STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, April 13, 2014

Azam yaivua Yanga ubingwa bila kupoteza

*Yaifumua Mbeya City 2-1, Bocco shujaa
*Yanga yaishusha Oljoro kwa hasira

Mabingwa wapya wa kandanda Tanzania 2013-2014 Azam Fc
HISTORIA imeandikwa nchini baada ya Azam kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifumua Mbeya City nyumbani kwao kwa mabao 2-1.
Azam imekuwa klabu ya tisa kutwaa taji hilo baada ya kufanikiwa kufikisha pointi 59 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote 13 zilizopo kwenye ligi hiyo ya msimu wa 2-13-2014.
Katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya Azam walitangulia kupata bao lililofungwa na Gaudence Mwaikimba lililodumu hadi wakati wa mapumziko kabla ya Mbeya City kuchomoa kipindi cha pili kupitia kwa Mwageni Yeya.
John Bocco 'Adebayor', alitumbukiza mpira kimiani na kuipa Azam ushindi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na kutwaa taji kabla ya ligi hiyo haijamalizika wiki ijayo wakiwavua ubingwa Yanga.
Yanga yenyewe ilikuwa jijini Arusha kuvaana na Oljoro JKT na kumalizia hasira zao kwa kuishusha daraja maafande hao kwa kuwalaza mabao 2-1, huku Simba ikikubali kipigo cha bao 1-0 toka kwa dhidi ya Ashanti United inayopigana kuepuka kushuka daraja kwa bao la Mohammed Nampaka aliyefunga katika dakika ya 17.
Nayo Mtibwa Sugar ikiwa uwanja wa nyumbani ikafungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting Stars bao lililofungwa na Elias Maguli huku Mtibwa wakipoteza penati.
Nayo Kagera Sugar ilisafiri hadi Tanga kuumana na Mgambo JKT na kumaliza mechi hiyo kwa kutoka suluhu ya bila kufungana na kuwafanya Wana Nkurukumbi kufikisha pointi 35 sawa na ilizonazo Ruvu Shooting japo wenyewe wanaendelea kubaki nafasi ya tano nyuma ya Simba yenye pointi 37.

No comments:

Post a Comment