STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 1, 2013

Zoezi la ukufuaji jengo lililoporomoka lakamilika 36 ndiyo waliokufa


Zoezi la kuondoa kifusi katika sehemu ya chini kabisa ya jengo lililoporomoka la ghorofa 16 likiendelea kukamilishwa leo April 1, 2013.
Duh... eti hili ndilo eneo lililokuwa na msingi wa jengo la ghorofa 16 kabla ya kuporomoka Ijumaa wakati likiendelea kujengwa katika makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam... uokoaji umekamilishwa leo April 1, 2013.
Timu ya waokoaji yenye wataalam mbalimbali ikiendelea kukamilisha kazi leo April 16, 2013. 
Kama siamini vile..! Hapa ndipo liliposimama jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa na kuua watu 36 huku wengine kibao wakijeruhiwa.
Waokoaji wakiendelea kukamilisha kazi yao leo April Mosi, 2013.
Askari wa JKT walikuwa bega kwa bega hadi mwisho... hapa wakisaka watu zaidi kwenye eneo la chini kabisa (basement) leo April Mosi, 2013.
Nd'o hapa paliposimama mjengo wa ghorofa 16... waokoaji wakiendelea kukamilisha kazi leo April 1, 2013.
Hakuna mwili wa mtu mwingine?
Haikuwa kazi ndogo mzee... kamanda mmoja wa JWTZ akimfafanulia jambo mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick aliyetembelea eneo la ajali wakati wa kukamilisha kazi ya uokoaji baada ya kufikiwa kwa jengo la chini kabisa lililobeba maghoroga 16 ya mjengo ulioanguka Ijumaa na kuua watu 36. Hapa ni leo April 1, 2013.
Tumemaliza kazi mzee...!
Miili ya watu walionasuliwa kutoka katika kifusi cha jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa asubuhi wakati likiendelea kujengwa kwenye makutano ya Morogoro Road na Indira Gandhi jijini Dar es Salaam sasa imeongezeka na kufikia 36.

Idadi hiyo inatokana na miili mengine saba kupatikana hadi kufikia leo wakati zoezi la uokoaji na kunasua miili ya watu waliofukiwa na vifusi vya jengo hilo kuelekea kukamilika baada ya leo (Aprili Mosi, 3013) vikosi vya uokoaji kufikia jengo la chini kabisa (basement).

Jengo hilo lililokuwa likiendelea kujengwa, liliporomoka Ijumaa katika siku iliyokuwa ya mapumziko ya 'Ijumaa Kuu', mishale ya saa 2:30 asubuhi.
 
Rais Jakaya Kikwete, ambaye alitembelea eneo la tukio masaa machache tu baada ya kutokea, aliagiza kwamba wahusika wote waliosababisha maafa hayo wafikishwe mbele ya mkono wa sheria na hadi sasa, polisi wamesema kuwa tayari wameshawatia mbaroni watuhumiwa wanne.

Katika hotuba yake ya kila mwezi jana, Rais Kikwete alisema amehuzunishwa sana na tukio hilo la kuanguka kwa jengo hilo lakini ameridhishwa na juhudi kubwa za uokoaji zilizofanywa na wanajeshi wakishirikiana na taasisi, mashirika binafsi na wananchi wa kawaida.

“Napenda kutumia nafasi hii kutoa shukrani maalum kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick kwa uongozi wake madhubuti.  Pia nampongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala,  Raymond Mushi, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Suleiman Kova pamoja na maafisa na askari wa JWTZ, na wale wote walioshiriki na wanaoendelea kushiriki katika juhudi za uokoaji,” alisema. 

Rais Kikwete aliwapa pole wale wote waliofiwa na akaagiza watakaothibitika kusababisha maafa hayo wachukuliwe hatua zinazostahili, ikiwa ni pamoja na kuwaburuza mahakamani na wengine kufutiwa leseni za kufanya shughuli za ujenzi.

Wakati Dar maiti zikifikia 36, maafa mengine yatokea Arusha


Picture

Picture

Picture

WAKATI idadi ya maiti zilizopatikana kwenye ajali ya jengo la ghorofa 16 lililoporomoka juzi jijini Dar es salaam ikifikia 36, habari kutoka Arusha zinasema kuwa watu wanaokadriwa kufikia 20 wamefukiwa kifusi katika machimbo ya changarawe, yaliyopo eneo la Mashono, Arusha.
 Taarifa zinasema kuwa kwa sasa wanajeshi wanaendelea na zoezi la uokoaji na tayari majeruhi mmoja ameokolewa na miili ya watu watatu.
MICHARAZO inaendelea kufuatilia taarifa hizo na itawafahamisha hapa hapa.

