STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 13, 2014

Tanzia! Mzee Gurumo Hatunaye

Mzee Gurumo enzi za uhai wake
TASNIA ya muziki nchini imepata pigo baada ya muasisi wa miondoko ya Msondo Ngoma, Sikinde Ngoma ya Ukae na Ndekule, Muhidini Mwalimu Gurumo kufariki dunia mchana huu.
Mkongwe huyo aliyestaafu shughuli za muziki katikati ya mwaka jana kutokana na kusumbuliwa na maradhi pamoja na uzee baada ya kuutumikia muziki kwa miaka zaidi ya 50.
Taarifa zilizotufikia zinasema mkongwe huyo ambaye atakumbukwa kwa mchango wake katika muziki kwa kuasisi bendi za NUTA Jazz (Msondo Ngoma Band kwa sasa) Mlimani Park alifariki saa 9 mchana.
Inaelezwa kuwa Mzee Gurumo aliyekuwa amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo alianguka wakati akielekea msalani katika hospitali hiyo na madaktari walijaribu kumpa tiba kutokana na hali yake kuwa mbaya na hatimaye mauti kumkuta.
Taarifa zaidi zitawajia kadri tutakavyokuwa tumezipata kwa usahihi ikiwa kujua mazishi ya gwiji hilo ambalo litakumbukwa na wanamuziki wengi nchini kutokana na tabia yake ya kutetea masilhai ya wasanii kiasi cha kutibuana na wamiliki wa bendi alizowahi kufanyia kazi.
MICHARAZO inaungana na familia, ndugu na jamaa za marehemu Mzee Gurumo pamoja na wadau wote wa muziki katika msiba huu mzito. Kwa hakika kila Nafsi itaonja Nafsi, yeye katangulia sisi tu nyuma yake.

No comments:

Post a Comment