STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, April 9, 2014

Rais Kikwete achaguliwa Kiongozi Bora Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na katika ubalozi wa Tanzania nchini Marekani  mjini Washington DC, Marekani, ambako atapokea tuzo ya Africa’s Most Impactful Leader of the Year kwa niaba ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania mjini humo jana.

RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amechaguliwa kuwa Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi katika Maendeleo Barani Afrika kwa mwaka 2013 . 
Heshima hiyo kwa Rais Kikwete imetolewa na jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine Group na Tuzo la heshima hiyo itatolewa jioni ya leo, Jumatano, Aprili 9, 2014, katika sherehe iliyopangwa kufanyika Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C ikiwa ni pamoja na chakula cha jioni. 
Tuzo hiyo itapokelewa kwa niaba ya Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, ambaye tayari amewasili mjini Washington kwa sherehe hiyo kubwa.
Tuzo hiyo ya heshima kubwa hutolewa kwa viongozi wa Afrika ambao hutoa mchango mkubwa zaidi wa kiuchumi na kijamii kila mwaka kwa watu wao na limetolewa kwa Rais Kikwete kwa mwelekeo wake usiokuwa wa kawaida na wenye mafanikio makubwa kwa masuala ya utawala bora. 
Jarida hilo linasema kuwa ukweli wa hali hiyo bora ya utawala bora chini ya  uongozi wa Rais Kikwete umeendelea kumiminiwa sifa kimataifa na leo umeifanya Tanzania kuwa nchi ya kuigwa mfano kama kituo cha uhakika cha uwezeshaji kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa katika sera na mifumo ya uchumi.
Jarida hilo linasema kuwa Rais Kikwete alikuwa chaguo kubwa na la kwanza la wasomaji wa Jarida hilo ambao walipiga kura kupitia njia mbali mbali za mawasiliano za jarida hilo.
Linasema Jarida hilo, “Kuhusu maoni ya wasomaji wetu juu ya kiongozi yupi wa Afrika ambaye ni hodari zaidi kwa maendeleo ya kiuchumi na maendeleo, matokeo ya majibu ya swali hilo yamedhihirisha bila shaka yoyote kuhusu nafasi ya Rais Kikwete katika uongozi wa nchi yake. Na ushahidi uko kila mahali – ameweza kusimamia uchumi ambao umekuwa kwa wastani wa asili mia saba kwa miaka yote ya uongozi wake.” Sherehe za leo, miongoni mwa mambo mengine, zitaliwezesha Jarida hilo kutangaza mafanikio ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Kikwete kwa Jumuia ya Kimataifa, ikiwa ni pamoja na Jumuia ya Kimataifa ya Kibiashara, wanadiplomasia na taasisi nyingine zenye ushawishi mkubwa katika medani za kimataifa na zenye makao yake katika Jiji la Washington na maeneo ya jirani.
         
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM

Ajabu! Simba amtafuta Nyani, akikiacha kichanga!

MPIGA picha Evan Schiller na Lisa Holzwarth wametumia muda wao wa kutosha tu kuchukua picha za tukio la kusisimua na kusikitisha huko Botswana baada ya kushuhudia nyani mwenye mtoto akikumbana na hasira za simba jike mwenye njaa ambaye alimfukuza na hatimaye kumkamata na kumuua.
Nyani huyo aliuawa huku mtoto wake mchanga akiwa amemkumbatia pasipokujua kuwa mama yake tayari alikuwa ameshakufa. 
Baada ya simba kuua nyani huyo sasa kibao alikigeuzia kwa mtoto ambapo aliaanza kumtisha pamoja na mtoto huyo wa nyani kutaka kukimbia simba alimkamata tena.
Baadae mtoto wa nyani alianza kucheza na simba na kumfanya kama mamayake. Tazama picha uone tukio kamili hatua kwa hatua.
Simba akiwa amembeba nyani baada ya kumuua, huku mtoto wa nyani akiwa amemkumbatia mama yake bado
Muda mfupi, mtoto wa nyani alitaka kutoroka lakini alishindwa kupanda mti, sasa simba akamfuata kuona nini kinaendelea.
Lakini cha ajabu badala ya simba kumuua mtoto huyo wa nyani alianza kucheza naye na kukafanya kanyani kasahau machungu.
hapa sijui nyani mtoto anawaza nini, weee usicheze na simba jamani.
Wacha weee, sasa hapa simba sijui ndo kamsamehe kweli huyu nyani au ndo amemuweka kiporo njaa ikiuma amtafune, lakini mtoto wa nyani anaonekana kuenjoy tu.
Nyani mtoto kashapagawa na joto la simba, anaanza kutafuta kunyonya kifuani kwa simba, ana hatari huyu mtoto.
Raha iliyochanganyikana na hofu, hatari tupu
Wasije simba wengine! simba jike akaanza kuwatimua sasa sijui alikuwa anakalinda katoto ka nyani kasiliwe au aliona wenzake watammalizie msosi wake wa baadae.
Haa! kumbe baba nyani alikuwa kando akifuatilia issue yote na wakati simba wanazinguana akapata upenyo wa kumuokoa mwanaye na kupanda nae kwenye mti, uuuh kweli kama siku yako haijafika unaweza hata kumkamua maziwa simba na akabaki kukuchekea tu
Stori hii ni ya kufurahisha, huzunisha na kushangaza na inaonyesha ni kwa kiasi gani kila jambo limepangwa kwa maksudi yake na kwamba hata tukiwa katika magumu ya hali gani ukombozi unaweza kupatikana kikubwa tu ni kujiamini kama mtoto wa Nyani.

