Azam Fc inayosubiriwa kuingiz kwenye rekodi ya kuwa klabu cha tisa kunyakua taji la Ligi Kuu Tanzania Bara tangu mwaka 1965 |
Azam yenye pointi 56 ikiwa imecheza michezo 24, ina asilimia kubwa ya kutangazwa kuwa bingwa wa msimu huu, licha ya watetezi Yanga watakaokuwa jijini Arusha jioni hii kuivaa Oljoro JKT kuendelea kuwapa presha ikiwa na pointi 52.
Azam iliyoshika nafasi ya pili misimu miwili mfululizo nyuma ya Simba na Azam, safari hii hakuna kinachoonekana kuweza kuizuia kunyakua ubingwa huo ikizingatiwa kuwa inasaka pointi tatu tu kati ya mechi mbili zilizosalia ukiwamo wa leo na ule wa kufungia msimu dhidi ya JKT Ruvu utakaochezwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi.
Ukiondoa Yanga na Simba walionyakua mataji mara nyingi, Azam itaingia kwenye orodha ya walionyakua ubingwa huo ikifuata nyayo za Cosmopolitan iliyofanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1967.
Baada ya Cosmo walifuata Mseto ya Morogoro waliofanya hivyo mwaka 1975, kisha Pan Africans iliyoweka rekodi mwaka 1982, ikafuata Tukuyu Stars iliyonyakua mwaka 1986 na kufuatiwa na Wagosi wa Kaya, Coastal Union mwaka 1988.
Klabu ya Mtibwa Sugar ilikuja kuweka rekodi ya kunyakua taji hilo la Ligi Kuu misimu mizili mfululizo mwaka 1999 na 2000 kabla ya Simba na Yanga kupokezana taji hilo tangu hapo hadi msimu huu ambapo inaelekea wazi Azam wanaingia kwenye orodha hiyo.
Tusubiri baada ya dakika 90 za mechi za mfululizo wa ligi hiyo zinazochezwa leo kwenye viwanja vitano tofauti kujua kama Azam itaweka rekodi hiyo ya kuwa timu ya tisa kunyakua taji hilo na kuisimamisha Yanga inayoshikilia kwa sasa likiwa ni taji la 24, ikiongoza orodha ya klabu zilizonyakua mara nyingi ikifuatiwa na Simba ilitwaa mara 18.
Orodha kamili ya Mabingwa wa Ligi Kuu tangu 1965-
1965 Sunderland (Simba)
1966 Sunderland
1967 Cosmopolitan
1968 Yanga
1969 Yanga
1970 Yanga
1971 Yanga
1972 Yanga
1973 Simba
1974 Yanga
1975 Mseto
1976 Simba
1977 Simba
1978 Simba
1979 Simba
1980 Simba
1981 Yanga
1982 Pan Africans
1983 Yanga
1984 Simba
1985 Yanga
1986 Tukuyu Stars
1987 Yanga
1988 Coastal Union
1989 Yanga
1990 Simba
1991 Yanga
1992 Yanga
1993 Yanga
1994 Simba
1995 Simba
1996 Yanga
1997 Yanga
1998 Yanga
1999 Mtibwa Sugar
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba
2002 Yanga
2003 Simba
2004 Simba
2005 Yanga
2006 Yanga
2007 Simba
2007/08 Yanga
2000-09 Yanga
2009-10 Simba SC
2010-11 Yanga
2011-12 Simba SC
2012-13 Yanga
2013-14 ???
No comments:
Post a Comment