STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 1, 2013

Polisi yaanika watu nane inayowashikilia ajali ya ghorofa Dar


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam imeyaanika majina ya watuhumiwa nane inaowashikilia kutokana na ajali ya jengo la ghorofa 16 lililoporoka juzi na kusababisha vifo vya watu kadhaa na wegine kujeruhiwa.

Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova alisema kuwa idadi ya watu wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo imeongezeka na kufikia wanane.
Kova aliwataja watu hao inawashikilia kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo ni pamoja na mmiliki wa ghorofa hilo, Raza Husein Damji (69) na mtoto wake, Ally Raza Damji (31) ambaye alikuwa akishirikiana naye.
"Wengine tunawashikilia ni wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,  Mhandisi Ogare Salu, Mhandisi wa Majengo , Goodluck Mbagaga, na Mkaguzi wa Majengo, Wilbroad Mugyabusu," alisema Kamanda Kova..
Aliongeza pia, Mkandarasi wa Kampuni ya Lucky Construction iliyokuwa ikijenga jengo hilo na ni Diwani wa Goba (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Ibrahim Mohamed Kisoki naye pia ni miongoni mwa watu hao wanaoshikiliwa na jeshi hilo.
Pia wamo Zonazea Anage Oushadada (53), ambaye ni Mhandisi Mshauri na Mohamed Abdulkarim (61), mshauri wa kujitegemea aliyekuwa akitumiwa na mmiliki wa jengo.
Kamanda Kova alisema watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kama wangekuwa makini, janga hilo lisingetokea na kwamba wakati wakiendelea kuhojiwa, Jeshi la Polisi nalo litaendelea kuchunguza.
Kova alisema wakati wa zoezi la kuokoa watu waliofukiwa na kifusi cha jengo hilo likiendelea, walikuta nondo na mifuko kadhaa ya saruji ambayo ilikuwa imefukiwa kabla ya kutumika.
Alisema kutokana na tukio hilo, serikali imemua kuchukua majina ya watu ambao ni wataalam wa masuala ya majanga ili kunapotokea janga wanaitwa haraka kusaidia.
Kamanda huyo alitoa onyo kwa watu wanaochukua nondo zinazotupwa pamoja na kifusi kutoka katika jengo lililoporomoka na kwenda kuziuza na kwamba wakikamatwa watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment