
Baada ya jina la katibu Mkuu wa Chadema Dk Wibroad Slaa likiwa limeteuliwa na UKAWA kuwa mgombea wake wa nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Dakika chache zilizopita kwenye ukurasa wa @twitter wa Dr Slaa kathibitisha kuteuliwa na UKAWA.

Nashukuru UKAWA kwa imani kubwa. Kazi ya mabadiliko iliyoanza 1992 kwa vyama vingi imebakiza miezi michache kushinda. Kura yako ni ukombozi.
Meneja
wa Manchester United Louis van Gaal Leo huko Old Trafford Jijini
Manchester alimtambulisha rasmi Mchezaji mpya Memphis Depay mbele ya
Wanahabari katika Mkutano maalum na pia kuthibitisha Mchezaji wa
Kimataifa wa Italy Matteo Darmian anaelekea England kukamilisha Uhamisho
wake kutoka Torino.
Nae Memphis Depay, mwenye Miaka 21 na
alienunuliwa Mwezi uliopita kutoka PSV Eindhoven ya Holland Klabu
aliyoisaidia kuwa Mabingwa Msimu uliopita huku yeye akiwa ndie Mfungaji
Bora wa Ligi, alisisitiza amejiunga na Manchester United ili kutwaa
Vikombe vyote vinavyowezekana na yeye atajituma hadi mwisho. 