIMU KWA WAKAZI WA BAGAMOYO NA DARES SALAAM WAKAZI HAOKWA LEO WAMEPATA USUNBUFU WA KURUDI IMELAZIMIKA KUPITIA KIBAHA NA KUPITIAMPIJI HADI BAGAMOYO
kibajaji nacho kimezama ene la tegeta

gari limwkwama katika mchanga eneo la Afrikana kutokana na mvua

HiviI ndivyo hali ilivyokuwa mvua za jana jijini Dar, 10 wafa

Mafuriko kila kona

Baadhi ya nyumba zikiwa zimefurika maji ya mvua zinazoendelea kunyesha Dar
Maisha haya mpaka lini?
Uokozi ulikuwepo Dah! Jiji la Dar Nouma
Uokozi na uopoaji wa waliosombwa na maji
Maji kila kona
Kubebana nako kulikuwapo
Kariakoo Jijini Dar hali ya mvua ipo hivi... ni hatari tupu
Foleni nayo usiombeeeeeeeeeeee....

Sehemu ya maduka yaliyopo eneo la Kituo cha daladala cha ITV yakiwa yamezingirwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Kutokana na mvua hizo na maji kujaa kumesababisha msongamano mkubwa wa magari kuanzia jana jioni na leo.
 Barabara ya kuelekea Goba....
 Barabara ya Goba ikiwa imeharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
 Maji yakitiririka kwa kasi katika Mto Mbezi eneo la Bondeni...
 Vijana wakitumia fursa vizuri kwa kujipatia mchanga unaotiririshwa na maji ambapo huwauzia madereva wa maroli.
 Eneo la Mwenge karibu na kituo cha daladala.....
 Moja ya daladala lililokuwa gereji likiwa limezingirwa na maji eneo la Mwenge....
 Maduka ya Mwenge yakiwa yamezingrwa na maji.....
 Mdada huyu alikuwa akipiga hesabu na kujiuliza jinsi ya kuvuka maji yaliyojaa na kukatiza barabara eneo la ITV.
 Mwenge karibu na Zahanati...... hakuna njia ya kuingilia Zahanati
 Maduka eneo la Mwenge yamejaa maji....
 Kazi haifanyiki leo katika maduka haya...
 Mwenge eneo la Nakiete......
 Maji yakikatiza barabara eneo la ITV.

MVUA kubwa ziliuzonyesha mfululizo kwa siku ya juzi mpaka leo hii imedaiwa kusababisha vifo vya watu 10 na maelfu kukosa makazi katyika maenepo mbalimbali ya jijini Dar na mkoani Morogoro.