STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 13, 2014

Inter Milan yaifumua Sampdoria x4 Italia

INTER Milan ikiwa ugenini jioni hii imeifumua timu ya Sampdoria kwa mabao 4-0, huku Napoli ikitoa kichapo cha mabao 4-2 dhidi ya wageni wao Lazio waliowafuata nyumbani kwao.
Mabingwa hao wa zamani wa Ulaya walianza kuisulubu Sampdoria dakika ya 13 baada ya Mauro Icardi kufunga bao la kuongoza akimalizia kazi ya Rodrigo Palacio bao hilo lilidumu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha pili wageni walicharuka na kuwapeleka puta wenyeji wao kwa kufunga mabao mengine matatu kupitia kwa Walter Samuel dakika ya 60 kabla ya Icardi kuongeza jingine na Palacio kumalizia udhia dakika ya 79.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo ya Seria A, Livorno ilikung'utwa nyumbani na Chievo kwa kufungwa mabao 4-2, Hellas Verona nayo kama ndugu zao wa Chievo walilala nyumbani kwa mabao 5-3.
Torino wakiwa nyumbani kwao waliifumua Genoa kwa mabao 2-1 na Napoli wakaikaribisha Lazio kwa kipigo cha mabao 4-2.

No comments:

Post a Comment