Chanzo:Tabia Nchi

 

Simanzi! Paroko wa RC afa ghafla

http://sw.radiovaticana.va/storico/2013/03/files/imm/1_0_669336.JPG 
BAADHI ya waamini wa Kanisa Katoliki la Bikira Maria wa Fatma mjini Geita, wameshitushwa na taarifa za kifo cha Paroko wa Parokia ya Geita, Padri Henry Kimisha aliyefariki dunia ghafla jana asubuhi.
Akitoa taarifa za kifo hicho, Msaidizi wa Askofu Jimbo Katoliki la Geita, Padri Nikodema Duba, alisema saa mbili asubuhi padre huyo aliugua ghafla na kulazimika kwenda hospitali ya wilaya ya Geita huku wakifanya maandalizi ya kumpeleka hospitali ya misheni Sengerema, lakini ghafla akafariki dunia.
Msaidizi huyo alisema Paroko Kimisha alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu, ugonjwa uliokatisha maisha yake ghafla huku akibainisha kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti cha Hospitali ya Bugando.
Padri Kimisha aliyezaliwa Juni 8, 1967 katika Kijiji cha Katunguru wilayani Sengerema, Mwanza na kupata daraja la upadrisho Julai 25, 1996 kwenye Parokia ya Nyantakubwa wilayani humo, maziko yake yatafanyika Ijumaa kwenye makaburi ya kanisa hilo.
Tanzania Daima

Roho Mkononi VPL, Azam kutawazwa mabingwa leo?


Azam wanaoweza kutawazwa kuwa mabingwa leo
Yanga kukubali kulitema taji kilaini kwa Azam leo dhidi ya Kagera Sugar
ROHO Mkononi kwenye viwanja viwili vya Ligi Kuu Tanzania Bara zitakavyozihusisha timu mbili zinazowania ubingwa wa msimu wa 2013-2014, watetezi Yanga na Azam Fc.
Yanga watakuwa uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuwakaribisha Kagera Sugar, huku wapinzani wao watakuwa uwanja wa Mabatini Mlandizi kuvaana na wenyeji wao Ruvu Shooting.
Matokeo ya aina yoyote leo yanaweza kumtangaza bingwa mpya na hasa kama Yanga ikapoteza ubingwa na Azam kushinda dhidi ya Ruvu Shooting kutokana na mahesabu ya pointi zilivyo.
Yanga wenyewe wana pointi 49, nne nyuma ya Azam wenye pointi 53 zote zikiwa zimeshacheza mechi 23 na leo zinashuka kuhitimisha raundi ya 24.
Iwapo Azam itaendeleza rekodi ya kutopoteza mechi katika ligi hiyo kwa kuwazabua Ruvu watafikisha pointi 56 ambapo kama Yanga itapoteza mechi yake ya jiji haitaweza kuzifikia hata iweje.
Kwa maana hiyo mechi hizo mbili kwa timu hizo ni kama mtu kuishikilia roho mkononi isiweze kuitoka kutokana na umuhimu wake na presha kubwa waliyonayo Yanga kuliko Azam.
Yanga waliotoka kuvuna ushindi mnono wa mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu, itakuwa na kila ulazima wa kuishinda Kagera Sugar iliyoikomalia Simba katika mechi yao iliyopita mjini Bukoba.
Kupoteza ina maana kwamba wamewavisha Azam taji hilo kwa mara ya kwanza katika historia yao tangu walipopanda Ligi Kuu mwaka 2008.
Kushinda na kisha Azam kushinda Mlandizi itaamaanisha watasubiri mechi ya Jumapili Azam wakiwafuata Mbeya City na Yanga kuifuata Oljoro mjini Arusha kuchanga tena karata zao.
Akizungumzia jana juu ya mechi hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kiziguto, alisema wanatarajia kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Kagera Sugar, lakini wamejipanga kupambana.
“Kagera ni timu nzuri, ila tumejipanga kupambana kushinda mechi hiyo na nyinginezo zilizobaki kwani hatuwezi kutetea ubingwa bila kwanza kushinda mechi zote,” alisema.
Alisema kutokana na ugumu wa mechi hiyo, ni muhimu mashabiki wao wakajitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao pamoja na kuwa watulivu wanapokuwa uwanjani kuepuka vitendo vya vurugu.
Kwa upande wa Azam, Kocha Msaidizi, Kali Ongala, alisema pointi tatu ni muhimu kwao katika mechi ya leo kuendelea kubaki kileleni hadi mwisho wa ligi hiyo, hivyo kubeba taji kwa mara ya kwanza.
“Kiukweli timu ipo vizuri na tuna uhakika tutashinda mchezo huo kutokana na maandalizi tuliyofanya, wachezaji wenyewe wanajua ni kitu gani tunataka, muhimu ni kuomba Mungu," alisema.
Hata hivyo Afisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire ametamba kwamba kikosi chao kipo tayari kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza msimu huu kuitungua Azam baada ya Simba na Yanga kushindwa.
"Tupo vyema na tunataka kuweka rekodi ya kuwa wa kwanza kuwafunga Azam, nadhani rekodi yetu kwenye uwanja wa nyumbani ipo wazi hatujapoteza mchezo Mabatini," alisema Bwire.
Naye kocha wa timu hiyo, Tom Olaba alitamba kuwa anaawaamini vijana wake watapambana dakika zote 90 kuhakikisha Ruvu wanapata ushindi ili kuzidi kusogea kwenye nafasi za juu.

Mourinho noma aivusha Chelsea nusu fainali

* Real Madrid nayo yafuzu licha ya kipigo ugenini
Winner: Demba Ba celebrates after scoring the goal that sent Chelsea into the semi-finals
Oyooooo! Demba Ba akishangilia bao lake dhidi ya PSG
Mourinho celebrates Porto's win at Old Trafford
Kocha Jose Mourinho akiwa katika furaha ya pekee usiku wa jana
Attack: Welsh winger Gareth Bale drives past Milos Jojic
Bale akijaribu kuipigania Real Madrid
Dejection: Dortmund players react at the end of the game - Lukasz Piszczek and Mats Hummels have their head in their hands
Wachezaji wa Dortmund wakiwa hawaamini kama wameng'oka Ulaya
KOCHA Jose Mourinho wa Chelsea amethibitisha kweli ni Special One kweli baada ya kuyapindua matokeo dhidi ya PSG na kutinga nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ualaya kwa faida ya bao la ugenini.
Chelsea iliyokuwa imelala wiki iliyopita kwa mabao 3-1 usiku wa jana ilipata ushindi wa mabao 2-0 na kufanya matokeo kuwa 3-3 na Chelsea kufuzu hatua inayofuata wakiwaacha PSG wakirudi Ufaransa vichwa chini.
Bao la dakika ya 88 lililofungwa na Demba Ba, lilitosha kumpa faraja kubwa Mourinho ambaye aliwashangaza mashabiki kwa kumtoa nyota wake Eden Hazard lakini kumbe alikuwa na maana yake.
Andre Schurrle aliyeingia badala ya Hazard aliifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika ya 32 akimaliza kazi nzuri ya David Luiz na kuwafanya The Blues waliokuwa uwanja wa nyumbani wa Stanford Bridge kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.
PSG iliyomkosa nyota wake, Zlatan Ibrahimovic ilipambana hadi mtokea benchi Demba Ba aliyechukua nafasi ya Frank Lampard alipofunga bao hilo dakika tatu kabla ya mchezo huo kumalizika.
Katika mechi nyingine ya robo fainali, Real Madrid iliungana na Chelsea kutinga Nusu Fainali licha ya kipigo cha mabao 2-0 toka kwa wenyeji wao Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Dortmund ikiwa kwenye uwanja wake wa Signal-Iduna-Park mjini Dortmund, ilifunga mabao yake katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Marco Reus dakika ya 24 na 37 lakini hayawakusaidia.
Katika mpambano la kwanza mjini Madrid, Wajerumani walilala mabao 3-0 na hivyo kujikuta wakiondoshwa mashindanoni na Real kwa jumla ya mabao 3-2.
Madrid pamoja na kuugulia kipigo, lakini inachekelea kuwatoa nishai wapinzani wao hao waliowang'oa kwenye Nusu Fainali ya michuano ya mwaka jana na kwenda kucheza fainali na Bayern Munich.