Demba Ba 'awaua' Mashetani Wekundu Darajani


Demba Ba wa Chelsea akiifungia timu yake bao pekee katika pambano la marudiano ya Kombe la FA jioni ya leo

BAO pekee lililofungwa kiufundi jioni ya leo na Demba Ba, lilitosha kuizamisha vinara wa Ligi Kuu ya England, Manchester United katika pambano la marudiano la Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi yao na Chelsea.
Pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, London lilishuhudiwa hadi wakati wa mapumziko timu zote kiuwa nguvu sawa kwa kutofungana.
Demba Ba alifunga bao hilo lililoipeleka Chelsea hadi fainali ya michuano hiyo alitumbukiza wavuni mbele ya mabeki wa Manchester United katika dakika ya 49.
Manchester walionyesha kulipania pambano hilo, baada ya pambano lao lililochezwa Machi 10 kwenye uwanja wa Old Trafford kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, lakini vijana wa darajani waliwakwamisha na kukifanya kikosi hicho cha Sir Alex Ferguson kuelekeza nguvu zake kwenye ligi kuu ili kuambulia taji mwaka huu.
Kwa ushindi huo Chelsea sasa imepata nafasi ya kukwaruzana na Manchester City katika pambano la nusu fainalik, litakalochezwa Aprili 14, siku mpoja baada ya Millwall kuumana na Wigan Athletic.

Wapinzani wa Azam kutua nchini kesho, Azam waiendea kambini


Na Boniface Wambura
TIMU ya Barrack Young Controllers II ya Liberia inatarajia kuwasili nchini kesho (Aprili 2 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam itakayochezwa Jumamosi (Aprili 6 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Young Controllers itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya PrecisionAir ikitokea Nairobi, Kenya inapounganisha safari hiyo inayoanzia Monrovia kupitia Accra, Ghana.

Msafara wa timu hiyo utakuwa na watu 37 wakiwemo wachezaji 21 na utaongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo Robert Alvin Sirleaf ambaye ni mtoto wa Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf.

Wachezaji waliomo kwenye kikosi hicho ni Abraham Andrew, Alfred Hargraves, Alpha Jalloh, Benjamin Gbamy, Cammue Tumamie, Erastu Wee, Ezekiel Doe, George Dauda, Hilton Varney, Ishmail Paasewe, Joekie Solo, Joseph Broh, Junior Barshall, Karleo Anderson, Mark Paye, Prince Jetoh, Prince Kennedy, Randy Dukuly, Raymond Blamonh na Winston Sayou.

Benchi la ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Robert Lartey akisaidiwa na Samuel Sumo wakati Meneja wa timu ni Clarence Murvee. Daktari wa timu ni Samuel Massaquoi.

Timu hiyo inatarajia kundoka kurejea Monrovia, Aprili 8 mwaka huu kupitia Nairobi, Kenya saa 11.10 alfajiri kwa ndege ya PrecisionAir.

MSIBA SOKA LA BONGO, TFF YATUMA RAMBIRAMBI


Na BONIFACE WAMBURA
SIMANZI katika medai ya soka baada ya mwishoni mwa wiki wachezaji wawili mmoja wa zamani na mwingine anayekipiga Polisi Tabora kufariki dunia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Coastal Union, TPC na Taifa Stars, Behewa Ali Sembwana (72) kilichotokea jana usiku (Machi 31 mwaka huu) mkoani Tanga.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Sembwana akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

Sembwana aliyekuwa akicheza wingi ya kulia alidumu katika Taifa Stars kwa miaka kumi, kama ilivyokuwa kwa kombaini ya Mkoa wa Tanga (Tanga Stars) aliyoiwakilisha katika michuano ya Kombe la Taifa (Taifa Cup).

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Sembwana, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tanga (TRFA) na klabu ya Coastal Union na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Maziko yanatarajiwa kufanyika leo (Aprili 1 mwaka huu) kijijini kwake Lusanga, Wilaya ya Muheza mkoani Tanga. Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi. Amina

Aidha TFF limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha mshambuliaji wa timu ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Polisi Tabora, Regan Mbuta kilichotokea jana (Machi 31 mwaka huu) usiku kwa ajali ya pikipiki mjini Tabora.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora (TAREFA), Yusuf Kitumbo, marehemu anatarajiwa kusafirishwa leo (Aprili 1 mwaka huu) kwenda kijijini kwao Kimamba, Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko.

Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani Mbuta alikuwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Polisi Tabora, na bao lake la mwisho aliyoifungia timu ilikuwa kwenye mechi ya mwisho ya FDL msimu huu dhidi ya Pamba ya Mwanza iliyochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Mbuta, TAREFA na klabu ya Polisi Tabora na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito. Mungu aiweke roho ya marehemu Mbuta mahali pema peponi. Amina

Golden Bush, Wahenga walipoisherehekea Pasaka uwanja wa Kinesi jana

TIMU ya soka ya veterani ya Golden Bush jana iliendeleza ubabe kwa wapinzani wao wa jadi, Wahenga Fc kwa kuwanyuka mabao 2-1 katika pambano maalum la kusherehekea sikukuu ya Pasaka, mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Kinesi na kuhudhuriwa na Kamanda Thobias Andengenye aliyekuwa mgeni rasmi.
Chini ni baadhi ya picha za matukio ya pambano hilo ambalo limeifanya Golden Bush Veterani kuitambia Wahenga kwa mara ya pili mfululizo ndani ya mwaka huu wa 2013, baada ya awali kung'ang'aniwa sare ya 1-1 na kucharazwa 4-3 katika pambano la kuuaga mwaka 2012 mechi zote zikichezwa uwanja wa TP Afrika.

Kamanda Thobias Andengenye (mwenye suti) akijiandaa kupokea zawadi wa Pasaka toka kwa aliyekuwa mwamuzi wa pambano hilo la jana Ally Mayay, huku vikosi vya timu zote mbili za Golden Bush (kulia) na Wahenga Fc (wenye jezi nyekundu ) wakishuhudia baada ya kukaguliwa na kamanda huyo aliyekuwa mgeni ramsi wa mchezo huo maalum wa Pasaka.



KARIBU TENA! Kamanda Thobias Andengenye akiagwa na viongozi wa Golden Bush, Godfrey Chambua (kati) na Onesmo Waziri 'Ticotico' mara baada ya kumalizika kwa pambano la Golden Bush dhidi ya Wahenga lililochezwa jana kwenye uwanja wa Kinesi.

Vikosi vya timu za Golden Bush na Wahenga Fc wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa mgeni rasmi wa mchezo wao maalum wa Pasaka, Afande Thobias Andengenye (kwenye shuti ya brown katikati).

Wahenga Fc wakisalimia uwanja kabla ya kukumbana na kipigo cha mabao 2-1 toka kwa wapinzani wao
Vikosi vya timu za Wahenga Fc (jezi nyekundu) na Golden Bush (kijani) wakiwa na mgeni rasmi Thobias Andengenye kabla ya kuanza kwa pambano lao ambalo lilikuja kutibuliwa na mvua kubwa iliyonyesha jana, ambapo hata hivyo haikuzuia kufanyika kwake na kushuhudia Wahenga wakifa kwa mabao 2-1.

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria pambano hilo kenye uwanja wa Kinesi, Ubungo Dar es Salaam.

Polisi yaanika watu nane inayowashikilia ajali ya ghorofa Dar


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam imeyaanika majina ya watuhumiwa nane inaowashikilia kutokana na ajali ya jengo la ghorofa 16 lililoporoka juzi na kusababisha vifo vya watu kadhaa na wegine kujeruhiwa.

Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema kuwa idadi ya watu wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo imeongezeka na kufikia wanane.
Kova aliwataja watu hao inawashikilia kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ni pamoja na mmiliki wa ghorofa hilo, Raza Husein Damji (69) na mtoto wake, Ally Raza Damji (31) ambaye alikuwa akishirikiana naye.
"Wengine tunawashikilia ni wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,  Mhandisi Ogare Salu, Mhandisi wa Majengo , Goodluck Mbagaga, na Mkaguzi wa Majengo, Wilbroad Mugyabusu," alisema Kamanda Kova..
Aliongeza pia, Mkandarasi wa Kampuni ya Lucky Construction iliyokuwa ikijenga jengo hilo na ni Diwani wa Goba (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed Kisoki naye pia ni miongoni mwa watu hao wanaoshikiliwa na jeshi hilo.
Pia wamo Zonazea Anage Oushadada (53), ambaye ni Mhandisi Mshauri na Mohamed Abdulkarim (61), mshauri wa kujitegemea aliyekuwa akitumiwa na mmiliki wa jengo.
Kamanda Kova alisema watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kama wangekuwa makini, janga hilo lisingetokea na kwamba wakati wakiendelea kuhojiwa, Jeshi la Polisi nalo litaendelea kuchunguza.
Kova alisema wakati wa zoezi la kuokoa watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo likiendelea, walikuta nondo na mifuko kadhaa ya saruji ambayo ilikuwa imefukiwa kabla ya kutumika.
Alisema kutokana na tukio hilo, serikali imemua kuchukua majina ya watu ambao ni wataalam wa masuala ya majanga ili kunapotokea janga wanaitwa haraka kusaidia.
Kamanda huyo alitoa onyo kwa watu wanaochukua nondo zinazotupwa pamoja na kifusi kutoka katika jengo lililoporomoka na kwenda kuziuza na kwamba wakikamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.