STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, April 1, 2013

Golden Bush, Wahenga walipoisherehekea Pasaka uwanja wa Kinesi jana

TIMU ya soka ya veterani ya Golden Bush jana iliendeleza ubabe kwa wapinzani wao wa jadi, Wahenga Fc kwa kuwanyuka mabao 2-1 katika pambano maalum la kusherehekea sikukuu ya Pasaka, mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Kinesi na kuhudhuriwa na Kamanda Thobias Andengenye aliyekuwa mgeni rasmi.
Chini ni baadhi ya picha za matukio ya pambano hilo ambalo limeifanya Golden Bush Veterani kuitambia Wahenga kwa mara ya pili mfululizo ndani ya mwaka huu wa 2013, baada ya awali kung'ang'aniwa sare ya 1-1 na kucharazwa 4-3 katika pambano la kuuaga mwaka 2012 mechi zote zikichezwa uwanja wa TP Afrika.

Kamanda Thobias Andengenye (mwenye suti) akijiandaa kupokea zawadi wa Pasaka toka kwa aliyekuwa mwamuzi wa pambano hilo la jana Ally Mayay, huku vikosi vya timu zote mbili za Golden Bush (kulia) na Wahenga Fc (wenye jezi nyekundu ) wakishuhudia baada ya kukaguliwa na kamanda huyo aliyekuwa mgeni ramsi wa mchezo huo maalum wa Pasaka.



KARIBU TENA! Kamanda Thobias Andengenye akiagwa na viongozi wa Golden Bush, Godfrey Chambua (kati) na Onesmo Waziri 'Ticotico' mara baada ya kumalizika kwa pambano la Golden Bush dhidi ya Wahenga lililochezwa jana kwenye uwanja wa Kinesi.

Vikosi vya timu za Golden Bush na Wahenga Fc wakiwa katika picha ya pamoja na aliyekuwa mgeni rasmi wa mchezo wao maalum wa Pasaka, Afande Thobias Andengenye (kwenye shuti ya brown katikati).

Wahenga Fc wakisalimia uwanja kabla ya kukumbana na kipigo cha mabao 2-1 toka kwa wapinzani wao
Vikosi vya timu za Wahenga Fc (jezi nyekundu) na Golden Bush (kijani) wakiwa na mgeni rasmi Thobias Andengenye kabla ya kuanza kwa pambano lao ambalo lilikuja kutibuliwa na mvua kubwa iliyonyesha jana, ambapo hata hivyo haikuzuia kufanyika kwake na kushuhudia Wahenga wakifa kwa mabao 2-1.

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria pambano hilo kenye uwanja wa Kinesi, Ubungo Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment